roselyne1
JF-Expert Member
- Feb 18, 2010
- 1,365
- 93
Aina fulani ya uandishi iliyo tofauti kidogo, inatia moyo kwamba waandishi wetu wengine wanaweza kukaa chini na kufikiria. Ingeelimisha zaidi kama muandishi angepata habari zaidi na kuongea na mabingwa wa afya ya akili kupata maoni yao kuhusu issue hii, na hali ya afya ya akili kiujumla nchini.
Mara nyingi naona watu wa magharibi wanaongelea mambo mengi ya afya ya akili, watu wengi wanapata therapy, wame categorize matatizo ya akili katika sehemu nyingi (schizophrenia, obsessive-compulsive disorder, post-traumatic stress disorder, social anxiety, phobias, depression, bipolar disorder etc ) najiuliza hivi haya ni matatizo ya watu wa west tu? Sisi kwetu hayapo ? Au sisi tunaya underdiagnose ? Mfano unaoweza kutetea kwamba yapo ila tuna ya underdiagnose ni wa miwani. Vijijini watu wachache sana wanavaa miwani, lakini hili halimaanishi kwamba wote wana macho yanayoona vizuri, karibu wote hawana access na eye exams na kuvaa miwani. Kwa hiyo si kweli kwamba hawana matatizo ya macho, bali inaonekana hawana access na huduma za afya.
Naamini muandishi wa makala hii kwa msaada wa watu kama Professor Kilonzo ana uwezo wa kuandika series inayohusu mental health, aka tie in effects za madawa ya kulevya (I hear heroinn and cocaine are taking a good chunk of our population, especially in Dar and Zanzibar ) lakini pia kuingia deeply huko kwenye disorders.
Haya ni mambo muhimu ambayo inabidi tuyafanyie utafiti zaidi. Napenda kumpongeza kila muandishi anayeonyesha utashi wa kutaka kuelewa na kuelewesha zaidi mzizi wa tatizo (of course the all encompassing ubiquitous socio-economic reasons)
Najua kwamba, ina way, kuongelea the intricacies of mental health kwa watu ambao largely hawana running water, therefore main concern yao inaweza kuwa hygiene na infectious disease, kunaweza onekana elitist au hata unreasonable. Lakini at the same time, there is no reason we can't present a multi-front attack on the causes of poverty, diseases and ignorance.
yapo mimi pia ni mgonjwa nina bipolar disorder na schizophrenia..na namshukuru mungu.niko ughaibuni napata madawa na free medical care....nimesikikitika sana kusoma habari ya huyu mama kwa sababu i know for a fact labda ningekuwepo tanzania ningeishia kuwa kama huyu mama.
naiomba serikali iliangalie tena swala hili-inawezekana wagonjwa ni wengi kuliko inavyodhaniwa-sababu case nyingi tunaziskia mitaani za kucomit suicide-binafsi nadhaniaga labda ni depression ambayo kama ingegundulika early na kuwa treated hao watu wasingefikia hatua za kujiua.nailaumu serikali inawalet down watu wenye mental diseases sababu hata nikikumbuka kuna hospitali mbili tu za vichaa-moja ni hapo muhimbili na nyingine ni milembe kule dodoma...wangefanya kama huku ughaibuni atleast kila mkoa kuwe na mental hospital-ingekuwa nafuu watu kupata access ya huduma hii muhimu.
sijui nini kinachomsumbua huyo mama,ila i certainly dont blieve mumewe has anything to do with her mental illness-i just think ugonjwa wake ni kama wangu ambao somehow uko genetic related na unahitaji madawa tu ya hospitalini and she will be back to her normal self.
kingine serikali ingejitahidi kucreate AWARENESS ya magonjwa ya akili,sababu wengi wanakimbilia kwa waganga na kuombewa which certainly doesnt work.
mie natumia dawa zinaitwa ABILIFY (apripazole)..kwa sasa,am sure huyo mama akianziwa dozi kama mimi she will be fine within a week-imenisikitisha amelost career yake na familia yake.
msiwe wepesi kuwahukumu familia yake kwa kumtelekeza its soo hard to live with mentally ill person katika mazingira kama hayo bongo.