JamiiForums: Tulikotoka, tulipo na tunakoelekea (hatua kwa hatua)

Nakumbuka 2007 ndio niliingia JamboForums, niliisikia toka kwa dada tangu, ile kuianza tu ikawa addiction mpaka Leo. Invisible ilikuwa ni 2007 au 2008 mlipokamatwa na kina Manumba mpaka kujaza na vurugu sana? Pia nakumbuka transition ya kutoka JamboForums kuja JamiiForums tulivyoipinga!

By the way ID yangu ya Ibambasi bado ipo? Manake nilipoteza ufunguo nikshindwa kuitumia tena. Long live JF!
 
wadau mimi toka nijiunge na hii forum nadhan nafikisha miaka 2 ingawa nimranza kuwa active mwaka huu..kikubwa nilitaka kujua jinsi ilivyoanza na mafounder waliwaza nn kutuletea huu uhondo kwani umesababisha nikache forum,na social networks zote kwa ajili ya hii.mamod na wajuvi huu uwanja wenu wa kutufumbua macho mamember wageni
 
JAmbo1.JPG
Jambo4.JPG
Jambo3.JPG
Jambo5.JPG
JAMBO6.JPG
Jambo2.JPG
 
[h=2]Wednesday, February 20, 2008[/h] [h=3]Jamboforums Chombo Cha Ugaidi Adai IGP Mwema[/h]
katika press conference jana IGP mwema alifafanua kisa cha kuwashikilia wana Jamboforum wawili. Akielezea kwa mbwembwe kabisa kwama jamboforum ni chombo cha kigaidi, mkuu huyo wa polisi alionyesha dhahiri kabisa kutofahamu kwakwe maana ya neno forums.

Hata hivyo mkuu huyo hakuzungumzia ni kwa nini hajamsweka lupongo Rostam Aziz, Jitu Patel au David Balali mpaka dakika hii. Hili limeonyesha ni jinsi gani kisiwa cha amani Tanzania kinavyotawaliwa na wababe wachache. Vilevile IGP huyo hakuelezea ni nini hitimisho la kampuni hewa za Kagoda, au Richmond.

Baadhi ya watanzania wengi waliojiwa na blog hiii walishangazwa kuona ya kwamba ni kwanini wezi wa shillingi million 152 kwa siku hawapo kizuizini mpaka leo. Na wanaokamatwa ni wale walio lia kwa miaka miwili mfululizo kuhusu wizi wa Richmond. Jee muheshimiwa IGP hii ndio haki sawa kwa wote? Jee aliyechafuliwa jina ni Rostam Azizi au Jitu Patel au? Na kama ni hao jee ni kwa nini usiwataje hadharani? Jee muheshimiwa IGP unamausiano gani na watu hao walio dai wamechafuliwa majina yao mpaka usiwataje?

Ni ufahamu wangu mdogo ya kwamba huitaji degree ya sheria ya Havard kufahamu ya kuwa muheshimiwa IGP na wenzie wametumia madaraka waliyonayo kusurpress democrasia. Wametumia jeshi na vifaa vyao vya moto kunyanyasa watanzania wachache. Jee kwa mwendo huu tutafika? Kama mtoa maoni anakwenda jela wakati Ditopile anatamba na STJ mtaani jee hiyo ni haki?

Ni wito wa wana Jamboforum kuzungumzia swala hili katika arena ya kimataifa, ni muda muwafaka kuwaumbua mandumilakuwili hawa, mandumilakuwili wajifanyao wao ni wapenda demokrasia kumbe ni madikteta. Ni muda muafaka wa kuwavua vilemba vyao vya ukoka vya kujidai wanaipenda Tanzania, kumbe wanapenda madaraka yao. Haki sawa kwa wote? Hii ni kauli ya muheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Jee haki ipo wapi? Jee ni haki hagi ambayo wengine wamekula zaidi ya million 500 na wapo mitaani, na wengine wameuwa raia kwa kusudia na wapo mtaani, na wengine wamechangia maoni yao kwenye mtandao na wako jela?

Kwa mwendo huu tunatofauti gani na iddi Amini Dada aliyewapa wahindi masaa kadhaa watimuke Uganda? Swala la kuifunga Jamboforum halina tofauti na swala la kumwagia waandishi tindikali. IGP tunaomba ufuatilie maswala yanayo ikwanza nchi kuendelea, na sio maswala yanayotia chachu maendeleo ya nchi.
Tunaomba Mh. Mwema ukamate wezi walioibia walipa kodi mabillioni ya shillingi na sio wachangiaji wa mtandao. Swala hili ni sawa na ukiukaji wa haki za msingi za binadamu, ni sawa na kuendesha gereza la siri la kutesa watu.

Jamboforums.blogspot.com copywright 2008
Posted by jamboforums at <a class="timestamp-link" href="http://jamboforums.blogspot.com/2008/02/jamboforums-chombo-cha-ugaidi-adai-igp.html" itemprop="url" rel="bookmark" title="permanent link"><abbr class="published" itemprop="datePublished" title="2008-02-20T23:20:00-08:00">11:20 PM</abbr>
 
[h=2]20 February, 2008[/h] [h=3]Jicho la Mnyika juu ya JAMBOFORUMS![/h]
Wednesday, February 20, 2008

Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA(BAVICHA), vijana wa CHADEMA tunaungana na wapenda uhuru, haki na ukweli kote nchini kulaani uamuzi wa Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwaweka ndani vijana wa wawili wa kitanzania Maxence Melo na Mike Mushi kwa sababu ya masuala ya mtandao wa Jambo Forum(www.jamboforums.com).

Uamuzi wa kuwakamata na kuwaweka ndani kwa takribani saa 24 na kuwahoji kwa zaidi ya saa 14(usiku na mchana) tunaona ni kinyume cha sheria ambayo inaeleza bayana mtuhumiwa anapaswa kuhojiwa si zaidi ya masaa manne kwa mfululizo na kwa ujumla ni uvunjaji wa haki za binadamu na haki za kikatiba za kupata na kutoa taarifa/habari. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika Jeshi la Polisi, vijana hawa wamekamatwa kwa kutuhumiwa kuendesha mtandao wa Jambo Forum ambao unadaiwa kuwachafua watu mbalimbali ambao vyanzo hivyo vya polisi mpaka sasa havijawataja.

Vyanzo mbambali vya polisi vimeeleza kuwa uamuzi wa kuwakamata vijana hawa umetokana na jeshi la polisi kupata mashtaka toka kwa watu wasiotajwa kwamba mtandao huo umekuwa ukiwachafua watu mbalimbali hususani viongozi wa serikali; suala hili nao linakwenda kinyume cha misingi ya kikatiba na kisheria. Sisi tunaamini kwamba kama kuna mtanzania yoyote ambaye anadhani amekashifiwa na mtandao huo ana haki ya kukanusha ama kuchukua hatua za kisheria kwa kwenda mahakamani. Mikakati hii ya kuzuia uhuru wa habari iliwahi kujitokeza siku za usoni pale upinzani ulipotoa &#8216;orodha ya mafisadi' na baadhi ya vyombo vya habari kuchapa majina hayo vilipewa vitisho mbalimbali na watuhumiwa hao wa ufisadi ambao walisema wamechafuliwa.

Serikali na vyombo vya dola ni vyema vikafahamu kwamba uhuru wa maoni kupitia katika mitandao unafaida zake na hasara zake, hivyo kuundoa uhuru wote kwa sababu za malalamiko ya watu wachache, masuala binafsi au migogoro ya familia Fulani ni kuukosesha umma faida ambazo zinatokana na mitandao kama Jambo Forum. Pia serikali ifahamu kwamba sheria nyingi za Tanzania zinasimamia masuala ya habari ziko kimya kuhusu masuala ya habari katika mitandao hivyo, mitandao kama Jambo Forum inalindwa kwa kanuni na mikataba ya kimataifa ambapo imesajiliwa.

Tunarudia tena kukumbusha kuwa mwanahabari ni mjumbe tu wakufikisha ujumbe katika jamii; ambaye anapaswa kulindwa na kuheshimiwa. Tabia inayoanza kuchipua ya kuwanyanyasa wajumbe au chombo kilichofikisha ujumbe tena kwa njia ambazo ni kinyume cha sheria na haki binadamu badala ya kuushughulikia ujumbe wenyewe; ikiachwa ikashamiri inaweza ikatishia ufanisi wa sekta ya habari ambayo inapaswa kudumishwa kama mhimili wa nne wa dola.

Aidha vijana wa CHADEMA tumesikitishwa na kutoweka hewani kwa mtandao wa Jambo Forum ambako kutokana na vyanzo mbalimbali inaelezwa kwamba waratibu wa mtandao huo wameshinikizwa kuufunga kutokana na shinikizo la &#8216;kigogo' mmoja wa jeshi la polisi kwa maelekezo toka serikalini.

Jambo Forum Wanahabari imekuwa mstari wa mbele kwa uwazi bila woga katika mapambano dhidi ya ufisadi na kutetea rasilimali za taifa, na kuwa sehemu ya jukwaa la sauti umma kusikika na habari kusambaa ndani na nje ya Tanzania kutia teknolojia ya habari na mawasiliano(TEKNOHAMA). Jambo Forum imekuwa mstari mbele katika kuandika tuhuma za ufisadi na/au matumizi mabaya ya madaraka zinazowakabili viongozi kadhaa wa serikali, makampuni na taasisi mbalimbali.

Mtandao wa Jambo Forums ni moja katika ya vyombo vya habari na majukwaa ya umma yaliyohusika kwa kiasi kikubwa kwa kulifunua na kuliweka wazi sakata la Richmond hasa baada ya kuweka hadharani mkataba wa Richmond na kuchambua mambo mbalimbali yanayohusiana na mkataba huo. Kashfa ya Richmond ndiyo iliyosababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Mhe. Edward Lowassa na baadaye kuvunjwa kwa baraza la Mawaziri. Jambo Forum imewezesha &#8216;siri' za ufisadi zinazofichwa na baadhi ya vigogo ikiwemo serikalini kuwekwa wazi kwa umma na watumishi mbalimbali wa serikali na taasisi mbalimbali bila majina yao kujulikana.

Mtandao wa Jambo Forum umekuwa ni changamoto kwa mitandao mingine ya serikali ikiwemo kitengo cha mawasiliano cha Ikulu kuboresha ufanisi wao katika kutumia TEKNOHAMA katika kuwasiliana kwa umma. Mtandao huo umekuwa ni ukumbi pia wa vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo polisi kupata mawazo mbalimbali ya umma kuhusu masuala ya uhalifu yanayopaswa kufuatiliwa.

"Inashangaza badala ya serikali kutoa ushirikiano kwa mitandao kama hii inakuwa mstari wa mbele kuona kwamba inafungwa. Huku ni kukinzana na dhamira ya Rais Kikwete ya kuongeza uhuru wa habari na haki ya Taarifa hapa nchini. Sisi tulitegemea vipaji vya vijana wanaotengeneza mitandao mbalimbali vikuzwe kwa maslahi ya Taifa badala ya kukamatwa".

Vijana wa CHADEMA tunatoa rai kwa umma kutochukulia suala hili kuwa ni tukio dogo linalowahusu vijana wawili waliokamatwa bali litazamwe kama tukio linalohusu maslahi ya taifa, uhuru wa vyombo vya habari na haki za kikatiba za kupata na kutoa taarifa/mawazo.

Hivyo tunaitaka serikali kutoa tamko la kina lenye kueleza ni kwa sababu zipi zilizopelekea kukamatwa na vijana hawa na walalamikaji ni wakina nani. Pia serikali itoe tamko rasmi kama imeufungia mtandao wa Jambo Forum au la na tunawataka watanzania wanaoratibu mtandao huo kwa mapenzi mema ya nchi yao waurudishe mtandao huo hewani mapema iwezakanavyo wakati tamko la serikali linasubiriwa. Kadhalika tunatoa rai kwa yoyote ambae anadhani hajatendewa haki ama amechafuliwa na Jambo Forum ajitokeze kukanusha au kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtandao huo badala ya kulitumia jeshi la polisi ama baadhi ya watu kuhujumu haki ya umma ya kupata na kutoa taarifa.

Katika mataifa mbalimbali duniani, mitandao kama Jambo Forum inachukuliwa kama sehemu ya vyombo vya habari na mahali pa umma kukutana kujadili masuala mbalimbali. Hivyo uamuzi wa kufungia Jambo Forum, ni sawa na uamuzi wa kufungia chombo kingine cha habari kama redio, televisheni na magazeti. Kadhalika, uamuzi wa kufungia Jambo Forum ambapo umma wa watanzania kwa maelfu umekuwa ukikutana kujadili masuala mbalimbali ni sawa na kupiga marufuku kukusanyika huko ambapo ni kinyume cha katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu. Mwisho, tunaitaka serikali na vyombo vya dola visidhani Jambo Forum ni Maxence Melo ama Mike Mushi bali mihimili ya Jambo Forums kwani ni umma wa wachangiaji na wasomaji waliosambaa hapa nchini na nchi mbalimbali ambao baadhi yao wanaweza kukamatwa, majukwaa yao kuweza kushambuliwa, lakini mawazo yao ya mabadiliko yataishi milele hata pale ndoto ya maendeleo, uhuru na umoja itakapotimia katika taifa letu.


Imetolewa tarehe 20 Februari 2008 na:


John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana
0754694553
 
Hongera sana mliokuwepo,
kumbe ukiona vinaelea vimeundwa.


Nakumbuka mie wakati naingia hapa wanachama hawakufika hata 1,500 sasa wanakaribia 90,000!!!! halafu akina dada walikuwa wachache mno!!! sidhani kama walifika hata 10 mpaka watu wakawa wanaombwa wahamasishe akina dada wajiunge hapa, leo hii wako wa kumwaga na michango yao imeenda shule sana. Waache wale magamba waiogope JF maana wanaiona ni tishio kubwa sana kwa wao kuweza kutimiza ndoto yao ya kuitawala Tanzania milele.
 
Donate VISA, MASTER CARD..(That was meant for foreigners, TZ leaving abroad and class of people, mostly with NBC and CRDB accounts (as then was)

Leo we dare to say. DONATE: M-PESA, TIGO PESA, AIRTEL MONEY NMB MOBILE, VODA/ TIGO RUSHA etc..:eyebrows:

Wekeni hizo number hadhalani tuchangie, wengi hatuzijui. Hongereni sana mpaka kufika hapa.
 
Back
Top Bottom