Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,398
Filamu; Jason Bourne
Mkurugenzi- Paul Greengrass
Wahusika : Matt Damon, Tommy Lee Jones, Alicia Vikander, Vincent Cassel, Julia Stiles, na Riz Ahmed.
Umri wa kuangalia - kuanzia miaka 12A
Dakika za filamu: 123
Baada ya kupotea kwa miaka karibu tisa katika filamu za Bourne na miaka 12 tangu acheze filamu ya mwisho ya Bourne Supremacy mwaka 2004, Matt Damon amerudi tena na filamu ingine toleo la tano iitwayo Jason Bourne.
Katika filamu hii Bourne anarudi kukumbushia kazi yake ya kutumiwa kama muuaji wa idara maalum ya serikali ambayo inatumia utaratibu maalum wa kuwatengeza wauaji hawa katika maabara zake maalum.
Lakini safari hii Jason Bourne anafahamu wazi kwamba yeye ni nani na ametokea wapi yaani jasusi wa kitengo maalum cha CIA ambacho kina wajibu wa kufanya mauaji maalum na lengo lake ni kutafuta ukweli halisi.
Mkurugenzi wa filamu bwana Greengrass anajaribu kuonyesha siku zote serikali huwa haiaminiki katika kuwatumia waajiriwa wake wa aina ya Jason Bourne na hiyo inadhihirishwa na utoaji siri "security breach" ya kuhusu mpango huo wa kumtengeneza Bourne unaofanywa na mchambuzi wa serikali bi Nicky Parsons (Julia Stiles) mpango unaoitwa “Treadstone".
Lakini lengo halisi na mkurugenzi bwana Greengrass ni kuelezea athari za utoaji siri za ujasusi kama uliofanywa na Edward Snowden ambae alitoa siri za namna taasisi ya ujasusi wa mawasiliano ya NSA na ambayo imepelekea kuwepo na mabadiliko makubwa ya kiutendaji ndani ya vyombo vya usalama vya Marekani au "protocals".
Pia mkurugenzi amejaribu kutofautisha kwa kiasi kikubwa filamu hii na ile ya Bourne Legacy iliyotoka mwaka 2012 kwa kuweka msisitizo shughuli za Bourne katika filamu nzima na kuifanya iwe ya kusisimua.
Pia wakiwa mjini Athens, Jason na bi Stiles wanakimbizwa na muuaji (Cassel) ambae anahangaika kutafuta kuwalenga risasi vizuri huku akiruka kutoka jengo moja kwenda jingine panakaribia kufanana na kitendo cha Tangier ambae alikuwa kifanya hivyo katika filamu ya Bourne Ultimatum.
Kuna mji wa Las Vegas ambako mzee Dewey (amecheza Tommy Lee Jones) ambae anajua siri ya Jason Bourne, anahangaika hotelini kupata mawasiliano ya mambo jinsi yanavyokwenda na kukumbushia mzee Brian Cox kwenye filamu ya Legacy ambae alikuwa mjini Berlin.
Pia Jason anaendelea kusakwa katika mji wa London na vyombo vya usalama vikiwa vinatumia nyenzo zote zilizo muhimu CCTV, satellite na ufuatiliaji wa mawasiliano ya simu kwa kila simu anayotumia.
Jason Bourne anaonekana kuhangaika na kumbukumbu za wapi mambo ambayo amekuwa akiyafanya na pia mihangaiko yake katika miji ya Athens London na Vegas ambapo anakuwa anafukuzana na wale waliotumwa kummaliza.
Yupo mwanadada Heather Lee ambae anacheza kama Alicia Vikander akiwa kuruta mpya wa CIA anapewa jukumu la kuhakikisha Jason Bourne anakamatwa akiwa hai. Pia anaonyeshwa kuwa ni mtu tofauti kabisa na Edward Snowden katika kutunza siri.
Lakini bado inaonekana amekosekana mwanamama Joan Allen ambae alicheza kwenye nafasi ya Vikander ya kuhakikisha Jason Bourne amekamatwa akiwa hai. Huyu mwanamama alikuwa ni mtulivu na asie na papara kumlinganisha na Vikander.
Kazi ya kumtafuta na kumkamata Jason Bourne si kazi ndogo na ambayo siku zote inataka kuiridhisha hadhira na pia kuhakikisha kazi hiyo inakamilishwa katika uda uliopangwa.
Lakini ni filamu nzuri na yenye kusisimua katika muda wote wa dakika 123.
Filamu hii inatarajiwa kuingiza kiasi cha dola za kimarekani kati ya 50-60 milioni katika kumbi 4025 za nchini Marekani pekee katika onyesho lake la kwanza mwishoni wa wiki..
Vyanzo vya uchambuzi huu: The Teleghraph, New York times, Wikipedia.