January Makamba kiongozi mwenye uzalendo licha ya kuwepo CCM

wenye nyumba wamezidi kutunyanyasa sie wapangaji, kama kutakuja kuwa na sheria kama hii jeuri ya wenye nyumba mjini zitakwisha
 
Yaani Januari Makamba. umetuwakilisha wengi. Msisubiri fanyeni sharp kuwabana watu hawa wanaokodisha nyumba kwa bei mbaya halafu kodi ya mapato hawailipi serikali.
 
January ni mmoja kati ya wabunge wachache sana wa magamba wanaowawakilisha vyema wananchi!
 
Kwa mara ya kwanza nampongeza January Makamba! Siasa sio uadui ila ni ushindaji wa hoja na sera, mtu anapostahili pongezi apongezwe regardless of political affiliation!
 
Kwa kweli nami nachukua naasi hii kumpongeza January Makamba kwa hoja ya kutaka wenye nyumba wadhibtiwe wasipandishe kodi kiholela maana wapangaji wengi mijini hunyanyaswa sana na wenye nyumba kutokana na kutokuwa na Sheria inayowadhibiti kuwanyanyasa wapangaji. Mheshimiwa Jan Makambani mmoja kati ya Vijana wanne ndani ya CCM ninaowakubali utendaji wao wa kazi ambao hauzingatii itikadi ya Chama chake binafsi bali kwa manufaa ya umma. Tunataka vijana kama J Makamba ili tupamabae na wale wasiopenda kusimamia kwenye ukweli na Haki.
 
Upuuzi mtupu, kama akikupandishia kodi si ujenge yako au uhame!! Kila kitu kimepanda bei, serikali yenyewe imepandisha bei ya umeme we hujaona? Huyo makamba wako badala ya kupeleka hoja ya kupanda bei za kila kitu yeye anaongelea wenye nyumba sasa unataka wenyewe wakale wp? Acha upuuzi wako.
 
Tononeka,mjinga akikaa kimya huonekana mwenye busara,ni bora ukae kimya usije onekana wa hovyo zaidi!
 
Hujaona kila kitu kimepanda bei, kivuko kgmboni, kiberiti hadi chumvi!!? Sasa ww na makamba wako mmeona wenye nyumba tu?
 
Sheria itakata pande zote mbili. wapangaji wataathitika manake wengine watahairisha kupangisha nyumba zao. wasiyokuwa na nyumba watahangaika.
 
Namuunga mkono mtoa hoja. Nina ombi la ziada. Sisi wapangaji wa nyumba za AICC Arusha tunalipa VAT kwenye kodi. Wapangaji wa NHC na nyumba za watu binafsi hawalipi VAT. Tutetewe na sisi.
 
Prof. Tibaijuka kamjibu huwezi nipangia kodi ya nyumba yangu niliyoijenga miaka 30, serikali kwanza ijenge zake ndio mje za watu binafsi.
Kuna mikoa/miji watu wanaogopa kulogwa kwa eti kujenga nyumba leo mnazinduka, basi watozeni hata wenye Bustani au mashamba
 
Hakuna jipya, upuuzi tu. Hana lolote la maana katika hoja yake, kaikopi ile ya Texas...
Nini kinakushangaza kwa mtu kukocopy kitu achia mbali hoja. Kuna vitu vingap vya kipuuzi tumecopy??unashangaa nn mtu kucopy kitu cha msingi kama hicho???wewe bado unakaa kwa shemeji nini??
 
Back
Top Bottom