Je anafaa kuwa mke wangu wa ndoa?

Mndendeule110

New Member
Dec 14, 2010
2
0
Habari ndugu wapendwa wana Jf, heshima kwenu wote. Naomba mchango wa mawazo juu ya hili: nina girl friend ni mzuri sana,kazaliwa 87, ila tayari anawatoto wawili ila ukimuona ni kama hajawahi kuwa na mtoto vile,umboni dogo na anavutia.Hajawahi olewa ila bwana aliyemzalisha hao watoto kamelekeza. binti kasomea secrtarial courses na nafanya kazi stationary. sijawahi kuonana naye kimwili hata mara 1 ila roho inasita saa coz tayari yeye ana watoto wawili. nilimtega kwa mengi lakini yote yupo tayari kutkeleza.mfano nilimdanganya kuwa mie nataka mwanamke ambaye atakuwa tayari kunipa section A na B na akasemacoz ananipenda yeye yupo tayari. Hana kipato kikubwa lakini haini kunipigia simu asubuhi,mchana, jioni, nakuhusu msg ndio usiseme hadi nahisi anamaliza pesa yake kwamatumizi ya simu kwa ajili yangu. waungwana naombeni ushauri ambao utanipa mwanga wa kuweza fanya maamuzi nimuoe au laa? nawasilisha wakuu!
 
Unampenda kwa dhati na kwa moyo wako wote? Umeridhika naye katika idara muhimu I.e. maadili, tabia, mienendo, n.k.?

Kama jibu ni 'ndiyo' basi wewe mvalishe pete umchukue jumla. Usiuweke usiku....
 
fuata moyo wako unavyokutuma mwaya,kuhusu kupigiwa simu inawezekana yupo desperate haoni wa kuolewa naye baada ya kuzaa watoto wawili...hilo lisikudanganye.:redfaces::redfaces:
 
Habari ndugu wapendwa wana Jf, heshima kwenu wote. Naomba mchango wa mawazo juu ya hili: nina girl friend ni mzuri sana,kazaliwa 87, ila tayari anawatoto wawili ila ukimuona ni kama hajawahi kuwa na mtoto vile,umboni dogo na anavutia.Hajawahi olewa ila bwana aliyemzalisha hao watoto kamelekeza. binti kasomea secrtarial courses na nafanya kazi stationary. sijawahi kuonana naye kimwili hata mara 1 ila roho inasita saa coz tayari yeye ana watoto wawili. nilimtega kwa mengi lakini yote yupo tayari kutkeleza.mfano nilimdanganya kuwa mie nataka mwanamke ambaye atakuwa tayari kunipa section A na B na akasemacoz ananipenda yeye yupo tayari. Hana kipato kikubwa lakini haini kunipigia simu asubuhi,mchana, jioni, nakuhusu msg ndio usiseme hadi nahisi anamaliza pesa yake kwamatumizi ya simu kwa ajili yangu. waungwana naombeni ushauri ambao utanipa mwanga wa kuweza fanya maamuzi nimuoe au laa? nawasilisha wakuu!

Wewe mambo ya kuwa na watoto wawili na mapenzi wapi na wapi bwana??? Wewe oa tu kama unampenda. ila hapo kwenye red and bold mmmhhh
 
Sikia dogo, huyo hakufai kabisa!!!!!!!!!!!!!!!!!!! mwanamke makini hata kama anashida hawezi kubali kutoa section A na B hata utani hawezi sema, suala la kupiga simu ni kutaka kukuchanganya ukikubali tu umeliwa, watoto siyo issue hata kidogo, tatizo ni yeye mwenyewe. Tafuta mwingine...achana naye!!
 
Jaaaamaani mi kweli namwone huruma sana huyu dada...
na we ka hujamwoa anaweza aulewe na mtu yeyote kwa sababu tu anataka maisha mazuri kwa wanae..
kwa kweli kama akiolewa si dhani kama atakuwa anaolewa ajili ya upendo bali ajili ya wanae...
anaweza aje mtu amwambie mimi sitaki kupima ngoma lakini nataka kuku oa.. naye akakubali..
mimi kweli hii thread imenihuzunisha sana....tena sana..
 
ni kweli huyu msichana( na muita msichana kulingana na umri wake 86 ingawa ana watoto 2) yuko desperate ndio maana yuko radhi kwa lolote, na inaonyesha kuwa atakuwa amepitia mateso si ajabu mengi sana mpaka ahapo alipo na anapofikiria na kuona kuwa yaani kwa sasaa ndio kama vile basi.
Il akwa ushauri wangu ,kuzaa sio tatizo kwani nau hakika kama kweli un mpenda na anakupenda kwa dhati manaweza kmaishi maisha mazuri sana na yakupendeza, nakwambia kuwa muhesimu sana mwanamke ambaye amepitia shida kwani hujifunza na ameshaona mengi hivyo anaweza akawa mzuri sana kuliko hawa wa kutoka nyumbani kwanza visichana vinakuwa na kiburiiiiii, havielezeki, ukishakaeka tu nyumbani mda si mrefu kelele zina anza.
Tafakari
 
wewe bdo uko immature sana.....
na kibaya zaidi unamdanganya mwenzio

kwanza u have to grow up....
halafu ndo uanze kufikria ndoa...............
 
Afrodenzi nakushukuru sana kwa mchango wako na wadau wengine japo wengine mananiponda lakini mimi napokea tu ushauri na nitatafakari kwa kina. Mfano Afrodenzi amegusia suala la kupima Ngoma, ni kweli hilo mimi nilimjaribu kumuliza je atakuwa tayari kunipa mzigo hata kama hatujapima ngoma, yeye akasema hilo hamna shida so long as anajua mie ni mumewe mtarajiwa ataanipa tu na chochote kile yupo tayari kufanya ili mradi tu ahakikishe hanikosi katika maisha yake. sasa hapo nikaanza kuwa na mashaka makubwa, yupo tayari hata bila kupima au hata bila kutumia kinga inakuaje, ni upendo wa kawaida kwa umpendaye or something else behind? I am still waiting for u're contributions wapendwa wana JF
 
kaka haya mambo ni magumu sana ila cha kufanya ni wewe kuangalia malengo yako kama unafit kwenye maamuzi yako utakayofanya
 
Afrodenzi nakushukuru sana kwa mchango wako na wadau wengine japo wengine mananiponda lakini mimi napokea tu ushauri na nitatafakari kwa kina. Mfano Afrodenzi amegusia suala la kupima Ngoma, ni kweli hilo mimi nilimjaribu kumuliza je atakuwa tayari kunipa mzigo hata kama hatujapima ngoma, yeye akasema hilo hamna shida so long as anajua mie ni mumewe mtarajiwa ataanipa tu na chochote kile yupo tayari kufanya ili mradi tu ahakikishe hanikosi katika maisha yake. sasa hapo nikaanza kuwa na mashaka makubwa, yupo tayari hata bila kupima au hata bila kutumia kinga inakuaje, ni upendo wa kawaida kwa umpendaye or something else behind? I am still waiting for u're contributions wapendwa wana JF

kwa kweli mi bado nasikitika sana kuna watu kama hao...
mi nishakwambia huyu aatafuta maisha mazuri tu kwa watoto wake..
ni mama mwenye upendo sana kwa watoto wake... hajali kabisa nii kitatokea maishani mwaka..
inaonekana hajali tu haya hiyo ngoma ilimradi tu watoto wake wawe kwenye mikono miziru...
kwa kweli ni mapenzi ya mama kwa watoto tu.... labda kweli anakupenda nawe lakini katika maelezo uliyotoa haionyeshi..
kitu ambacho mi naona anataka kukuridhisha tu.... ili muoane... poleni sana...
sasa mimi ntakacho kushauri kama kweli kweli unampenda pitieni angaza halafu maisha yaendelee...
lakini kama ka unaona we bado hauko tayari usimpotezee muda mtoto wa watu...
mwambie tu ukweli .... lakini sasa unatakiwa kuwa makini sana kwa sababu alisha kuabali kila kitu.....(chunga maneno yako)

mie nawatakia kula lakheri...

AD
 
Hahaahah watoto wawili! Mmmhh hiyo ni disqualification tosha. Kwanini usiwe na subira wapo wanawake wengi na hawana watoto! Kwanini ujiweke sehemu itakayokukondesha kwa mawazo na matumizi. Kwanza fatilia kwanini jamaa aliyemzalisha amesepa? Wanawake ni wajanja sana hawezi kukwambia ukweli wa mume wa kwanza. Zaidi utaambiwa ubaya wa jamaa. Halafu wewe umekaa kingono ngono zaidi, mke huwezi zungumzia mambo ya A na B hatua za mwanzo hivyo. Kutokana na post yako wewe bado una utoto! Dada kupiga simu amewekeza ingia uuvae mkenge mchana mchana.

Hao watoto wake watakuita nani wewe? Uncle ama baba mdogo? Jamaa siku akitaka kukumbushia je? maana hao ni wazazi na hawala hana talaka.
 
Jipende mwenye kwanza kabla ya kutafuta mwingine wa kumpenda.

Jaribu kumwomba Mungu akuepusha na majaribu makuwa kuliko uwezo wako wa kuyamudu.

Kila mtu ana mtazamo wake lakini hapo una kazi kubwa ya kurekebisha mambo. Huyo mwenzio naona uaminifu na uadilifu bado ni kazi kwake.
 
Jamani hii kula samaki pande zote ni ishu ya kawaida eee, yaani ni kitu mtu anaweza fanya kama kigezo ili afanye maamuzi ee, nanyi wadada humu ndani mnaipenda hiyo? Maoni please kabla sijashauri.
 
Kijana wewe sijapata umri wako ila wa demu wako tu.

Je watoto wa huyo demu walizaliwa ndani ya ndoa au kwa kujirusha tu?

Je baba watoto anawahudumia hao watoto au hata ndugu wa huyo baba watoto?

Lakini kwa ujumla inaonekana huyo demu kajikatia tamaa ya maisha ya mapenzi kiasi cha kuwa yes kwa kila jambo, hapo mimi inanishitua sana
 
Nadhani anafaa kuwa mke mzuri kama utakuwa naye karibu kwa kila aina ya maelekezo LAKINI SUALA LA KUKUBALI KILA KITU NINA MASHAKA NALO amevunjika sana moyo na hiyo inaweza kusababisha akawa mtumwa zaidi ya mpenzi ili asikupoteze kitu ambacho siyo na pia ninadhani kama wewe ni mbinafsi zaidi haujatafuta muda wa kumjua kuwa anapenda nini na kuchukia nini na umepoteza mwelekeo kabisa kuanza kutamani A na B hii siyo sifa nzuri
 
pole sana,inaonekana huyu dada ana hamu sana ya kuolewa.eidha amehisi baada ya kuzaa asingeweza kuolewa na labda heshima yake ilipotea.hivyo anataka arudishe heshima yake aolewe. anakupenda na yuko radhi kwa lolote.na vipi kuhusu baba wa watoto??? chunguza mahusiano yao yapoje kwa sasa ndio ujue umuoe au la. ushauri mkapime kwanza afya zenu ndio muendelee na mpango mzima.
 
Afrodenzi nakushukuru sana kwa mchango wako na wadau wengine japo wengine mananiponda lakini mimi napokea tu ushauri na nitatafakari kwa kina. Mfano Afrodenzi amegusia suala la kupima Ngoma, ni kweli hilo mimi nilimjaribu kumuliza je atakuwa tayari kunipa mzigo hata kama hatujapima ngoma, yeye akasema hilo hamna shida so long as anajua mie ni mumewe mtarajiwa ataanipa tu na chochote kile yupo tayari kufanya ili mradi tu ahakikishe hanikosi katika maisha yake. sasa hapo nikaanza kuwa na mashaka makubwa, yupo tayari hata bila kupima au hata bila kutumia kinga inakuaje, ni upendo wa kawaida kwa umpendaye or something else behind? I am still waiting for u're contributions wapendwa wana JF
Dogo unaokekana hujadhamiria kuoa ila unachokifanya unachezea hisia za binti, na kuhusu kupima chukua hatua ukapime hamna haja ya kumtega, ila inaonekana nimkosefu wa maadili kwanini uombe kumla pande zote yaani mkeo mtarajiwa ndiyo wakumueleza yote hayo hufai hatakuwa baba wa familia kabisa bahati yako binti amepitia mapito mengi na amekuwa na infiriority complex ndo maana maamuzi yake yamelenga kumpata mume tu haijalishi ni asiye na maadili kama wewe au la. Ninachokuomba kama kweli dhamira imekutuma umuoe vinginevyo wewe ni mtu wa kuogopwa kupita maelezo.
 
Back
Top Bottom