Japokua nampenda lakini ukewenza sikubali...

Asabaya

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
1,310
414
Babari zenu waungwana,
Kwamasitiko makubwa sana naandika haya,mimi ni mama wa watoto 2 tumeishi na mumewangu kwa dhiki kiasi ambacho hata hela ya kodi nalipa
Mimi na haikunikera nilijua kua ipo siku mumewangu atafanikisha,nilikua kipenzi cha wazazi wake mpaka mawifi mungu akajalia nikapata uwezo
Wakujenga nyumba tuka hamia, wazazi wangu walikua wanaishi nchi za nje nilikwenda kuwaona wakati wa kujifungua ili wanangu wawe raia
Nikaongea na mzee iliamchukue mumewangu sababu maisha ni mwanamme kufanya kazi kweli wazazi wakamchukua baada ya mda kapata
Urai wa kigeni akapata kazi mambo yakawa safi, nikaondoka TZ ili kuishi na mumewangu tukawa sote mambo alhamdulillah,
Nikaona kwanini nisimchukue mkwe wangu aje atutembele nikafanya matayarisho yote mama mkwe akaja sikujua kumbe alikua ndio adui

Baada ya kuondoka kurudi TZ ndio alipo aanza kumwambia mumewangu yeye hana radhi nae kama hajaoa mtoto wa kaka yake
Na family yetu wote ni watu wanaojiweza kwahiyo mwanawe anaonekana kama mende wa chooni, kilicho ni kera ni mumewangu
Kukubali anavyotaka mama yake na anasema mimi mke ntamuoa lakini sito lalanae nafanya kumridhisha MAMA.
Yani nimekosa hata lakusema kwakweli sijawahi kumuona mumewangu na uzinzi wa aina yoyote na tuna furaha sikuzote
Sijawahi kumjibu kitu ambacho kitamfanya ajione sio mwanamme lakini huyu mama sumu aloniwekea ndani ya familia yangu
Sitokaa nimsahau na chazaidi anamwambia mwanawe tena kuanzia sasa mali utakazo nunua nisikusikie kumuandikia huyo

Alokufanya Ndondocha manake kila kitu Wangu hivi, wangu unaonaje, wangu nifanyeje? Wangu ni jina ambalo anapenda
Kuniiita, sasa waungwana nilicho mwambia ni kwamba mimi nakupenda na daima ntakupenda mumewangu ila sitopenda
Uwe na mke wapili Yes dini imesema unahaki ya hata 4 lakini mbona sijawaona kukushobokea wakati apeche na hao
Walikua wanamsema maneno kibao ya kejeli mpaka analia na mwisho walifikia kumwambia kua yeye hana mbele wala
Nyuma kama mche wa sabauni ya mbuni, leo kasahau? Kwaupande wangu waungwana naona moyo wa uvumilivu
Utanishinda nasubiri hatima lakini moyo unaniuma sijui nifanyeje…...
 
Pole sana dada, wanaume wengine sijui wakoje,sasa atamuoa lakini halali nae ndio kafanya nini? au anashindwa kumueleza mama yake ukweli kama anakosa wallahi inauma na inakera lakini vuta subra na Inshallah yataishi mtakua na masikizano na mumeo.
 
Asabaya,

Inasikitisha sana hasa baada ya wewe kujua kuwa, the bad animal of the issue is your mother inlaw....

Mumeo nae kasahau kabisa alikotoka!!! acha aendelee kukutenda naye muda si mrefu BWANA atamtenda kwani malipo ni hapa hapa.

Vipi ukimuuliza kilichopungua kwako ambacho huyo binamuye anacho ni nini, anajibuje???

Ama kweli ilisemwa, "laki si pesa milioni uadui"... Endelea kumlilia Mola kwake hakuna lisilowezekana.
 
Pole sana

Mwenzako anatimiza sunnah!
Ahsante,
Inshallah kheir, Nnaimani hakuna dhiki wa dhiki,na wala sijakata lakini kwanini awe jamaa yake na huyu mwanamke Leo kasahau nilipo mtoa mwanawe?
 
Pole sana bidada,i can imagine your pain
Ahsante sio Siri shoga inaniuma ndani ya Moyo ukizingatia Sina mama wakumpa machungu yangu,yey ndio nilimpenda zaidi baada ya kufariki mama,lakini sawa Alivyofanya labda anajua Huyo mtoto wa ndugu yake ndio atampenda zaidi yangu...
 
pole sana dada, kufika peponi ni vigumu sana, kwani dini yako si inaruhusu mumeo aoe akiweza mpaka muwe wanne? huyu mmoja tu asikukoseshe raha, mshauri mumeo aoe wawili kwa mpigo, halafu usifikiri wenzio roho haziwaumi unavyo warusha roho na mr. wako, mswalie mtume, kubaliana na matokeo. kumbuka huyo mama ndo aliyemzaa huyo mumeo hivyo basi anapaswa kumtii. manake sijui utajenga utetezi wako kwa kuegemea dini au historia ya maisha yenu uone kama kwa mtume inaswihi. kwa ajili ya mzoga fisi alisema uislamu mgumu wewe wasemaje fisi alikuwa sahihi ama hakuwa?
 
Mchawi wako ni mmeo ndio kakugeuka japo waweza usiamini,
ye ndio kaendekeza tamaa zake na kukosa shukrani halafu kaamua amtumie mama ake kama kafara ya ubaya wake,
 
Hapo mbaya wako ni imani maana inamruhusu hivyo okoka na Yesu atakutendea maajabu
 
Na kuoa wake 4 pia iwe na sababu ya msingi au kuwe na tatizo, hainamana unaenda kuoa sababu eti mama kasema angenambia anao kampenda mkeo wala Sina Shaka ningeamua kukaa au kuondoka,lakini sio sababu mama kasema,Mimi pia ni mama na sitokaa nimuingilie mtoto wangu kwenye maisha yake ya ndoa labda kuwena tatizo na pia ajekunielezea Kama hakunambia pia ntakaakimnya.
 
Hapo mbaya wako ni imani maana inamruhusu hivyo okoka na Yesu atakutendea maajabu

mtoto tuliaa weeweee sisi tumemchagua wewe, ukitaka utamuoa usipotaka utamuoaa, sawa nitamuoa yeye ila sinto LALA NA YEYE, NITAMUOAAA ILI NIMRIDHISHE MAAMAAA.... "SIJUI TUMUITE MKE WA MAMA AU WA MUMEO. POLE DADA, LEO NTAKUJUMUISHA KATIKA MAOMBI ILI BWANA MUNGU AKUEPUSHE. NA UKEWENZA.
 
Mchawi wako ni mmeo ndio kakugeuka japo waweza usiamini,
ye ndio kaendekeza tamaa zake na kukosa shukrani halafu kaamua amtumie mama ake kama kafara ya ubaya wake,

Inawezekana kua kweli kwani binadamu anasiri kubwa moyoni lakini inshallah ntaujua ukweli.
 
mama mkwe ndo walivyo

Yani siamini masikio yangu huyu mama nilikua nampenda Sanaa,yani nikimkumbuka sichanganyi yani Lu iota mwanangu mwanangu yote ulikua ufisadi wake,lakini mwenyezi mungu yupo na yeye pia watoto anao..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom