Jamuhuri ya Watu wa Zanzibar ni lazima irudishwe!

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,759
12,175
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar SIYO NCHI! Lakini ina kila alama zinazoashiria kuwa ni nchi huru yaani; ina Rais, ina bendera yake na pia ina wimbo wa taifa.

Harakati zinazoendelea hivi sasa ni kuwa Zanzibar inataka kuwa na vitu vifuatavyo: Benki kuu yake, sarafu yake na kubwa zaidi inataka iwe na uhuru wa kujiamulia mambo yake yenyewe bila ya kuingiliwa.

Wazanzibari wanataka nchi yao iwe na uhusiano na Tanganyika katika mfumo unaoshabihi uhusiano wa nchi zilizo katika jumuiya ya Ulaya.
​SWALI: Kwa nini tusiwaunge mkono katika adhma yao hiyo ili sisi Watanganyika tupate muda wa kutosha kujadili na kutatua changamoto zinazotukabili?
 
Kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa hakuna mtu aliyeqwahi kuwakatalia hawa ndugu zetu kufanya haya yote. tatizo ni kuwa wanapoambiwa wafuate taratibu, wao wanaona kuwa wanaonewa. nadhani wakifuata taratibu watayapata haya yote na mengine zaidi
 
Ni nani anawang'ang'ania hawa watu?

Wajitoe na umeme tuwakatie moja kwa moja
 
Irudishwe? Kwani ilichukuliwa au kuibiwa? Wao kama wanataka waendelee na mchakato(kwa maana walishauanzisha). Kimsingi hakuna haja ya kuwang'anganiza muungano. Sisi tunaojua tunaamini siku moja Taifa la TANGANYIKA nalo litatoka mapumzikoni,na hapo ndo itakuwa mwanzo mwingine wa ustawi na maendeleo mapya ya maisha ya watu wake(Watanganyika). Uchafu wote uliofanywa na TAN ZAN ia utasafishwa wakati huo. Wazanzibari endelezeni mchakato wenu kwa hoja,bila jazba na najua mnajitambua(sio kama WATANGANYIKA tulio katikati ya usingizi wa pono) na mnajua hatma(destiny) yenu. Nanyi WATANGANYIKA msiwe na jazba wala msikasirike Wazanzibari wanapotaka taifa lao.lilikuwepo.
 
Kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa hakuna mtu aliyeqwahi kuwakatalia hawa ndugu zetu kufanya haya yote. tatizo ni kuwa wanapoambiwa wafuate taratibu, wao wanaona kuwa wanaonewa. nadhani wakifuata taratibu watayapata haya yote na mengine zaidi

Hawa si kwamba hawajui kufuata utaratibu wanaujua sana! Ila wananufaika na mfumo huu uliopo!
 
Kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa hakuna mtu aliyeqwahi kuwakatalia hawa ndugu zetu kufanya haya yote. tatizo ni kuwa wanapoambiwa wafuate taratibu, wao wanaona kuwa wanaonewa. nadhani wakifuata taratibu watayapata haya yote na mengine zaidi

Kama mambo ndivyo yalivyo basi ni vema sheria ya mabadiliko ya katiba iliyofanyiwa marekebisho hivi karibuni irekebishwe tena ili swala la Muungano au kurejesha serikali ya Watu wa Zanzibar liwe wazi na lijadiliwe kwa uhuru!
 
Wakimaliza hapo, wale wazee wa Pemba watadai Jamhuri ya Pemba maana watasema Unguja haiwajali
 
Zanzibar ni mzigo.
Na pia muombe Mh. Ngeleja amuagize Kamanda Malima akuonyeshe angalu kidogo yale yanayojiri katika makbrasha anayaotembea nayo katika mabegi!!!!!!!! pengine unaweza ukaliona lile linalohusiana na huko kwenye mzigo
 
kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa tanzania, zanzibar siyo nchi! Lakini ina kila alama zinazoashiria kuwa ni nchi huru yaani; ina rais, ina bendera yake na pia ina wimbo wa taifa.

Harakati zinazoendelea hivi sasa ni kuwa zanzibar inataka kuwa na vitu vifuatavyo: Benki kuu yake, sarafu yake na kubwa zaidi inataka iwe na uhuru wa kujiamulia mambo yake yenyewe bila ya kuingiliwa.

Wazanzibari wanataka nchi yao iwe na uhusiano na tanganyika katika mfumo unaoshabihi uhusiano wa nchi zilizo katika jumuiya ya ulaya.
​swali: Kwa nini tusiwaunge mkono katika adhma yao hiyo ili sisi watanganyika tupate muda wa kutosha kujadili na kutatua changamoto zinazotukabili?

zaidi ya yote zanzibar haina hata jeshi,na askari wa zanzibar wanatambulika kama vikosi vya smz siyo jeshi. Na hata katika kesi ya uhaini ilishindikana kupata matokeo mazuri kwa upande wa serikali/waendesha mashitaka kudhibitisha kosa la mapinduzi. Maana kikatiba zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya muungano wa tanzania hivyo huwezi kupindua zanzibar.
 
zaidi ya yote hata katika michezo ya mpira wa miguu(soka) fifa zanzibar haitambuliki siyo mwanachama.Mwanachama ni tanzania.
 
At last Tanzania ndiyo inayotambulika Umoja wa Mataifa, na rais wake, wimbo wake na bendera yake. Ukumbuke kuwa Pepsi wana wimbo wao, TFF ina rais, magurudumu ya Michelin yana bendera yake. Kwa hiyo hata Zanzibar wakiwa na vyote hivyo, kama hawatambuliki haina maana yoyote. Acha Shein ajiite rais wa nchi, lakini JK ndiye atahudhuria vikao vya UN
 
Kumbuka kuwa Wazanzibari wameapa kuwa kama muundo wa muungano uliopo hivi sasa hautaondolewa katika katiba mpya itakayopendekezwa watajiondoa katika kura za maoni na kimsingi muungano utakuwa umevunjika kwa kuwa katiba iliyopo sasa itakuwa haitekelezeki!

Katiba ya Zanzibar ya sasa inasema Zanzibar ni nchi wakati katiba ya Muungano inasema Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom