Mama Mdogo
JF-Expert Member
- Nov 21, 2007
- 2,961
- 2,138
Sinema za bongo zina mapungufu mengi, leo nitajadili matano tu. (1) UTAALAMU: Hatuna professional screen writers, Directors, Actors/Actresses, wapiga picha za sinema. (2) FEDHA: Bajeti za sinema za bongo ni ndogo sana, na hivyo huwezi kupanda mchicha ukavuna iliki au karafuu. (3) TAMAA/UBINAFSI/UPENDELEO: Mtu yule yule na ujinga wake ule ule na mapungufu yake yale yale ataigiza sinema A leo, kesho B halafu C. Matokeo anakuwa amedharaulika na amechujkas na sinema haiuziki. Na katika kipengele hiki yamo masuala ya rushwa za kila aina ili angalau upate nafasi ya kuigiza / kuonekana kwenye sinema za bongo ikiwemo ya ngono. (4) TAMTHILIA DUNI: Sinema za bongo hazina msingi mzuri wa tamthlia na hivyo zinapwaya, na hivyo mtazamaji anashindwa kujihusisha na matukio yalioyoko kwenye maigizo; inashangaza kuwaona wanangangania kuigiza mambo ya mapenzi, kutumia magari makubwa, kuwa katika majumba makubwa, kuongea wanachanganya broken english na kiswahili cha mjini. (5) UNYONYAJI: Producers wa hapa bongo wanawalalia sana waigizaji, ni wizi kwa kwenda mbele. Kwa ujumla, sinema za bongo zina safari ndefu kufikia kiwango ya kile kilichofikiwa na wenzetu wa Afrika Magharibi. Tuwaombee viongozi wa Idara ya Utamaduni wapate kufumbua macho na kuwasaidia hawa wanaojiita watayarishaji na waigizaji wa 'BongoWood'.