Jana nienda saloon kunyoa.....

Kwa vituko alivyonifanyia yule binti anayepashwa kunisafosha kichwa tu sasa naamini wanaume wengi sasa hivi salooni wanafuata mambo tofauti na kunyolewa. Hawa wake zetu wangejua yanayojiri huko saloon walahi mwenye uchungu na mzigo wake asingeuacha utinge hizi saloon alone.

"Kaka kaa hapa. Unafanya skraibu?" (Sijui ndo nini)
"Hapana, naosha kichwa tu." Halafu ukimwangalia analipaaa! Na mapozi ya kichokozi kibao!
Mara kang'ata kidole, kaanza kunipapasa kuanzia mabegani, shingoni hadi kaingiza vidole kwenye masikio yangu. "Ungefanya skraibu tu kaka, ona mafuta yalivyomengi kwenye pua." kanishika pua ananikamuakamua........

Mablazameni najua mnazijua hizi lugha, ebu tupeni mapana na marefu ya huma kwenye saloon zetu. Huwa zinawakera au zinawafurahisha?
Sinza mazee! Hiyo kitu iko Sinza bana! Vile vibinti vitabaka watu sasa hivi!
 
Ee bhana huwa ni bonge la raha we acha tu,hiyo skraibu sasa akianza mbona utaenjoy,ile tu anakupeleka kwenye chumba ndogo anakuuliza kama kuna huduma zingine unataka,aisee kwanza kuanzia huko mabegani,shingoni,unajikuta unasinzia aisee kitu ambacho hata sijafanyiwa na gf wangu
Halafu ukivitolea nje vinamindi kishenzi! Sasa unajua mablazameni wengi huwa tuna kaaibu ka kuwaudhi mademu hasa wazuri.
 
Hahahahaa! Punguza monkari BD, hizo huduma kama huwa huzitoi kwa mwenziyo ujue kuna wajanja wanampatia kikamilifu. Chunga mzigo mamie, ujue unawashindani. Si umeona mwenyewe mablazameni wanavyoshuka live?

hhhhaaaa hawa mabrazamen wametuangusha aisee....badala ya kulinda himaya wanamfungulia mlango mwizi....
 
hili nililijua mapema....my sweet mashed potato nimemnunulia mashine na namnyoa mwenyewe.....

mie nilikuwa namruhusu mara moja moja, siku nyingine naenda nae ....wananunaje????????

Kwa style hii nafikiria kumpa ban ya kwenda huko......
 
we mbona raha sana,sijui mikono ya watu wengine imejaliwa nini,akikugusa tu mabegani mbona unakuwa crazy

Kuanzia kesho marufuku kwenda kunyoa saloon ntakuwa napitisha wembe kichwa kizima masaji nnayokufanyia huridhiki nayo! lol una kiranga sasa wewe.
 
mie nilikuwa namruhusu mara moja moja, siku nyingine naenda nae ....wananunaje????????

Kwa style hii nafikiria kumpa ban ya kwenda huko......

mmh...wananunaga sana...ili kukata mzizi wa fitna nilijifunza kunyoa na mashine nkanunua....na facial products tunashare.....
 
hahahahaha hadi kusinzia mkuu we noma.!!! Unakuta anakuscrub shingon afu anapitisha mikono mpka kifuani kichokozi, akimaliza utasikia kaka na mi ela ya soda...
sijawahi kuwaambiwa ila hela ya soda nitatoa aisee,kingono hapana ila zile miguso ni mitam
 
Back
Top Bottom