Jamii ya wacheza kamali na bahati nasibu

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
JAMII YA WACHEZA KAMALI NA MAZINGAOMBWE

Wiki chache nilipokuwa arusha kuna jambo moja niliona ni zuri kuona watu haswa vijana wanatumia sana computer katika masuala mbali mbali ya mtandao hata hivyo vijana hawa sio kwamba walikuwa wanatafuta mambo ya kusoma na kujenga kama wengine wanavyofikiri wakiwaona

Wengi wao ni watu ambao hushinda kwenye ma internet café na sehemu zingine za huduma ya mtandao kwa ajili ya kucheza kamari kwa njia ya mtandao au kucheza michezo ya kubashiri matokeo ya mechi haswa kwenye lig mbali mbali za ulaya .

Hii tabia imekomaa sana , watu hawafanyi kazi za maana za kutuma maarifa wanakesha kwenye café hizi kwa ajili ya kubashiri matokeo ya mpira wa miguu , hili liko sana kwenye miji ya arusha na dare s salaam pamoja na nairobi sijui miji mingine kwa sababu huwa sitembelei huko sana .

Kuna umuhimu wa wahusika kuangalia suala hili kwa umakini sana linaloendelea kupendwa na vijana wengi kwa sababu ni kazi ya kubashiri tu na mtu kwenda zake kitandani kulala hafanyi kazi nyngine kama akifanya basi ni ile inayoweza kumpatia hela ya kwenda kulipia huduma hiyo ya mtandao .

Kingine ni mitindo ambayo imeibuka sasa hivi ya bahati nasibu ya kila aina , juzi hapa nilipita kariakoo nikaona watu Fulani wanachezesha bahati nasibu ambapo mtu alitakiwa kununua kitu kwa alfu 1 kisha kulenga shabaha kitufe Fulani ukishinda basi unaweza kuibuka na gari , watu kwa mamia walikuwa pale wameacha kazi zao kununua huduma hiyo ya kulenga shabaha .

Nafikiri sasa ufike wakati watu wakubali kuwajibika katika kufanya kazi na shuguli zingine mbali mbali ambazo zinatija kwa jamii zao kuliko hizi bahati nasibu na michezo mingine ya kubahatisha ingawa mingine inakuwa ni mazinga ombwe
 
Heshima mbele Shy,

Hii tabia kweli imekomaa sana hapa mjini Arusha,vijana wengi wamefanya kutabiri matokeo ya mechi za mpira wa miguu hasa ligi ya wingereza ndiyo kazi badala ya kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.

Shughuli ya kutabiri matokeo ya mechi mbali mbali inamlazimu mtabiri kuchukua muda mrefu sana kuzijua timu mbali mbali kwa undani ili kuwa katika nafasi nzuri ya kubashiri matokeo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom