Jambo zuri limefanyika Tanzania - hongera TRA

Mwafrika

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,490
226
Hii nimeona kwa michuzi (toka kwa subi toka somewhere) kuhusu DL mpya....safi sana na hongera:

8869158.jpg


Mamlaka ya mapato Tanzania, TRA, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini wameanza utekelezaji wa mfumo mpya wa utoaji leseni za udereva wa vyombo vya moto kwa lengo la kudhibiti ajali za barabarani na utoaji holela wa leseni na kudhibiti mapato ya Serikali.

Kadhalika, Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani, Johansen Katahano, amesema kuwa madaraja ya leseni hizo yameongezwa kutoka 8 hadi 14. Madaraja hayo yameongezwa katika daraja A na C na yameongezwa kutokanana na uwezo wa vyombo vya moto vya madaraja husika na idadi ya abiria watakaobebwa na vyombo hivyo.

Uzinduzi wa matumizi wa leseni hiyo yatafanyika
kesho Jumatano jijini Dar.

Leseni hizo mpya zitakuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu za kielektroniki za mtumiaji ikiwemo idadi ya makosa aliyoyafanya akiendesha chombo cha moto, gari na pikipiki.

Leseni hizi mpya zitahitimisha matumizi ya leseni za zamani.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Protas Mmanda amewataka madereva wanaotumia leseni zao za kawaida kutokuwa na wasiwasi kwani kwa muda huu wataendelea kutumia leseni hizo kihalali na watapewa leseni mpya watakapokuwa wanakwenda kwa ajili ya kuzihaishi. Watu wenye leseni za Daraja C wataanza kupata leseni hizo mara moja lakini watahitajika kupata mafunzo maalumu kwanza.
 
Safi best ila mwombe invisible aipeleke kwenye forum husika manake hapa 100% si mahali pake!
 
Kumbe drivin license ni ishu ya kisiasa?
ndo nimejua leo

Kila kitu kinaweza kuwa huko ndani - kuanzia kuandikisha wapiga kura hadi kuthibitisha uraia wa wagombea. Si umesoma hapo mambo ambayo yanaweza kuingizwa huko.

Anyway.... Binafsi niko happy kuona mambo mazuri once in a while yanatokea Tanzania.
Imewekwa hapa jukwaa la siasa kwa vile wengi wataiona - Invisible pia atapata credit kwa "kuruhusu" habari nzuri za Tanzania kusomwa na wana JF ...LoL
 
........Safi sana haya ndio maendeleo.Nilikuwa nachukia hizi driving license tunazotumia sasa hivi zimekaa kishamba kweli kweli.......hata kwenye wallet zilikuwa zinakaa vibaya.
 
swali dogo tu? kuna infrastructure za kusupport hii technology?maana nakumbuka wakati flan UDSM wali introduce ID zenye uwezo wa kubeba taarifa nyingi lakini zikawazinatumika kuingilia Library tu wakati mwingine unashangaa kwa nini waliamua kuanzisha kadi zile.
 
swali dogo tu? kuna infrastructure za kusupport hii technology?maana nakumbuka wakati flan UDSM wali introduce ID zenye uwezo wa kubeba taarifa nyingi lakini zikawazinatumika kuingilia Library tu wakati mwingine unashangaa kwa nini waliamua kuanzisha kadi zile.

Hii nadhani itakuwa tofauti (na bora zaidi) kuliko zile za mlimani
 
hii safi ila je kwa ukiritimba wetu huu itakwenda kama inavyotakiwa kweli
 
Back
Top Bottom