James Millya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Arusha ajivua GAMBA akimbilia Chadema

CDM kuweni makini na mkakati wa magamba wa kuua upinzani! Magamba wamejitahidi sana kuiua CDM lakini kila wanajaribu wanashindwa!
Nina mashaka sana na huyu bwana, huenda akawa ametumwa na magamba hata kama anajifanya kuwakandia magamba!
Chonde chonde Magamba wanajua fika nguvu yenu CDM Arusha na kanda yote ya kaskazini, huyu jamaa ametumwa kuwapunguza kasi hata kama atakaa miaka mitano bado ni mfuasi mzuri wa magamba hasa EL.
 
Huyu El tunamkuza tu! Kijana apokelewe kama mwanachama wa kawaida tu.
Bado nina imani na Mwigamba, atamtuliza tu....
Hamna cha El wala bibi yake El, tumempiga alipotuletea Batilda, tukampiga Arumeru alipotuletea Mkwe wake!
Natangaza simuogopi EL , sababu hamna cha kufanya aogopwe.
Mtu anionyeshe nilipokosea!
teh teh teh!
pamoja sana mkuu. unajua tena ukipita kwenye msitu wenye wanyama wakali lazima kila kishindo unachosikia ukichunguze kwanza isije ikawa ni mnyama mkali anakufuata.
 
Twamkaribisha sana milya,amechagua nyumba ya watu makini,wasafi na wazalendo.nae twamtaka kuwa nguzo muhimu ktk ujenzi makini wa taifa,chadema hatuna pesa bali akili ambazo mtoaji ni mwenyezi,ndiyo maana chadema inafanya kazi ya ukombozi.milya karibu sana tujenge tanzania yetu kwa moyo wa dhati na muumba akijalia utafaa sana tukutume kufanya kazi ya ukombozi simanjiro kwa ole sendeka kwa kuwa si mkweli hata kidogo kwaye tumbo lake ni mhm kuliko masilahi ya watz,nafaham una ushawishi wa kipekee arusha hasa kwa upande ulikotoka tunapenda kuutumia uwezo wako ktk kujenga ngome kuwa imara,nina kupongeza kwa uamuzi wako wa busara wa kuichagua nyumba na familia njema ktk maisha ya kisiasa.karibu bwana milya!tunaamini ktk nguvu ya umma!!
 
vipi sendeka habari anazo au anazungusha tu kitambi bungeni.hebu pandisheni presha na alafu shusheni kisukari ili afe akibisa,mwenye namba yake ampigie au hata amtumie sms
 
Source radio 5 arusha!

Anaongea kwa hasira sana akisema CCM siyo baba wala mama yake! Anadai chama kinatumia fedha za walipa kodi kuzunguka nchi nzima kumchafua.

Karibu CDM! Apewe katiba ya chama atumike kwenye M4C
 
Hapo CCM wanaandaa mpango wa kuicukua Arusha mjini.

huyu jamaa ni kama akina SHIBUDA na wenzake,wakati mwingine CDM wawe na kasumba ya kuwa na uvumilivu wa kuwasoma watu,hii tabia ya kukubali matakwa ya kila mwansiaasa.mtayavua mabua

Mkuu kuna tofauti ya mtu kuwa mwanachama wa kawaida na kuwa kiongozi katika chama. Kila raia ana haki ya kujiunga na chama anachokipenda.
Pale kwa Shibuda, somo limepatikana naamini.
 
inasemekana anahamia CDM na lowasa baada ya kupata hizi habari leo asubui yuko hoi taabani kisukari kimepanda....
 
au anataka kujiweka sawa kugombea ubunge Arusha mjini akisikilizia rufaa ya Lema??
 
Christopher Ole sendeka kasalimu amri kwa Lowassa kijana kakata kamba zizini ametoroka.......Tuna maswali mengi ya kujiuliza kabla ya kumpa imani kubwa kwenye chama kipya.
 
DSC00089_800x600.jpg

huyu hapaaaaaaaa
 
Akaribishwe.
Lkn isije ikawa katumwa ili aje kuomba agombee Arusha Mjini kwa CDM. Akiruhusiwa, itakuwa maafa. Magamba na UWT wana sura nyingi
 
Back
Top Bottom