du nafasi ya kazi hiyo. job seekers kazi kwenu
Jamani! Ni lazima useme jambo? Si ukae kimya tu? Ila umenikumbusha jambo.
Siku moja niliingia ofisi moja mahali nikakuta kuna staff amefariki. Waliweka picha ya huyo dada na maua na kadi kibao meza aliyokuwa anakaa. Akaingia staff mmoja alikuwa safari, akaonyesha masikitiko yake kuwa - ooh, its so sad, she was so gooood. Mwenziye akamwambia yeah, that's true, ila tumeshatangaza nafasi yake ya kazi. Hapo hata mwezi haujapita tangu afariki dada wa watu.
Nilijifunza jambo katika hilo. Afya yako ni yako mwenyewe, maisha yako ni yako mwenyewe. Tunza afya na maisha yako, ukiondoka wanakusahau siku hiyo hiyo...siyo unakaa ofisini masaa 20 na deadlines zinakuua, ukifa wanakuwekea maua wanatangaza nafasi yako.