"Dola lazima isimamie sheria ili kulinda haki na kuhifadhi amani. Wajibu huu usipozingatiwa, wataibuka manabii wenye kuihubiri haki kwa kuwahukumu wengine. Hamtabaki salama mkifikia hapo"
J.K. Nyerere
Mbona jamaa wanaenda mbali na off point wakati issue ni staright forward?
Nadhani madhumuni yalikuwa kulinganisha utabiri huo wa Mwalimu na hali ilivyo sasa. Hebu sasa angalieni issue ya Mengi na Rostam. Wote hawa wamekuwa manabii wenye kuhubiri haki kwa kuwahukumu wengine. Sababu yake? Dola haikusimamia sheria ili kulinda haki na kuhifadhi amani i.e. kama wote, mafisadi papa na mafisadi nyangumi wangechukuliwa hatua za kisheria, hali hii isingejitokeza.
Hali hii ikiendelea na wakiibuka manabii wengi zaidi, hatutabaki salama. Watu watachapana mitaani.