JamiiForums ilivyosaidia (Mengine ya Upinzani yana Ukweli, Polisi wanatumiwa)

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,910
Baada ya kufunguwa nyuzi humu JF tarehe 27-09-2012 "Mengine ya Upinzani yana Ukweli... Polisi wanatumiwa", siku ya pili yake (28-09-2012) niliweka hii update:

Latest Update:

Watuhumiwa 3 wamewachiwa leo kwa dhamana, mtuhumiwa mmoja hana mashtaka ya kujibu, kawachiwa huru.

Kesi imebadilishwa badala ya Millioni 80 imekuwa Elfu 80!.

OCD wa Wazo Hill kahamishwa kituo.

RPC Kinondoni na RCO wabishana kuhusu hili sakata!

Nimeongea kwa simu na mmoja kati ya ndugu wa watuhumiwa, anakuja kunielezea kwa kirefu jinsi hii nyuzi ilivyosaidia. Nikipata habari kamili ntakuja ifungulia nyuzi.

Katika hiyo update niliahidi kurudi na kufunguwa nyuzi kuelezea kwa kirefu jinsi "nyuzi" ile ilivyosaidia. Ukweli ni kwamba nyuzi ile isingekuwepo "Jamii Forums" isingepelekea kuwa na "impact" iliyodhamiriwa.

Siku ya pili (28-09-2012) ilibidi watuhumiwa wapelekwe mbio mbio mahakamani asubuhi na mapema, licha ya kuwa jalada lao lilishafikishwa kwa Polisi wapelelezi (mmoja wao anaitwa David) kutoka kwa (DPP) siku mbili kabla likielekeza kuwa watuhumiwa hawana mashtaka ya kujibu na wawachiwe. Cha kusikitisha ni kuwa huyu David amma alikuwa anafanya makusudi kabisa kuendelea kuwazuia watuhumiwa dhidi ya hitimisho la DPP, huyu David ana kila sababu ya kufanya makusudi kwani baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho cha mafuta wanasema toka hii kesi ilipoanza (inawezekana na kabla pia kwani wafanyakazi waliobaki hapo ni wapya) huyu David alikuwa akienda kumiminiwa petroli ya bure mara kwa mara pale pale kituo cha GBP kinachomilikiwa na Bwana Badr, amma huyu David alikuwa na shinikizo kutoka kwa OCD wa Wazo Hill (kahamishwa kituo juzi) ambae nae alikuwa na shinikizo kwa wakubwa zake kuwa asiwawachie, ukweli ni upi? sijui. Lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Walipofikishwa asubuhi hapo mahakamani, mwendesha mashtaka hakuwa na kesi ya kuwasomea wala kuwafungulia kwani ilishaelekezwa waachiwe. Mpelelezi David, badala ya kuwawachia, akawachukuwa tena na kuwarudisha rumande kituo cha Polisi Wazo Hill ili mradi tu, kwanini waachiwe. Hapo ndipo kikundi cha watu waliokwenda mahakamani kuwawekea dhamana hawa watuhumiwa walipopaza sauti zao na kusema leo "mpaka kieleweke" na hatukubali warudishwe Polisi. Mpelelezi David wakati huo anaambiwa maneno hayo alikuwa anatabasamu na kucheka kidharau, kuonesha kuwa ndio wanakwenda na hamna mtachoweza kufanya.

Naomba ieleweke kuwa siku hiyo mahakamani walikuwepo watu wengi waliojitolea kwenda kuwawekea dhamana hawa vijana kiasi cha kustaajabisha, vipi wezi wa Millioni 80 wawe na wadhamini wengi namna hiyo, wake kwa waume? Waliojitolea na kupeleka hati za nyumba zilizothaminiwa walikuwa hawapungui 6, watumishi wa idara za Serikali ambao ndiyo mara nyingi huwa wanatakiwa wa wadhamini watuhumiwa wenye kesi kubwa walikuwa hawapungui 20 kila mmoja na barua ya dhamana, licha ya wafanya biashara na wengineo wengi waliojitokeza kuwadhamini hawa vijana. Wengi wao, habari zilizopelekea wajitokeze kwa wingi ni hizi zilizorushwa Jamii Forums.

Baada ya watuhumiwa kurudishwa tena Polisi pasi na haki, akajitokeza Wakili na kujitolea kufatilia hili sakata kwa RCO hapo Oyster Bay Police, baada ya wakili kukutana na RCO na RPC, mpelelezi David akaitwa na baada ya kujadiliana humo ndani na "Mtandao wa Kijamii" ukitajwa mara kadhaa ikaamuriwa warudishwe tena Mahakamani, DPP akapigiwa simu atayarishe mashtaka ya wizi wa lita 40 za mafuta yenye thamani ya Shillingi 80,000 (elfu themanini) na kituo cha Polisi cha Wazo Hill wakaamuriwa wawarudishe tena watuhumiwa mahakamani wasomewe mashtaka.

Watuhumiwa waliporudishwa mahakamani, mmoja akaachiwa kabla ya kufikishwa kwa hakimu, (Huyu ni dereva Mzee wa Zaidi ya miaka 65) na alipoachiwa alibubujikwa na machozi huku akisema "hii dhulma italipwa na Mwenyeezi Mungu hapa hapa duniani, iwe Badr au yeyote yule, Mwenyeezi Mungu atanihukumia". Wengiine watatu wakafikishwa kwa hakimu na kushtakiwa kwa shtaka la wizi wa mafuta Lita 40. Wakaambiwa dhamana iko wazi na wakadhaminiwa kwa dhamana ya mdhamini mmoja mmoja kila mmoja na kwa thamani ya elfu 30 (za maandiko) kila mmoja.

Jamani, Mheshimiwa Rais Kikwete alipoona Polisi inaadhibu na kutesa watu kwa kuwabambikia kesi za ajabu ajabu na kupunguza msongamano magerezani, akaanzisha mfumo wa waendesha mashtaka (DPP) ambao hawahusiani na Polisi, cha kushangaza ni kwenye tukio kama hili na nna uhakika yapo mengine mengi tu, pale DPP anapoona watuhumiwa hawana mashtaka ya kujibu lakini Polisi wanapokuwa na kiburi na ushupavu wa kuwarudisha tena polisi watuhumiwa na kuwafungulia kesi za kuwabambikia na wakubwa wa Polisi kushinikiza yafunguliwe mashtaka haraka haraka mradi tu wajilinde wao na waoneshe kuwa hawakuwashikilia bure bure kwa siku 9.

Sitaki kuyasema mengi kwa kuwa hii kesi ipo mahakamani kwa sasa, nimejaribu kuelezea yaliyojiri kabla ya hii kesi kufikishwa mahakamani na yaliojiri kupelekea kurudishwa tena mahakamani na kuwachiwa amma kupewa dhamanana jinsi Jamii Forums ilivyosaidia.

Ni dhahiri kuna uonevu wa hali ya juu katika hili sakata na kuna shinikizo la kifedha, cha kushangaza zaidi ni pale ambapo hakuonekana mahakamani bwana Badr mmiliki wa GBP ambae ndio walalamikaji, wala mawakala wa GBP Nassoro (Nasa) na Musa ambao walikuwa wakionekana mara kwa mara huko kituo cha Polisi cha Wazo Hill wakiingia ofisini kwa OCD (licha ya huyu OCD kukataa katakata kuonana na ndugu, jamaa na marafiki wa watuhumiwa, lakini alivyofika Nassoro na Musa walikuwa wanaingia ofisini kwake kama wako nyumbani kwao!). Jee Mwakilishi wao mahakamani alikuwa Mpelelezi David? inashangaza sana!

Halima Mdee upo? haya yanatendeka jimboni kwako. Nna uhakika umeisoma hii habari lakini labda kwako kufunguwa matawi huko Boko ni bora zaidi kuliko kusimamia dhulma ya wana jimbo lako.

Wote waliochangia ile nyuzi (Mengine ya Upinzani yana Ukweli... Polisi wanatumiwa), walioniponda na walioniunga mkono napenda kuwajulisha kuwa mmechangia kwa njia moja amma nyingine kupaza sauti za wanyonge walioshikiliwa bila dhamana kinyume cha sheria. Naomba muendelee kutoa maoni yenu kistaarabu zaidi ili wanaoyasoma haya wasichoke kuyasoma, yana impact kubwa sana, tukubaliane kutokukubalina.

Kwa mara nyingine ahsante JF.
 
Huwezi kuandika bila kumtaja Halima, kama umemdondokea si umweleze.

Hata hivyo nakupongeza sana kwa jitihada zako ulizofanya kuhakikisha kuwa haki inatendeka.

kukubaliana kutokubaliana kuanze na magamba wenzio ambao hawataki kukubaliana kutokubaliana na kufanya mpaka hila za kishetani ili wakubaliwe wao.
 
Usinambie magwanda walipoongozwa na Mbowe na Slaa kwenda Ikulu kukubaliana kuto-kukubaliana na Kikwete (gamba Orijino) umesha sahau!
 
MDEE kwake ni bora kufungua matawi kuliko kujihusisha na masuala ya kutetea wanyonge, Hii ndio true colour ya CHADEMA, Hongera mkuu zomba kwa msaada wako.
 
Nikwambie tu kwamba kuna mazingira mengine yanakuwa magumu kwa wabunge zaidi ya ilivyokuwa kwako... Sio wa CCM, sio wa upinzani, inapofika kukabiliana na dola, hali ni mbaya sana hapa Tz. Hongera angalau wewe uliweza kuongea OCD akitembea, akakuacha. Muulize Dk Kigwangala yaliyomkuta kule Nzega alipotetea wananchi dhidi ya polisi. Muulize yule mama wa CUF (mbunge viti maalum Tabora, jina limenitoka), alivyolala rumande siku chungu nzima kwa kukabiliana na polisi akitetea wananchi. Kwa hiyo ndugu yangu zomba usione wengine tunapigia upinzani debe hapa, sio kwamba tunataka chama fulani kiingie madarakani, no. Tunaamini hiyo inaweza kuwa njia mojawapo ya kupaaza sauti za wanyonge dhidi ya waonevu wanatetea matumbo yao. Kwa taarifa yako mimi (na wengine wengi), siku chama cha upinzani ninachosapoti kikiingia madarakani, ndio siku nitakapokipa talaka, na kusapoti chama kitakachokuwa kikuu cha upinzani, lengo ni kuhakiisha serikali yeyote itakayokuwa madarakani inakuwa na wamulikaji na wapiga kelele, ili kwa kiasi fulani iwe makini.
 
Last edited by a moderator:
Naona sasa Zomba umeanza kuona jinsi hii serikali yako yenye watumishi waonevu!

Hongera kwa kutujuza zomba!

Ila hipo siku utaachana na siasa uchwara!

Asante kwa kutujuza!
 
Naona sasa Zomba umeanza kuona jinsi hii serikali yako yenye watumishi waonevu!

Hongera kwa kutujuza zomba!

Ila hipo siku utaachana na siasa uchwara!

Asante kwa kutujuza!

Naomba nimnukuu Ramos, kaandika maneno mazito sana hapa:

Nikwambie tu kwamba kuna mazingira mengine yanakuwa magumu kwa wabunge zaidi ya ilivyokuwa kwako... Sio wa CCM, sio wa upinzani, inapofika kukabiliana na dola, hali ni mbaya sana hapa Tz. Hongera angalau wewe uliweza kuongea OCD akitembea, akakuacha. Muulize Dk Kigwangala yaliyomkuta kule Nzega alipotetea wananchi dhidi ya polisi. Muulize yule mama wa CUF (mbunge viti maalum Tabora, jina limenitoka), alivyolala rumande siku chungu nzima kwa kukabiliana na polisi akitetea wananchi. Kwa hiyo ndugu yangu zomba usione wengine tunapigia upinzani debe hapa, sio kwamba tunataka chama fulani kiingie madarakani, no. Tunaamini hiyo inaweza kuwa njia mojawapo ya kupaaza sauti za wanyonge dhidi ya waonevu wanatetea matumbo yao. Kwa taarifa yako mimi (na wengine wengi), siku chama cha upinzani ninachosapoti kikiingia madarakani, ndio siku nitakapokipa talaka, na kusapoti chama kitakachokuwa kikuu cha upinzani, lengo ni kuhakiisha serikali yeyote itakayokuwa madarakani inakuwa na wamulikaji na wapiga kelele, ili kwa kiasi fulani iwe makini.
 
Last edited by a moderator:
Usinambie magwanda walipoongozwa na Mbowe na Slaa kwenda Ikulu kukubaliana kuto-kukubaliana na Kikwete (gamba Orijino) umesha sahau!
sasa nadhani akili imekukaa sawa baada ya masahiba haya kukukuta na siku nyingine ukiona mwenzio anapaza sauti jaribu kumsikiliza na sio kubeza kama mnavyofanyaga hapa na jamii yako i.e rejao,ritz n.k, kwani umewaona hata kwenye series ya hizi thread zako walijaribu hata kukupa mawazo, bora sisi tuliokuponda lakini mwisho wa siku umeona juhudi zetu. Ila pole kwa masahiba hayo na mungu awaongoze kujinasua na udhari huu wa policcm
 
Nikwambie tu kwamba kuna mazingira mengine yanakuwa magumu kwa wabunge zaidi ya ilivyokuwa kwako... Sio wa CCM, sio wa upinzani, inapofika kukabiliana na dola, hali ni mbaya sana hapa Tz. Hongera angalau wewe uliweza kuongea OCD akitembea, akakuacha. Muulize Dk Kigwangala yaliyomkuta kule Nzega alipotetea wananchi dhidi ya polisi. Muulize yule mama wa CUF (mbunge viti maalum Tabora, jina limenitoka), alivyolala rumande siku chungu nzima kwa kukabiliana na polisi akitetea wananchi. Kwa hiyo ndugu yangu zomba usione wengine tunapigia upinzani debe hapa, sio kwamba tunataka chama fulani kiingie madarakani, no. Tunaamini hiyo inaweza kuwa njia mojawapo ya kupaaza sauti za wanyonge dhidi ya waonevu wanatetea matumbo yao. Kwa taarifa yako mimi (na wengine wengi), siku chama cha upinzani ninachosapoti kikiingia madarakani, ndio siku nitakapokipa talaka, na kusapoti chama kitakachokuwa kikuu cha upinzani, lengo ni kuhakiisha serikali yeyote itakayokuwa madarakani inakuwa na wamulikaji na wapiga kelele, ili kwa kiasi fulani iwe makini.

Hapo kwenye wino mwekundu......

mimi niko pamoja sana na wewe Ramos...mimi nilikuwa kada mzuri sana wa CCM.....tangu nikiwa chuo kikuu......kutokana na kushindwa kusikika sauti ya wanyonge nikachukua hatua makusudi kujiunga na CDM, wakati huo nimeishakuwa msomi mzuri tu mwenye shahada ya PhD mkononi....

wanaMAZOEA walinishangaa sana na baadhi ya macollege mates wangu ambao sasa hivi ni wanene wazuri tu hapa nchini kuwa nimepata KICHAA......kwa upande mmoja unaweza kukiita ni ukichaa kwani nilipishana na mambo mema ya nchi hii...kwani ulikuwa umefika wakati wa mimi kuenjoy mema ya nchi kama wao wanavyoenjoy,,,,,....

argument yangu ni kuwa nilishindwa kushindana na conscience yangu......ninaamimni kabisa kuwa katika nchi ambayo huduma za jamii na za msingi kama elimu, afya makazi bora nk zimegeuzwa kuwa bidhaa na sio HAKI maisha hayawezi kuwa mazuri hata uwe na magunia elfu zaba ya noti za buku ten ten......

nashukuru pamoja na adhabu nyingi ninazopewa na state, kwa kupitia mwajiri wangu... umma umeanza kuelewa kidogo kidogo na tafsiri yangu imeanza kuonekana..hivyo bakora ninazochapwa sio za bure.....

kwa sasa ninapigania kuona CCM iliyokaa kushoto lakini isiyokufa..... nawaencourage vijana wangu ninaokutana nao kikazi ambapo wako ccm na wako upright kuwa wajitahidi ili ccm iendelee kuwepo kama taasisi imara ya kuifunga chadema kengele......naendelea kuwahimiza kuwa vyama vingi hutoa fursa kwa wagombea wazuri kutoka pande zote kuonekana kugombea na kuheshimiwa.....

pengine Chadema itapoingia madarakani, nitaacha akujihusisha kabisa na siasa kwani system itakuwa na checks na balances......sasa hivi ninajitahidi tu kuwa mwekezaji ili niwezi kumantain position ya MSHAURI NASAHA anayesikilizwa na wote......with neutral position....rather that FRONTLINE PARTICIPANT!

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Binafsi Zomba huwa nakupinga ktk mambo mengi sio kwa sababu ya sura yako, ni kwa sababu ya unazi wako kwa ccm kiasi cha kufumbia macho hata maovu ya serikali hii. Hata hili sijui uliwaza nini kulileta hapa, maana huwa naona kwako wewe kila kitu cha serikali hii ni kizuri. Zomba utakubaliana na mimi na watanzania wengi kuwa mazuri ya hii serikali ni machache kuliko mabaya, MABAYA NI MENGI MNO.

mbaya zaidi sehemu ambayo serikali imezembea na ambayo ni nyeti kabisa ni hiki kitengo cha usimamizi wa sheria. Kero nyingi za watanzania zipo kwenye hili eneo, na kama mambo yanafanywa bila kuzingatia sheria tegemea hakuna haki. na kama hakuna haki, hakuna haja ya kuwa na serikali maana mwenye nguvu atamdhulumu mnyonge na hakuna kitakachofanyika kumtetea zaidi ya kumuachia Mwenyezi Mungu.
 
Mkuu, hongera kwa kazi nzuri uliyoifanya kuwaokoa hao watu waliokuwa wameandaliwa jehanam ya Tz kwa makosa ya kubambikizwa kwa kuwa tu ni wanyonge.

Waswahili husema, "hakuna marefu yasiyo na ncha".
 
sasa nadhani akili imekukaa sawa baada ya masahiba haya kukukuta na siku nyingine ukiona mwenzio anapaza sauti jaribu kumsikiliza na sio kubeza kama mnavyofanyaga hapa na jamii yako i.e rejao,ritz n.k, kwani umewaona hata kwenye series ya hizi thread zako walijaribu hata kukupa mawazo, bora sisi tuliokuponda lakini mwisho wa siku umeona juhudi zetu. Ila pole kwa masahiba hayo na mungu awaongoze kujinasua na udhari huu wa policcm

Tafadhali sana. Hakuna masahiba wala maswahiba yaliyonikuta mimi binafsi au ndugu, jamaa au rafiki yangu yeyote katika haya niliyoyaleta. Hao watuhumiwa hawanijui siwajui lakini matatizo yao yalinigusa niliposikia wapo kituo cha Wazo Hill na ni karibu sana na mradi wangu na nilikuwa huko ikanibidi niende kujionea kwa macho yangu ndipo nikakutana na jamaa za hao watuhumiwa na kiburi cha OCD wa hapo ndicho kilichonihamasisha zaidi kuja kuyaanika haya maovu hapa. Nawasiliana na baadhi ya hao ndugu wa watuhumiwa niliokutana nao hapa Wazo Hill wakifatilia hili sakata na tumejuana hapo hapo.

Pia ieleweke hapa kituo cha Polisi cha Wazo Hill, kuna watu wanawekwa hapo zaidi ya mwezi mzima bila dhamana na bila kufunguliwa mashtaka yoyote. Jee. vituo vingine kukoje?

Nchimbi unayajuwa haya?

Enyi wana harakati wa kugombea haki za binaadam mnayajuwa hayo? au mmekalia kuwashindikiza kina Ulimboka tu wanapogoma? au na nyie mnashinikizwa na wengine? kama ni haki za binaadamu, basi kwanza zingeelekezwa kwenye hivi vituo vya Polisi kuliko mahospitali, huko ndio kwenye dhulma ya hali ya juu. Ni wakati muafaka wale wapenda haki waliopo Serikalini wayaelewe haya na wayafanyie kazi.
 
Nadhani sasa zomba utakuwa umeshuhudia mwenyewe ni kwanini sisi wengine tumeamua kusimama upande wa wanyonge siku nyingi. Na bila shaka kuanzia sasa utaacha kuimba taarabu za kuisifia hii serikali dhulmati na dhaifu!
 
Last edited by a moderator:
Nadhani sasa zomba utakuwa umeshuhudia mwenyewe ni kwanini sisi wengine tumeamua kusimama upande wa wanyonge siku nyingi. Na bila shaka kuanzia sasa utaacha kuimba taarabu za kuisifia hii serikali dhulmati na dhaifu!

Mimi nasimamia ya wanyonge toka wakati wa Nyerere aliyekuwa akiwarundika watu ndani bila kujuwa ni kwa nini na ndiye aliyewapa mabavu hawa Polisi yasio na mfano mpaka hii leo. Ushawahi kumshutumu Nyerere kwa hilo hata siku moja?

Kuwa kwangu mwanachama wa chama alichokianzisha Nyerere hakumaanishi ni lazima nikubaliane nae kwa kila kitu, kuna mema yake na kuna mabaya yake na hata yeye alikiri kuwa sheria za nchi hii zinamfanya awe "dikteta" au hulijui hilo? Na kuwepo kwa upinzani hakumaanishi kila wanachosimamia upinzani ni kibaya ingawa mengine mengi ya upinzani siafikiani nayo.

Kikwete anajaribu sana kubadilisha huu mfumo wa kuoneana hata juu hapo nimekuandikia kuwa kaanzisha ofisi za DPP kwa nia njema kabisa lakini sasa mapolisi wanarundika watu ndani vituoni kwa masiku kadhaa kwa kujuwa kuwa wakipeleka mafaili yao kwa DPP ni lazima wataambiwa hakuna kesi hapo. Hapo ndio tunataka pasimamiwe na hayo mamlaka ya Polisi kuweka watu ndani zaidi ya masaa 24 wasiwe nayo kabisa.

Ni sheria ipi inawalinda kufanya hayo? Au niile aliyoipitisha Mkapa mbio mbio ambayo Wakenya waliikataa?

Tusilete uchama katika kugombea haki za wanyonge. Hao upinzani hususan chadema, nna uhakika kabisa wao ndio watakuwa nuksi kuliko CCM ikiwa tu watapewa madaraka, kwani kila dalili zinaonesha hivyo hata ndani ya chama chao ni ubabe na hakuna demokrasia, vyeo wanapeana kiukoo, kazi wanapeana ki fulani.

Nimeuliza Halima Mdee yuko wapi Mbunge wa huko? haingii JF? wapasha habari wake hawampashi haya? hayajui haya? kazi yake kama si kutetea watu wa jimbo lake ni nini? naambiwa watuhumiwa walipofika mahakama ya Kinondoni mwakilishi wa Azzan mbunge wa Kinondoni alikuwepo pale na akakaa na ndugu wa hawa watuhumiwa mpaka walipopata dhamana, pengine ni yeye aliyempigia simu huyu wakili aliyekuja na kusema kajitolea.
 
zomba, shukrani kwa kutupa update. Pamoja na faraja kidogo waliyopata jamaa zako bado naona kuna kazi ya kufanya.

Huyo mkuu wa police Wazo Hill kahamishwa kwenda wapi? Na kama inawezekana ingekuwa vizuri tukapata nakala ya barua aliyopewa. Tujue ni nani huko juu ali-sign barua ya kumhamisha huyu 'mwajiriwa wa Badr'. Mtandao wa mafia huko police ni mkubwa na unazidi kuwa mkubwa.

Baada ya Mahita sikutegemea kabisa kama tungeona 'organised crime' toka kwa police kama tunavyoona sasa! IGP Mwema hana interest hata kidogo na usalama/haki za raia. Kuna mambo ya kutisha yanafanywa na police huku Ma-RPC na OCD wakiwa ndio vinara wa kusimamia maovu. IGP yuko wapi?

Jambo moja bado sijaelewa ni kwanini kamati ya kudumu ya bunge inayoshughulika na ulinzi na usalama haisemi chochote kuhusu 'hofu' waliyonayo wananchi kutokana na uharamia wa jeshi la police. Raia hawana amani kabisa na chanzo ni Police. Kwanini Mh Lowassa haoni ulazima wa kuitisha kikao na timu nzima ya wizara ya mambo ya ndani jeshi la polisi likiwemo? Na wananchi wakiandamana watasema wanasukumwa na wanasiasa?

Kwa katiba yetu, wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho juu ya uongozi wa nchi hii. Bunge linawajibu wa kuisamamia na kuhoji utendaji wa serikali kwa niaba ya wananchi. Huu ndio utaratibu wa uongozi kikatiba. Wananchi wanauwawa, wengine wanawekwa ndani, lakini bado kamati ya bunge inakaa kimya!

Nadhani mwelekeo sasa uwe kelele za kulitaka bunge kupitia kamati ya ulinzi na usalama lingiingilie kati, police wanatishia usalama wa hii nchi.
 
Mkuu kwa uliyoandika hapa tupo pamoja sana!

Nikwambie tu kwamba kuna mazingira mengine yanakuwa magumu kwa wabunge zaidi ya ilivyokuwa kwako... Sio wa CCM, sio wa upinzani, inapofika kukabiliana na dola, hali ni mbaya sana hapa Tz. Hongera angalau wewe uliweza kuongea OCD akitembea, akakuacha. Muulize Dk Kigwangala yaliyomkuta kule Nzega alipotetea wananchi dhidi ya polisi. Muulize yule mama wa CUF (mbunge viti maalum Tabora, jina limenitoka), alivyolala rumande siku chungu nzima kwa kukabiliana na polisi akitetea wananchi. Kwa hiyo ndugu yangu zomba usione wengine tunapigia upinzani debe hapa, sio kwamba tunataka chama fulani kiingie madarakani, no. Tunaamini hiyo inaweza kuwa njia mojawapo ya kupaaza sauti za wanyonge dhidi ya waonevu wanatetea matumbo yao. Kwa taarifa yako mimi (na wengine wengi), siku chama cha upinzani ninachosapoti kikiingia madarakani, ndio siku nitakapokipa talaka, na kusapoti chama kitakachokuwa kikuu cha upinzani, lengo ni kuhakiisha serikali yeyote itakayokuwa madarakani inakuwa na wamulikaji na wapiga kelele, ili kwa kiasi fulani iwe makini.
 
Last edited by a moderator:
Naona sasa Zomba umeanza kuona jinsi hii serikali yako yenye watumishi waonevu!

Hongera kwa kutujuza zomba!

Ila hipo siku utaachana na siasa uchwara!

Asante kwa kutujuza!
Hata mimi naona Zomba naye ameanza kuona mwanga! kwamba system ya utawala wa magamba, ambayo amekuwa akiitetea kwa nguvu zote, sasa amegundua haitendi haki, mara nyingi raia wasio na hatia wanabambikiziwa kesi, na kwa sababu mfumo wa utawala, uko so corrupt, Polisi wanaofanya uovu huo hawawajibishwi, na badala yake, mara nyingi polisi wa aina hiyo, ndiyo wanaopandishwa vyeo!! Itakuwa vyema wafadhihina wengime wa aina ya Zomba, wakaanza kufunguka na kuyaona maovu makubwa yanayofanywa na serikaki hii ya Magamba, na wakayakemea kwa nguvu zote!!!
 
Back
Top Bottom