HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,566
Najaribu kufikiria, kuna akina mama wangapi wanaoweza kumkubali mtoto wa mwanamke mwingine kama alivyo? Ni wachache kupindukia. Wengi juhudi yao siku zote ni kuona watoto wa kambo wanakorofishana na baba zao, wanateswa na kutupwa nje ya familia. Lakini ni kwa faida ya nani? Siku zote ni kwa hasara zao. Huja kugundua wamepata hasara wakiwa wamechelewa uzeeni. Ninampenda na nitampenda kuliko mtu mwingine yeyote, mama yangu ambaye amenionesha maana ya kweli kuhusu maisha. Amenifundisha kwamba, suala siyo mama wa kambo, bali ubinadamu, kujua kupenda.
Alikuwa ni mama………………
Simuliza yako imenigusa sana, na nafikiri imemgusa kila mwenye nia njema na jamii iliyomzunguka. Daaa, natamani kama wenye familia wote hususan akina mama wangekuwa na mioyo kama ya huyu mama!
Ushauri wangu, kwa kila aliyesoma uzi huu, nafikiri bado tuna muda na nafasi ya kutosha kufanya mabadiliko ndani ya familia na jamii iliyotuzunguka. Kuna wale mnaoishi na yatima na watoto wa ndg zenu, Mungu awatie nguvu muwapende kama watoto wenu kabisa wa kuwazaa. Kuna wale ambao mnauwezo kimaisha, na mna ndg wasio na uwezo. Hawa wanaweza kuchukua hii kama changamoto kuwasaidia hao wasio na uwezo. Pia wapo wenye uwezo na wasio na ndg, nafikiri hawa nao wanaweza kutusaidia kwa ishu ya watoto wa mitaani ... Kwa wale wenye uwezo wa kutosha, tafadhali na tujitahidi kuzisaidia familia pamoja na jamii iliyotuzunguka wakiwemo watoto wa mitaani.
Natamani tuwe na mioyo ya huruma na upendo kufikia level hii ...
Mungu na atubariki, Mungu na utukirimie roho za huruma na upendo, Mungu na atuondolee roho za choyo, wivu na manyanyaso na ubinafsi.
Amina.