Elections 2010 James Shigongo: Sijakamatwa na TAKUKURU jamani

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,268
17,097
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric James Shigongo amekanusha uvumi unaoendelea kwenye Jimbo la Buchosa kuwa amekamatwa na TAKUKURU.

Shigongo, aliliambia gazeti hili juzi (Jumatano) kuwa kuna mchezo mchafu ambao anachezewa kwa baadhi ya wagombea kumtangaza kuwa alikamatwa na maofisa wa TAKUKURU.

Kada huyo alisema kuwa ni uvumi unaoendelea Buchosa kwa lengo la kumchafua kwa wana CCM wanaomuamini na ambao wameahidi kumchagua ili agombee kwenye Uchaguzi Mkuu 2010.

“Sijakamatwa jamani, kwanza nashangaa hiyo habari imetoka wapi. Mimi nipo na naendelea na shughuli zangu za kujinadi kwa wana CCM kama kawaida,” alisema Shigongo.

Aliendelea: “Muhimu nimedhamiria kufanya kazi na ndugu zangu wa Buchosa na nimejipanga kikamilifu kuhakikisha nasimama kama mgombea ubunge Buchosa kwa tiketi ya chama changu.”

Shigongo alisema kuwa yanayovumishwa, lengo lake ni kumchafua baada ya kuona kasi yake haishikiki.
“Sijakamatwa na TAKUKURU na wala haitotokea. Binafsi sikubaliani na rafu za uchaguzi. uchaguzi huru na wa haki,” alisema Shigongo.

Alisema kuwa kitu kikubwa ambacho anakifanya ni kuendelea kuwaeleza wana CCM kile ambacho anakusudia kuwafanyia endapo watampitisha kuwa mgombea ubunge wa chama hicho na baadaye kuwa mbunge wa Buchosa.

Katika hatua nyingine, mwana CCM mwingine anayewania nafasi ya kugombea ubunge Buchosa, Makanza Nsumilabana, amekuwa kivutio kutokana na mtindo wake wa kujinadi.
Makanza amekuwa akiwaahidi wana Buchosa kuwa atawaletea maji, umeme wa upepo, barabara na kadhalika huku akiwasisitiza kwamba wasingoje kumchagua.

Wagombea wengine ni Samuel Chitalilo, Charles Tizeba, Philemon Sengoti, Pius Lwamimi, Joa Kasika, Kulwa Shindika, Steven Mselu na Mgozi Benedict.
Wakati huo huo, mastaa wa filamu nchini, Steven Kanumba, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Jacob Steven ‘JB’ wapo njia moja kwenda Buchosa kumuunga mkono Shigongo.
 
Mnatuletea wasaniii bungeni haya!!!!!!kazi kwenu watanzania
 
Alisema kuwa kitu kikubwa ambacho anakifanya ni kuendelea kuwaeleza wana CCM kile ambacho anakusudia kuwafanyia endapo watampitisha kuwa mgombea ubunge wa chama hicho na baadaye kuwa mbunge wa Buchosa.
Ama kweli siasa za Bongo ni maajabu matupu. Mgombea anaahidi wnanchi kuwaletea vitu badala ya mgombea kunadi sera na ilani ya chama kulingana na matakwa ya wananchi.
Mimi naona kama siasa zetu ni kinyume nyume yaani mbunge sii mwakilishi wa wananchi bungeni bali ni yule mwenye uwezo wa kutimiza ahadi zake.
 
Back
Top Bottom