January Makamba: Kamwe CCM haiwezi kuachia dola mwaka 2015

Sishangai,hata Gachuma jana kawambia vijana wavute bange ili wawe fit 2015,na ameomba makambi ya kufundisha vijana ukakamavu kukabiliana na wapinzani
 
Toka lini mtoto wa nyoka akawa mjusi? Aliye zaliwa na FISADI NI FISADI TU! Januari wewe ni Januari tu 2015 huwezi kuwa Desember.
 
Nimevutwa kusema haya kwani CDM kushika dola 2015 ni sawa na ndoto za mchana,huu ni ujanja wa kuwatia moyo wanachama ili wasikate tamaa,nayasema haya kwa kulinganisha nguvu yakisiasa kwa wapinzani kati ya zanzibar na bara,nguvu ya wapinzani zanzibar ni kubwa huwezi kulinganisha na hawa ndugu zangu CDM wanao jipa moyo japo kupeana matumaini lakini ndio hao kila siku wanafurukuta na wanachemka,CDM jaribuni kulinganisha pumzi yenu na CUF kule zanzibar kisha mjipange upya muache ndoto zenu za kushika dola 2015
 
Nakuombea upate kuwa na maisha marefu ili ushuhudia hii ndoto yako itakavyokua kinyume.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Jamaa anajitibu kisaikolojia baada ya kujitoa fahamu! Sasa hivi anaogopa kivuli chake, na bado utakapo jua kuwa magamba wanaenda kuwa chama cha upinzani tayari shampeni zimeshafunguliwa na pale jangwani vizibo vinadondokea ikulu.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Kiongozi shupavu hawezi kutumia mabavu kuongoza, ni kiongozi dhaifu tu ndio atatumia mabavu kuficha udhaifu wake - Jenerali Ulimwengu
 
Binafsi siwez linganisha siasa za cuf kule zanzibar, na cdm bara, cdm bara wamejipanga vizuri na wamedhamiria kuwakomboa watanzania. Cuf imebaki ikipigana na cdm badala ya kupambana na ccm.
 
We can see the hand of god displacing ccm on ruling track,its the matter of time.wakati ukifika hakuna atakayezuia
 
Hizi kauli zinanikumbusha anguko la Sadam Hussein, yule Waziri wake wa habari Bwana Aziz (kama sijakosea jina).
 
  • Thanks
Reactions: kui
Hizi kauli zinanikumbusha anguko la Sadam Hussein, yule Waziri wake wa habari Bwana Aziz (kama sijakosea jina).

Ni kweli kabisa mkuu, jina lake ni Tarik Aziz, uwanja wa ndege wa Baghdad ulipozingilwa na maadui akawatangazia wairaq kuwa mtego wetu sasa umekamilika hakuna hata mmarekani mmoja atakayesalimika kumbe muongo maji yamezidi unga, Gaddafi naye Bengazi ilipodhibitiwa akasema waasi ni panya tu atawateketeza wote lkn tunajua matokeo yalikuwaje. Watawala uwa wanajisahau sana kwa kudhani kila siku ni jumamosi. Lakini ukweli uliopo na labda ndicho alichokimaanisha ni kwamba hata kama kura za upinzani zitakuwa nyingi ccm hawatakabidhi nchi kirahisi, kilichotokea Ivory cost kitajirudia marais watakuwa wawili. Tuombe uzima tuone sinema itakavyokuwa.
 
1.GADDAF hakupenda kuachia madaraka na aliita wapinzani wake mende na panya leo yuko wapi?
2. BAGBO alikataa kutoka madarakani akakamatwa mtaroni kama kambale
3. Al assad wa Syria hataki lakini hali ilivyo makamba anaiona na kwa sasa Al Assad ni maiti inayotembea kwani siku zake za kuishi ni chache

** Yote hayo yaliyotokea na yanayotokea katika nchi hizo ni kwa sababu ya watawala kutokubaliana na Demokrasia na kung'ang'ania madaraka**

HAWATAKABIDHI, LAKINI WAKISHINDWA NGUVU YA UMMA ITAFANYA KAZI YAKE KUIKOMBOA NCHI HII
 
Nimevutwa kusema haya kwani CDM kushika dola 2015 ni sawa na ndoto za mchana,huu ni ujanja wa kuwatia moyo wanachama ili wasikate tamaa,nayasema haya kwa kulinganisha nguvu yakisiasa kwa wapinzani kati ya zanzibar na bara,nguvu ya wapinzani zanzibar ni kubwa huwezi kulinganisha na hawa ndugu zangu CDM wanao jipa moyo japo kupeana matumaini lakini ndio hao kila siku wanafurukuta na wanachemka,CDM jaribuni kulinganisha pumzi yenu na CUF kule zanzibar kisha mjipange upya muache ndoto zenu za kushika dola 2015
Huwezi kusema CUF kina nguvu Zenji kwani tunavyoelewa 1995 kilishinda kulingana na habari kutoka vyombo vya kimataifa wakadhurumiwa wakaandamana wakabutuliwa na polisi wakafyata CCM ikatawala, 2010 walishinda wakadanganywa wakakubali ndoa na ndo ukawa mwisho wao, usitegemee kama CUF itaimalika labda Maalim Seif na Lipumba wapigwe chini wapatikane viongozi wengine wenye mtazamo tofauti na hao.
 
Hawa jamaa kwa kauli za umilele hawajambo, walianza siku hizo, zidumu fikra za mwenyekiti (leo hii wamebadilisha). Shoka liko kwenye shina, wasubiri nguvu ya umma 2015
 
Baba yake alimwachia yeye atawaachia wanae sasa sisi ambao hatuna majina ya Makamba kwisha habari yetu!!!! Vijana wengi wanakimbia usultani na wizi uliokidhiri ndani ya ccm

Kalewa harufu ya vijisenti unategemea aseme nini zaidi ya hivyo?? Hata yule mwanae GHADAFI seif al islam aliwahi kusema serikali ya baba yake kamwe haita anguka, yu wapi leo?? iko siku tutajiuliza yu wapi JANUARI yule mtoto wa aliyeiangamizi NCHI YETU? Hakuna marefu yasiyo na mwisho na yeye lazima atashuhudia mwisho wa ccm.
 
........hivi ccm iking'oka chama gani kitatawala? nani atakuwa rais ...nani atakuwa pm...nani ataongoza nchi?...Je nchi itaongozwa au itauzwa...........makao makuu ya nchi yatakuwa wapi - KARATU AU HAI?...............HAHAHAHAHAHAHAHAH
 
Back
Top Bottom