Japan yaipa Tanzania mabilioni ya chakula

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,108
Serikali ya Japan imesaini makubaliano ya kuipatia Tanzania msaada wa Sh. bilioni 14 zitakazotumika kununulia mchele kutoka Japan ili kukabiliana na upungufu wa chakula uliosababishwa na ukosefu wa mvua msimu uliopita.
Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo, ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Balozi wa Japan nchini, Hiroshi Nakagawa, aliiwakilisha serikali ya nchi yake, wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi, Ramadhan Khijjah, aliiwakilisha serikali ya Tanzania.
Khijjah alisema msaada huo utasaidia mambo mbalimbali, ikiwamo kuongeza chakula nchini.
Vilevile, alisema fedha zitakazopatikana katika mauzo ya mchele huo baada ya serikali kuununua, zitapelekwa katika kilimo cha umwagiliaji. Naye Balozi Nakagawa alisema msaada huo ni sehemu ya misaada, ambayo serikali ya nchi yake inaipa kipaumbele cha kwanza katika maendeleo ya Tanzania.
Alisema lengo kubwa la Japan kutoa misaada hiyo kwa Tanzania ni kupunguza umaskini na kukuza uchumi, hasa katika maeneo ya kilimo na maendeleo vijijini.




CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom