JamiiForums: Msimamo wetu na maelezo kidogo

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu,

Kadiri siku zinavyokwenda ndivyo idadi ya watumiaji na watembeleaji wa mtandao huu wanavyoongezeka. Tungependa kutoa ufafanuzi juu ya mambo kadhaa ambayo watumiaji wa mtandao huu wanatakiwa kufahamu:

  1. JamiiForums ni mtandao ambapo mtu yeyote anayejisajili anaweza kuanzisha hoja (user generated content) hivyo maoni yanayotolewa na wadau tofauti ni misimamo yao na hayawakilishi maoni ya waendeshaji na waratibu wa mtandao huu kwa namna yoyote ile. Waendeshaji wa mtandao huu wapo kusimamia sheria zilizowekwa pamoja na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
  2. Waendeshaji wa mtandao huu hawataweza kukuzuia kama mtumiaji kutumia mtandao huu bila kuvunja sheria zilizowekwa au kama hujakosea kulingana na maelezo haya.
Tunatoa tahadhari kwa wale wenye kudhania JamiiForums ipo kisiasa na kila kitu ni siasa tu kuwa jukwaa hili lipo na maeneo tofauti, kama huziwezi siasa basi achana nazo na ingia eneo unaloona unastahili.

Hatutowavumilia wale wanaotaka kuharibu mijadala makusudi ili aidha kuwakatisha tamaa washiriki au kuligawa taifa kwa udini, ukabila au rangi.

Kwa pamoja tunaweza kushirikiana kuhakikisha JamiiForums inabaki kuwa sehemu nzuri na ya kushiriki mijadala anuai bila kukerana au kuchafuana.

Kama umejisajili, unaweza kutufahamisha hoja yoyote unayoona inapelekea kuvurugika kwa mjadala (si kuijibu wala kuinukuu) kwa kubonyeza alama hii chini ya hoja husika:

report.png


Tunaendelea kusisitiza kusoma hoja hizi kwani tunaamini zitarahisisha kuelewa nini kinafanyika hapa na kwanini:

  1. JamiiForums Rules
  2. How to use JamiiForums effectively
  3. JF: Majina bandia na uhuru wa maoni
  4. Topic gani hufungwa au kufutwa kabisa JF?
Kama una maswali wasiliana nasi tukusaidie haraka iwezekanavyo kupitia: support@jamiiforums.com
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom