Jasusi la kitanzania lilivyowatoka wanajeshi Uganda

Hii story nimeisoma sana kwenye gazeti la Raia
Mwema. Ila kuna wadau wawaliokuwepo enzi hizo za vita wanadai 90% ni fix tu/ chumvi nyiiiingi. Kwani majasusi walihusika kwenye ile vita taarifa zao zinafamika.
Muulizeni mzee Hans Kitine aliyekuwa mshauri wa Ikulu na Mzee Gimonge aliyekuwa JWTZ
 
Hata mimi nakubaliana na wewe. Kwamba sehemu kubwa zaidi ya hii habari ni fiction kwa mtindo wa zile riwaya za Willy Gamba.
 
Kilichojiri nikiwa mafichoni Kampala – Kitabu cha Kachero 7
Habari Zinazoendana
……………
KWA wiki kadhaa sasa tumekuwa tukiendelea na mfululizo wa simulizi kuhusu kachero wa Tanzania, pamoja na wenzake wawili walivyotekwa na makachero wa aliyekuwa Rais wa Uganda, Idi Amin. Tuliona namna kachero wa Tanzania alivyotoroka na kupata msaada katika moja ya makanisa jijini Kampala, Uganda. Leo tunaendelea na sehemu nyingine ya simulizi za kachero huyo, Frowin Kageuka, ambaye ameandika kitabu kuwaenzi wenzake hao wawili. Endelea
…………………….
BAADA ya padre yule kunifunga dawa katika jeraha la risasi akafungua boksi moja lenye nguo akanipa shati, suruali, fulana, jaketi na viatu ambayo ingawa vyote hivyo vilikuwa ni mitumba lakini ‘zilinikaa’ sana. Akafungua boksi jingine akanipa viatu vya michezo na kofia aina ya “cap” ya rangi nyeusi.
Nilizivaa nguo hizo ambazo kwa kweli nilizipenda sana na padre alinithibitishia kwamba ‘zimenichukua’ sana. “Sasa twende ukale,” aliniambia huku akitabasamu. “Asante sana, lakini padre unaitwa nani?” “Oh! Jina langu ni padre Franz au wengine huita Francis.”
“Ah! Vizuri sana, kwa jina hilo bila shaka wewe ni mswiss au sivyo?” “Kweli kabisa, umejuaje? Aliuliza huku akinikazia macho.
“Familia yangu ni wacha Mungu wa kikatoliki na mimi mwenyewe nimesomea shule za kikatoliki kwa hiyo majina ya mapadre wa kizungu siyo mageni kwangu.”
“Ohoo!” alijibu huku tukiingia sehemu ya chakula. Tulikaa hapo kisha padre Franz akamwagiza mhudumu mmoja mwafrika aliyevaa sare nyeupe aniletee chakula kingi na maziwa.
Awali nilifikiri kwamba chakula hicho kitakuwa ugali au wali, kumbe nikaletewa vipande vya mikate iliyotiwa siagi, nyama nyingi ya kukaanga, supu ya mboga na maziwa moto glasi moja ya nusu lita. Kwa kweli mlo huo ulikuwa mzuri sana kuliko ningepewa ugali au wali niliouzoea.
Kabla ya kula aliniambia nisalie chakula hicho, nikajua ananitega ili athibitishe kama kweli mimi ni mkristo au nimemdanganya. Kwa vile nimelelewa katika ukatoliki sala za kikatoliki hazikunipiga chenga, nikasali sala ile ile ya kikatoliki ya kubariki chakula na kumfanya padre huyo afurahi sana. “Wewe kweli ni mkatoliki,” aliniambia huku akitabasamu.
“Kumbe ulifikiri nakudanganya?” nilimuuliza huku nikianza kula. “Sikuamini sana maneno yako, lakini sasa nimeanza kuamini. Hilo tuliache, lakini utarudi vipi nchini kwako kwa sababu nimesikia kuna vita mpakani?” “Vita! Mpakani wapi?” niling’aka kama vile sijasikia.
“Nimesikia majeshi ya Idi Amin yamevuka mpaka na kuiteka Kagera. Hata hivyo siyo mkoa wote wa Kagera, bali mji wa Kakunga, Masanya, Mutukula, Minziro na Murongo ndiyo nimesikia imetekwa. Raia wengi wameuawa na mali zao kuteketezwa,” alinieleza kwa huzuni.
“Umesikia kwenye redio?” niliuliza ghafla. “Redio nimesikia, na watu wamenieleza pia, sasa swali langu ni jinsi wewe utakavyofika huko, kwa sababu siwezi kukuweka hapa ni hatari.”
“Loh! Umenistua sana, lakini naomba kitu kimoja, unipe japo fedha ili ziweze kunifikisha Tanzania kwa kupitia Kenya.” “Fedha? Fedha itabidi usubiri kwa siku tatu au nne hivi kwa sababu hivi sasa hatuna fedha za kutosha hapa.”
“Sasa kwa muda wote huo nitakaa wapi?” niliuliza kwa hofu. “Mimi naweza kukuficha kwenye gereji ya magari, lakini utakuwa hutoki nje na kula mpaka usiku, unaweza?” “Naweza sana” nilijibu kwa furaha baada ya kuhisi mafanikio ya kurudi nyumbani yapo.
Niliishi kwenye chumba kimoja cha hapo gereji ambacho ni stoo kwa wiki nzima bila kugundulika hata na wafanyakazi wa gereji hiyo. Usiku padre Franz alikuwa akinifungulia mlango na kunipeleka kula na kuoga kisha saa mbili usiku nashiriki naye ibada ya rozari (tasbihi) chumbani mwake hadi saa sita usiku ambapo hunifungia tena katika chumba hicho cha gereji. Kwa kweli sikupata taabu sana humo chumbani kwa vile nililala kwenye godoro dogo la inchi tatu na upana wa futi mbili na kujisaidia haja kwenye ndoo.
Kadiri siku zilivyopita ndivyo padre Franz alivyonipenda na hasa kwa jinsi tulivyoshirikiana katika sala ya rozari. Baada ya kama wiki mbili hivi, usiku mmoja padre Franz alinipa habari ya kunishtua sana. Hatukusali siku hiyo kwa vile mazungumzo yetu yalichukua muda mrefu na kwa kweli yalimtia hofu padre huyo.
“Leo hatusali rozari Nelson.” Aliniambia kwa hofu kiasi cha kunifanya na mie niingiwe na wasiwasi. “Kumetokea nini padre?” nilimuuliza kwa shauku. “Maafisa wa usalama wa taifa wa Idi Amin walifika hapa kuuliza habari zako,” alinieleza kisha akanikazia macho. “Maafisa wa SRB?” enhee!”
Mimi niliwaambia kweli ulifika hapa lakini sikukubali kukupokea, kwa hiyo uliondoka zako, wakaridhika na majibu hayo wakaondoka. Lakini nahisi wanaweza kurudi tena hapa kwa hiyo ni lazima kesho asubuhi uondoke. Nitakupa nguo, pesa, dawa na chakula cha makopo kwa cha siku mbili kisha uondoke zako.
Hata hivyo nimesikia kwenye redio kuwa majeshi ya Tanzania yamewatimua askari wa Idi Amin pale Bukoba na sasa wamevuka mpaka wamo ndani ya Uganda. Umenielewa?
“Nimekuelewa sana, kama hali ndiyo hiyo naomba hivyo vitu utakavyonipa nipe pamoja na silaha yoyote ambayo utaona inaweza kunisaidia kujilinda.”
“Hebu subiri kidogo,” aliniambia kisha akatoka. Dakika kama ishiriki hivi alirudi akiwa na begi dogo. “Humu mna jaketi, suruali mbili, shati mbili, kandambili, fulana, makopo sita ya nyama, makopo mawili ya samaki, siagi na mikate na mswaki, silaha niliyokuwekea ya kukusaidia wakati wa shida au matatizo ni biblia, sawa?”
“Sawa padre nashukuru,” nilijibu huku nikitabasamu. “Shika na hizi shilingi laki tatu na dola mia tatu zikusaidie.” Hizi shilingi laki tatu ni sawa na shilingi thelathini elfu kule kwenu Tanzania. Sasa piga magoti nikuombee ili ukalale, kisha kesho asubuhi na mapema uondoke zako. Umenielewa?”
“Nimekuelewa padre lakini naomba labda unitajie mtu au watu unaofikiri wanapinga utawala wa Idi Amin ili kama nikishindwa kuondoka nikimbilie kwao,” nilimwambia huku nikipiga magoti.
Akaniombea dua njema kwa dakika kama tatu hivi kisha akanibariki. “Ukianza kutafuta wapinzani wa Idi Amin utakuwa unajitafutia balaa. Hata hivyo mimi siwajui kwa sababu hata kama wapo hiyo itakuwa siri yao mioyoni mwao. Wengi waliojitokeza kufanya upinzani wa waziwazi wameishia kufia mikononi mwa maofisa wa SRB,” alinieleza huku akinishika kichwa.
“Haya asante padre, kwa heri, nikifika nyumbani Tanzania nitakuandikia barua kwa hiyo naomba anuani yako ya Posta na namba ya simu.” Aliniandikia anuani yake na namba za simu baadaye alinisindikiza chumbani kwangu na kunifungulia.
“Kesho asubuhi kufuli hii ukitoka utaifunga mlangoni,” aliniambia na kuondoka zake.
Kwa kweli usiku huo sikulala, mawazo ya vita yalinijaa, nikaona siwezi kukimbilia kurudi Tanzania kupitia Kenya na mimi ni askari, tena kachero. “Ni lazima nifanye kazi yangu, kazi ya ukachero. Lakini nani atanisaidia na fedha zangu ni kidogo? Itabidi nitafute kazi ili nipate fedha za kuniwezesha kuishi hapa Kampala. Lazima niwapate wapinzani wa Idi Amin ili wanipe habari za Jeshi la Idi Amin na vile vile nitafute mawasiliano ya kuniwezesha kuwasiliana na makao makuu ya Jeshi nyumbani. Loh! Nina kazi kubwa lakini lazima niifanye, kwanza labda ningelazimika kuifanya tangu pale mpakani mkoani Kagera. Nikifa basi, nitakuwa nimekufa nikiwa kazini lakini ole wangu nani atajua kwamba nipo hai? Hapana, lazima nirudi nyumbani nikaonane na familia yangu,” niliwaza mpaka karibu
 
Tunaanzia hapa

WIKI iliyopita tulianza kuchapisha sehemu ya kwanza ya uchambuzi wa kitabu kipya “Mateka Mpakani” kilichoandikwa na kachero wa Tanzania, Frowin Kagauka, kumuenzi mwenzake aliyeuawa mpakani mwa Tanzania na Uganda. Leo tunaendelea na sehemu ya pili.
…………………….
“AMESEMAJE wakati mlipomuuliza juu ya bastola hiyo? Amekubali ni yake lakini amekataa katakata kuwa yeye ni askari wa Idi Amin,” alinijibu Sajin Mkuu wa Kituo.
“OK. Sajin Binda wajulishe Bukoba ili waje kumhoji.” Niliamuru haraka. Sajini Binda alinipigia saluti nami nikaijibu kwa kubana mikono kwa vile sikuvaa sare za kijeshi na baadaye akaondoka haraka.
“Msimtoe humu mahabusu mpaka wakubwa zangu wafike kutoka Bukoba, sawa?” niliagiza. “Sawa afande,” alijibu Sajini ambaye ndiye mkuu wa kituo hicho kidogo cha polisi hapo kijijini Murongo.
Niliondoka hapo kituoni na ilipofika saa sita na nusu mchana nikijua wakubwa zangu watakuwa wanakaribia kufika hapo kituo cha polisi lakini hawakutokea mpaka saa nane na dakika kumi. Walifika kwa gari aina ya Landrover na wote walivalia sare za kijeshi isipokuwa dereva na mtu mwingine mmoja ndiyo walivaa kiraia.
Hao watatu waliovaa kijeshi mmoja alikuwa luteni na wawili makapteni. Waliovaa kiraia niliambiwa ni Luteni Emir wa Idara ya Usalama wa Jeshi ambaye ndiye aliyeendesha gari hiyo na Meja Stephen kutoka Idara ya Usalama wa Taifa mkoani Kagera. Wakuu hao waliamuru Kafumba atolewe mahabusu na alipotolewa wakamchukua na bastola yake kwenda naye Bukoba.
Sikumuona rafiki yangu Kafumba kwa zaidi ya wiki mbili ndipo siku moja bila ya kutarajia nikakutana naye sokoni hapo Murongo akizungumza na yule mpenzi wake.
“Ah! Rafiki wewe ni mbaya, umenipeleka polisi ili nifungwe bila kosa,” alilalamika. “Siyo hivyo, mimi nilishangaa kuona rafiki tangu una bastola na wewe ni bwana shamba. Naogopa sana askari ndiyo niliipeleka bastola yako polisi. Sasa wamekwambiaje?”
“Walinipeleka Bukoba nikaingizwa kwenye nyumba moja sijui ya nani, nikaulizwa maswali mengi ya Uganda na watu wawili ambao hawakuvaa kiaskari. Lakini watu wale walikuwa wema sana hawakunipiga wala kunisumbua na waliporidhika waliniachia nirudi lakini bastola yangu wamebaki nayo,” alinieleza huku akinikazia macho.
“Sawa bwana, basi tutaonana siku nyingine au leo kama bado upo hapa kwetu” nilimjibu kwa unyonge baada ya kuhisi yeye ni jasusi wa Idi Amin na ameweza kuwahadaa wakubwa zangu hadi wakaridhika kumuachia.
Wiki moja baadaye nikaletewa mwaliko kutoka kwa mzee niliyekuwa namheshimu sana, mzee Idris wa Green Hotel nikahudhurie sherehe yake aliyopanga ifanyike Jumamosi kuanzia saa tano asubuhi hapo hapo Green Hotel. Nikamjulisha Koplo Sudi na Sajin Binda juu ya mwaliko huo, kwa hiyo tukaondoka Murongo hadi Kivukoni. Tulipofika Kivukoni kama kawaida tukapanda boti na kuvuka mto Kagera ambao maji yake yanakwenda kasi sana kiasi cha kuwafanya wenyeji kushindwa kuvuka kwa kuogolea.
Baada ya boti kutuvusha tukatembea kwa miguu kilomita mbili na nusu hivi tukafika kijiji cha Kikagati ambacho kwa kweli ni kizuri kidogo kuliko kijiji chetu cha Murongo. Hapo Kikagati kuna kituo kidogo cha polisi ambacho kimejengewa badi tupu chini hadi juu, wengine huita mtindo huo ‘full suit’, vile vile kuna nyumba ya mkuu wa wilaya ambaye wenyewe walimwita DC na jengo moja kubwa la kampuni ya uchimbaji madini inayoitwa BMC.
Ilipotimia saa tano na dakika tano tulikwenda hapo Green Hotel huku tukiwa tumejaa shauku ya kunywa bia na kuvunja mifupa ya nyama ya kuku na mbuzi ya kuchoma. Kwa mshangao hapo Green Hotel hatukuona dalili yoyote ya sherehe na wala hakukuwa an watu wanaokula au kunywa kama ilivyokuwa kawaida. Kkilichonishangaza zaidi ni kutowaona hata watoto wake wakicheza nje ya hoteli hiyo ambayo mwenyewe mzee Idris anaishi humo humo kwenye vyumba vya uwani.
Kabla hajaamua kuuliza alifika mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa kati ya miaka sita na nane ambaye alituambia ameagizwa na mzee Idris atukaribishe ndani tumsubiri. Bila ya hofu tuliongozana na kijana huyo hadi kwenye sebule yam zee Idris ambayo kwa kweli hata siku moja hakuwahi kunikaribisha. Mtoto huyo alitutolea bia tatu za baridi kutoka kwenye hokofu, akatuwekea glasi kisha akaondoka. Dakika kama tano baadaye mzee Idris alifika na kutusalimu lakini hakukaa alituambia ana shughuli itakayochukua kama robo saa hivi lakini alitupa uhuru wa kujichukulia vinywaji kwenye jokofu. Wakati tunaanza kunywa bia huku bado nikitafakari jinsi ya sherehe hiyo tuliyoitiwa ilivyo, ghafla tukasikia mlio wa gari kubwa likisimama nje ya nyumba hiyo, bila shaka wote tulielewa huo ulikuwa ni mlio wa gari la kijeshi maana tulitazamana kwa mshangao.
Kabla hatujahamaki nini kinafanyika tukasikia vishindo vya hatua nzito za viatu vya kijeshi vikiizunguka hoteli hiyo. Tulipotazamana tena bila ya kusema lolote mlango ulifunguliwa na askari sita waliovalia kivita wakiwa na bunduki aina ya AK47 kila mmoja, wakatuzunguka. Moyo ulinilipuka, mate yakanikauka kinywani, bia yote niliiona chungu na balaa tupu.
“Simama juu.” Aliamuru mmoja wa askari hao ambaye alikuwa na cheo cha Sajini. Wote tulisimama huku mikono yetu ikiwa juu kuomba amani. “Songa mbele haraka.” Aliamuru tena. Tulitoka nje ambako tulikuta askari wengine wanane waliovalia kivita wakiwa na bunduki mikononii wameizunguka hoteli hiyo. Raia wa kijiji hicho au niseme kimji hicho walisimama kwa mbali sana wakishuhudia tunavyokuwa MATEKA MPAKANI.
Tuliingizwa katika lori moja la kijeshi aina ya Liaz na safari ya kwenda tusikokujua ikaanza. Tulipofika njia panda ya kwenda Kabale ambayo ipo upande wa kushoto na Mbarara ambayo ipo upande wa kulia, lori hilo lilitimua vumbi kuelekea kushoto yaani Kabale.
Baada ya mwendo wa kama kilomita nne hivi kutoka hapo Kikagati tukaingia katika kambi ndogo ya jeshi inayoitwa Kabiyanda. Tuliteremshwa katika kambi hiyo ndogo na kuingizwa katika kijumba cha mabati matupu ambapo ndani hakukuwa na lolote mbali ya joto na hewa nzito kwa vile hakukuwa na dirisha bali vitundu vidogo vipatavyo sita tu.
“Tunakuwa mateka mpakani, sijui watatufanyaje. Nahisi hizi ni njama za Kafumba, Kafumba lazima ni jasusi, alikuwa anatupeleleza. Sijui Idi Amini ana nia gani na sisi au nchi yetu…niliwaeleza wenzangu huku nikitetemeka. “Ni dhahiri Kafumba amelipiza kisasi. Lakini nahisi mpango huu ulikuwa ni wa muda mrefu,” alijibu Koplo Sudi.
Saa tisa tulitolewa humo kwenye kijumba na kukalishwa chini kwenye uwanja niliohisi ni wa kufanyia kwata. Koplo Sudi na Sajini Binda walikuwa wananitazama mara kwa mara kama vile wananiulaumu kwa kuwaingiza katika janga hili, lakini sio kosa langu bali ni tamaa yetu ya kunywa bia na kumuheshimu mzee Idris.
“Nani mkubwa kati yenu?” aliuliza Luteni mmoja mweusi mwenye sura mbaya. Hakuna aliyejibu hivyo akaona tumemdharau kaamua kumwita koplo mmoja aliyekuwa amesimama kwa mbali akituangalia.
“Funsa adabu hawa” alimwamuru koplo huyo aliyevalia kivita kwa Kiswahili kibaya kisha akaondoka zake kwa hasira.
“Ah! Mnataka ‘kufunswa’ heshima, hebu simameni.” Tuliinuka kwa hofu huku tukimwangalia nini anachodhamiria kutufanyia. “Nyinyi ni askari?” “Hakuna askari hapa kati yetu” nilimjibu haraka kwa hasira. “Eh! Wewe ndiyo mkubwa enh!” “Mkubwa wa nini?” nilimjibu na kumfanya acheke kidogo.
“O.K nyinyi mnajua Kiswahili kingi sana, hebu chuchumaeni chini huku mkishika masikio yenu.” “Tuonyeshe mfano,” nilimwambia bila hofu.
“Eh! Nyinyi jeuri sana, hebu laleni chini kifudifudi niwachape kidogo fimbo,” alitamka huku akitabasamu. Wakati tunalala kifudifudi ghafla alikuja askari mmoja asiye na cheo na kumwambia mwenzake kwamba tunatakiwa tuingie ndani ya gari tupelekwe katika kambi ya Mbarara. Tuliingizwa ndani ya Landrover moja ya jeshi la Idi Amin huku tukilindwa na askari sita waliovalia kivita wakiwa na bunduki aian ya AK 47 mikononi. Landrover ikapigwa moto na safari ya Mbarara ikaanza. Ilibidi turudi tena mpakani Kikagati kisha tufuate barabara inayoelekea Mbarara ni kama kilomita 150. Tulipofika Mbarara giza lilikuwa limekwishaingia, dereva akasimamisha gari nje ya lango kuu la kambi kubwa ya jehsi ambayo baadaye niliitambua inaitwa Simba Battalion. Taa kubwa ya usalama ikawashwa na kuzimwa kama ilivyo kawaida katika kambi nyingi za jeshi kisha sauti kali ilitaka utambulisho.
“Tumeleta mateka kutoka Kabale” alijibu askari mmoja aliyekaa mbele. Taa iliwashwa tena na kuzimwa halafu mlango ukafunguliwa. Niliona sanamu mbili za samba zilizokuwa upande wa kulia na kushoto mwa lango hilo ambazo zilinifanya nielewe maana ya kambi hiyo kuitwa Simba. Gari iliingia na kuegeshwa nje ya jengo dogo ambalo hata mtu asiyekuwa askari angegundua ni mahabusu.
Tuliamriwa kuteremka na mlango wa mahabusu ukafunguliwa, tukaingizwa. Mahabusu hiyo ilikuwa karibu na lundo la kuni na kwa mbele kidogo kulikuwa na msikiti mdogo. Ndani ya mahabusu hiyo hakukuwa na taa kwa hiyo ilibidi tutulie kimya bila kuongea wala kutembea.
Ulikuwa usiku mgumu sana kwetu hasa kwa mimi kiongozi kwa vile wenzangu walionyesha wamekata tamaa kabisa. Kama kawaida ya usiku ni lazima uche hata kama unapata taabu au raha ni lazima asubuhi ifike. Asubuhi ilipofika tulitolewa nje na kupelekwa katika ukumbi mmoja mdogo ambapo tulikalishwa chini. Dakika kama kumi baadaye waliingia wanajeshi wanne, watatu wakiwa na cheo cha meja na mmoja alikuwa kanali. Kwa jinsi walivyoonekana, walikuja kutuhoji.
“O.K Watanzania, tunaanza na wewe, inuka ujibu maswali yetu.” Alitamka kanali huyo huku akimuonyesha kidole Koplo Sudi. Koplo Sudi aliinuka wima huku akigwaya. “Unacho kitambulisho chochote hapo ulipo?” aliuliza meja mmoja ambaye ni mrefu zaidi ya wenzake. “Sina kitambulisho.” “Sawa, vua shati na suruali yako,” aliamuru kanali huyo.
Koplo Sudi akavua suruali na shati lake na kuviweka mbele yake. “Wewe unafanya kazi gani pale Murongo?” aliuliza meja mwingine ambaye ndiye aliyekuwa akinukuu maelezo yetu.
“Nafanya biashara ya kuuza vitabu sokoni,” alijibu Koplo Sudi huku akigwaya.
Ukisema kweli utapona, lakini ukitudanganya ujue hutaiona tena Murongo,” alitamka kanali huyo kwa Kiswahili kizuri. “Kwani sisi tumewakosea nini? Kosa letu ni nini mpaka mnataka kutuhukumu?” “Hamjafanya kosa lolote, lakini tunataka majibu y kweli,” alisisitiza kanali huyo.
“Unajua sisi tunawaelewa nyinyi vizuri sana, na kuonya tena. Usiseme uongo” alifoka kanali. “Sisemi uongo,” alisisitiza Koplo Sudi. “Jina lako nani?” aliuliza kanali huyo mweusi tii. “Abdallah Salum,” alidanganya. “Hatuna jina la Abdallah katika orodha tuliyoletewa.” “Kama mnayo orodha ya majina yetu kwa nini mnaniuliza jina?”
“Nyinyi wote ni wanajeshi, hiyo tunajua kwa hakika, sasa wewe unajifanya mfanyabiashara. Nakwambia mara ya mwisho, sema ukweli wako vinginevyo huwezi kurudi kwenu. Hatupo hapa kufanya mchezo,” alifoka kanali huyo.
“Umeelewa sasa, yajibu maswali yetu kwa ukweli” aliongeza meja anayeandika.
“Jina lako nani na unafanya kazi gani pale Murongo?” aliuliza meja huyo. Swali hilo lilimfanya Koplo Sudi aanze kutoa mchozi ambao uliniumiza sana moyo.
“Unalia kabla hujateswa, sasa ukiteswa si utakufa kabisa” alitamba meja. Maneno hayo hayakupunguza kasi ya machozi ya Koplo Sudi, kwa hiyo kanali akamwambia arudi aka echini.
“Zamu yako wewe, inuka kuja hapa” alitamka kanali huku akinielekezea kidole. Niliinuka nikapiga hatua tatu na kusimama. “Wewe ujibu maswali yetu kwa ukweli, hatutaki uwongo wala kilio hapa.”
“Sawa,” nilijibu kisha nikakohoa kidogo ili kusafisha koo. “Jina lako nani,” aliuliza kanali. “Nelson,” nilijibu. “Jina lako lingine” “Njata, Nelson Njata. “Yah! Jina la Njata lipo hapa” alidakia meja aliyekuwa anaandika. “Unafanya kazi gani pale Murongo?” aliuliza kanali. “Mimi ni bwana shamba.”
“Tunajua ni bwana shamba, lakini una kazi nyingine pale?” alidakia meja mwingine. “Kazi gani nyingine?” niliwauliza bila wasiwasi. “Unamjua Dan Kafumba?” aliuliza kanali na kunifanya nishtuke. “Namjua ni Mganda na pia ni rafiki yangu.” “Nani alimfikisha polisi?” aliuliza kanali huku akinikazia macho.
“Alijipeleka mwenyewe baada ya kupoteza bastola yake.” “Unaonyesha wewe ni mtu jasiri na mjuba, bila shaka wewe ni mwanajeshi, tena mwenye cheo kikubwa au sivyo? Alidakia meja anayeandika.
“Sivyo, mimi ni bwana shamba, hata Kafumba angekuwapo hapa angenisaidia kuwathibitishia.” “Pale Murongo kuna kituo chochote cha jeshi?” aliniuliza kanali. “Mimi sijui na wala sioni umuhimu wa kujua mambo ya jeshi.”
“Naona wewe nmi mwerevu sana kwa hiyo itabidi uhojiwe kwa nguvu, nenda ukakae,” alitamka kanali kwa ukali.
Nilirudi nyuma polepole na kukaa chini. Sasa ilifia zamu ya Sajini Binda kusimama, lakini maofisa hao walinong’ona kidogo kisha ghafla waliinuka na kuondoka zao. Kwa jinsi walivyoonekana walivyokuwa, kwa vyovyote ni maofisa wa Idara ya Ujasusi wa Kijeshi au ni maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa. Kama nusu saa baada ya maofisa hao kuondoka mlango ulifunguliwa na askari mmoja asiye na cheo akiwa amebeba chano iliyokuwa na bakuli tatu zilizokuwa na uji, akatugawia kila mmoja bakuli lake, tukaanza kunywa huku akituangalia.
Uji huo wa unga wa mahindi ulikuwa wa moto sana na haukuwa na sukari, hata hivyo hiyo haikutuzuia kunywa kutokana na njaa tuliyokuwa nayo. Baada ya kama robo saa hivi tulishamaliza kunywa uji huo na askari huyo akachukua bakuli zake na kuondoka.
“Sijui wanataka nini kwetu?” aliuliza Koplo Sudi kwa unyonge. “Hii yote ni kazi ya yule rafiki yangu Kafumba ni lazima ni jasusi wa Idara ya Usalama wa Taifa ya nchi hii yaani State Research Bureau” lakini kwa vyovyote itakavyokuwa asitokee mtu kati yetu akavunja kiapo chetu” nilitamka huku nikiwakazia macho.
Wakati Koplo Sudi anavaa nguo zake alizokuwa amezivua, mlango ulifunguliwa na askari mmoja aliyekuwa na bunduki aina ya AK 47 mgongoni, akatuamuru tutoke nje. Tulipotoka nje tulikuta askari zaidi ya kumi wenye silaha wakitusubiri. Tulipekuliwa kama tuna silaha na walipoona hatuna walitunyang’anya saa zetu na viatu. Baadaye wakatuamuru tuingie katika lori moja aina ya Benz lililoegeshwa mita kama kumi kutoka hapo. Humo ndani ya lori tulifungwa kamba mikononi na miguuni na safari ya tusikokujua ikaanza lakini njiani askari mmoja aliripoka kwa mwenzake kwamba tutafika katika kambi ya Makindye saa kumi na mbili jioni.
Kambi ya Makindye niliwahi kuisikia kutokana na sifa zake za utesaji na uuaji na ni maalumu kwa kutesea mateka wa vita au askari waasi. Kambi hii niliambiwa ni ya Polisi jeshi tupu (Military Police).
 
TULIFIKA Makindye usiku, eneo hilo lilifanana sana na Manzese ya Dar es Salaam. Kwa hakika safari yetu ilikuwa ndefu sana kwa hiyo nilihisi tumeingia ndani sana ya nchi ya Uganda na labda tulikuwa karibu na Kampala.
Tuliteremshwa ‘kikuku’ na kuingizwa katika nyumba moja ambayo nilihisi ni mahabusu. Tuliachwa humo tukiwa bado na kamba miguuni na mikononi hadi alfajiri. Usiku wote hatukuweza kuongea lakini asubuhi nilijua tupo wote pamoja baada ya Koplo Sudi kumwambia Sajini Binda kwamba ana njaa sana. Kwa kweli hata mimi nilikuwa na njaa sana lakini hatukuwa na la kufanya. Jua lilipoanza kuonesha makali yake tulifunguliwa kamba tulizofungwa na askari mmoja mwenye cheo cha Sajin.
“Mnataka chai au uji? Aliuliza Sajini huyo ambaye alionyesha ni katili sana. “Chochote unachoona tunastahili,” nilijib kwa upole. “Mimi nawapa uchaguzi nyinyi wafungwa,” alijibu Sajin huyo na kuondoka.
Dakika kama tano hivi baadaye mlango ulifunguliwa na Sajini yule yule aliyekuwapo awali, akaingia ndani akifuatiwa na askari mmoja asiye na cheo ambaye amebeba birika na vikombe vitatu vya bati.
“Haya punguzeni njaa kwa mlo huu nyie wafungwa” alitamka Sajin huyo kwa kebehi huku mwenzake akiweka birika na vikombe karibu yetu na kuondoka.
“Kwani sisi ni wafungwa?” niliuliza kwa upole huku nikimkazia macho. “Eh! Kumbe nyinyi ni kina nani?” alijibu Sajenti huyo huku akinitolea macho. “Sisi sio wafungwa bwana. Tunashangaa jinsi mlivyotukamata na kutuleta hapa.” “Hayo mimi sijui, ninachokijua nyingi ni askati mateka kutoka Tanzania kwa hiyo ni wafungwa.”
“Sisi sio askari bwana, kama mmeambiwa hivyo mmedanganywa kabisa. Mmeshindwa kuwapata askari halisi mkatukamata sisi raia na kutuita askari. Huo ni uonevu mkubwa,” nilimwambia kwa upole.
“Nyinyi watu wa Tanzania Kiswahili kirefu sana, kama siyo askari mmmefikaje hapa Makindye?” aliuliza kwa mshangao huku akituthitibishia hapo tulipo ni Makindye.
“Lakini kama sisi ni wanajeshi kama mnavyotaka tuwe, basi inabidi mtupe huduma sawa na mkataba wa Geneva unaohusu wafungwa wa kivita.” “Wewe mbona unaongea sana? Au ndiyo mkubwa?” aliniuliza kwa ukali na kuondoka zake.
“Inaonyesha hawa wanampango mbaya na sisi, hapa walipotuleta ni ndani kabisa ya nchi yao, ni maili chache tu kufika mjini Kampala. Sijui kama tutarudi salama. Iddi Amin hajawahi kuachia mtu salama na hasa waliokamatwa kimya kimya kama sisi. Ni lazima tufanye kitu ili tujiokoe” niliwaeleza wenzangu kwa sauti ya chini lakini kabla hawajanijibu mlango ulifunguliwa. Askari mmoja aliyevalia rasmi kipolisi jeshi (Military Police) alituamuru tutoke nje haraka. Hapo nje tuliwakuta askari wengine sita waliokuwa na bunduki aina ya AK 47 kila mmoja.
Tulifungwa pingu mikononi na kuongozwa hadi kwenye uwanja ambao bila ya kuamiwa nilijua ni sehemu ya kuulia watu kwa kupigwa risasi. Tulifungwa katika miti iliyokuwa mbele ya magunia mengi ya mchanga ambayo nilijua ni maalumu kwa kuzuia risasi isiende mbali ya hapo.
Baada ya kufungwa kamba kuzunguka mti nilijiona nimeshakuwa mfu. Koplo Sudi na Sajini Binda walianza kulia kama watoto wadogo. Niliogopa sana hali hiyo, kwa vile nilijua Waganda hao watagundua mimi ni kiongozi wao kutokana na ujasiri wa kutoogopa kifo na pia hiyo ilinithibitishia kwamba wenzangu sasa watakuwa tayari kutoa siri zetu zote. Dakika kama mbili baadaye askari jeshi watatu walisimama hatua kama tano mbele yetu na kutulenga kwa bunduki zao.
Wakati nikianza kumuomba Mungu anisamehe makosa yangu niliyomkosea ili anipokee huko mbinguni, ghafla ilifika gari moja aina ya Jeep ikiwa na askari mmoja mwenye cheo cha kanali na mwingine aliyevaa Kaunda suti ya rangi ya kijivu ambaye nilimuhisi ni afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Iddi Amin inayoitwa SRB. Maofisa hao waliteremka kwenye gari na kutusogelea.
“Naona nyinyi ni vijana wadogo sana, kwa hiyo najua hampendi kufa au siyo?” aliuliza kanali huyo huku akitukazia macho. Wote tulikaa kimya bila kutoa jibu lolote wala kukohoa.
“Nani mkubwa kati yenu kwa cheo? Aliuliza ofisa aliyevaa kiraia lakini naye hakupata jibu.
“Nataka kuwahakikishieni kitu kimoja, atakayekuwa mkweli hatutamuua na kwa kuwa tutamhoji kila mtu peke yake inabidi hapa tuwafunge mmoja mmoja. Mtu mjeuri hapa ndio utakuwa mwisho wake” alitamka kanali huyo kwa ukali. “O.K fungua hawa wawili abakie huyu,” aliamuru aliyevaa kiraia.
Mimi na Koplo Sudi tulifunguliwa na kurudishwa mahabusu, Sajini Binda tukamwacha akiwa bado amefungwa. “Hata kama ukisema ukweli haiwezi kuwazuia kutuua. Kumbuka kiapo chako usiwe mwoga.” Nilimkumbusha Koplo Sudi. “Lakini, lakini afande….” “Shii, kumbuka kiapo , usiwe mwoga, kama ni kifo acha tukikabili.” Nilisisitiza.
Kabla ya Koplo Sudi hajaendelea kutamka neno linguine tukasikia mlio wa risasi tatu ambazo zilitufanya tupate kiwewe cha ghafla.
“Wameshamuua, wameshamuua.” Alilalamika Koplo Sudi. Mimi sikumjibu lolote bali nilimkazia macho tu, alipoona hivyo aliinuka haraka alipokaa na kuniangukia miguuni kwangu huku akilia.
“Watatuua wote afande,” alilalamika. “Wacha tufe lakini kumbuka kiapo, usiwe mwoga,” nilimjibu huku na mimi nikitoa mchozi wa chuki.
“Nisaidie afande, naogopa sana.” Alizidi kulalamika. “Nyamaza!” nilimwamuru kwa ukali, akanyamaza. Punde kidogo mlango ulifunguliwa na polisi jeshi mmoja. “Nani ndiye Koplo Sudi?” aliuliza askari huyo akiwa amesimama mlangoni. Koplo Sudi hakujibu bali aliongeza kasi ya kulia na kumfanya askari huyo aje juu.
“Nauliza nani ndiye Koplo Sudi sitaki kusikia kilio.” Alifoka. “Ni mimi, ni mimi.” Hatimaye alijibu. “Kuja hapa haraka.” Aliamuru kwa ukali. Koplo Sudi aliinuka na kumfuata.
Alipotoka mlango ukafungwa, nikabaki ndani peke yangu. Sasa nikajua siri zimeanza kutoka, kama wamemjua Koplo Sudi bila shaka Sajini Binda amekwishawaeleza mengi. Hofu ikazidi kuniingia, nikajua sasa watanishughulikia mimi kikamilifu wapate siri. Niliwaza sana bila kupata jibu lolote, tama ya kujiokoa ikaanza kujengeka polepole akilini mwangu.
“Wakishajua mimi ndiye kiongozi hasira zao zote zitaniangukia mimi.” Nilijisemea peke yangu kama mwehu. Dakika kama ishiriki baadaye nikasikia mlio wa risasi mbili nikajua Koplo Sudi naye ameshauawa. Hofu ikanizidi, nikajua zamu yangu ya kutolewa roho imekaribia. Nilimkumbuka Mungu, nikamwomba aniokoe na kifo hicho, nikalia sana, lakini sikulia kwa hofu ya kifo bali nilimlilia Mungu aniepushie balaa hilo. Kilio change kilikatizwa ghafla na sauti ya polisi jeshi aliyekuwa mlangoni.
“Unalia huku umepiga magoti na mikono juu unamwomba Mungu eee! Alitamka askari huyo kunigutua. Haraka nilifuta machozi yangu, kwa kweli nilipata nguvu mpya, hofu ya kifo ilinitoka kabisa, nilihisi ni sababu ya kilio changu kwa Mungu.
“Wewe ndiyo Luteni, siyo?” aliniuliza huku akitabasamu. “Umetumwa unite au uniulize swali?” nilijibu kwa upole huku nikitabasamu.
“Haya unaitwa,” alitamka huku akiendelea kutabasamu. Niliinuka haraka tukaongozana hadi kule kwenye uwanja wa mauaji ambako nilipaita machinjioni. Nilipofika hapo nikafungwa kamba kama awali kisha askari wanne wenye silaha wakajipanga mbele yangu wakingoja amri ya kunifyatulia risasi. Baada ya kufungwa kamba nikaoiona tena ile gari aina ya Jeep ikija na baadaye ikasimama palepale iliposimama mwanzoni. Yule kanali na mwenzake aliyevaa kiraia ambaye nilimuhisi ni afisa usalama wa taifa kutoka SRB, walinisogelea tena kama walivyofanya mwanzoni. Muda wote huo nilikuwa naichunguza ile miti kuona kama ina damu ili nipate uhakika kama wenzangu kweli wameuawa.
Hata hivyo sikuona damu yoyote katika miti hiyo kwa hiyo nikahisi umetumika ujanja wa kututisha lakini kama wametumia mbinu hiyo basi wamesahau kupata miti hiyo japo rangi inayofanana na damu.
“Wewe ndiyo Luteni Njata au siyo?” aliniuliza huyo aliyevaa kiraia. “Unaniambia au unaniuliza?” nilimjibu bila hofu. “Wenzako wote wamekubali kushirikiana nasi na wamejibu vizuri lakini tumewaua kwa ujeuri wao.” Alieleza kanali huyo.
Maneno haya niliyatafakari na kugundua wenzangu hawajauawa bali wamenigeresha mimi kwa milio ya risasi tu. “Sasa jibu maswali yetu vizuri na kwa usahihi, udanganyifu wowote utakaofanya utasababisha uwafuate wenzako huko ahera, umenielewa?” alitamka.
“Nimekuelewa bwana.” Nilijibu kwa upole. “Wewe tumeambiwa ndiyo kiongozi wa wenzako na cheo chako ni luteni, kweli?”. “Kweli” nilijibu kwa upole huku nikimkazia macho. “Unaongoza askari wangapi pale Murongo?” ofisa aliyevaa kiraia aliniuliza.
“Nawaongoza hao hao wawili waliowaambia mimi ni kiongozi wao.” “Yaani wewe ni kiongozi wa askari wawili tu, kambi gani hiyo ya watu wawili?” aliuliza kanali. “Kwani wameaambia tupo wangapi?” “Ah? Yaani wewe badala ya kutujibu maswali yetu, unatuuliza sisi maswali tukujibu?” alifoka huyo aliyevaa kiraia.
“Siyo hivyo wakubwa, maswali yenu mengine najua majibu mnayo wenyewe, sasa mimi nashangaa mkiniuliza. Mnanichelewesha bure kunipiga risasi, niuweni roho zenu zitulie.” Nilijibu kwa utulivu mkubwa uliowafanya wanishangae. “Wewe huogopi kufa?” aliniuliza kanali huku akinikazia macho.
“Kila mtu atakufa hapa duniani hata kama utamtanguliza mwenzio kufa ujue iko siku na wewe utamfuata.” Nilijibu na kuwafanya wazidi kunishangaa. “O.k. sawa bwana, sasa pale Murongo kuna kambi ya jeshi?” aliuliza kanali. “Hakuna” nilijibu kwa mkato.
“Kumbe nyinyi ni askari mnaofanya nini pale kijijini?” alifoka aliyevaa kiraia. “Tunataka kufundisha askari raia yaani mgambo.” “Mmeshaanza kuwafundisha?” alizidi kuuliza. “Bado labda mwezi ujao tutaanza.” “Kitu gani kinachowafanya muanze kufundisha mwezi ujao?” ofisa huyo aliuliza. “Bado hatujakamilisha mipango ya kupata vifaa na watu wa kuwafundisha.” “Unaona unavyojibu vizuri? Wewe sasa utakuwa rafiki yetu hatuwezi kukuua.” Alitamka kanali huku akitabasamu.
“Pale Murongo kuna redio ya mawasiliano?” alizidi kuuliza ofisa huyo huku akiandika. “Ipo.” Nilijibu nikijua wenzangu wameshaeleza yote. “Ipo sehemu gani pale Murongo?” aliuliza kanali.
“Kwa kweli ni vigumu, labda twendeni nikawaonyeshe huko huko,” nilijibu kwa upole na kuwafanya wacheke sana. “Wewe mjanja sana, kweli wewe ni ofisa wa jeshi,” alisifu ofisa huyo aliyevaa kiraia.
“Hebu mfungueni kamba, huyu sasa ni rafiki yetu, ameonesha ushirikiano, tutawarudishia Murongo,” aliamuru kanali kisha wakaingia kwenye gari yao na kuondoka. Polisi jeshi mmoja alinifungua kamba na baadaye wakanirudisha mahabusu ambako niliwakuta Sajini Binda na Koplo Sudi wakinywa uji. Sikuwasemesha kitu nilikaa kwa huzuni huku nikiwakazia macho.
“Mmewaeleza mambo mengi sana mkifirikia ni njia ya kujinusuru katika mikono yao, siyo?” niliwauliza kwa upole lakini sikupata jibu. “Tuone sasa kama kweli wataturudisha Murongo baada ya kuwapa wanachokitaka,” nilizidi kueleza.
“Nani kati yenu aliulizwa juu ya masafa (frequency) ya redio yetu ya mawasiliano?” niliwauliza lakini hakuna aliyenijibu.
Hali hiyo ilinithibitishia kwamba wameeleza mambo mengi sana na sasa wanaona aibu hata kuongea na mimi. “Ndiyo maana hawakuniuliza maswali mengi kwa kuwa mengi wamekwishaelezwa na hawa.” Niliwaza.
Jioni ilipofika tulitolewa humo mahabusu tukiwa tumefungwa vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi, tukaingizwa ndani ya lori moja. Dakika chache baadaye lori hilo liliondoka kuelekea tusipopafahamu lakini tulitumia muda wa dakika kama ishirini au ishirini na tano hivi ndipo lori hilo liliposimama. Tuliteremshwa na kuongozwa hadi kwenye ngazi fulani ambako tuliteremka chini hadi kwenye chumba kimoja chenye hewa nzito na harufu mbaya ya mikojo na damu.
Humo tulifunguliwa vitambaa tulivyofungwa lakini ikawa sawa na tulivyofungwa kutokana na giza la humo ndani. Hali ya mahabusu ile ya Makindye ilikuwa ni afadhali kuliko hii inayotisha. Tulitulia kimya sakafuni bila kusemezana kitu kutokana na utisho wa humo ndani. Hata hivyo kwa kawaida maongezi yananoga unapoongea na mtu huku unamuona, sasa hii giza imevunja hata hamu ya kuongea.
Tulikaa humo ndani bila kufahamu kama ni jioni, usiku au asubuhi imefika. Kwa kadiri nilivyotafakari jinsi tulivyokamatwa na tulivyofanyiwa ni dhahifi kifo kilikuwa bado kinatuandama. Uchovu na njaa ndiyo vitu vya kwanza kutishia maisha yetu hasa mimi ambaye nilikuwa sijaonja kitu chochote kwa siku mbili. Wakati tukiwa bado hatujui la kufanya tulisikia sauti kutoka kwenye kipaza sauti kidogo kilichokuwa humo ndani.
“Luteni Njata na Sajini Binda kuja nje haraka.” Sauti hiyo iliamuru na wakati huo huo mlango mzito wa chuma ulijifungua tukaona mwanga kidogo mbele yetu. Mimi na Sajini Binda tuliinuka na kuuendea mlango huo lakini Koplo Sudi alimshika Sajini Binda huku akilia sana akimuomba asimuache. Nilishangaa sana kwa nini amshikilie Sajini binda badala ya mimi mkubwa wao. Hata hivyo baadaye nilihisi labda kwa vile mimi amekwishaniudhi kwa kusaliti kiapo cha jeshi letu. Sajini Binda alipoona Koplo Sudi hamuachi, akaamua kutoka naye. Tulitokea kwenye ukumbi mrefu ambako tuliwakuta vijana wawili waliovalia Kaunda suti zao maridadi wakitusibiri.
“Mmeitwa wawili mnakuja watatu, nyinyi watu vipi?” alifoka mmoja wao ambaye ni mfupi kidogo kuliko mwenzake. “Huyu mwenzetu anaogopa kubaki peke yake” alijibu Sajini Binda.
“O.K. njooni huku.” Alitamka huku akitangulia mbele. Kwa kweli humo ndani kulionesha wazi ni sehemu ya mauaji. Tuliongozana na maofisa hao katika ukumbi huo mrefu uliokuwa unawake taa hadi kwenye mlango mwingine wa chuma uliokuwa upande wa kushoto. Ofisa huyo aliugonga mlango huo kwa kutumia chuma cha kufungia nje na baada ya sekunde chache ukafunguliwa.
Bila kuongea na aliyeufungua mlango huo, akatuonyesha ishara tuingie ndani. Sajini Binda na Koplo Sudi walitangulia kuingia wakifuatiwa na mimi. Maofisa waliotuleta wakafunga mlango huo kwa nje na kuondoka zao. Humo ndani tulikuta ukumbi mrefu kidogo uliojaa harufu mbaya zaidi kuliko kule tulipowekwa mwanzo. Kulikuwa na nyororo nyingi zilizofungwa ukutani ambazo zilinijulisha ni za kufungia watu. Mbele kidogo ya ukumbi tulikuta watu wanne wamefungwa nyororo mikononi wakiwa wamesimama wima lakini vichwa vyao upande wa sura wameangushia vifuani mwao huku damu zikiwatoka mdomoni, puani na masikioni. Walionesha uhai umekwishawatoka. Kuona hivyo, Koplo Sudi alianza kutapika hatimaye akazirai.
Wakati tunamhudumia Koplo Sudi kwa kumpepea kwa mashati yetu tuliyoyavua, mlango uliokuwa juu ya ngazi mbele yetu ukafunguliwa. Wanaume sita vipande vya baba wakaingia na kusimama mbele yetu. Miamba hiyo ya watu ilikuwa vidari wazi na walivaa chupi tupu. Hakika unaweza kuzimia kabla hawajakugusa. Jinsi maumbile yao yalivyo na sura zao mbaya za kutisha ni dhahiri wamewekwa maalumu kwa ajili ya utesaji hadi kuua. Moyoni nilijua wazi tupo katika jengo maalumu la Idara ya Ujasusi ya Iddi Amin (SRB) la kuhojia watu. Tukaamriwa tuvue nguo zetu zote tubaki kama tulivyozaliwa. Baadaye watu hao wakaanza kutupiga mgongoni kwa kutumia waya fulani bila ya kutusemesha kitu. Ulikuwa ni muda wa adha kubwa ambayo tangu nizaliwe sijawahi kuipata. Koplo Sudi alizimia tena akifuatiwa na Sajini Binda lakini wauaji hao waliendelea kuwapiga hadi mimi nikaona niwaokoe.
 
Sorry tuanzieni hapa sehem ya kwanza
LIKUWA mkoani Kagera, miezi michache kabla ya Vita ya Kagera, mmoja wa makachero wa Tanzania aliuawa na maofisa wa Idara ya Usalama ya Uganda (SRB) chini ya aliyekuwa Rais wa Uganda, Idi Amin Dada. Afisa huyo alikuwa na maofisa wenzake wawili wa jeshi ambao Serikali ya Idi Amin iliwawekea mtego kwa kuwaalika kwenye tafrija kijiji cha Kikagati ndani ya Uganda katika hoteli moja mashuhuri ambako walizoea kufika kwa ajili ya burudani wakitokea kijiji cha Murongo, Karagwe. Kwa kumbukumbu ya kuuawa kwa mwenzake, kachero mmojawapo kwenye tukio hilo, Frowin Kageuka, ameandika kitabu maalumu chenye jina “MATEKA MPAKANI”. Kachero huyo mstaafu kwa sasa, alisoma na mwenzake huyo aliyeuawa, wakahitimu pamoja katika Shule ya Sekondari Tambaza mwaka 1975 na wakaanza kazi pamoja mwaka 1977. MWANDISHI WETU anaeleza kwa muhtasari kinachojitokeza kwenye kitabu hicho ambacho kwa sasa kimefikia hatua za mwisho kwa ajili ya uchapishaji.
………………..
Sura ya kwanza
KATIKA sura ya kwanza ya kitabu chake, kachero Frowin anaelezea hatua za awali kabisa akiwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), akiikumbuka siku aliyopewa uhamisho wa kijeshi kwenda katika kijiji cha Murongo, Karagwe mkoani Kagera.
Anasema; “…ilikuwa haijapita hata miezi mitatu tangu nilipohamia katika kambi ya Jeshi ya Nyumbu, Kibaha kutoka Makao Makuu ya Jeshi (MMJ) nilipopewa taarifa iliyonishtua sana moyo ya kuitwa katika ofisi ya utawala ambako nilidokezwa na ‘makomredi’ wenzangu kuwa kuna barua yangu.
Nikafunga roho, nikaingia ofisi ya utawala na kumkuta afande wa utawala mwenye cheo cha meja ambaye alinikabidhi barua ya uhamisho bila kunisemesha, nami bila kusita nikaipokea na kuisoma na baadaye nikatia sahihi kwenye barua hiyo kama kawaida ya Jeshi.
Baada ya kutoka katika ofisi ya utawala baadhi ya makomredi wenzangu walikuwa na hamu kubwa ya kutaka kujua nilichoitiwa huko ofisi ya utawala, kila niliyekutana naye alinisimamisha na kuniuliza hiyo nikaiona kero, nikaamua kumuaga kila askari niliyekutana naye kama mwehu ili mradi kuyakwepa maswali. Hata hivyo, hali hiyo iliongeza shauku ya askari wengi kutaka kujua kilichonisibu.
Kwa kweli moyo wangu ulijaa chuki kwa Jeshi lote na kila ofisa wa Jeshi nilimuona kuwa ni adui yangu. Nikafikiria jinsi nilivyolizoea Jiji la Dar es Salaam na sasa natakiwa nikaishi mkoani Kagera, Wilaya ya Karagwe katika kijiji cha Murongo. Hakika nilijua muda wa utumishi wangu katika Jeshi la Ulinzi unafikia mwisho.
Lakini nilikuwa na kila sababu ya kulizoea Jiji la Dar es Salaam, hebu fikiria nilianza shule darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Magomeni Kota, halafu nikasoma katika Shule ya Msingi Msimbazi hadi kumalizia masomo sekondari pale Tambaza. Si unaona jinsi nilivyokuwa mtoto wa Jiji hili halafu naambiwa nihame.
Sasa unaweza kupima hali nitakayokuwa nayo mkoani Kagera na hasa ukizingatia kwamba hiyo itakuwa ni mara yangu ya kwanza kutoka katika Jiji la Dar es Salaam ukiondoa nilipokwenda mafunzo ya kijeshi kule Monduli na mafunzo ya ushushushu maeneo mengine, pamoja na likizo nilizokuwa nikienda kijijini kwetu.
Huu ulikuwa mtihani mkubwa kwangu, lakini wakati mwingine nilijipa moyo wa kiaskari na wa kijasusi kwa sababu mimi nilikuwa ni ofisa wa usalama wa taifa niliyekubuhu na kupelekwa kufanya kazi za mawasiliano katika Jeshi la Ulinzi. Hata hivyo wakati mwingine nilijiona ninaonewa kwa hiyo nastahili kuliacha Jeshi.
Nimekosa nini? Sijui, nimemuudhi mkubwa gani? Sijui. Mungu pekee ndiye anayejua, nilijisemea moyoni mara kwa mara. Barua yangu ya uhamisho ilinitaka niwe nimefika katika kituo changu cha kazi kijijini Murongo si zaidi ya Agosti 24, 1978, kwa maana hiyo nilikuwa nimebakiwa na siku sita tu. Wakati natafuta usafiri wa kwenda huko baada ya ‘kuzikunja’ shilingi laki tatu na nusu za uhamisho, ghafla nikakutana na rubani wa jeshi ambaye ni kabila langu, aliyejulikana kwa jina la Meja Fox.
Nilipomueleza juu ya uhamisho wangu wa kwenda Kagera, aliniambia anatarajia kwenda Bukoba kesho kutwa kwa ndege aina ya Buffalo anayoiendesha kwa hiyo nisiwe na wasiwasi atanifikisha. Habari hizo zilikuwa njema sana kwangu, nilifurahi sana kupata usafiri huo wa dezo na kwa kudhihirisha furaha yangu tunaingia katika baa moja pale Kariakoo kuburudika na Meja Fox.
Meja Fox ni mmoja wa marubani waliotegemewa sana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kurusha ndege za mizigo aina ya Buffalo na Carribou. Siku ya kuondoka kama ilivyokuwa kawaida ya ndege za jeshi, tulipitia Zanzibar, Dodoma, Mwanza na kutua Bukoba jioni. Hapo katika uwanja wa ndege wa Bukoba ambao ni wa nyasi tupu na upo karibu sana na Ziwa Victoria hakukuwa na heka heka zozote mbali ya watu wachache wakiwamo askari wa Jeshi la Ulinzi waliofika kupokea mizigo yao.
Ingawa nililiona gari la jeshi limeegeshwa hapo kiwanjani lakini kutokana na chuki ya uhamisho niliopewa sikutaka kuomba msaada wowote kwa askari wenzangu. Nikamsogelea mwanaume mmoja aliyekuwa anapita katikati ya uwanja kuelekea upande wa pili ambako kulikuwa na nyumba nyingi za watu nikamuuliza mahali ilipo hoteli ya karibu na hapo.
“Lake Hotel ipo palee, siyo mbali,” alinijibu huku akinielekeza. Baada ya kuelekezwa, nikabeba begi langu na kuelekea Lake Hotel ambako kwa kweli ulikuwa ni mwendo wa dakika kama kumi hivi kutoka hapo uwanja wa ndege. Nilifika.
Kesho yake asubuhi, baada ya kifungua kinywa nikaenda mjini kutafuta gari la kunipeleka kwenye kambi ya Jeshi ya Rwamishenye lakini nilipokosa gari ya jeshi nikaamua kupandisha mlima kwa miguu. Kambi ya Rwemishenye imewekwa mahali pazuri sana, hali ya hewa ni nzuri na kiulinzi walipachagua panapofaa sana. Hata hivyo, katika kambi hiyo sikupata msaada wowote mbali ya kuniambia watatuma habari kwa redio ya mawasiliano ili wanipokee huko Murongo na baada ya maelekezo hayo niliondoka hapo kambini huku nikiwa nimefura kwa hasira, nikaelekea mjini kutafuta basi la kwenda Karagwe.
Nilipofika mjini nilihaha eneo la Soko Kuu la Bukoba na stendi ya basi kwa zaidi ya saa nzima lakini sikupata basi la kwenda Karagwe ingawa baadaye nilipanda lori moja la ushirika wa kahawa ambalo lilinifikisha Karagwe saa tisa jioni.
Kutoka Karagwe nikapanda gari moja aina ya Toyota ililokuwa limejaa watu na mizigo hadi kijiji cha Murongo ambacho kipo mpakani kabisa na nchi ya Uganda. Hapo Murongo nilipokelewa na Sajin mmoja ambaye alivalia sare za kijeshi lakini kwa kuwa mimi nilivaa kiraia na pia huwa mara nyingi sivai kijeshi kutokana na kazi zangu, ilibidi nijitambulishe kwake naye akajibu amefika kunipokea baada ya kujulishwa kwa simu ya upepo kutoka Bukoba.
Sajini huyo kijana alinieleza anaitwa Binda na kwao ni Korogwe mkoani Tanga. Alisema ana miaka mitatu hapo Murongo na awali alikuwa mjini Bukoba. “Mimi ndiye ninayeshughulikia mawasiliano hapa Murongo,” alinieleza.
“Mawasiliano ya nini unafanya hapa? Kwani kuna kambi yoyote ya jeshi kama zile za Bukoba? Niliuliza kwa hasira. Hakuna kambi yoyote hapa ni zile za Bukoba tu, Rwamishenye na Kaboya. Sasa itasaidia nini adui akiingia sasa hivi na wewe ukaarifu Kagera? …“Sijui afande, wakubwa walioanzisha kituo hiki labda wanajua zaidi.”
Mpo wangapi hapa? “Tupo mimi na msaidizi wangu Koplo Sudi.” Koplo Sudi ni kabila gani na amefika lini hapa? Niliuliza kwa ukali, utafikiri Sajenti Binda ndiye aliyenihamishia hapo Murongo. “Yeye nilimkuta hapa, alifika mwaka mmoja kabla yangu, kwao ni Zanzibar.”
Kwani ulipoambiwa mimi nakuja ulielezwaje? Niliambiwa Luteni Njata anakuja kuwa mkuu wa kituo hiki cha mawasiliano, lakiini ni afisa usalama.” O.K vyema, sasa nipeleke nitakakoishi au hakuna nyumba? “Ipo afande.”
Sajini Binda alinipeleka katika nyumba moja iliyokuwa mita kama thelathini kutoka hapo nilipoteremka ambako wenyewe wanaita mjini lakini si mjini si lolote ni balaa tu. Nyumba hiyo nzuri kidogo, iliezekwa vigae na ilikuwa ya matofali. Nilihisi hapo alikuwa akiishi mzungu fulani mkulima zamani. Aliniambia vyumba viwili vya ndani na sebule ni vyangu na yeye na Koplo Sudi walikuwa na chumba kimoja kila mmoja ubavuni mwa nyumba hiyo, wote wawili walikuwa makapera kwa hiyo na mimi nikawa nimeongeza idadi ya makapera lakini ukapera wangu ni hapo Murongo tu.
Licha ya kupachukia sana hapo kijijini lakini nilipoona kitanda na makochi uchwara hapo nyumbani nilipata moyo sana. “Sina sababu ya kununua upya kitanda wala makochi, kwanza nani atanitembelea huku. Hata zile laki tatu nilizoziacha benki mambo yakinishinda zitanisaidia kuanzisha mradi, lakini mradi gani huo wa laki tatu? Nilijisemea peke yangu baada ya Sajini Binda kuondoka.
Maisha yangu hapo kijijini yalikuwa ya taabu sana, kila siku nilikuwa nakumbuka Jiji la Dar es Salaam na vimbwanga vyake vyote. Hakika nilikuwa na wakati mgumu sana lakini kadiri siku zilivyoyoyoma ndivyo nilivyozoeana na watu hasa askari wa Magereza ambao kila siku tulikuwa tunakutana katika klabu yao ambako chai yangu, chakula cha mchana, cha usiku na bia nilivipata hapo.
Baada ya miezi miwili nilikuwa nimekwishazoea maisha ya hapo Murongo na nilipata rafiki mzuri wa kike mwenye asili ya Kihutu, huyu alikuwa mwalimu wa Shule ya Msingi Murongo. Lakini pamoja na kumpata binti huyo tabia yangu ya kula katika klabu ya Magereza iliendelea na wakati huo wa ‘kutamba’ na binti huyo nilipata rafiki mwingine lakini wa kiume, anaitwa Dan Kafumba. Huyu alikuwa raia wa Uganda na alikuwa kijana mpole.
Kafumba aliniambia yeye anaishi katika kijiji cha Kikagati ambacho kipo mpakani upande wa Uganda kilomita mbili na nusu kutoka kivuko cha mto Kagera unaotenganisha Tanzania na Uganda. Nilifurahi sana kumpata rafiki Mganda na hasa kwa vile wakati huo serikali yetu ilikuwa inapigana vita ya maneno na serikali ya Idi Amin Dada, kwa hiyo nikajua atanipa habari za kwao. Kafumba aliniambia yeye ni bwana shamba huko kijijini kwao Kikagati na mimi ili nisiwe mbali naye nikamweleza nami ni bwana shamba.
Urafiki wangu na Kafumba ulizidi kushamiri siku hadi siku, tulitembea pamoja, kunywa pombe pamoja katika klabu ya Magereza na wakati mwingine tulivuka mpaka kwenda kwao Kikagati kunywa pombe katika baa nzuri iliyomo ndani ya Green Hotel.
Hoteli hiyo nzuri iliyoezekwa bati zilizopakwa rangi ya kijani na taa zake za ndani zilikuwa za rangi ya kijani ni mali ya mzee mmoja wa miraba minne aliyeitwa Idris. Mzee Idris alinizoea sana na kwa kweli alinipenda, kwa hiyo nikawa simalizi wiki bila kumwambia Kafumba twende Green Hotel. Hata hivyo, Kafumba alikuwa anapenda sana kunywa pombe katika klabu ya Magereza lakini hiyo haikunishtua kwa vile alikuwa na msichana wake katika klabu hiyo ambaye alikuwa muhudumu hapo hapo.
Msichana huyo alikuwa mwenyeji wa hapo na ingawa mimi na Kafumba tulikuwa marafiki sana lakini wasichana wetu hawakuelewana hata kidogo, labda ni kwa sababu ya kasumba za asili za kike. Siku moja nilinunua sanduku moja la bia na kuliweka nyumbani kwangu na Kafumba aliponifuata nyumbani mchana kama saa tano hivi akanikuta nipo peke yangu ‘napiga’ maji.
Nilimkaribisha bia moja lakini akaipiga ule mtindo wa tarumbeta kisha akaniambia tuondoke tukanywe katika klabu ya Magereza. “Hapana leo tunywe hapa hapa ndani hadi sanduku hili la bia tulimalize,” nilimwambia bila kufahamu kwamba hiyo ni siku maalumu ambayo Mungu alitaka kunionyesha siri za rafiki yangu huyo.
“O.K. lakini kesho lazima Magereza au siyo?” alijibu ili kuniridhisha nisichukie.
“Hakuna taabu kesho utamwona tu, hata leo jioni ukitaka” nilimridhisha. Tulikunywa pombe mpaka saa tisa mchana, wakati huo mimi nilikwishakunywa chupa nane na mwenzangu chupa kumi, ingawa mimi nililewa lakini Kafumba alilewa zaidi yangu.
Wakati ananiaga kwamba lazima arudi nyumbani mapema kwa vile ameshalewa sana alinyanyuka kwa taabu kwenye kochi na bila kujua bastola aliyovaa katika mkanda kiuononi ndani ya shati lake ambalo hakulichomekea ndani ya suruali ikaanguka kwenye kochi. Mimi niliona kitendo hicho lakini nikasita kumgutua kwa vile nikajua yeye kumbe si mtu mzuri. Nikamsindikiza nje kisha haraka nikarudi nyumbani kuichukua bastola hiyo iliyokuwa imetulia kwenye kochi. Bastola hiyo ilikuwa aina ya Star na ilikuwa na risasi sita.
“Kwa nini Kafumba atembee na bastola?” nilijiuliza bila kupata jibu. “Je, ni askari au afisa wa SRB (State Research Bureua) yaani Idara ya Usalama ya Taifa ya Idi Amin? Kwa kweli sikupata jibu la kuniridhisha. Aliniambia yeye ni bwana shamba, sasa bwana shamba na bastola ni kweli hayo? Basi kama ni jasusi ametumwa kunipeleleza mimi, Mungu kamuumbua na mwisho wake umefika.”
Niliichukua bastola hiyo haraka na kuipeleka kituo kidogo cha polisi cha hapo Murongo kisha nikawaamuru polisi hao wakamsubiri Kafumba kivukoni ili wamkamate na kumrudisha kabla hajapanda boti na kuvuka mpaka. Polisi walifanya hivyo. Asubuhi yake nilipokwenda kituoni nikiwa na Sajini Binda nikaambiwa Katumba yumo ndani mahabusu. Nikamwambia mkuu wa kituo hicho asimtoe mpaka niarifu Bukoba.
Kati ya mambo yatakayofuata ni namna kachero huyo na wenzake walivyowekewa mtego kisha kunaswa na Idara ya Usalama wa Taifa ya Idi Amin. Ili kujua zaidi, endelea kufuatilia mfululizo wa muhtasari huu wa kitabu kipya cha kachero huyu alichokiandika kwa ajili ya kumuenzi marehemu rafiki yake.
 
"Tuliamuriwa kutoka nje ya jengo kupitia mlango wa bustanini na majasusi wa shirika la ujasusi la Idi Amin.
Nje ya jengo kulikuwa na bustani nzuri iliyojaa miti midogo midogo na barabara zenye kokoto. Mbele yetu hatua kama 200 hivi iliegeshwa Land Rover.
Koplo Sudi akawa na kiherehere, akatangulia kuifata Landrover hiyo akifuatiwa na Sajini Binda.
Mimi nilikuwa nyuma yao lakini mawazo yangu yalihisi kuna hatari mbele yetu, haiwezekani watuachie kirahisi namna ile.
SAJINI BINDA NA KOPLO SUDI WAUAWA BAADA YA KUISOGELEA LANDROVER
"Wakati akili yangu ikiwaza bila kupata majibu, ghafla nikamwona Koplo Sudi ambaye alikuwa anajitayarisha kuingia ndani ya Landrover hiyo akianguka chini.
Kabla sijamuangalia vizuri, nikasikia Sajini Binda akitoa sauti ya kung'aka na kuanguka chini.
Bila kuzubaa nikaruka na kujiviringisha kama gogo linalobiringika kutoka mlimani.
Niliingia uvunguni mwa Landrover na kusikilizia wakati huo Koplo Sudi na Sajini Binda walikuwa wamelala kando huku damu zikiwavuja kwa wingi.
Utulivu waliouonesha na damu zilivyokuwa zikiwatoka nilijua kuwa wameshakufa.

JASUSI LA KITANZANIA LAWATOROKA WANAJESHI WA UGANDA KININJA

"Sasa milio ya bunduki na risasi kutoboa gari hilo zilisikika vizuri masikioni mwangu lakini gari halikulipuka.
Hii ilidhihirisha kuwa Landrover hiyo iliwekwa hapo kama chambo tu, haikuwa na petroli na labda hata haikuwa na injini.
Kilichonishangaza ni jinsi risasi hizo zilivyonikosa, sijui wapigaji hawakuwa na shabaha au ni Mungu tu.
"Huu ndio mlango wa bustanini, mlango wa mauaji unaotumiwa na wauaji wasioonekana wakiwa na bunduki zisizotoa mlio," nilijisemea kama mwehu kisha kama umeme nilitoka hapo uvunguni na kukimbia kwa kasi kwa mtindo wa zigizaga.
Risasi zilivuma karibu yangu na moja ikanipata begani lakini sikusimama.
Niliacha barabara inayoelekea kwenye mlango ambako kulikuwa na kibanda cha walinzi, nikapinda upande wa kushoto bila kujua ninapoelekea.
Walinzi hao waliponiona nao walianza kunifyatulia risasi ambazo zilitoa sauti ya kutisha lakini Mungu alikwishasema hapana.
Maofisa Usalama wa Taifa wa Idi Amin nao hawakukubali kunikosa, walikuja nyuma yangu kwa kasi sana lakini kwa vile nilishawaacha mbali hawakufanikiwa kunipata.

ARUKA SENG'ENGE ZENYE MIIBA NA KUDANDIA LORI HUKU RISASI ZA WANAJESHI WA ZIKIMKOSA KOSA

"Nilipofika kwenye seng'enge zenye miiba na urefu wa kama mita mbili hivi kwenda juu nikashtukia naruka kama karatasi kwenye upepo na kujikuta naangukia upande wa nje wa eneo hilo la wauaji.
Bila ya kufanya ajizi nikainuka na kutimua mbio huku risasi zikiendelea lakini hazikunipata.
Nilikimbia mbele zaidi nikatokea kwenye barabara kubwa ya lami ambako nililiona lori moja lililobeba mifuko ya saruji likijikongoja.
Niliongeza kasi ya mbio na kulirukia nyuma ambako nilijibwaga juu ya mifuko hiyo ya sementi huku nikitweta.
Nilipotazama nyuma sikuwaona maadui zangu hivyo nikajua wameenda kufuata magari ili wanifate.
Tulipita eneo lililoandikwa Nakulabye na baadae tukaelekea barabara inayoelekea eneo liitwalo Bombo lakini tulipofika eneo la Namirembe, lori likaanza kupunguza mwendo, nikahisi linakaribia kusimama.
Niliruka haraka na kuanza kutembea kufuata barabara ya Balintuma hadi kwenye mzunguko wa barabara iliyooneshwa kwa kibao inaelekea Chuo Kikuu cha Makerere.
Baadhi ya watu walinishangaa kutokana na damu ilivyokuwa ikinitoka lakini mimi nilisonga mbele huku nikiwakwepa polisi na askari wengine waliovaa sare.

AINGIA KANISANI NA KUANGUA KILIO KILICHOMSHITUA PADRE

"Ghafla bila kutarajia nikaona bango kubwa mbele yangu limeandikwa 'Namirembe Cathedral'.
Nilihisi hapo ndipo mahali pekee napoweza kuonewa huruma. Nikaangazo macho huku na huku kuthibitisha hakuna anayenifuata au kuniangalia kisha haraka nikaingia kwenye mlango wa uwa wa ukuta wa kanisa hilo ambako ndani nilikuta ibada ikiendele kukiwa na waumini wapatao hamsini huku padre wa kizungu akiongoza ibada.
Nikatafuta sehemu nzuri ya peke yangu nyuma kabisa na kusikiliza ibada hiyo iliyokuwa ikiendeshwa kwa lugha ya Kiingereza.
Mwisho wa ibada watu wote walitoka nje lakini mimi nikabaki ndani na kupiga magoti nikainamisha kichwa chini na kuanza kububujika machozi kama bomba la maji lililopasuka.
Nililia sana na hatimaye nikalia kwa sauti kubwa.
Kilio changu hakikuwa cha kumuomba Mungu bali maumivu, njaa na uchovu ambao binadamu mwenye afya ya kawaida lazima angezimia.

PADRE AMSAFISHA JERAHA NA KUMTOA RISASI MWILINI

"Baada ya kama nusu saa nikasikia mtu akinisemesha na kunigusa kwa mkono begani kisha akaniinua kichwa.
"Pole sana kijana, umepatwa na nini?" aliniuliza mtu huyo kwa kiingereza.
"Umetoka wapi na umeumia na nini?" aliniuliza.
Nilimuomba kwanza anisaidie chakula na matibabu ya jeraha nililokuwa nalo kisha nitamueleza kilichonisibu.
Alinitoa nje ya kanisa na kunipeleka kwenye jengo moja la ghorofa ambapo alinipa chakula na kunisafisha jeraha ambapo alinitoa risasi moja mwilini".
Nukuu ya jasusi wa Tanzania aliyetekwa nyara na wanajeshi wa Uganda.
Kama
 
Sehemu ya pili

cha ukachero wa kachero wa Tanzania – 2
Habari Zinazoendana
Share
………………………….
WIKI iliyopita tulianza kuchapisha sehemu ya kwanza ya uchambuzi wa kitabu kipya “Mateka Mpakani” kilichoandikwa na kachero wa Tanzania, Frowin Kagauka, kumuenzi mwenzake aliyeuawa mpakani mwa Tanzania na Uganda. Leo tunaendelea na sehemu ya pili.
…………………….
“AMESEMAJE wakati mlipomuuliza juu ya bastola hiyo? Amekubali ni yake lakini amekataa katakata kuwa yeye ni askari wa Idi Amin,” alinijibu Sajin Mkuu wa Kituo.
“OK. Sajin Binda wajulishe Bukoba ili waje kumhoji.” Niliamuru haraka. Sajini Binda alinipigia saluti nami nikaijibu kwa kubana mikono kwa vile sikuvaa sare za kijeshi na baadaye akaondoka haraka.
“Msimtoe humu mahabusu mpaka wakubwa zangu wafike kutoka Bukoba, sawa?” niliagiza. “Sawa afande,” alijibu Sajini ambaye ndiye mkuu wa kituo hicho kidogo cha polisi hapo kijijini Murongo.
Niliondoka hapo kituoni na ilipofika saa sita na nusu mchana nikijua wakubwa zangu watakuwa wanakaribia kufika hapo kituo cha polisi lakini hawakutokea mpaka saa nane na dakika kumi. Walifika kwa gari aina ya Landrover na wote walivalia sare za kijeshi isipokuwa dereva na mtu mwingine mmoja ndiyo walivaa kiraia.
Hao watatu waliovaa kijeshi mmoja alikuwa luteni na wawili makapteni. Waliovaa kiraia niliambiwa ni Luteni Emir wa Idara ya Usalama wa Jeshi ambaye ndiye aliyeendesha gari hiyo na Meja Stephen kutoka Idara ya Usalama wa Taifa mkoani Kagera. Wakuu hao waliamuru Kafumba atolewe mahabusu na alipotolewa wakamchukua na bastola yake kwenda naye Bukoba.
Sikumuona rafiki yangu Kafumba kwa zaidi ya wiki mbili ndipo siku moja bila ya kutarajia nikakutana naye sokoni hapo Murongo akizungumza na yule mpenzi wake.
“Ah! Rafiki wewe ni mbaya, umenipeleka polisi ili nifungwe bila kosa,” alilalamika. “Siyo hivyo, mimi nilishangaa kuona rafiki tangu una bastola na wewe ni bwana shamba. Naogopa sana askari ndiyo niliipeleka bastola yako polisi. Sasa wamekwambiaje?”
“Walinipeleka Bukoba nikaingizwa kwenye nyumba moja sijui ya nani, nikaulizwa maswali mengi ya Uganda na watu wawili ambao hawakuvaa kiaskari. Lakini watu wale walikuwa wema sana hawakunipiga wala kunisumbua na waliporidhika waliniachia nirudi lakini bastola yangu wamebaki nayo,” alinieleza huku akinikazia macho.
“Sawa bwana, basi tutaonana siku nyingine au leo kama bado upo hapa kwetu” nilimjibu kwa unyonge baada ya kuhisi yeye ni jasusi wa Idi Amin na ameweza kuwahadaa wakubwa zangu hadi wakaridhika kumuachia.
Wiki moja baadaye nikaletewa mwaliko kutoka kwa mzee niliyekuwa namheshimu sana, mzee Idris wa Green Hotel nikahudhurie sherehe yake aliyopanga ifanyike Jumamosi kuanzia saa tano asubuhi hapo hapo Green Hotel. Nikamjulisha Koplo Sudi na Sajin Binda juu ya mwaliko huo, kwa hiyo tukaondoka Murongo hadi Kivukoni. Tulipofika Kivukoni kama kawaida tukapanda boti na kuvuka mto Kagera ambao maji yake yanakwenda kasi sana kiasi cha kuwafanya wenyeji kushindwa kuvuka kwa kuogolea.
Baada ya boti kutuvusha tukatembea kwa miguu kilomita mbili na nusu hivi tukafika kijiji cha Kikagati ambacho kwa kweli ni kizuri kidogo kuliko kijiji chetu cha Murongo. Hapo Kikagati kuna kituo kidogo cha polisi ambacho kimejengewa badi tupu chini hadi juu, wengine huita mtindo huo ‘full suit’, vile vile kuna nyumba ya mkuu wa wilaya ambaye wenyewe walimwita DC na jengo moja kubwa la kampuni ya uchimbaji madini inayoitwa BMC.
Ilipotimia saa tano na dakika tano tulikwenda hapo Green Hotel huku tukiwa tumejaa shauku ya kunywa bia na kuvunja mifupa ya nyama ya kuku na mbuzi ya kuchoma. Kwa mshangao hapo Green Hotel hatukuona dalili yoyote ya sherehe na wala hakukuwa an watu wanaokula au kunywa kama ilivyokuwa kawaida. Kkilichonishangaza zaidi ni kutowaona hata watoto wake wakicheza nje ya hoteli hiyo ambayo mwenyewe mzee Idris anaishi humo humo kwenye vyumba vya uwani.
Kabla hajaamua kuuliza alifika mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa kati ya miaka sita na nane ambaye alituambia ameagizwa na mzee Idris atukaribishe ndani tumsubiri. Bila ya hofu tuliongozana na kijana huyo hadi kwenye sebule yam zee Idris ambayo kwa kweli hata siku moja hakuwahi kunikaribisha. Mtoto huyo alitutolea bia tatu za baridi kutoka kwenye hokofu, akatuwekea glasi kisha akaondoka. Dakika kama tano baadaye mzee Idris alifika na kutusalimu lakini hakukaa alituambia ana shughuli itakayochukua kama robo saa hivi lakini alitupa uhuru wa kujichukulia vinywaji kwenye jokofu. Wakati tunaanza kunywa bia huku bado nikitafakari jinsi ya sherehe hiyo tuliyoitiwa ilivyo, ghafla tukasikia mlio wa gari kubwa likisimama nje ya nyumba hiyo, bila shaka wote tulielewa huo ulikuwa ni mlio wa gari la kijeshi maana tulitazamana kwa mshangao.
Kabla hatujahamaki nini kinafanyika tukasikia vishindo vya hatua nzito za viatu vya kijeshi vikiizunguka hoteli hiyo. Tulipotazamana tena bila ya kusema lolote mlango ulifunguliwa na askari sita waliovalia kivita wakiwa na bunduki aina ya AK47 kila mmoja, wakatuzunguka. Moyo ulinilipuka, mate yakanikauka kinywani, bia yote niliiona chungu na balaa tupu.
“Simama juu.” Aliamuru mmoja wa askari hao ambaye alikuwa na cheo cha Sajini. Wote tulisimama huku mikono yetu ikiwa juu kuomba amani. “Songa mbele haraka.” Aliamuru tena. Tulitoka nje ambako tulikuta askari wengine wanane waliovalia kivita wakiwa na bunduki mikononii wameizunguka hoteli hiyo. Raia wa kijiji hicho au niseme kimji hicho walisimama kwa mbali sana wakishuhudia tunavyokuwa MATEKA MPAKANI.
Tuliingizwa katika lori moja la kijeshi aina ya Liaz na safari ya kwenda tusikokujua ikaanza. Tulipofika njia panda ya kwenda Kabale ambayo ipo upande wa kushoto na Mbarara ambayo ipo upande wa kulia, lori hilo lilitimua vumbi kuelekea kushoto yaani Kabale.
Baada ya mwendo wa kama kilomita nne hivi kutoka hapo Kikagati tukaingia katika kambi ndogo ya jeshi inayoitwa Kabiyanda. Tuliteremshwa katika kambi hiyo ndogo na kuingizwa katika kijumba cha mabati matupu ambapo ndani hakukuwa na lolote mbali ya joto na hewa nzito kwa vile hakukuwa na dirisha bali vitundu vidogo vipatavyo sita tu.
“Tunakuwa mateka mpakani, sijui watatufanyaje. Nahisi hizi ni njama za Kafumba, Kafumba lazima ni jasusi, alikuwa anatupeleleza. Sijui Idi Amini ana nia gani na sisi au nchi yetu…niliwaeleza wenzangu huku nikitetemeka. “Ni dhahiri Kafumba amelipiza kisasi. Lakini nahisi mpango huu ulikuwa ni wa muda mrefu,” alijibu Koplo Sudi.
Saa tisa tulitolewa humo kwenye kijumba na kukalishwa chini kwenye uwanja niliohisi ni wa kufanyia kwata. Koplo Sudi na Sajini Binda walikuwa wananitazama mara kwa mara kama vile wananiulaumu kwa kuwaingiza katika janga hili, lakini sio kosa langu bali ni tamaa yetu ya kunywa bia na kumuheshimu mzee Idris.
“Nani mkubwa kati yenu?” aliuliza Luteni mmoja mweusi mwenye sura mbaya. Hakuna aliyejibu hivyo akaona tumemdharau kaamua kumwita koplo mmoja aliyekuwa amesimama kwa mbali akituangalia.
“Funsa adabu hawa” alimwamuru koplo huyo aliyevalia kivita kwa Kiswahili kibaya kisha akaondoka zake kwa hasira.
“Ah! Mnataka ‘kufunswa’ heshima, hebu simameni.” Tuliinuka kwa hofu huku tukimwangalia nini anachodhamiria kutufanyia. “Nyinyi ni askari?” “Hakuna askari hapa kati yetu” nilimjibu haraka kwa hasira. “Eh! Wewe ndiyo mkubwa enh!” “Mkubwa wa nini?” nilimjibu na kumfanya acheke kidogo.
“O.K nyinyi mnajua Kiswahili kingi sana, hebu chuchumaeni chini huku mkishika masikio yenu.” “Tuonyeshe mfano,” nilimwambia bila hofu.
“Eh! Nyinyi jeuri sana, hebu laleni chini kifudifudi niwachape kidogo fimbo,” alitamka huku akitabasamu. Wakati tunalala kifudifudi ghafla alikuja askari mmoja asiye na cheo na kumwambia mwenzake kwamba tunatakiwa tuingie ndani ya gari tupelekwe katika kambi ya Mbarara. Tuliingizwa ndani ya Landrover moja ya jeshi la Idi Amin huku tukilindwa na askari sita waliovalia kivita wakiwa na bunduki aian ya AK 47 mikononi. Landrover ikapigwa moto na safari ya Mbarara ikaanza. Ilibidi turudi tena mpakani Kikagati kisha tufuate barabara inayoelekea Mbarara ni kama kilomita 150. Tulipofika Mbarara giza lilikuwa limekwishaingia, dereva akasimamisha gari nje ya lango kuu la kambi kubwa ya jehsi ambayo baadaye niliitambua inaitwa Simba Battalion. Taa kubwa ya usalama ikawashwa na kuzimwa kama ilivyo kawaida katika kambi nyingi za jeshi kisha sauti kali ilitaka utambulisho.
“Tumeleta mateka kutoka Kabale” alijibu askari mmoja aliyekaa mbele. Taa iliwashwa tena na kuzimwa halafu mlango ukafunguliwa. Niliona sanamu mbili za samba zilizokuwa upande wa kulia na kushoto mwa lango hilo ambazo zilinifanya nielewe maana ya kambi hiyo kuitwa Simba. Gari iliingia na kuegeshwa nje ya jengo dogo ambalo hata mtu asiyekuwa askari angegundua ni mahabusu.
Tuliamriwa kuteremka na mlango wa mahabusu ukafunguliwa, tukaingizwa. Mahabusu hiyo ilikuwa karibu na lundo la kuni na kwa mbele kidogo kulikuwa na msikiti mdogo. Ndani ya mahabusu hiyo hakukuwa na taa kwa hiyo ilibidi tutulie kimya bila kuongea wala kutembea.
Ulikuwa usiku mgumu sana kwetu hasa kwa mimi kiongozi kwa vile wenzangu walionyesha wamekata tamaa kabisa. Kama kawaida ya usiku ni lazima uche hata kama unapata taabu au raha ni lazima asubuhi ifike. Asubuhi ilipofika tulitolewa nje na kupelekwa katika ukumbi mmoja mdogo ambapo tulikalishwa chini. Dakika kama kumi baadaye waliingia wanajeshi wanne, watatu wakiwa na cheo cha meja na mmoja alikuwa kanali. Kwa jinsi walivyoonekana, walikuja kutuhoji.
“O.K Watanzania, tunaanza na wewe, inuka ujibu maswali yetu.” Alitamka kanali huyo huku akimuonyesha kidole Koplo Sudi. Koplo Sudi aliinuka wima huku akigwaya. “Unacho kitambulisho chochote hapo ulipo?” aliuliza meja mmoja ambaye ni mrefu zaidi ya wenzake. “Sina kitambulisho.” “Sawa, vua shati na suruali yako,” aliamuru kanali huyo.
Koplo Sudi akavua suruali na shati lake na kuviweka mbele yake. “Wewe unafanya kazi gani pale Murongo?” aliuliza meja mwingine ambaye ndiye aliyekuwa akinukuu maelezo yetu.
“Nafanya biashara ya kuuza vitabu sokoni,” alijibu Koplo Sudi huku akigwaya.
Ukisema kweli utapona, lakini ukitudanganya ujue hutaiona tena Murongo,” alitamka kanali huyo kwa Kiswahili kizuri. “Kwani sisi tumewakosea nini? Kosa letu ni nini mpaka mnataka kutuhukumu?” “Hamjafanya kosa lolote, lakini tunataka majibu y kweli,” alisisitiza kanali huyo.
“Unajua sisi tunawaelewa nyinyi vizuri sana, na kuonya tena. Usiseme uongo” alifoka kanali. “Sisemi uongo,” alisisitiza Koplo Sudi. “Jina lako nani?” aliuliza kanali huyo mweusi tii. “Abdallah Salum,” alidanganya. “Hatuna jina la Abdallah katika orodha tuliyoletewa.” “Kama mnayo orodha ya majina yetu kwa nini mnaniuliza jina?”
“Nyinyi wote ni wanajeshi, hiyo tunajua kwa hakika, sasa wewe unajifanya mfanyabiashara. Nakwambia mara ya mwisho, sema ukweli wako vinginevyo huwezi kurudi kwenu. Hatupo hapa kufanya mchezo,” alifoka kanali huyo.
“Umeelewa sasa, yajibu maswali yetu kwa ukweli” aliongeza meja anayeandika.
“Jina lako nani na unafanya kazi gani pale Murongo?” aliuliza meja huyo. Swali hilo lilimfanya Koplo Sudi aanze kutoa mchozi ambao uliniumiza sana moyo.
“Unalia kabla hujateswa, sasa ukiteswa si utakufa kabisa” alitamba meja. Maneno hayo hayakupunguza kasi ya machozi ya Koplo Sudi, kwa hiyo kanali akamwambia arudi aka echini.
“Zamu yako wewe, inuka kuja hapa” alitamka kanali huku akinielekezea kidole. Niliinuka nikapiga hatua tatu na kusimama. “Wewe ujibu maswali yetu kwa ukweli, hatutaki uwongo wala kilio hapa.”
“Sawa,” nilijibu kisha nikakohoa kidogo ili kusafisha koo. “Jina lako nani,” aliuliza kanali. “Nelson,” nilijibu. “Jina lako lingine” “Njata, Nelson Njata. “Yah! Jina la Njata lipo hapa” alidakia meja aliyekuwa anaandika. “Unafanya kazi gani pale Murongo?” aliuliza kanali. “Mimi ni bwana shamba.”
“Tunajua ni bwana shamba, lakini una kazi nyingine pale?” alidakia meja mwingine. “Kazi gani nyingine?” niliwauliza bila wasiwasi. “Unamjua Dan Kafumba?” aliuliza kanali na kunifanya nishtuke. “Namjua ni Mganda na pia ni rafiki yangu.” “Nani alimfikisha polisi?” aliuliza kanali huku akinikazia macho.
“Alijipeleka mwenyewe baada ya kupoteza bastola yake.” “Unaonyesha wewe ni mtu jasiri na mjuba, bila shaka wewe ni mwanajeshi, tena mwenye cheo kikubwa au sivyo? Alidakia meja anayeandika.
“Sivyo, mimi ni bwana shamba, hata Kafumba angekuwapo hapa angenisaidia kuwathibitishia.” “Pale Murongo kuna kituo chochote cha jeshi?” aliniuliza kanali. “Mimi sijui na wala sioni umuhimu wa kujua mambo ya jeshi.”
“Naona wewe nmi mwerevu sana kwa hiyo itabidi uhojiwe kwa nguvu, nenda ukakae,” alitamka kanali kwa ukali.
Nilirudi nyuma polepole na kukaa chini. Sasa ilifia zamu ya Sajini Binda kusimama, lakini maofisa hao walinong’ona kidogo kisha ghafla waliinuka na kuondoka zao. Kwa jinsi walivyoonekana walivyokuwa, kwa vyovyote ni maofisa wa Idara ya Ujasusi wa Kijeshi au ni maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa. Kama nusu saa baada ya maofisa hao kuondoka mlango ulifunguliwa na askari mmoja asiye na cheo akiwa amebeba chano iliyokuwa na bakuli tatu zilizokuwa na uji, akatugawia kila mmoja bakuli lake, tukaanza kunywa huku akituangalia.
Uji huo wa unga wa mahindi ulikuwa wa moto sana na haukuwa na sukari, hata hivyo hiyo haikutuzuia kunywa kutokana na njaa tuliyokuwa nayo. Baada ya kama robo saa hivi tulishamaliza kunywa uji huo na askari huyo akachukua bakuli zake na kuondoka.
“Sijui wanataka nini kwetu?” aliuliza Koplo Sudi kwa unyonge. “Hii yote ni kazi ya yule rafiki yangu Kafumba ni lazima ni jasusi wa Idara ya Usalama wa Taifa ya nchi hii yaani State Research Bureau” lakini kwa vyovyote itakavyokuwa asitokee mtu kati yetu akavunja kiapo chetu” nilitamka huku nikiwakazia macho.
Wakati Koplo Sudi anavaa nguo zake alizokuwa amezivua, mlango ulifunguliwa na askari mmoja aliyekuwa na bunduki aina ya AK 47 mgongoni, akatuamuru tutoke nje. Tulipotoka nje tulikuta askari zaidi ya kumi wenye silaha wakitusubiri. Tulipekuliwa kama tuna silaha na walipoona hatuna walitunyang’anya saa zetu na viatu. Baadaye wakatuamuru tuingie katika lori moja aina ya Benz lililoegeshwa mita kama kumi kutoka hapo. Humo ndani ya lori tulifungwa kamba mikononi na miguuni na safari ya tusikokujua ikaanza lakini njiani askari mmoja aliripoka kwa mwenzake kwamba tutafika katika kambi ya Makindye saa kumi na mbili jioni.
Kambi ya Makindye niliwahi kuisikia kutokana na sifa zake za utesaji na uuaji na ni maalumu kwa kutesea mateka wa vita au askari waasi. Kambi hii niliambiwa ni ya Polisi jeshi tupu
 
Back
Top Bottom