masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,171
Tanganyika si shamba la bibi!Wanabodi,
Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa nchi mbili mbili, iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na Jamhuri ya Tanganyika, zikaunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo baadaye Tanyanyika ukauliwa kinyemela na kuunda jina la Tanzania.
Muungano huu umeleta mataifa mawili yenye haki sawa na hadhi sawa ndani ya muungano. Moja ya taasisi kubwa kabisa za Muungano ni taasisi ya urais, "presidential institution" ambayo inapaswa kushikwa kwa kupokezana baina ya Tanganyika na Zanzibar.
Japo hakuna utaratibu rasmi wa kupokezana kikatiba, bali busara ya kawaida imekuwa ikitumika kwenye hili, kwa rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, baada ya kutawala kwa miaka 23, alijenga mazingira kwa rais atakayemfuata atoke Zanzibar, na hili lilifanyika kwa rais Ali Hasssan Mwinyi kumpokea Kambarage!.
Mwinyi alipomaliza muda wake, masingira yale yale ya kupokezana yalifanyika na akaingia Benjamin Mkapa kutoka bara.
Kipindi chote cha Mkapa ilijulikana atafuatiwa na mtu kutoka Zanzibar, na mtu mwenyewe alijulikana fika!, na kwa wanaojua mambo ya ndani, jikoni au chumbani, uvunguni kabisa wanajua kilichotokea, labda niwadokezee kidogo tuu toka kwa huyu mwana jf mwenzetu. Mkuu Utaki Unaacha, katika uzi wake huu JK, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza .. amesema na hapa ninamnukuu
Hivi ndivyo zamu ya Zanzibar ilivyopokwa!.
Hivyo sasa kuelekea 2015, japo haijaandikwa popote, lakini tukubali, tukatae, Japo Hakuna Kupokezana!, Kiukweli, KiHaki, Kihalali na Ki Muungano, 2015 Ni Zamu ya Zanzibar!.
CCM has a duty kuteua Wanzanzibar wenye sifa, uwezo na kukubalika kwa urais wa JMT mmoja wapo ni Dr. Ali Mohamed Shein, tena huyu ni mtu asiye na makuu, mpole, mnyenyekevu, mstahilivu, muadilifu, asiye na makundi na mwenye uwezo wa kudumisha muungano.
Akipendekezwa yeye, ata defuse makundi yote na migawanyiko yote ndani ya CCM!, CCM itakuwa ni moja stronger than ever!.
Tatizo litabaki ni kama wapinzani wataweza kuungana na kum field mgombea mmoja, na itokee awe ni Mkristo!.
Baadhi wa Wakristo walioko CCM ambao walikumbwa sumu ya udini wa dhana ya urais ni kupokezana kati ya Mkristo na Muislamu, wataona this time CCM has not been fair kwa dini yao, baada ya Muislamu, wamewaletea tena Muislamu!, watampiga chini na CCM yake!. Ikitokea CCM isimsimamishe Mzanzibari, then the only reason ni kitisho hiki!.
Nauliza, Jee CCM itawatendea haki Watanzania kwa kuwasimamishia mgombea kutoka Zanzibar?! au itaendelea kupandikiza sumu ya udini kwa ku bow down kwenye the fact and fallacy ya zamu za kupokezana kwa dini?!.
Is in not Kiukweli kabisa, Kihaki kabisa, Kihalali kabisa na kwa lengo la kudumisha, Muungano, 2015 ni Zamu halali ya Zanzibar kutupatia Rais wa JMT?!.
Pasco
Kutawala Tanganyika tuachieni wenye nchi, nchi yenu Zanzibar jikiteni huko.
Ni kama unataka zamu ya kuingia unyumba na mke wa mtu.