January Makamba kukopa $10 mil. kwa ajili ya Bumbuli

Unachanganya mambo, yeye anakopa Wall street na ata-invest East Africa, dividends atapewa kutokana na investment zake hapa EA ambapo anatakiwa atumie sehemu ya hizo ku-service mkopo. sasa swala matumizi linatokea wapi? yeye atapewa dola 700, 000 wakati costs zimeshakatwa. Issue hapa ni kwamba January kasoma history, peace and conflicts management haya mambo ya investment analysis yamempita mbali, lakini poa kaweza kuwadanganya wenzake wa bumbuli huko wamempa shavu, lakini huo upupu wake wa kutaka kuwa Rais wetu kwa mipango hewa kama hii aishie hukohuko bumbuli!
Kama mtu alivyosema hapo juu the article is too general.Dola milioni10, kulipa kwa miaka 10 kwa gawio la dola 700,000 kama ni kosa JM asingeshindwa kuliona.Nime assume ana kopa kama kampuni,hiyo kampuni ndiyo itakayompa devidends.
 
Nadhani Tanzania inahitaji dreamers, who dream big and differently kama January Makamba. Mikopo imekuwapo tangu enzi za uhuru, serikali yetu imekopa ila matumizi yake yamekua ya anasa na yakifisadi kama kununulia rada mbovu au mitambo ya richmond. Ila tofauti yake huu mkopo sasa utakuwa rahisi kuu-manage kwa kuwa umekuwa specified kwa jimbo na uko wazi. Tukumbuke kuwa amedhamiria kukopa kutoka kwa 'philanthropists' hivyo tutegemee mkopo wenye riba nafuu au usio na riba kabisa. Nadhani Makamba anatoa changamoto kwa wabunge wengine vijana kama Halima Mdee, Mr. Sugu, Mnyika, Zitto kuondokana na namna zilezile na kubuni namna mpya ya kupata mitaji na kushughulikia kero za wapiga kura wao. Ingawa yupo chama cha mafisadi lakini mawazo yake si mgando! Mh. Mnyika akija na ubunifu kama huo kwa kuongea na donors na investors na kuweza kuwapatia wanaubungo maji safi na salama kwa 100% ana uhakika tutamchagua tena!
 
Mimi jamani concern yangu ni moja tu, embu tu-assume wazo lake ni zuri, hivi COLATERAL SECURITY ya huu mkopo ni nini?....January anataka kuwauza watu wa bumbuli eeh? yasije yakajirudia mambo ya Chief Mangungu wa usagara alivyowauza watu wake kwa Karl Peters!

Hahitaji colateral yeyote. Atawa- threat tu wampe mkopo. Hujui January Makamba aka Ernesto Sheka ni bingwa wa kutisha watu (remember threats to Lisa Rockefeller.) Akishindikana atawaambia ameahidiwa uwaziri na Baba yake (yule pimbi katibu mkuu wa CCM.) Nafikiri hio itawalainisha na mkopo watatoa :smile:
 
Hahitaji colateral yeyote. Atawa- threat tu wampe mkopo. Hujui January Makamba aka Ernesto Sheka ni bingwa wa kutisha watu (remember threats to Lisa Rockefeller.) Akishindikana atawaambia ameahidiwa uwaziri na Baba yake (yule pimbi katibu mkuu wa CCM.) Nafikiri hio itawalainisha na mkopo watatoa :smile:
ha haaa haaaa haaaa hee heeeeeheeeee eeeeeharafu huyu jamaa atakuwa ni primitive sana
 
Mimi jamani concern yangu ni moja tu, embu tu-assume wazo lake ni zuri, hivi COLATERAL SECURITY ya huu mkopo ni nini?....January anataka kuwauza watu wa bumbuli eeh? yasije yakajirudia mambo ya Chief Mangungu wa usagara alivyowauza watu wake kwa Karl Peters!

slide-2.png




Bumbuli is among Tanzania's most densely populated constituencies. Most of its people farm tiny plots too small to be subdivided further. But Mr Makamba has a plan. He wants to borrow $10m from Wall Street philanthropists, to be repaid in ten years. The sum, he says, will be invested in east African treasury bonds and stocks, in the hope of dividends producing $700,000 a year to invest in Bumbuli.

http://www.economist.com/node/17369767


WEBSITE YA BUMBULI.ORG imekufa

january team yako ishaanza kuwa sleki vipi?
 
Anayekopa ni nani? Bumbuli au January?

Naomba mnifahamishe ili niweze ku comment
 
Huyu January anapenda kuongea ongea tu ili apate umaarufu kama vile ana akili nzuri za kubuni, tatizo la mkopo si kupata ni vipi utawafanya wanaokukopesha wukubali mradi wako, vipi utaweza lipa huo mkopo, yeye sasa anaongelea mkopo tu lakini hatujui ataurudisha vipi na watu wake pia wae wamefaidika, bora afanye kwanza alafu azungumzie siyo kuwataka kuwateka watu wake kisaikologia kuwafanya wamepata mbunge shupafu.
 
Moja ya mikakati ya January Makamba ni kwenda kukopa karibu $10 milioni kwa ajili ya kuikomboa Bumbuli. Sasa hii ndio kazi ya Mbunge kweli? Au ndio mwanzo wa kuuza jimbo lake kwa Wall Street Philanthropists?

Tanzania's election: Promises, promises | The Economist


Huyu mheshimiwa mwaka 2010 alipokuwa akijipigia debe kupitia the Economist aliahidi kuleta malori yenye Friji kupooza matunda ya wapigakura wake kuyapeleka sokoni.

Hilo hajalifanya sasa huku kukopa ni nani mdhamini na urudishaji wa mkopo ukoje na kwa riba ya kiasi gani na kwa muda gani.

Huku anataka uraisi huku jimboni ni hakuna alichofanya umasikini unashamiri hii kama siyo laana sijui ni nini!

Inatosha kusema hana mamlaka kama mbunge kukopa kwa niaba ya jimbo la Bumbuli. Kuwategemea wageni kwa kuwauza wapigakura ni uthibitisho kafilisika kimawazo.

Nchi deni limekuwa hivi badala ya kuja na mikakati ya kulilipa yeye anatafuta namna ya kutubebesha zigo zito zaidi la madeni.

Hakuna wa kununua bonds au hisa kwa kampuni hewa huu ni utapeli usio na kifani.
 
Sina hakika una maana gani kwenye neno kukomaa. Lakini kama una maana ya umri, ndio, nimekomaa. Umri uliowekwa kwenye Katiba ya nchi yetu kwa nafasi ya Urais ni miaka 40 ambao nimeshaupita. Kuna nchi kubwa kama vile Marekani wameweka miaka 35.

Mwaka huu ninafikisha miaka 41, na kwa umri huu, nina umri mkubwa zaidi ya asilimia 85 ya Watanzania. Waasisi wa taifa letu walioweka umri wa miaka 40 kama kigezo cha Urais kwenye Katiba walikuwa na busara ya kuona kwamba umri huo ni umri wa mtu mzima aliyekomaa.

Kama una maana ya kukomaa kwa maana ya kuzifahamu kero za Watanzania na uwezo wa kuzipatia majawabu, jibu pia ni ndio, nimekomaa. Na tena sio kuyafahamu majawabu ya siku zote bali maarifa mapya yanayoendana na karne hii mpya. Kama ni kukomaa kwa maana ya kuwepo kwenye siasa kwa miaka mingi, sina hakika Watanzania wanatafuta kiongozi ambaye kwa miaka 40 ameshiriki kuuweka mfumo tunaoulalamikia.

Watanzania hawatafuti mwanasiasa mkongwe kuwaongoza, wanatafuta kiongozi mahiri na mwadilifu wa zama mpya.

Kama ni kukomaa kwa maana ya nafasi za uongozi nilizoshika, jibu pia ni ndio, nafasi hizo zimenikomaza: nimefanya kazi jikoni kabisa Ikulu, nikimsaidia Rais; nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati muhimu ya Bunge ya Nishati na Madini; nimekuwa kwenye Sekretarieti ya Chama chetu kama Mkuu wa Idara ya Siasa na Mambo ya Nje ya CCM; nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM; pia nimekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa; nimekuwa Mbunge na nimekuwa ndani ya Serikali. Naijua Serikali na uendeshaji wake vizuri sana. Nakijua Chama chetu vizuri sana.

Kama ni kukomaa kwa maana ya busara, hekima na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, jibu pia ni ndio, nimekomaa. Sina rekodi ya kuropoka, kutukana, kuhamaki, kushambuliana na watu na kufanya maamuzi ya papara. Najua uzito wa dhamana ya uongozi. Watanzania wengi ninaokutana nao wanataka nchi yetu ifungue ukurasa mpya.

Ukomavu wa kiongozi haupo kwenye umri wake bali kwenye maarifa yake na busara zake na malezi yake na uadilifu na uzalendo wake. Historia inaonyesha kwamba uwezo wa uthubutu hautokani na umri mkubwa wala uzoefu mrefu kwenye siasa. Na ukweli ni kwamba kwa kadri unapokuwa kwenye system miaka mingi ndipo mazoea ya kufanya uliyozoea unapunguza uthubutu wa kufanya mambo mapya na hivyo kupunguza uwezekano wa kufanya mabadiliko makubwa. Wakati wazee wanamchagua Mwalimu Julius Nyerere kuwa Rais wa TANU mwaka 1954 ili aongoze harakati za uhuru, ambazo ni ngumu na hatari kuliko hata uongozi wa nchi, ukomavu wake haukutazamwa kwenye umri wake mdogo wa miaka 32. Wakati Tony Blair anachaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa taifa kubwa la Uingereza, akiwa na miaka 43 tu, na akiwa hajawahi kushika nafasi yoyote ya uongozi Serikali, hata Unaibu Waziri, ukomavu wake haukutizamwa kutokana na umri wake au uzoefu wake kwenye siasa. Wakati Rais Obama anagombea alikuwa Mbunge kwa miaka mitatu tu na kulikuwa na maneno mengi pia kwamba hajakomaa. Lakini wananchi waliona anatosha. Mifano ipo mingi sana. Cha msingi ni kwamba wenye kuamua kiongozi awe nani ni Watanzania wenyewe kwa msaada wa Mungu.

Jingine ninaloweza kusema ni kwamba hakuna kazi yoyote inayomuandaa au kumkomaza mtu kuwa Rais wa Tanzania. Kuna watu wanne tu hapa Tanzania ambao tunaweza kusema kuwa wana uzoefu wa Urais: Mwalimu Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin William Mkapa, na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kinachomfanya mtu awe tayari ni makuzi yake, maadili yake, busara yake, hekima zake, dira yake pamoja na vipaji na talanta na karama alizojaliwa na Mungu.

Kama nilivyosema, Watanzania wanataka kiongozi mahiri na sio mwanasiasa mkongwe. Wanataka kiongozi atakayefanya maamuzi, lakini atakayefanya maamuzi makini. Wanataka kiongozi mwadilifu.

Unaweza ukawa na umri wa miaka 40 na ukawa na ukomavu na hekima na busara na vipaji vya kufanya maamuzi makini na unaweza ukawa ndani ya siasa kwa miaka 40 na ukafanya maamuzi ya papara. Ushahidi tunauona kila siku.

Umeuliza pia kuhusu Shirika la Maendeleo Bumbuli au BDC. Moja ya sababu zangu za kuingia kwenye siasa ni kuleta ubunifu katika kutatua kero za wananchi. Kwa mfumo wa utawala na maendeleo wa nchi yetu, Serikali bado ina mkono mkubwa kwenye kuleta maendeleo ya watu. Kwa kutambua kwamba mchango na jitihada za Serikali pekee hazitoshi kusukuma maendeleo kwa kasi ambayo mimi naipenda, niliamua kutengeneza utaratibu wa ziada wa kusukuma maendeleo ya watu wa Bumbuli. Kwanza, nilifanya utafiti wa kina juu ya changamoto zilizopo na sababu zake, kisha tukafanya uchambuzi wa baadhi ya changamoto ambazo Serikali inaziweza na nyingine ambazo Serikali haina uwezo wa kuzitatua. Tukaanzisha Shirika la Maendeleo Bumbuli kwa ajili ya kusukuma shughuli za maendeleo kwa kasi zaidi. Falsafa yetu ni kuwezesha na kuvutia biashara zitakazoongeza chachu ya uwekezaji na mzunguko wa fedha jimboni, kutoa ushawishi, huduma, ushauri na msaada kwa watu wengine wanaotaka kuwekeza Bumbuli, na kutafuta na kuunganisha wabia wa maendeleo katika jimbo la Bumbuli, na kufanya shughuli nyingine za kijamii.

Shirika hili nililianzisha kwa mtaji wa fedha yangu ya mfukoni ambayo ilikuwa ni mkopo wa magari ya Wabunge. Tumefanikiwa sana kwenye mambo kadhaa lakini pia tumekabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo fedha za uendeshaji wa shughuli zetu. Kwa kiasi kikubwa bado natumia fedha zangu kusaidia shughuli za Shirika. Tulitegemea misaada kadhaa kutoka maeneo mbalimbali lakini imechelewa. Hata hivyo, nafarijika kwamba program tulizozianzisha zinaenda vizuri

Program kubwa ni ile ya ukopeshaji, ambapo hadi sasa tumekopesha karibu shilingi milioni 250 kwa vikundi vya wajasiriamali Bumbuli, wengi wao wakiwa kina mama.

Kuna baadhi ya maeneo watu niliowaamini kuendesha shughuli za ukopeshaji wametuangusha na wamewaangusha wananchi kwa hiyo tunalazimika kurekebisha hali hiyo. Tuna mipango mingine mikubwa kwa mwaka wa 2015.

Kwa kuzingatia mazingira magumu ya hali ya hewa ya baridi kali, Shirika hili limeanzisha programu ya kugawa viatu vya shule kwa wanafunzi wote wa Shule za Msingi katika Jimbo la Bumbuli kila mwaka. Tumeanza mwaka huu kwa kugawa pea 45,000 na tutaendelea kufanya hivyo kila mwaka. Pia tumeanzisha programu za kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha nne kufanya vyema katika mitihani yao ya taifa. Tunaendelea na jitihada za kwenye kiwanda cha kusindika mboga na matunda. Pia tunatoa ushauri na kushirikiana na Halmashauri ya Bumbuli kuiwezesha kupata mtaji wa shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuwekeza kwenye shughuli za maendeleo.

Umeuliza pia kuhusu mafanikio ambayo tumeyapata Wizarani hadi tuaminiwe kwa nafasi za juu. Labda niseme kwamba Wizara haiendeshwi na mtu mmoja au wawili. Kuna timu ya watendaji, wataalam na watumishi wa Wizara pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara. Na pia kuna wenzetu wengine ndani ya Serikali nzima ambao bila wao Wizara moja haiwezi kutimiza majukumu yake. Mara nyingi sijisikii vyema pale Wizara moja au Serikali inapotimiza majukumu yake, basi hujitokeza mtu mmoja kusema yeye kafanya kwamba ni mafanikio yake. Mafanikio yote ya Serikali huwa ni mafanikio ya timu nzima inayoongozwa na Rais, ambaye ndio kiongozi wa Serikali.

Naamini pia ni muhimu kuondokana na hii dhana kwamba madaraka ya juu ni kama zawadi kwa mtu akitimiza majukumu yake aliyopewa. Hii habari ya kusema kwamba bwana fulani akiwa Waziri wa wizara fulani alitimiza wajibu wake kwa hiyo tumzawadie uongozi wa juu haina maana.

Wakati Mwalimu Nyerere anachaguliwa kuwa Rais wa TANU mwaka 1954, akiwa na miaka 32 tu, ili kuongoza harakati za kutafuta uhuru wa nchi yetu, kama kungekuwa na swali kwamba kwani kafanya nini hadi awe Rais wa TANU, kwamba kuna wanaostahili zaidi Urais wa TANU kwa sababu wamefanya makubwa zaidi hata kabla Mwalimu hajatia mguu Dar es Salaam, basi historia ya nchi yetu ingekuwa tofauti na ilivyo leo.

Hata hivyo, nikisema nikusimulie mafanikio ya Wizara yetu hapa tutakesha. Lakini niseme kwa kifupi tu kwamba Serikali ya Rais Kikwete, na nasisitiza hapa kwamba Serikali ya Rais Kikwete kwa sababu ndio kiongozi wetu, imepata mafanikio makubwa sana katika sekta ya mawasiliano. Ndio sekta inayoongoza kwa kukua kwa kasi na kwa muda mrefu kwa kiwango cha wastani wa asilimia 20 katika kipindi cha miaka saba. Hakuna sekta yoyote ya uchumi iliyokuwa kwa kasi hiyo na kwa kipindi kirefu kama hicho. Kwamba sasa hivi karibu kila mtu ana simu ya mkononi na anaweza kumudu kuitumia sio jambo lililotokea lenyewe tu kwa ajali ni matokeo ya uamuzi wa Serikali, ni matokeo ya Sera za Serikali, ni matokeo ya Sheria na Kanuni tulizoziandika Serikalini. Maisha ya Watanzania yamebadilika kwa kiwango kikubwa sana kutokana na sera muafaka tulizoweka, zilizowezesha uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya mawasiliano ikiwemo kwenye mitandao ya simu za mikononi. Huduma ya fedha,kutuma na kupokea fedha, sasa inapatikana kwa Watanzania karibu wote hata wale wasio na akaunti za Benki. Biashara za aina zote zimeshamirishwa kutokana na urahisi wa mawasiliano jambo lililowezeshwa na uwekezaji wa Serikali kwenye kujenga mkongo wa mawasiliano wa taifa.

Kumekuwepo na mashaka kwamba Serikali haipati mapato stahiki kutoka kwenye makampuni ya simu. Suala la usimamizi wa kodi na mapato ni suala la Wizara ya Fedha sio la Wizara za kisekta. Hata hivyo, mwezi Oktoba 2013, tumefunga mtambo wa kisasa wa kufuatilia mapato ya makampuni ya simu na sasa mapato ya Serikali yameongezeka kwa kiwango kikubwa. Pia, kutokana na usimamizi mzuri wa sekta hii, ajira zimeongezeka sana kwanza kwenye makampuni yenyewe lakini pia kwa Watanzania wengi hasa kina mama walioingia kwenye biashara za kuuza vocha na huduma za kuhamisha fedha. Karibu katika kila kona ya nchi yetu wapo watu wanaofanya biashara hizi na hizi ni ajira nyingi sana zinazowasaidia Watanzania wa kawaida.

Tumejenga Chuo Kikuu kikubwa cha Sayansi na Teknolojia na chenye hadhi ya kimataifa pale Arusha ambacho kinafundisha wanasayansi na watafiti wa ubora wa juu, waliojikita katika kutumia elimu ya sayansi kutafuta majawabu ya matatizo ya msingi ya Watanzania. Kuanzia mwakani tutakuwa tunatoa wahitimu watafiti wa sayansi, yaani PhDs, 500 kila mwaka na tutaendelea kuongeza. Tumeinua hadhi ya Chuo cha Ufundi Mbeya na sasa ni Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia. Tume ya Sayansi na Teknolojia iliyo chini ya Wizara yetu nayo inafanya kazi nzuri ya kutoa chachu kwenye tasnia za utafiti na uvumbuzi. Hata hivyo, msingi wa maendeleo ya sayansi na teknolojia unaanzia kwenye elimu ya sayansi na hesabu kwenye shule za Sekondari. Na sote tunafahamu kwamba kuna changamoto kubwa kwenye eneo hili. Ndio maana nilisema hapo awali kwamba ili Wizara moja ifanikiwe lazima Serikali nzima ifanye vizuri.

Bado changamoto zipo nyingi ikiwemo ubora wa huduma za mawasiliano, gharama za kupiga simu na kukosekana kwa huduma za mawasiliano vijijini, fedha chache zinazopangwa kwa ajili ya utafiti na kadhalika. Serikali imejipanga vizuri na iko mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto hizi. Labda moja ya tatizo kwenye Wizara yetu ni kwamba tunafanya kazi kimya kimya. Kuhusu jimbo, kama nakumbuka nadhani umeuliza iwapo kama mtu jimbo lake bado lina changamoto za maendeleo, kwanini apewe nafasi ya uongozi wa nchi. Kwanza niseme kwamba hakuna jimbo hata moja hapa nchini ambalo halina changamoto iwe maji, umeme, afya, barabara, au ajira. Hakuna mtu hata mmoja anayeweza kujitokeza na kusema kwamba kamaliza changamoto jimboni kwake na kwa hiyo huo ndio msingi wa kuchaguliwa kwa nafasi ya juu.

Rais wetu mstaafu, Mzee Mkapa, na Rais wetu wa sasa, Mheshimiwa Kikwete, walikuwa Wabunge. Walifanya kazi nzuri sana kwenye majimbo yao lakini hawakumaliza changamoto na hadi leo Masasi na Chalinze kuna changamoto. Tungesema mwaka 1995 kwamba Mheshimiwa Mkapa hafai kuwa Rais kwa sababu Masasi au Nanyumbu kuna wanafunzi wanafeli au kuna barabara hazipitiki, basi nchi yetu ingekosa kiongozi mzuri. Tungesema mwaka 2005, kwamba Mheshimiwa Kikwete hafai kuwa Rais kwa sababu kuna watu katika baadhi ya maeneo ya Chalinze hawana maji au kuna shule watoto wanakaa chini, basi tungekosa Rais mzuri ambaye anaifanyia nchi yetu kazi kubwa. Kwa hiyo hii habari ya kusema huyu bwana au yule bwana hafai uongozi wa nchi kwa sababu mvua ikinyesha jimboni kwake kuna barabara moja magari yanakwama mara nyingi inakuwa ni siasa tu.

Kama ambavyo Rais Mkapa na Rais Kikwete, licha ya kutomaliza changamoto za majimbo waliyoyaongoza, waliweka misingi ya maendeleo tunayoyaona katika majimbo hayo leo, na mimi nimejitahidi kuweka misingi imara kwa ajili ya maendeleo katika jimbo letu. Shirika la Maendeleo la Bumbuli litaendelea kubaki milele na kuwasaidia wananchi. Lakini pia, baada ya miaka mingi ya kunyimwa Halmashauri mpya, binafsi nililisukuma kwa nguvu kubwa na kuhakikisha kwamba tunapata Halmashauri. Sasa hivi kila mwaka tunapata pesa mpya za maendeleo shilingi bilioni 18 ambazo huko nyuma hazijawahi kuwepo. Mji wa Bumbuli umechangamka, mzunguko wa pesa ni mkubwa sasa. Pia, wananchi, hasa wakulima wa chai, sasa wameondokana na dhuluma iliyokuwa inafanywa kwenye zao la chai na sasa tumepata ukombozi baada ya kupata maumivu ya muda mrefu.


 
Mlikuwepo wapi kutangaza huu upuuzi kabla ya kusikia fununu kuwa ni yeye ndie behind mswada wa kufungia mitandao......wazushi na wanafiki wakubwa nyie na mnaprove mnafaa kufungiwa.
 
Du mimi sijauona mchanganuo wa biashara anayotaka kufanyia hizo hele,Matarajio yake kimapato uko vipi,Sijui amekopa kama Mbunge wa Bumburi ama kama january makamba,Ila akibugi kwenye matarajio inaweza kula kwake.
Atalipa tu, huyu ndiye Waziri wa nishati na madini kwenye serikali ya awamu ya tano. Kuna waraka wa dada yake kwenda kwa wamiliki wa migodi!
 
ukweli ni kwamba ameweza kuwafungulia wan bumbuli microfinance na sasa hivi upo mpango wa usindikaji wa matunda yote yanayotoka lushoto na sehemu zake,hivyo kila mwannchi atawezeshwa kwenye hilo ,acheni propaganda chafu leo wanabumbuli wananufaika na mikopo nyenye riba nafuu,pia wanafunzi wanapatiwa viatu bure,sasa huo uongo ninyi bavicha manao ueneza ni wa kijinga,acheni kukaa mijini tembeeni muone nini kinafanyika na si longolongo,
 
kazi ipo ...huyu January ikifika June bado wazii basi hafukuzwi tena
 
kazi ipo ...huyu January ikifika June bado wazii basi hafukuzwi tena
January Makamba ni story teller...anawaona watanzania wote ni watu waliolemewa na usingizi na kama ujuavyo, 'sinzia ni tamu kuliko lala'.
Kwa kuona jinsi watanzania wanavyosinzia yeye ameamua kuwapa bed time stories kutoka kwenye vitabu asomavyo.
He is full of theories.
 
Back
Top Bottom