Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,492
- 92,927
na Hellen Ngoromera
Mtandao huo ulianzishwa mwaka 2006 na madai hayo kwamba mtandao huo unafanya kazi hatarishi dhidi ya CCM na serikali yana lengo la kuuchafua na kuuvunjia hadhi ambayo imejijengea kwa gharama kubwa na kwa muda mrefu.
"…Ni jaribio dhaifu la Chama cha Mapinduzi kubebesha lawama mitandao ya intaneti kwa mapungufu na migongano iliyojitokeza ndani ya chama chao katika miaka michache iliyopita na siku za karibuni," ilisema taarifa hiyo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, mtandao huo unaotembelewa na wastani wa watu 20,000 kwa siku umekanusha madai hayo kwa maelezo kuwa hayana msingi wala ukweli.
"Tunapinga vikali madai yasiyo na msingi ya Chama cha Mapinduzi kuhusu umiliki, malengo na nafasi ya JF (Jamii Forums) katika medani ya vyombo vya habari nchini na mchango wake katika mijadala ya kisiasa nchini," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Ilisema kwa mara ya kwanza waliyasoma madai hayo yakiwa yameripotiwa kwenye magazeti mawili ya kila siku.
Kwa mujibu wa mtandao huo hawajawahi kufadhiliwa na CHADEMA lakini wanaamini kuwa wamelengwa na CCM kwa sababu katika miaka mitano iliyopita mtandao wao umekuwa ukishiriki vilivyo kufichua kashfa mbalimbali ambazo zimelindima nchini hatimaye kusababisha chama tawala kuamua kujivua gamba.
Mtandao huo umesema madai hayo yamesomwa na kusikiwa na watu wengi nchini hivyo kuwasababishia usumbufu mkubwa. Yamesababisha wasiwasi usio wa lazima kwa wanachama 40,000 ambao wametawanyika pote nchini na katika kila kona ya dunia.
Madai hayo ya CCM yalitolewa hivi karibuni mkoani Dodoma na Msekwa wakati wa kutambulisha uongozi mpya wa chama hicho.