Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,459
- 29,153
- Thread starter
- #21
inaniuma saana. siku ya shindano la mfalme wa rhymes sugu ndo aliyekuwa anampa saport hadi kumbeba mabegani. angalia video ya DARUBINI KALI utamuona SUGU akimbeba AFANDE SELE. Lakini leo anamgeuka. Kweli sanaa ya bongo yataka moyo. Mwenye access atubandikie hapa video ya DARUBINI KALI watu waone. SUGU alikuwa anamtetea hadi anataka kulia.mia
Ukiacha kagari kamoja alikokapata Afande kama zawadi kwenye Ushindi wake wa kumchakachua Msafiri (Solo Thang) , maisha yake ndio yaleyale tu ya kubangaiza waliyonayo wanamuziki wengine baada ya kudhulumiwa sana na hawa Clouds.
Tuongee tu ukweli, kwa uwepo wa hawa mapromoter wa Couds, mwanamuziki gani anaeweza kujivunia kua uzuri wa maisha yake umechangiwa na hawa matapeli?
Sio Prof. Jay wala Juma Nature.
Kwa mbaali anaweza kua Lady Jay Dee sababu ya kutembea na Ruge + Vipromo vya hapa na pale from Gadner.