January Makamba kiongozi mwenye uzalendo licha ya kuwepo CCM

Sikwepeshi

Senior Member
Jan 26, 2012
162
18
Mh January Makamba mbunge wa Bumbuli (CCM) amepanga kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu upangaji wa nyumba, jinsi gani wapangaji wanavyopata wakati mgumu, kiasi gani madalali wamekuwa chanzo cha kupanda ovyo kwa bei za nyumba.

Ni kweli serikali inatakiwa iweke sheria za kumlinda mpangaji.

Big up January!
 
Hili linamgusa kila mtu,kama kuna jambo serikali ikilisimamia vizuri na wakafanikiwa watajingea heshima.bei za nyumba balaa, imefikia wakati mtu anaenda kupanga nje kabisa ya mji lakini still bei ni za kutisha! Hata Mbagala bei zimepaa!
 
At least! suala la upangaji mjini imechangia sana ufisadi na rusha. we mtu anapata mshahara kwa mwezi mwenye nyumba anadai pango la mwaka unategemea nini kama si watu kuiba? hongera sana January
 
kwa hili kwa kweli nimemsifu. Wapangaji tunapata sana shuda na hawa ma faza/maza kemp/haus. Naona sasa price ceiling na floor vinanukia kwenye upangaji
 
Kuna mambo makubwa zaidi yanayohitaji kusimamiwa na mtu akaonekana makini na sio nyumba...ufisadi unaoendelea serikalini ni moja ya maeneo muhimu...kinachoendelea mtaani au kwa wananchi kinahakisi kinachoendelea kwa watawala wetu.
 
kwa hili kwa kweli nimemsifu. Wapangaji tunapata sana shuda na hawa ma faza/maza kemp/haus. Naona sasa price ceiling na floor vinanukia kwenye upangaji

Kwa kweli mimi nadhani hii hoja imekuja kwa wakati mwafaka. Hali za maisha zimekuwa ngumu sana kwa sababu ya pango isiyothibitiwa
 
Yaani wala huhitaji ufafanuzi zaidi kwa jinsi kijana Huyu anavyoibua issues zinazogusa maisha ya watanzania na mnaobeza wabunge wapo zaidi ya 300 wengine wako mjengoni kwa zaidi ya robo karne, tujiulize kila mbunge angecheza karata zake (neno karata nimelipata kupitia hotuba ya Pinda ) basi matatizo mengi yangemalizika, Huyu Ana mwaka tu bungeni lakini hoja zake zina mshiko sana, just give it to him!
 
Kuna mambo makubwa zaidi yanayohitaji kusimamiwa na mtu akaonekana makini na sio nyumba...ufisadi unaoendelea serikalini ni moja ya maeneo muhimu...kinachoendelea mtaani au kwa wananchi kinahakisi kinachoendelea kwa watawala wetu.

kwa ulichoandika unaunekana wazi unanuka maziwa. Shit! You dont know a damn thing about rent, boy!
 
Kuna mambo makubwa zaidi yanayohitaji kusimamiwa na mtu akaonekana makini na sio nyumba...ufisadi unaoendelea serikalini ni moja ya maeneo muhimu...kinachoendelea mtaani au kwa wananchi kinahakisi kinachoendelea kwa watawala wetu.

Issue ya upangaji umeona ni jambo la kitoto?! Basi we utakuwa unakaa kwenye nyumba yenu urithi
 
Mh january makamba mbunge wa bumbuli(ccm) amepanga kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu upangaji wa nyumba,jinsi gani wapangaji wanavyopata wakati mgumu,kiasi gani madalali wamekuwa chanzo cha kupanda ovyo kwa bei za nyumba.ni kweli serikali inatakiwa iweke sheria za kumlinda mpangaju..big up january!

january na SUGU wote ni wageni bungeni ... ukienda jimboni kwake january kafanya mambo makubwa sana... SUGU yeye anazunguka tanzania kuzindua album yake....

hongera sana january :poa wewe ni mbunge ninaye kukubali ikifuatiwa na zito na mnyika
 
Hakuna ubishi ni kijana anayekuja juu sana kwenye siasa za nchi hii. Nimemsikia leo na mpango mkakati wake wa kuwakilisha bungeni hoja binafsi kuhusu upangaji wa nyumba na ulipaji kodi wa wenye nyumba za kupangisha.
 
Kijana anajitahidi sana. Aende mbele zaidi ili tujue kama mtu anapochangiwa zaidi ya billioni mbili kwenye kampeni hazistahili kulipiwa kodi!
 
Kuna watu wanataka tuamini kila jambo la kizalendo linafanywa na cdm. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Kabisa mkuu mimi mwenyewe cdm ila kwa hili dogo namuunga mkono na walaaniwe wanaombeza katika hili,go January gooooooooo
 
Back
Top Bottom