James Millya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Arusha ajivua GAMBA akimbilia Chadema

Dik

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,204
416
Source radio 5 arusha!

Anaongea kwa hasira sana akisema CCM siyo baba wala mama yake! Anadai chama kinatumia fedha za walipa kodi kuzunguka nchi nzima kumchafua.

Millya ambaye ni mfuasi mkuu wa Edward Lowassa, anaelezwa kutaka kupata nafasi ya kuwania ubunge Arusha mjini, lakini Chadema wamemkatalia, kama walivyomkatalia Lowassa, kwa maelezo kwamba bado si wasafi kubeba bendera ya chama chenye nia ya kupambana na ufisadi. Chadema wanawakaribisha wote kwa sharti la kuwa wanachama wa kawaida, na watapewa muda wa kujisafisha na kuwaomba radhi Watanzania.
Mkiti wa CDM Freeman Mbowe amesema CDM kinamkaribisha Millya kwa mikono miwili kwani ni mwanasiasa safi na CDM hawana historia chafu inayomhusu James Millya.

Mbowe amesema watashirikiana kikamilifu na Millya na kama mwanachama watampatia majukumu ya kuharakisha ukombozi wa Taifa hili.

Mbowe amesema ni uamuzi wa kishujaa ambao kila mwanademokrasia wa kweli anapaswa kuufurahia.Amesema anamfahamu vizuri Millya ni mpambanaji na mpiganaji hasa.

Mbowe pia amesema anawakaribisha wale wanachama wote wa CCM wanaojijua ni wasafi waje CDM kushiriki ukombozi wa Taifa lao.

Source:TBC Habari
 
Source radio 5 arusha!anaongea kwa hasira san,akisema ccm siyo baba wala mama yake!anadai chama kina2mia fedha za walipa kodi kuzunguka nchi nzima kumchafua.

James Ole Millya yule mwenyekiti wa UVCCM arusha au yupi?

Kwa mara ya mwisho huyu jamaa kamwagwa kwenye kinyang'anyilo cha ubunge EAC kwenye ngazi ya chini kabisa ya kamati kuu ya chama (CCM). Hata yule mgeni kutoka marekani William Malecela alimshinda
 
James Ole Millya yule mwenyekiti wa UVCCM arusha au yupi?

Kwa mara ya mwisho huyu jamaa kamwagwa kwenye kinyang'anyilo cha ubunge EAC kwenye ngazi ya chini kabisa ya kamati kuu ya chama (CCM). Hata yule mgeni kutoka marekani William Malecela alimshinda
CCM is not used to Majembe... Milya ni mashine hivyo hawezi kufit kwenye agenda ya CCM

Sintashangaa vijana kama akina Mpoki, Gambo, na hata January kuhamia CHADEMA
 
haya ni masihara ua ni ukweli? kama ni ukweli tunamkaribisha ila isijekuwa mamluki mbona atakiona cha mtemakuni
Mkuu, hata mimi bado sijaamini! lakini kama ni kweli basi itakuwapigo kubwa sana kwa ccm na kambi mzima ya EL.
Lakini itakuwa sherehe na sifa kubwa sana kwa CDM...eeee mungu mwenyezi ifanye habari hii kuwa ni ya kweli
 
Ni mtu makini anayejiamini sana , , ni kiongozi mzuri sana ,elimu nzuri ashirikiane na wapiganaji wengine kukomboa Taifa hasa maeneo ya umasaini ni matumaini yangu wengi watamfuata James Milya ni uamuzi wa wakati . hongera milya ulikuwa umepotea sasa umerudi nyumbani shirikiana na Makamanda wengine kuleta ukombozi
 
Back
Top Bottom