Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Zakumi,
Mkuu hata sikuelewi kabisa.. unaposema makabila yetu hayakupitia feudalism una maana gani?. Kwani hao kina Mkwawa, Mirambo, Mengi Sina na wengine wote walitawala vipi sehemu zao..Ni step zipi ambazo zilirukwa ikiwa tuliweza kuunganisha tawala hizi na kuunda chama cha TAA chini ya mwenyekiti ambaye hakuwa mtawala wa makabila..ebu nifahamishe vizuri.
Na kuhusu Botswana hakuna aliyesema ukubwa wa pua ni wingi wa makamasi ila nimesema makamasi mengi toka pua ndogo..huwezi kujikamua jipua lako kubwa ukafikiri ni sifa wakati huna makamasi..Wewe ndiye unataka kulinganisha pua hizi kupata wingi wa makamasi..Utafananishaje Tanzania na Botswana nchi yenye maendeleo eneo lisilozidi mkoa mmoja wa Tanzania..Barabara ya Pugu road peke yake ni highway ya Botswana mwanzo hadi mwisho..Kama uliwahi kuona ile sinema ya Gods must be crazy, basi hiyo ndio hali halisi ya mazingira na makazi ya watu huko vijijini (3/4 ya nchi hiyo).
Mkuu wangu tunajipima maendeleo yetu kutokana na uwezo wetu, waswahili wanasema cha mtu mavi..Usitegemee yaliyoko Botswana au Dubai yanawezekana au yaigwe yataboresha maisha ya WaTanzania..wala Kuiga kunywa kwa Tembo kwa sababu tu Unayaona maendeleo toka Marekani basi nasi tunaweza kuwa kama wao... tutapasuka msamba..
Mkuu hawa jamaa wametoka mbali sana na nikufahamishe tu kwamba Ujamaa ulianzwa hatra nchi hizo.. Marekani, Ufaransa na hata Uingereza walipitia Ujamaa kufika hapa walipo na hadi leo hii wana vitu kibao viko chini ya serikali wanaviuza (privatise) taratibu kulingana na wakati..Sio sisi tuliokuja uvamia Ubepari kwa sababu tu IMF imezungumza wakati tukijua fika walitaka kuingia na Ukoloni mamboleo tukashindwa hata kuweka guard zetu sawa.
Ndio maana hapa tutakaa tunabishana mpaka asubuhi. Unakataa kulinganisha Botswana na Tanzania. Lakini yakija masuala ya ujamaa mpo tayari kulinganisha Tanzania na Marekani, Ufaransa au Uingereza. Huo kwamba hapa unaBugi step.
Kuhusu feudalism, Mirambo, Mkwawa na ... walikuwa ni slave traders. Sijuhi kama hii itakusaidia kutofautisha kati ya feudalism na slave trade.
Ukoloni mamboleo ni myth iliyotungwa na viongozi kama Nyerere walioshindwa kuleta maendeleo katika nchi zao. Viongozi hawa na wananchi wao walikuwa na matumaini makubwa ya kupata maendeleo baada ya kupata uhuru.
Lakini waliposhindwa kuleta maendeleo, wakaanza kumtafuta mystical mchawi (mkoloni mamboleo)>