JAVA expert, ready to help!

Ukiwa kama mimi haitakusaidia, kwa sababu mimi mwenyewe nahitaji kujifunza zaidi na zaidi. Ukijua java ina class 230, na method 600 itakusaidia nini? sidhani kama kuna programer yeyote ambaye anajua packages na classes zote za java ziko ngapi. Ila unajifunza pale unapotaka kufanya kitu flani. Kwa mfano ukitaka ku add session kwenye application yako, unatafuta ni namna gani, then unakuta class ambayo inakusaidia kufanya hivyo. Katika forum kama hizi si rahisi kujifunza kutoka zero to somewhere. you need first to understand the basic concepts, the unauliza nataka kufanya kitu fulani nifanyaje? ndo unaelekezwa. unaona mimi nilikuwa nataka kuweka reporting tools kwenye ki application changu nimesaidiwa link....nikishindwa kuzitumia nasema nimefanya hivi na hivi then lakini sijafanikiwa ni wapi nimekosea?

Mwalimu wangu wa kwanza wa programming alikuwa anaitwa Funajivu UDM (siyo spelling sahihi), yeye siku zote alikuwa anasisitiza ukija kwangu usiniambie hujui kitu, ila sema unachojua na umeshindwa kufanya nini! The same phisophy applies here. Tafuta vitabu na links usome at least basic syntax. Wengine tunategemea kutumia hii tread very seriously kujifunza so tafadhali msifanye jokes. Dubo please anza darasa bwana... i realy need to learn tricks and how to's from experts. Dont start with the basic please there are alot of materials which teachs basic java programming on the net. Nilikuwa najaribu ku appload kitabu cha teach yourself java for 21 days lakini kime fail ku appload. Anayetaka anipe address yake nitamtumia kwenye CD. Kina all the basics that a begginer needs......
Nashukuru kwa mawazo yako,nadhani hili ni darasa huru mtu yoyote yule anaruhusiwa kushiriki,sasa ndugu yangu mbona unaonesha fikra mgando za kuninyanyapaa au kwakua nimekua muwazi kuwa sijui?? Mwalimu mwenyewe aliyeanzisha thread hii hajalionesha hilo iweje wewe mwanafunzi mwenzangu? Kwani mtu akisema hajui hapo anakua anatania kweli? Au mie ndio sikuelewa pale uliposema ''msifanye jokes'' au kwakua wewe unajua so asiyejua kwako hana maana mhn?? Je Daba asemeje sasa?? Nadhani wakati mwingine kauli zako zinaweza zikamkatisha mtu tamaa badala ya kumpatia changamoto na sidhani kama hilo ndio lengo la JF!! Asante kwa maoni yako,ubarikiwe sana!!!
 
i realy need to learn tricks and how to's from experts. Dont start with the basic please there are alot of materials which teachs basic java programming on the net. Nilikuwa najaribu ku appload kitabu cha teach yourself java for 21 days lakini kime fail ku appload. Anayetaka anipe address yake nitamtumia kwenye CD. Kina all the basics that a begginer needs......

Mkuu mbona maelozo yako yanajichanganya kimtindo usimyanyanyape hata kama anataka kuanza basic. kwanza wewe ndo ulikosea kumpa jibu la spoon feeding ambalo halimsaidii sana. alafu baada ya muda unamgeuka tena.

Ndio maana mimi mwazo nilimpa jibu ambalo nadhani alielewa lengo hasa la jibu lile ni kwa mufaa yake . wewe mwazo ulimpa jibu la 1+1= 2. Sasa akiuliza 2+2 unashtuka.... teh teh teh

Njia sahii ilikuwa sio kuweka jibu kama ulivyofanya wewe ulitakiwa kuambabia kasome hesabu za kujumlisha. Then akija na jibu anauliza je jibu hili 1+1=3 ni sahihi? ndo unamuelewesha.

Waache hata beginner waulize maswali yao but cha msingi waonyeshe wamefanya nini?
Ukweli ni kuwa there is a lot of material wich teach everything on the internet. but bado tunawahitaji kina dubos.
 
Beginner courses and materials in various programming languages are available at Programming and Web Development Help | DreamInCode.net Dubo, endelea na shule hii as planned, maswali yatatokana na kile utakachokuwa unafundisha na maelezo zaidi on techniques will be appropriate to the task at hand na hapo watu wataweza kujifunza. Suggestions on clean thread for the lessons, preferably of a sub-topic ni vyema iandaliwe.
 
Mimi nina background ya uwalimu, kwahiyo sitovumilia kuona watu wanadharauliana na kutoa lugha chafu na kali. Naomba tutiane moyo pale tunapokuwa tumekwama ili tuweze kuwa wazuri kwenye Java. Mimi sio kusema ni mzuri sana, kinachonisaidia ninajua resources nyingi sana za java na wakati gani wa kuzitumia.
 
thank you for your advice,seriously am new in java programming kabisaa,its true nasoma na hiyo ni assignment ya kwanza baada ya mwalimu kupiga lecture 2,ambazo hajafundisha vitu hizo!! Atleast ungetoa idea ya wapi nitapata materials ya kujifunza JAVA nikaelewa zaidi badala ya kutoa maelezo ambayo hayasaidii kunipa jibu la kile nikitakacho! Haya mwishoe ukaniuliza swali la ajabu,haya natumia NetBeans IDE version 6.9.1. Nashukuru kwa ushauri wako,nitaufanyia kazi,Ubarikiwe sana!!
Unapokuwa unajifunza java kwa mara ya kwanza haishauriwi kutumia IDE, inashauriwa utumie command line prompt ku-compile na ku-run program zako. Tumia command kama javac, java na jar.

Ni PM nikutumie softe copyya kitabu cha Java 6 kitakusaidia, siwezi kukiweka hapa hadharani wenye nacho wanaweza kuishitaki JF.
Tumia kitabu cha C kujifunza Java kama lengo lako ni kujua basic things kama loop, switch statements, selection, control etc. Java ni pure Object Oriented Programming language na C ni Conventional Programming Language. Kuna dhana(concepts) tofauti kwenye hizo lugha kwahiyo kwa beginner si busara kutumia kitabu cha lugha moja kujifunzia nyingine. Kama wewe ni beginner wa Java tu, ila unaijua C unaweza kukitumia kitabu cha C kitakusaidia kama 10% hivi.
 
Darasa linaanza jmosi hii.

Kwa kuanza itabidi tupakue/tushushe/download zana zifuatazo:
1. JDK 1.6_x http://www.oracle.com/technetwork/java/javase/downloads/index.html
2. StarUML 5 http://staruml.sourceforge.net/en/download.php
3. Glassfish 3.1 na kuendelea http://glassfish.java.net/ au JBoss 4.2 na kuendelea http://www.jboss.org/jbossas/downloads/
4. Netbeans 6.9.x http://netbeans.org/ au Eclipse 3.4 http://www.eclipse.org/downloads/

Kwa wale watakaopakua Netbeans, hakikisha unapakua full bundle na wakati wa ku-install netbeans tafadhari don't install Glassfish. Glassfish inatakiwa ku-install peke yake bila kutumia netbeans installer.
 
Ukiwa kama mimi haitakusaidia, kwa sababu mimi mwenyewe nahitaji kujifunza zaidi na zaidi. Ukijua java ina class 230, na method 600 itakusaidia nini? sidhani kama kuna programer yeyote ambaye anajua packages na classes zote za java ziko ngapi. Ila unajifunza pale unapotaka kufanya kitu flani. Kwa mfano ukitaka ku add session kwenye application yako, unatafuta ni namna gani, then unakuta class ambayo inakusaidia kufanya hivyo. Katika forum kama hizi si rahisi kujifunza kutoka zero to somewhere. you need first to understand the basic concepts, the unauliza nataka kufanya kitu fulani nifanyaje? ndo unaelekezwa. unaona mimi nilikuwa nataka kuweka reporting tools kwenye ki application changu nimesaidiwa link....nikishindwa kuzitumia nasema nimefanya hivi na hivi then lakini sijafanikiwa ni wapi nimekosea?

Mwalimu wangu wa kwanza wa programming alikuwa anaitwa Funajivu UDM (siyo spelling sahihi), yeye siku zote alikuwa anasisitiza ukija kwangu usiniambie hujui kitu, ila sema unachojua na umeshindwa kufanya nini! The same phisophy applies here. Tafuta vitabu na links usome at least basic syntax. Wengine tunategemea kutumia hii tread very seriously kujifunza so tafadhali msifanye jokes. Dubo please anza darasa bwana... i realy need to learn tricks and how to's from experts. Dont start with the basic please there are alot of materials which teachs basic java programming on the net. Nilikuwa najaribu ku appload kitabu cha teach yourself java for 21 days lakini kime fail ku appload. Anayetaka anipe address yake nitamtumia kwenye CD. Kina all the basics that a begginer needs......

Kama umefundishwa na "Funa" utakuwa na msingi mzuri sana wa code, "Funa" ndio mwalimu wangu wa kwanza wa Programming alinifundisha Pascal programming language. Please kama umenifahamu potezea tu don't expose my identity.
 
Funa mbona katufundisha wengi tu, Wote waliopita UDSM 1999-2003 wamefundishwa na Funa, so siyo rahisi kukufahamu mkuu. Ni kweli alitupa msingi mzuri wa programming.
 
Adding a calendar picker on a JSP page.

I have three combo boxes named Date,Month,Year on a JSP form. A user can scrow down and select the date, month and year. Now I wish to complicate it a bit to have a calendar image in front of the Year combo box that when a user clicks on it, can fill these valuest graphically by selecting the year,month and date. That is all for today. Good day
 
Hiyo tumia java script, check na google.
 
Utangulizi:
Tunatakiwa kusanifu na kuunda mfumo wa kifedha wa kompyuta (Financial System). Mfumo wetu utakuwa na uwezo wa kutoa huduma za kibenki na za mikopo kwa kutumia credit card. Huduma za kibenki wengi wetu tunazifahamu ila kwa kuwa huduma ya credit card ni ngeni Tz, ninachukua nafasi hii kuielezea kwa kifupi:

Mteja wa kampuni ya credit card ufungua akaunti kama unavyofungua akaunti ya benki. Akaunti hiyo inakuruhusu kutumia na kutoa pesa ambazo haujaziweka kwenye akaunti na utatakiwa kuzilipa mwisho wa mwezi. Kila akaunti huwa na kikomo cha matumizi (credit limit) mfano Tsh. 2,000,000. Kila unapo fanya muhamala (transaction) mfano kununua bidhaa kwa kutumia credit card au kutoa pesa kwenye ATM kampuni husika utoza tozo (Charge) la matumizi. Ukinunua bidhaa tozo linaweza kuwa mfano 3.5% ya pesa uliyotumia na ukitoa pesa kwenye ATM tozo ilinaweza kuwa mfano 10% ya pesa ulizotoa. Ikifika mwisho wa mwezi kampuni ya credit itakutumia bill yako na itabidi ulipe stahili (total due) isiyopungua kiwango cha chini cha malipo (minimum payment). Mfano umetumia Tsh. 1,000,000 na kiwango cha malipo cha chini ni 10% ya matumizi, itabidi ulipe stahili isiyopungua Tsh. 100,000 na isiyozidii Tsh. 1,000,000. Kampuni hizi uongeza faida(riba) kwenye kiasi unachodaiwa kila mwezi, mfano ulitumia Tsh. 1,000,000 na ukalipa (payment) 200,000 ukabaki na deni la Tsh. 800,000, katika hili deni kampuni ya credit itaongeza riba mfano riba ni 20% deni lako jipya (salio jipya) litakuwa ni Tsh. 960,000.

Mahitaji:

Sanifu mchoro class (Class diagram) wa mfumo wa kifedha wa kompyuta (Financial System).

Zifuatazo hapo chini ni "use cases" zinazohusu sehemu ya kibenki ya mfumo tunaotegemea kuunda.

  • Unda/umba akaunti binafsi
  • Unda/umba akaunti ya kampuni (akiba au cheki)
  • Weka pesa
  • Toa pesa
  • Ongeza faida
  • Fanyiza (generate) ripoti za akaunti

Yanayofanyika kwa kila kitendo ni kama ifuatavyo

  • Mteja anaweza kuwa na zaidi ya akaunti moja, Mfumo wa kibenki uhitajika kutunza kumbukumbu zote za kuweka na kutoa pesa kwenye akaunti.
  • Pale pesa inapowekwa au kutolewa kwenye akaunti ya kampuni, mfumo wa kibenki utama barua pepe kuhusiana na muhamala uliyofanyika.
  • Pale pesa inapowekwa au kutolewa kwenye akaunti binafsi na pesa hizo zikiwa ni zaidi ya Tsh. 400,000 au salio likiwa hasi baada ya kufanya muhamala, benki utuma barua pepe ikihusu muhamala husika kwa mwenye akaunti.
  • Pale kitufe cha Ongeza faida kinapo bonyezwa, mfumo wa kibenki uongeza faida kwenye akaunti zote.

Huu mfumo wa kifedha wa kompyuta unatumika pia kwenye Benki/kampuni zinazotoa huduma ya "credit card".
Kwenye "credit card" tuna "use cases" zifuatazo.

  • Unda/Umba akaunti ya kadi ya mkopo (credit card)
  • Toza akaunti
  • Weka pesa/Fanya malipo
  • Ongeza faida
  • Fanyiza ripoti za bill za kila mwezi

Mfumo wa kifedha wa kompyuta utakao tengenezwa utakimu (support) kadi za aina tatu

__________________________________________Dhahabu _ Fedha ___Shaba
Riba kwa mwezi (RM)
__________________________12% ______16% ____ 18%
Kiwango cha chini cha malipo kwa mwezi(MM)
_______14% ______16% ____ 20%

Yanayofanyika kwa kila tendo ni:

  • Kadi inapo tozwa zaidi ya Tsh. 600,000, Benki / kampuni ya credit kadi hutuma barua pepe kuhusu muhamala kwa mwenye kadi.
  • Mteja anweza kuwa na zaidi ya credit kadi moja (akaunti), kila credit kadi husiana na akaunti.
  • Mfumo wa kibenki unatakiwa kutunza kumbukumbu ya malipo na tozo zote. Kwa kila malipo au tozo, mfumo unatakiwa kuhifadhi tarehe, jina na kiasi cha pesa cha muhamala.
  • Ankra(bill) ya kila mwezi, inayofanyizwa kwa kubofya kitufe cha ripoti ya mwezi inatakiwa kuonesha

  • Salio la nyuma/ lilotangulia (previous balance): Salio la mwezi uliopita
  • Jumla ya tozo (Total charges): Jumla ya tozo zote za mwezi huu.
  • Jumla muamana (total credits): Jumla ya malipo yote yalifanywa mwezi huu.
  • Salio jipya (new balance) = salio la nyuma – jumla ya muamana+ Jumla ya tozo+RM*( salio la nyuma – jumla ya muamana)
  • Jumla ya stahili (Total due) = MM*salio jipya
Mchoro class (Class diagram) unatakiwa kuonesha class zote, mahusiano (relationships) n.k.
Vile vile itabidi kuchora mchoro mfuatano (sequence diagram) kwa kila "use case" hapo juu.

TAFADHARI UNAPOJIBU USIKARIRI HUU UJUMBE.
Please don't quote this message in your reply.
 
Mwanzo mzuri,
What about maximum daily withdrawals? sijaona ikitajwa hapo juu. Hata kama una multiple accounts, ni vyema hii iwe implemented kuwa, kama total credit unayoruhusiwa ni 2,000,000 basi, max per day ni 500,000 across all cards (mfano (shaba account holders)
Pia kuna offers ambazo credit card companies hutumia kuwavutia wateja mfano, 6Months 0% credit. Au hizi features za baadae?
 
Mbona watu hamtoi maoni kuhusiana na project yetu. Mpaka sasa ni mtu mmoja tu aliyechangia
 
Mwanzo mzuri,
What about maximum daily withdrawals? sijaona ikitajwa hapo juu. Hata kama una multiple accounts, ni vyema hii iwe implemented kuwa, kama total credit unayoruhusiwa ni 2,000,000 basi, max per day ni 500,000 across all cards (mfano (shaba account holders)
Pia kuna offers ambazo credit card companies hutumia kuwavutia wateja mfano, 6Months 0% credit. Au hizi features za baadae?

Nimekupa hizo pointi mbili itabidi tuziongeze kwenye FRD (Functional Requirements definition) yetu.
 
......................................
Game unalotaka wewe la wachezaji wawili kwenye computer tofauti ni dhana ya distributing system. Unabidi utumie Java RMI/socket.............................

Hii darasa lako zuri lakini nashindwa kuhudhuria sababu tayari nina viproject viwili nimejipa vya kujifunza.

Having said that unaweza kunisaidi kunipa refence nzuri ya kusoma na kuelewa mambo ya RMI ili game iliyo kwenye applet iwezeshe watu wawili wa sehemu tofauti wacheze.
 
Tengeneza web application, deploy hiyo application yako kwenye tomcat au Java application server yoyote.
 
ahsante sana mkuu kwa kupost hii mambo,i need some notes about object oriented programing as a whole na java stuff,let me know,,pamoja mkuu
 
Darasa linaendelea, nimeambatanisha class diagrams za system yetu.
Kwanzia ninatoa michoro mitatu
  1. Financial Institution Framework
  2. Swing Bank Application
  3. Swing Credit Card Application

Ukiangalia kwa makini hiyo michoro utaona ukuwa inatumia dhana ya MVC na GUI application. Sasa itabidi tubadilishe upande wa View ili iwe web application.
Nikipata muda nitachora mchoro mwingine ambao utaunganisha Credit card application na Bank application katika application moja.

Mtutu yoyote atakaye kuwa na swali kwenye huu usanifu hasisite kuuliza.

Taasisi Ya Fedha Framework

attachment.php

Benki Application
attachment.php

Bank Application Class Diagram.jpg (Click to enlarge)

Kadi ya Mkopo Application
attachment.php

Credit Card Application Class Diagram.jpg (Click to enlarge)
 
Attachments

  • Farmework Class Diagram.jpg
    Farmework Class Diagram.jpg
    168.5 KB · Views: 44
Back
Top Bottom