JamiiForums SMS Alert is LIVE

Status
Not open for further replies.

Mike Mushi

JF-Expert Member
Feb 10, 2006
253
572
Wakuu

Kwa muda sasa (miezi nane) tumekuwa tukihangaika kutengeneza huduma ambayo itatupa sisi uwezo wa kuweza kutumia watu ujumbe mfupi kwa njia ya simu (SMS) habari na mambo motomoto pale yanapoingia JamiiForums. Na lengo limekuwa pamoja na sisi kutuma hizo habari, basi iwe pia ni njia ya kupata kipato tuweze kujiendesha kwa ufanisi.


Katika harakati za kuanzisha huduma hii tuliamua kusajili 'short code' yetu TCRA (15346).

Tumekumbana na matatizo kwenye kukubaliana na makampuni ya simu, ili waweze kuwaunganisha wateja wao na hiyo short code yao kwenye mitambo yao sisi tuweze kuanza kutoa huduma:

TiGo walisema "NO" (Yes just the word NO bila maelezo zaidi) kwa proposal yetu.

Airtel & Zantel Revenue Sharing ilikuwa mbaya sana.

Vodacom wakakubali; Tunaanza na Vodcom kwa exclusivity deal ya miezi sita ya kwamba tusi-approach mitandao mingine kwa ajili ya kujiunga na baada ya hapo tutaweza ku approach tena mitandao mingine. Wao kwa upande wao Wata-advertise hii kampeni kwenye blog zote (Michuzi, Global Publisher, Millard Ayo.... na nyingine kama 20) na kama mambo yote yatakwenda kama tunavyotarajia, basi itatangazwa kwenye magazeti na radio. Na pia tutagawana mapato JF na Vodacom 50/50. Ambapo sisi (JF) hiyo 50 tutagawana na Aggregator (Kampuni inayo-handle maswala ya kuunganisha kati yetu sisi na vodacom) Makampuni yote Tigo, Airtel, Vodacom na Zantel revenue sharing ya premium sms kama sisi tunayotoa ni 75/25.


Kujiunga ili uweze kupata breaking news and news alerts kutoka JF Tuma sms "Jiunge JF" kwenda 15346

Vigezo na Masharti


1. Ujumbe zote zitatozwa gharama ya Tshs 150
2. Mteja hatatozwa kwa kujiunga ama kujitoa kutoka Jamii alerts
3. Mteja anakubaliana na vigezo na masharti za Jamii forums.
4. Jumbe zitatumwa kwa umuhimu na wakati habari zinapochipuka.
5. Huduma hii inapatikana kwa wateja wa Vodacom pekee (kwa kuanzia)

Kujiondoa tuma neno Jiondoe JF kwenda 15346

Ukipenda pia uwe unapokea taarifa kuhusu Biashara, Kazi, Mapenzi na Michezo ... Bonyeza hapa kujiunga

Unaruhusiwa kuwaambia Ndugu, Jamaa na Marafiki ambao hawapo JamiiForums kujisajili.

Habari zitakazotumwa ni ambazo zimekuwa verified na JF administration





 
Nice one...hongereni sana kwa kunzisha huduma bora...ni hatua kubwa sana mliyofikia...too bad sitaweza kuifaidi mapema maana mimi sio mtumiaji wa Vodacom.
 
Mkuu shukran sana, ntaconnect muda si mrefu.......just wanted to know ni nyuzi zipi hasa tutakuwa notified? zile ambazo ziko verified au any post inayowekwa?

Ambazo zipo verified.
 
Mkuu nimekupata lakini mie namba yangu ya VODA ni Post-paid, kwa makato hayo ya 150, yakionekana kwenye ankara ya mwezi, huenda kibarua changu kwa MUHINDI kikaota nyasi, CHEZEA MUHINDI WEYE......! LOL

Nasubiri mkiiingia mkataba na TIGO, nitasongesha.........
 
Mkuu nimekupata lakini mie namba yangu ya VODA ni Post-paid, kwa makato hayo ya 150, yakionekana kwenye ankara ya mwezi, huenda kibarua changu kwa MUHINDI kikaota nyasi, CHEZEA MUHINDI WEYE......! LOL

Nasubiri mkiiingia mkataba na TIGO, nitasongesha.........

Baada ya miezi sita kama hii program ikifanya vizuri. Naamini tukirudi tena Tigo tutakubaliwa. Tatizo ni kwamba kila Makampuni ya simu yanaogopa JAMIIFORUMS hawataki kufanya chochote kinachohusu JAMIIFORUMS. Ni kwamba nani atakuwa wakwanza then wengine wote watafuata.

Kazi nzuri wadau...nimejiunga tayari!

Charge ya Tzs 150 ni pamoja na VAT?

Yes VAT inclusive

Asante mkuu, tayari nimeregister

Shukran sana!
 
Naomba kueleweshwa, hiyo charge ya Tzs 150 ni kwa kila breaking news, ama kwa siku? manake kwa Jf breaking news zitakuja ka 50 kwa siku! ufafanuzi tafadhali.
 
hongereni wakuu mimi niko Airtel na Tigo anyway nitafanya utaratibu nipate simu nyingine ili niweke line ya Voda..
 
Naomba kueleweshwa, hiyo charge ya Tzs 150 ni kwa kila breaking news, ama kwa siku? manake kwa Jf breaking news zitakuja ka 50 kwa siku! ufafanuzi tafadhali.

Sio kila thread ikiingia JF basi utakuwa unatumiwa SMS hapana. Ni pale tuu tutakapopata breaking news ambayo tunaamini it worth sending an sms kutaarifu watu ndipo tutatuma sms. 150 kwa kila sms utakayopokea and mostly, ni moja kwa siku au siku zingine hakuna sms kabisa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom