Elections 2010 Janja ya CCM hii hapa

Ramos

JF-Expert Member
May 13, 2010
498
130
Hi wanaJF

Kuna uvumi ambao unaenea kwenye jamii kuwa "CCM ni wezi wa kura na hata watu wapigie kura vyama vingine lakini mara nyingi CCM hufanya kila namna anatangazwa mgombea wao kuwa mshindi"

Pamoja na ukweli ilioko katika jambo hilo lakini tumegundua mpango wa CCM (katika jimbo letu) kutumia jambo hilo kama mtaji kwao. Wameamua kueneza taarifa kuwa hata iweje CCM wataiba kura na watashinda. Lengo ni kuwakatisha tamaa watu wasiotarajia kuwapigia kura ili wakate tamaa ya kupiga kura. Hii ni falsafa ambayo hutumiwa hata katika ajira ambapo baadhi ya watu hupenda kueneza uvumi kuwa kazi fulani tayari imeshaandaliwa mtu ili kudiscourage watu wasiapply inapotangazwa au wasiattend interview na matokeo yake wanapunguza ushindani kwa watakaojitokeza! Kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kwani kwa sasa vijana wengi wakiulizwa kama watapiga kura wanasema haina haja ya kwenda kupoteza mda wakati mshindi hatokani na kura. Hii ina maana kuwa CCM watashinda kirahisi kwani wengi wa wapinzani wao hawatapiga kura.

Ushauri: Hata kama una hakika kuwa utakayempigia kura hatashinda, we piga kura kwani idadi ya kura itampa moyo na hamasa ya kujaribu tena.
Hata kama wataiba, kazi ya kuiba itakuwa ngumu kadiri margin ya kushindwa kwao itakavyokuwa ngumu.

TUJITOKEZE KUPIGA KURA
 
Mimi sipo tayari kupoteza kura yangu kwa atakayeshindwa,hilo lazima muelewe!
 
Ziko nyingi bado na zingine ni za kibabe, kwa mfano kutangaza mtu aliyeshindwa kuwa ndiye kashinda.
 
Lakini hawa tume ya uchaguzi ndio wahumu wenyewe, watakwambia kili kitu kiko tayari, utaenda piga kura, watakwambia karatasi zimechelewa, tena wanafanya hayo hata hapa dar, utakaa kwa sa 3-4 utaondoka, wana ccm hawaondonki, au watachelewesha ili wakati wa kuhesabu kula ufanyike usiku, lazima muibiwe, dawa ni kuanzisha ngo kuelimisha wapiga kula,.....................
 
Hi wanaJF

Kuna uvumi ambao unaenea kwenye jamii kuwa "CCM ni wezi wa kura na hata watu wapigie kura vyama vingine lakini mara nyingi CCM hufanya kila namna anatangazwa mgombea wao kuwa mshindi"

Pamoja na ukweli ilioko katika jambo hilo lakini tumegundua mpango wa CCM (katika jimbo letu) kutumia jambo hilo kama mtaji kwao. Wameamua kueneza taarifa kuwa hata iweje CCM wataiba kura na watashinda. Lengo ni kuwakatisha tamaa watu wasiotarajia kuwapigia kura ili wakate tamaa ya kupiga kura. Hii ni falsafa ambayo hutumiwa hata katika ajira ambapo baadhi ya watu hupenda kueneza uvumi kuwa kazi fulani tayari imeshaandaliwa mtu ili kudiscourage watu wasiapply inapotangazwa au wasiattend interview na matokeo yake wanapunguza ushindani kwa watakaojitokeza! Kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kwani kwa sasa vijana wengi wakiulizwa kama watapiga kura wanasema haina haja ya kwenda kupoteza mda wakati mshindi hatokani na kura. Hii ina maana kuwa CCM watashinda kirahisi kwani wengi wa wapinzani wao hawatapiga kura.

Ushauri: Hata kama una hakika kuwa utakayempigia kura hatashinda, we piga kura kwani idadi ya kura itampa moyo na hamasa ya kujaribu tena.
Hata kama wataiba, kazi ya kuiba itakuwa ngumu kadiri margin ya kushindwa kwao itakavyokuwa ngumu.

TUJITOKEZE KUPIGA KURA

Jamaa ana hoja sana huyu, tujaribuni kumsikiliza! Kuna saikolojia kali hapa huwa inatumioka kusaidia watu kushinda wanapokuwa worried kuwa watashindwa. Jamaa ana hoja nzuri sana!
 
Hizo mbinu mbona hazijatumika kumshinda Dr. Slaa kule Karatu au mzee Ndesa kule Moshi?

Acheni kutafuta visingizio, sio siri kwamba uchaguzi TZ sio fair kwa maana ya kwamba vyombo vingi vya umma vinakuwa kwenye chama tawala. Lakini mara nyingi wanaoshinda huwa wanashinda kikweli kweli.

Kama wana mbinu mbona hao CCM hawashindi Pemba?

Mkiwa na mawazo ya kuibiwa vichwani, ni kweli mtaibiwa. Kuweni ngangari na kujiamini na hata kuwe na dhuluma kiasi gani, wananchi wakiamua kukuchagua, watakuchagua tu.

Hoja ya Ramos ina ukweli na inatumika hata kwenye nchi zilizoendelea. Watu hawapotezi muda kumuunga mkono mtu ambaye wanajua atashindwa. CCM wamejua mnaogopa mno kuhusu kuibiwa kiasi kwamba sasa wanatumia njia hiyo kuwatisha.

Mkiwa na mawazo ya kuibiwa vichwani, ni kweli mtaibiwa. Kuweni ngangari na kujiamini na hata kuwe na dhuluma kiasi gani, wananchi wakiamua kukuchagua, watakuchagua tu
 
Back
Top Bottom