January, Zitto live TBC1 wakizungumzia hoja binafsi

Habari za kutoka ndani ya CCM zinasema J. Makamba na Zitto Kabwe wametwa na kutishiwa kuachana na misimamo yao ya kutaa posho ya vikao vya wabunge. Habari zinasema wameambiwa wanafanya mchezo huo wa kuigiza kwa kuwa wao hawahitaji fedha hizo kutokana na uwezo wa kifedha walionao kutokana na vitega uchumi walivyo navyo. Mtoa habari alisema wakiendelea na usanii huo mambo yao yanaweza kuwekwa hadharani.

Hiyo ndo ccm, kutishiana badala ya kutumia muda wao kujadili mambo ya msingi ni upuuzi. kama wanavitega uchumi vya kutosha posho wanataka za nini, si bora wawape madaktari kupunguza vifo huko muhimbili
 
hamna hiyo kitu....hajatishwa nafikiri zito akipta muda atajitokeza kujibu menyewe...sema wamemtisha makamba...galanosi
 
tuuze jengo la bunge tuwalipe madakatari na walimu, hivi wabunge wanatusaidia nini hasa? wawepo wasiwepo yote sawa, SIASA ZA TANZANIA NI BIASHARA, hivi mbona wenzetu KENYA wanatushinda kwa kuwa na misingi imara ya uelewa wa kidemokrasia na elimu ya uraia, WATANZANIA TUMELAANIWA
 
Mh Zitto Kabwe amewadanganya vijana wa kitanzania,baada ya kuwaahidi kuwa atapeleka bungeni hoja binafsi kuhusu tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekuwa ni disaster kwa sasa..badala yake amesikika akipeleka hoja binafsi ya mambo ya kilimo cha mkonge na kupuuzia ile hoja ya ajira kwa vijana aliyowahaidi kupitia chombo kimoja cha redio hapa Tanzania..

Namuomba Zitto na wanasiasa wengine vijana msiwatumie vijana wenzenu kwa maslahi yenu binafsi,kama mmeshindwa kuwapigania basi waacheni waendelee ku-hustle kimpango wao msijifanye mnaumizwa sana na matatizo yao ikifika suala la kuwawakilisha inakuwa usanii mtupu..vijana ni waelevu wanausoma tu mchezo.

Akili yako ni utumbo kweli, hakuna kitu ambacho kitaongeza ajira kwa watanzania kama kufufua zao la mkonge, strategy aliyoitumia zitto na mahususi kabisa ikilenga eneo la uzalishaji wa mkonge ambao utatoa ajira za kutosha mashambani, viwandani na katika sekta ya nishati kupitia mkonge. Ameleta hoja ya kuinua ajira kimkakati zaidi badala ya kuwa kama lowassa unalalamika kuwa ajira kwa vijana ni bomu lakini husemi tuanawezaje kutengeneza ajira mpya.
 
Mh Zitto Kabwe amewadanganya vijana wa kitanzania,baada ya kuwaahidi kuwa atapeleka bungeni hoja binafsi kuhusu tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekuwa ni disaster kwa sasa..badala yake amesikika akipeleka hoja binafsi ya mambo ya kilimo cha mkonge na kupuuzia ile hoja ya ajira kwa vijana aliyowahaidi kupitia chombo kimoja cha redio hapa Tanzania..

Namuomba Zitto na wanasiasa wengine vijana msiwatumie vijana wenzenu kwa maslahi yenu binafsi,kama mmeshindwa kuwapigania basi waacheni waendelee ku-hustle kimpango wao msijifanye mnaumizwa sana na matatizo yao ikifika suala la kuwawakilisha inakuwa usanii mtupu..vijana ni waelevu wanausoma tu mchezo.

Mkuu hizo ni ajira,udanganyifu upo wapi?
 
Ama kweli CCM inajilisha sumu yenyewe, taratiiibu uhai wake unaondoka. Juzi wamegomea maslahi ya madaktari; leo wanapitisha nyongeza ya posho za wabunge.........

Mwisho wa siku, January na Zitto wanachokipata ni heshima kubwa mbele ya umma, which matters the most. Serikali au Bunge kuwaona vinginevyo, should not shake them at all. Kazi nzuri vijana.

Mchambuzi upo sahihi kabisa yaani serikali inazidi kujitiz kitanzi shingoni. Hivi kama hali ni ngumu si tushee wote? Hii nchi kila mwananchi ni partner hivyo tunatakiwa kushare loss/profit kwa pamoja hata kama ratio zitatofautiana lakini siyo kihivyo.

nadhani Ntamaholo amekujibu hiyo hoja yako.una swali la nyongeza kuhusu Zitto?
 
Habari za kutoka ndani ya CCM zinasema J. Makamba na Zitto Kabwe wametwa na kutishiwa kuachana na misimamo yao ya kutaa posho ya vikao vya wabunge. Habari zinasema wameambiwa wanafanya mchezo huo wa kuigiza kwa kuwa wao hawahitaji fedha hizo kutokana na uwezo wa kifedha walionao kutokana na vitega uchumi walivyo navyo. Mtoa habari alisema wakiendelea na usanii huo mambo yao yanaweza kuwekwa hadharani.

Uwe unaweka habari timilifu sio unaandika haraka haraka km unaenda msalani. Zitto atatishwaje na CCM wakati yeye sio mbunge wa chama hicho ?. Hebu lete ufafanuzi juu ya hili kwani hujaeleweka

Back
Top Bottom