Son of Alaska
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 2,812
- 1,054
god have mercy,and let your creation jane,bounce back to normal life.So sad indeed
Hivi hao watoto wake si watu wazima kabisa? wanajisikiaje kuona mama yao analandalanda pale posta. Naamini kama watoto wake wangemwonyesha upendo wa dhati bila shaka Jane angepata faraja ya watoto na kurudi kwenye hali yake. Very sad story real.
Ndugu wa Jane aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mariamu, anasema mama huyo wa watoto wawili akiwa Chuo Kikuu, mwaka 1984 alibeba ujauzito wa mtoto wake wa kwanza Daudi kabla ya kufunga ndoa mwaka 1986. Mwaka mmoja baadaye aliamua kumfuata mumewe Ujerumani pamoja na kusoma.
Safari yake ya Ujerumani ilimgharimu kwani kwa mujibu wa taarifa ya Utafu, aliomba likizo ya bila malipo ambayo ilikataliwa na mwenyewe kuamua kuondoka bila kibali hivyo kufutwa kazi Januari, 1988.
Mama Mariamu anasema wakati ndugu yake huyo akiwa safarini Ujerumani alikuwa na ujauzito wa mtoto wake wa pili, Ibrahim na matatizo ya ndoa yalianzia huko kwani aliporudi hakuwa na amani tena.
Akizungumzia madai hayo, mume wa Jane, Profesa Hussein Sosovele anasema: "Mimi na Jane tumeachana muda mrefu. Mambo yake na yangu yaliisha miaka zaidi ya 10 iliyopita kwa hiyo habari zake sizijui."
sasa kilichokufanya u quote habari yote ni nini?una picha yake uweke?
well said mkuu, sijui wanajua kilichomfika mama yao au ndiyo walifichwa, kama wapo na wanafahamu inabidi wachukue hatua.Hivi hao watoto wake si watu wazima kabisa? wanajisikiaje kuona mama yao analandalanda pale posta. Naamini kama watoto wake wangemwonyesha upendo wa dhati bila shaka Jane angepata faraja ya watoto na kurudi kwenye hali yake. Very sad story real.
Serikali inamtaka mtu pale anapokuwa mzima na nguvu za kuitumikia, baada ya hapo ni majaliwa. Vilevile ina ubaguzi. Juzijuzi nilimsikia yule Mbunge alokuwa amelazwa anasaidiwa na serikali kuenda matibabu India, wakati yule mama alokuwa Mkuu wa Wilaya walikuwa wanampigia danadana. Vivyo hivyo kwa Mzee Moris, niliumia sana siku alipokuwa anahojiwa na DW kusikitika Serikali ilivyomtelekeza. Hali ya huyu dada inasikitisha, lakini Mungu ni muweza. Tumwombeeni.kusaini mikataba mbalimbali!
Aina fulani ya uandishi iliyo tofauti kidogo, inatia moyo kwamba waandishi wetu wengine wanaweza kukaa chini na kufikiria. Ingeelimisha zaidi kama muandishi angepata habari zaidi na kuongea na mabingwa wa afya ya akili kupata maoni yao kuhusu issue hii, na hali ya afya ya akili kiujumla nchini.
Mtazamaji, hao maafisa ustawi wa jamii ndiyo wanaitwa "social workers" kwa kizungu?
kilimasera said:UMKINI wengi wanaomuona Jane Sosovele katika maeneo ya Posta Mpya na mengine ya jirani hudhani kwamba ugonjwa wake wa akili alionao haukumpa fursa ya kujua kusoma na kuandika.
Wanapomuaona akiongea maneno yasiyokuwa na mbele wala nyuma, akiwa amebeba mfuko wa plastiki ambao ndani yake huwa na makaratasi ya kuokoteza, huku akiomba chochote kwa wapita njia huamini kwamba hana analolijua.
Hao wamekosea. Mwanamke huyu ni msomi aliyekuwa tegemeo kubwa katika fani ya mawasiliano ya simu katika Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)...............
Yah hao hao hivi Tanzania wapo????? Kazi yao nini?
wanaume sisi!!!!!!!
wanaume sisi!!!!!!!