January Makamba na Nape Nnauye on Jenerali Ulimwengu on Monday

Nimeamini magamba ni magamba tu hawa jamaa wanashindwa kujieleza kabisa!
 
Nape anasema kuruhusu mgombea binafsi ni pigo kwa vyama vya upinzani.
 
Nape anadai kuwa anaichukia Rushwa, ni sawa lakini huwezi kuutenganisha uchaguzi wowote uwe wa ndani au nje ya CCM na vitendo vya Rushwa. Naona Nape anapaza sauti but what matters is not the voice but the point!!!!!

Akianza kuongea Nape napunguza sauti ya TV hadi moja but sauti iko juu balaa!!!
 
Jenerali anauliza maswali mazuri sana lakini anaangushwa na Nape na Januari, hawayatendei haki maswali hayo!
 
Hahaha nape anasema hapendi kuwataja chadema lakini bado anawataja
 
Wanapiga pambio tu hakuna kitu wanajilambalamba tu hakuna anayeweza kujibu maswali kiufasaha. Watoto wa Juzi hata CCM yenyewe hawaijui ilikotokea..
 
Nape,Anasema wamepanga kudhibiti rushwa kwa wagombea wa nafasi mbalimbali!

Hivi ssm inadhibiti rushwa au inapalilia na kulinda watoa rushwa wakati wa uchaguzi?
 
Swali langu kuhusu sera nzuri kwa maendeleo ya taifa...(Serikali ya majimbo) kwa nini tusifanyie utafiti?pia nafasi za wakuu wa wilaya na wakuu mikoa!kwa nini ccm wasichukue sera nzuri hata kama si zao kwa maendeleo ya taifa??
 
Hawa wanaopiga cm wanaipenda sana ccm but hawasikilizwi na hapo ndo mwisho waccm unapokuwa
 
Sijaona krimu ya majibu niliyotaraji kuyasikia kutoka kwa Nape na Januari,
Mr Jenerali anawauliza maswali ya musingi na mazito lakini aina ya ujibuji ni upuuzi mtupu!
 
The look on Jenerali's face tells a lot! kashamaliza kipindi zamaaani kwa sababu wanakwepa sana maswali,hawatoi majibu ya msingi. Kawaachia tu wabwabwaje mpaka kipindi kiishe.
 
Kweli nape anajibu kilahisi sana, na anaposema rushwa ni tatizo la kidunia anamaanisha kuwa ccm imeshindwa kudhibiti?
 
Nape, Nape, Nape........ Unazungumzia mabadiliko ya kimazingira ukihusiha na chama alichokiacha Baba wa taifa! Cjaelewa kitu hapa cjui ana maanisha nini!
 
The look on Jenerali's face tells a lot! kashamaliza kipindi zamaaani kwa sababu wanakwepa sana maswali,hawatoi majibu ya msingi. Kawaachia tu wabwabwaje mpaka kipindi kiishe.

definately indeed. Alidhani angepata majibu yenye upeo na kizalendo matokeo yake amepata VUMBI NA MOSHI WA KIJANI.
 
Jenerali ni kiboko hawa jamaa confidence kwisha kabisa,,,halafu kuhusu rusha makamba usijidanganye wewe ulimwaga pesa kupata jimbo la bumbuli..bisha
 
Naona Nape anatoka povu tu,nadhani amekuja kwenye huo mjadala bila kujiandaa na hajui anachokiongea,hajajibu swali hata moja.huyu kijana nimemuondolea hata heshima kidogo niliyoukwa nayo kwake. Anadai ccm hii haiwezi kuwa sawa na ya mwalimu.!!!
 
Afadhali kipindi kimeisha kumbe january nae kilaza kama nape tu! Hakuna jinsi ccm inakufa vijana wenyewe ni hawa!
 
Back
Top Bottom