January Makamba ajifananisha na Sokoine na Mrema, anafanana nao?

Mpitagwa

JF-Expert Member
Feb 10, 2012
2,339
1,119
WanaJF, kwenye gazeti la Guardian la jana Mh. January Makamba aliandika makala yake ya kujitetea dhidi ya mtazamo wa mwandishi wa habari aliyesema si vizuri kwa yeye kuingilia TCRA.

Katika kuhitimisha makala yake akajiweka kundi moja na Hayati Moringe Sokoine na Mh. Mrema katika utendaji wao serikalini.

Swali ni je anafanana na watu hao kiutendaji au ndoo yale ya kutaka kujua watu wanamfikiriaje yeye?
 
Wapiga Kura wake wanamjua zaidi!, lakini kwa upande wangu naona yupo tofauti sana na wachumia tumbo wengi wa ccm!!!!.
 
jmakamba acha kutafuta umaarufu usio na tija huwez kufanana na sokoine koz uadilifu na uzalendo wa hivyo ww huna.
 
Anafanana na william Mubosi..le mutuz rais ya wa....pi vile? Wakuu malizieni
 
Ni lugha au? maana katika makala Jozeni ndie aliye suggest "...Edward Moringe Sokoine, the MP for Vunjo, A. L. Mrema and January Makamba are cut from the same cloth"

Hili la kuwa January kajifananisha...nadhani tusome mambo kama yalivyo!
 
Binafsi namlheshimu kuwa ni kijana mwenye uwezo, lakini kupita kwake ubunge bila kupingwa na malalamiko ya mzee Shelukindo juu ya mbinu chafu alizotumia wakati wa mchakato ndani ya chama na kumfanya shelukindo aachie ngazi sio sifa za hayati Sokoine wala Mrema pale vunjo. Na hata muda aliofanyakazi serikalini ni mdogo sana kuanza kujifanananisha na wao
 
Wapiga Kura wake wanamjua zaidi!, lakini kwa upande wangu naona yupo tofauti sana na wachumia tumbo wengi wa ccm!!!!.
Naungana na wewe sana, yuko tofauti sana na walafi wa CCM. Ni vizuri kuwa wakweli kwa huyu kijana.
 
Hajamaliza hata mwezi kama Waziri tayari anajifananisha na Sokoine? Hivi Sokoine ana dada mwenye hekalu?
 
January anafanana sana na Babake kitabia. Amekaa kimajisifusifu tu, anapenda madaraka kuliko maelezo. Ni mchumia tumbo tu huyo.
 
Jamani ndo kwanza anaanza kazi ya uwaziri, vipi mnampima sasa? Tumpe mda, tukimjaji sasa tunamwonea, ubunge na uwaziri ni vitu 2 tofauti.
 
Mwanzo mlimfananisha Baba MwanaAsha na Nyerere.wabongo kwa kupenda cfa ukimfananisha na Rostam atachukia.
 
Huyujamaa nihovyo kabisa maana kamawatuwangejua rafu alizomchezea mzee sherukindo wangeona alivyo wa hovyo
 
Back
Top Bottom