JamiiForums Issues an Official Responce to CCM allegations: (Press Release)

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
From Fikra Pevu - Political Paranoia? Tanzania's Ruling Party threatens online social media | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

The above (LINK) is the statement issued earlier today by JamiiForums - the most prominent Tanzanian online social gathering. The popular political forum played a crucial role in a lead up to the General Elections in October 2010 by being the most authoritative source of politica news, discussion and debate. However, few days ago JamiiForums came under a well calculated and targeted attack by the ruling party - Chama cha Mapinduzi - which accused the forum for being "anti-CCM" and "anti-government".

The statement was distributed to a variety of media outlets in the country and abroad as well as to a number of interested parties.

NIPASHE:

Mtandao wa Kijamii wa Jamii Forums, umekanusha madai yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Pius Msekwa, kuwa umeanzishwa na vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwamba unatumiwa na chama hicho katika harakati zake za kisiasa hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jamii Forums, unafanya kazi kwa kujitegemea na kwamba haumilikiwi na chama chochote cha kisiasa wala kufadhiliwa na Chadema kama alivyodai Msekwa.

Taarifa hiyo ilisema Msekwa alitoa madai hayo wiki iliyopita wakati akitambulisha Sekretarieti mpya ya CCM mjini Dodoma ambapo alitumia muda wake kushutumu mtandao huo.

Mtandao huo ulisema kwa sasa una wanachama 40,000 waliojiandikisha na kwamba unafanya kazi kama chanzo huru cha habari bila kutumiwa na mtu wala chama chochote cha siasa.

Shutuma hizo za Msekwa zilitolewa Aprili 14, mwaka huu mjini Dodoma ambapo pia mwanasiasa huyo alisema mtandao huo ulichangia kukikosesha kura CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba shutuma zinazotolewa dhidi yao kwamba unatumika kuivuruga CCM na serikali yake sio za kweli na kwamba zinalenga kuukwamisha mtandao huo katika harakati zake za kuielimisha jamii na kuipasha habari.

Mtandao huo ulisema CCM inauandama kutokana na wao kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita vitendo vya rushwa ambavyo hivi karibuni vimekichafua chama hicho na serikali yake.

Shutuma hizo zimewasababishia usumbufu kutoka kwa wanachama wao walioenea kona zote za nchi na nje ya nchi na kwamba hatua hiyo ya CCM ni ishara kuwa kimeanza kuuogopa mtandao huo.
 
This is good...but I also think at the end the forumist owner should have encourage sekretarieti mpya kujiunga na JF and engage in useful discussion just like other politicians do e.g Kabwe Z, and Slaa W.
 
This is good...but I also think at the end the forumist owner should have encourage sekretarieti mpya kujiunga na JF and engage in useful discussion just like other politicians do e.g Kabwe Z, and Slaa W.

Nsiande, kina Kabwe na Slaa hawakukaribishwa; kwanini tuwape huo umuhimu hao watu wa sekretariati ya CCM? kwa ujiko gani walionao. Wanajua anuani ya JF - https://www.jamiiforums.com kuna mahali pale juu panasema "register"...
 
Dawa ya moto sio maji, ni moto. CCM waache unazi. Kama walikuwa na MAGAMBA, wangeshindaje kwa kishindo. Wavue magamba (wawe makini wasijejikuta bila kivazi) watoe na sumu walizozipanda hao MAGAMBA.

Msekwa alipokuwa spika hakuwa GAMBA kama sasa.

Keep it up JF.
 
Eti JF imekuwa anti CCM & anti government! hao magamba wasitafute visingizio. Wafanye utafiti wajue nini ni MOOD ya taifa hivi sasa. Hivi ni nani aipende CCM kwa dharau wanazozifanya kwa watanzania?
 
Nsiande, kina Kabwe na Slaa hawakukaribishwa; kwanini tuwape huo umuhimu hao watu wa sekretariati ya CCM? kwa ujiko gani walionao. Wanajua anuani ya JF - https://www.jamiiforums.com kuna mahali pale juu panasema "register"...

Kwa kuongezea ni kwamba hiyo CCM mpaka ikajua kwamba kuna JF maana yake ni kwamba huwa wanaingia kusoma threads as guests, kwanini wasichukue jukumu la kujiandikisha rasmi?

Nina uhakika kwamba akina Makamba (Januari) na Nape ni members wa hapa lakini hawana ujasiri wa kuhimili madongo mazito ambayo huelekezwa kwa CCM.

Tatizo la CCM hawataki kuwa criticized, na ukionekana unawa-criticize watataka wakutumie ili kuficha uozo wao. Ninakumbuka kuna siku Mwanakijiji amlimhoji Ngeleja, mwisho wa hiyo Interview Ngeleja bila aibu alitamka kwamba Mwanakijiji naomba utupigie debe maana wewe una-influence kubwa au watu wanakuelewa [sina hakika na hayo niliyopigia mstari specifically, lakini aliomba kupigiwa debe]. Hilo pekee linaonyesha kwamba hawana uwezo wa kujenga au kutetea hoja zao, wanataka mtu wa nje awatetee wao. Ndio maana kila kukicha wakishaona kuna mpinzani anawapelekesha puta wanaishia kumrubuni na kumhamishia kwenye chama chao, akishafika huko anakuwa mpiga debe ambaye hana hoja.
 
Thans kwa press release. Magambaparty, jf always ni watu makini. Kama mwaweza anzisheni yenu.
 
Hivi kwa ujuba walionao wanafikiri jf kurejista unaulizwa chama gani??mpaka waone wana jf na jf niwapinga ccm na sirikali??Nachokijua jf ilianza na moja mpaka namba ilipo haikuanza na anti ccm!or gvnmnt!!Hivyo unaowaona humu niwatu waliochoka kudhurumiwa na kulipwa kwa maneno na upande wa kanga ba tshart,kapelo!!Hawataki kusikia!
 
Wanadhani bado tupo enzi za zidumu fikra za mwenyekiti, waache unazi wao.
Tatizo ccm hawataki kubadilika, sasa mabadiliko lazima yaendelee either waadapt au waperish.
Najua wamo humu tatizo mnashindwa kujibu hoja.
Mlidhani kama mlivyochagua speaker wakuwapendelea basi mtapata mamods wa kuwabeba.
sasa CCM MJUE JF NI BUNGE MBADALA,
@#$%^&*()_+ U
 
Nsiande, kina Kabwe na Slaa hawakukaribishwa; kwanini tuwape huo umuhimu hao watu wa sekretariati ya CCM? kwa ujiko gani walionao. Wanajua anuani ya JF - https://www.jamiiforums.com kuna mahali pale juu panasema "register"...

Kama mwenyekiti wa chama cha magamba alimkimbia mgombea mwenzake wa urais Dr Slaa kwenye midahalo ya wazi, unadhani ndani ya chama hicho kuna watu wenye uwezo wa kujenga hoja na kuzisimamia? wao kazi yao ni kuingia humu nakuwa upande wa Guests basi, na ndio maana hata makuwadi wao wanaowatumia kuja humu hawaji na hoja yoyote, zaidi ya kuvuruga mada za msingi wanazojadili watu. wao siasa zao ni Dr Slaa tu. kumbe kama kuna mtu wanaotakiwa kumuogopa sana kwa sasa ni Tundu Lissu.
 
Nsiande, kina Kabwe na Slaa hawakukaribishwa; kwanini tuwape huo umuhimu hao watu wa sekretariati ya CCM? kwa ujiko gani walionao. Wanajua anuani ya JF - https://www.jamiiforums.com kuna mahali pale juu panasema "register"...
Mtu mwenye hoja hahitaji mwaliko na yule asiye na hoja ukimbia midahalo na haoni umuhimu wake,CCM kutokana na ufinyu wa mawazo na mazoea ya kua CCM tofauti na juu ya vitu vyote.Tatizo hili limevifanya vichwa vyao kua vivivu kufikiri na kukimbilia njia za mkato "KUTAFUTA WACHAWI WAO"wakati wa uchaguzi ambapo ni wakati mzuri wa kunadi sela kwenye midahalo wao waliingia mitini.CCM WAKATI WA KUONGOZA KWA MAZOEA UMEPITWA NA WAKATI!Mungu ibariki Tanzania
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom