Jamii mbili za viumbe wenye akili ulimwenguni

Mkuu Eiyer hebu pitia hapa uone ulicho quote ni nini?
jaribu kufatilia hoja ilipotokea mpaka kufikia hapo(kuhusu miungu)maana nilikuwa naongea na Crocodiletooth, naomba kwanza ufatilie post tulizoanza mpaka kufikia hapo... sio unakua kama kitenzi kikurupushi.
alafu jaribu kuyaweka maneno yako katika sentensi moja ambayo inaleta maana.

Nimecheka sanaaa

Kitenzi kikurupushi.... Lol
 
Last edited by a moderator:
Sasa mtoa mada.. hii elimu ya unajimu inasemaje kuhusu hatma ya wanadamu na dunia
 
Mkuu Eiyer hebu pitia hapa uone ulicho quote ni nini?
Nilichokinukuu nakijua na ndio maana naendelea kukuona wa ajabu tu
jaribu kufatilia hoja ilipotokea mpaka kufikia hapo(kuhusu miungu)maana nilikuwa naongea na Crocodiletooth, naomba kwanza ufatilie post tulizoanza mpaka kufikia hapo... sio unakua kama kitenzi kikurupushi.
Nukuu yako ilikuwa umejitosheleza kwa kile ambacho nimekunukuu na kukujibu,hakuna haja ya kufuata mtiririko wa majibizano yako na huyo mwenzako,unachopaswa kujua ni kwamba ulichoandika kumhusu Mungu ni matokeo ya kutokujua unachoikiongelea na hilo ndilo tatizo lako kubwa
alafu jaribu kuyaweka maneno yako katika sentensi moja ambayo inaleta maana.
Kusema tu maelezo yangu hayaleti maana bila kuonesha ni kwa namna ipi hayaleti maana unageukla wewe kuwa ndio huleti maana...
 
Eiyer naomba uwe muelewa kidogo tu inatosha.
mtoa mada hajazungumza kuhusu habari ya neno mungu ni nini?...mtoa mada hajazungumza habari za miungu n.k ila hayo yote nimesema mimi..... na ndio maana nimekuomba ufatilie post zangu nilizoanza mpaka kufikia hapo ili ujue nilikuwa nazungumza na nani sio unakurupuka tuuu kiongozi,

huoni kuwa unazidi kujiongezea credt za upumbavu???

Hata mwendawazimu anaona kula chakula kwenye vyombo visafi ni upumbavu,hivyo sishangai wewe kuona nilichokuambia ni kujiongezea upumbavu....
 
Mwanzilishi wa huu uzi ni mwandishi wa riwaya na msomaji nguli wa riwaya za Kigiriki.

Maelezo yote aliyoyatoa ni mchanganyiko wa biblia na hadithi za kale za Kigiriki zenye kuonyesha chanzo cha binadamu na uwepo wa miungu yao.
 
Mwanzilishi wa huu uzi ni mwandishi wa riwaya na msomaji nguli wa riwaya za Kigiriki.

Maelezo yote aliyoyatoa ni mchanganyiko wa biblia na hadithi za kale za Kigiriki zenye kuonyesha chanzo cha binadamu na uwepo wa miungu yao.

Alishawahi kuandika riwaya gani? Hebu twende pole pole....
 
Mbona niliweka yote imekuwaje ipo nusu?
Any way.... Ngoja niiendeleze hapa hapaa

Ni ndani ya mfululizo huu alimozaliwa binadamu....

Uhai hapa duniani uliletwa kutoka katika Constellation ya Lyra. Hawa viumbe wa Lyran Humanoids ni Wenye bidii sana katika kueneza uhai ulimwenguni miongoni mwa Jamii za Humanoids. Viumbe hao ndio waliuhamisha uhai wa kimazingira (environment ecosystem) kutoka sayari yao kwa maana ya mimea, wanyama, hewa yenye bacteria nk kupitia vyombo vyao vya anga za juu vilivyojulikana kama Makerubi. Waliandaa mazingira vizuri na kuotesha uhai wote wa kiikolojia. Kama desturi ya nyakati zote waliwafanyia cloning watoto wawili wadogo mmoja wa kiume na mwingine wa kike kutokana na jamii yao ili waweze kuwiana vya kutosha na mazingira yao mapya ya maisha.
Viumbe hawa waliwaandalia mazingira mazuri ya kuishi ndani ya bustani na kuwaweka humo. Watoto hawa wadogo walihitaji usimamizi mwingi kutoka kwa Wazazi wao na kwa hiyo, viumbe hawa wa Lyrans waliwatembelea hapa na pale ili kuangalia makuzi yao. Hatimaye waliridhika kwamba ni watu wazima na hivyo wakawakabidhi rasmi utawala wa dunia kama sayari yao.
Ugomvi mkuu waibuka baina ya Humanoids na Reptoids.
Muda mchache kabla ya Lyrans kupanda uhai duniani ugomvi mkubwa ulikuwa umetokea baina ya Jamii hizi mbili yaani Humanoids wa Lyrans na Reptoids wa Alpha draconians. Ugomvi huu uliletwa na Reptoids wa Alpha draconians waliotaka kuzimiliki baadhi ya sayari za Humanoids wa Lyrans ziwe makao yao ya kuishi. Viumbe hawa walikuwa katika galaxy moja japo nyota mbali mbali. Reptoids hawa wa Alpha walipoiona sayari ya Bila walivutiwa kabisa na mazingira yake nao wakawa wamenuia kabisa kuichukua sayari hiyo. Humanoids hawa wa Lyrans waliomba kwanza kuwajua vizuri kabla ya kukubali ombi lao kwa kuwauliza swali kwamba tungependa kwanza tuwajue vizuri, je ninyi ni watu wa aina gani?
Swali hili lilipokelewa kama kauli ya kukataliwa na matokeo yake ndani ya muda mfupi walizusha vita kubwa dhidi ya sayari hiyo ya Bila sayari ambayo ilikuwa imewavutia sana Reptoids hawa. Ndani ya muda mfupi sayari tatu miongoni mwa sayari kumi na nne za Humanoids wa Lyrans zilikuwa zimeharibiwa vibaya sana. Sayari zilizokuwa zimeharibiwa ni Bila, Teka na Merok. Humanoids wa Lyrans walikuwa ni wakulima, hawakuwahi kujishughulisha na silaha za maangamizi, walikuwa ni viumbe wapole sana,hawakuwahi kujishughulisha na vita ya aina yoyote. Kwa hiyo waliangamizwa sana. Msaada mkubwa wa katika vita hiyo uliletwa na Humanoids wanaojulikana kama Arcturians. Humanoids hawa wa Arcturus wana upendo sana, wameboresha sana teknolojia yao kwa ajili yao lakini zaidi sana kwa ajili ya jamii zingine. Kwa hiyo pia hujulikana kama Walinzi wa mbingu. Humanoids hawa wa Arcturians walipoingia katika vita hiyo waliwaangamiza vibaya sana wale Reptoids hao wa Alpha draconians na kuwafanya wakimbie kurudi kwao wakiziachia sayari hizo walizokuwa wamezishikilia. Ni katikati ya uhasama huo Reptoid mmoja alipojipenyeza hadi bustanini walimokuwa binadamu wa kwanza na kuamua kuwachochea kinyume cha Wazazi wao hao wa kimbingu. Ni kweli kwamba mambo mengi bado Wazazi hawa wa kimbingu wa wanadamu walikuwa hawajawaeleza bado, hii ni busara kabisa kutowaeleza mambo yote nje ya kiwango chao cha kustahimili. Lakini hili likatumiwa vibaya na draconian huyu kwamba Wazazi wao hao wa kimbingu hawakuwapenda wala kuwatakia mafanikio makubwa. Muunganiko huu wa binadamu na adui zao uliahirisha zawadi nyingi nzuri walizokuwa wapendelewe na Wazazi wao, mojawapo ni zawadi ya uhai wa milele. Zawadi hii ilitokana na jamii ya miti yenye kuleta uzima usio na kikomo. Kama nilivyoandika Jamii hii ya Humanoid Lyrans ni Jamii ya wakulima kwa hiyo muda mrefu walishagundua miti yenye kuboresha uhai wa mtu ambaye hajafanyiwa cloning ya uhai. Kwa hiyo walimuondolea zawadi hii kusudi asije kuutumia uzima wa milele vibaya kinyume na Wazazi wake. Na hivyo uhai wa milele wakaamua kuuweka miongoni mwa gharama za Mamlaka ya Nafsi, badala ya kuwa zawadi isiyogharimiwa.
Draconian huyu alipogundua kuwa amegundulika alitoroka na kurudi kwenye himaya yao ya Alpha draconians na kuwaeleza kile kinachoendelezwa hapa duniani na humanoid wa Lyrans na ubora wa sayari hii kama makao ya kuishi. Hivyo viumbe hao wa Reptoids wakaja kwa wingi wao pamoja na watumwa wao wa Zeta Reticulians ili kuwaangamiza Lyrans hao waliokuwa duniani na kuwaangamiza pia na binadamu ili kulipiza kisasi na kuichukua sayari hii. Lakini zoezi lao hilo halikufanikiwa kwa sababu kumbe viumbe wa Arcturians walishaweka kituo chao kisichoonekana cha ulinzi wa anga hizi za chini. Kituo hiki kisichoonekana kinachojulikana kama Athena, kipo Kati ya anga ya sayari ya Saturn na Jupiter. Reptoids hao wa draconians bila kujua uwepo wa kituo hicho waliangamizwa kabisa. Hivyo mpango wao wa maangamizi haukufanikiwa. Hata hivyo Reptoids hao waliobakia bila madhara walikimbilia duniani na kuwaambia Arcturians kwamba endapo watawafuatilia zaidi basi wao watawaeleza binadamu siri nyingi zaidi za ulimwengu, jambo ambalo binadamu alikuwa hajakomaa kuelezwa. Kwa hiyo Arcturians wakaamua kuwaacha wakae duniani bila kubughudhiwa tena. Arcturians wakawaacha maadamu hawana tena madhara ya kuangamiza Jamii ya binadamu. Hata hivyo Reptoids hao wala nyama walianza kuleta ghasia duniani kwa kutawala wanadamu kwa ukatili na mateso na kula nyama za wanadamu. Kipindi hicho katika historia ya wanadamu ndio chanzo cha masimulizi kuhusiana na Manefili pamoja na Mazimwi wala watu. Huo ukawa mwanzo wa binadamu kula nyama na kutoa Sadaka za binadamu
Ujio wa Humanoids wa Pleiades hapa duniani
Miaka mingi baadaye, wanadamu wakiwa wameongezeka duniani. Yapata miaka elf kumi iliyopita, kulitokea ujio wa viumbe wengineo wa Jamii ya Humanoids kutoka galaxy ya Pleiades. Viumbe hao ni watoto wa Lyrans kama ilivyo kwa binadamu. Kwa hiyo ni kana kwamba walisafiri hadi duniani ili kuona hao ndugu zao wa kibinadamu ni watu wa namna gani. Humanoids hawa waliishi duniani kwa muda mrefu kabisa na hata wakaamua kuishi kinyumba na mabinti za wanadamu na kuzaa nao watoto. Kwa vile ingawa viumbe hao ni kutoka sayari tofauti lakini ni specie moja tu ile ile ya anga nyingine, ndio maana waliweza kuzaa watoto. Hadi leo wanasayansi wanakubali kwamba kuna genetics mpya iliingia ghafla miongoni mwa binadamu. Genetics hiyo inapatikana wa ukanda wa Kaskazini mwa dunia. Kwa wenyeji wa Scandinavia, Sweden Na Norway. Wana wanakubali kwamba genetics hiyo iliingia ghafla katika Jamii ya binadamu miaka elfu kumi iliyopita. Wazazi wao kutoka Lyrans wakaamua kuwaangamiza wote watatu, kwa gharika ya maji yaani Terrans, Pleiades, na draconians. Kasoro tu kuhifadhi mbegu chache za wanadamu na wanyama.

Hahahaaaa....naona umeamua kuwatengeneza watu, hiz story ndio zimekuvuruga so unataka vuruga na wengine, kwa kitwist misingi iliyowekwa katika Biblia....kazi ya Giza hii
 
Mbona sivioni sasa kwenye hii thread au inaendelea?
Maswali pia mtoa mada anajibu kifupi kama yupo chooni.

Thread ndefu majb mafupi.
Uskasirike
 
Mbona sivioni sasa kwenye hii thread au inaendelea?
Maswali pia mtoa mada anajibu kifupi kama yupo chooni.

Thread ndefu majb mafupi.
Uskasirike

kwahyo wewe unataka majibu marefu kama thread ilivyo?
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom