Jambo Usilolijua: Nyerere alipokea Taifa la namna gani? Mpango wa Kwanza wa Maendeleo 1961

Ndugu MMM popote ulipo,

Respect mkuu!

Nimeipitia kidogo but for sure later nitaisoma kwa makini.

Nimeguswa sana na ilivyo clear, na kujitahidi kugusa nyanja zote kwa wakati huo.

Zile project za community zimenigusa na kunikumbusha mbali.

Ubarikiwe na upate ujasiri, wakati na nguvu ya kutujuvya zaidi.

Ahsante sana.
 
Duh! nimesoma mpaka nimetikisa kichwa ina maana barabara nyingi possibly more than 95% za changarawe kupita tarafa na tarafa mpaka kijiji na kijiji hazikuwepo before 1961. Mpaka the famous Tanzam highway ilikuwa lami mpaka Morogoro tu! kweli tumetoka mbali.
Ndio maana tunapochangia humu utawezas kuwajua watoto wa juzi juzi kutokana na maneno yao. Nakupongeza kwa kukiri hilo hio wazi wazi.
 
MMM Heshima mbele!
Sikuwepo enzi hizo lakini kwa habari chache nilizozikia na kuzisoma nilim-admire Mwalimu,lakini katika 'documentary' zako (kumhusu Mwalimu) za hivi karibuni zinazidi kunifanya niamini kwamba pamoja na mapungufu ya kibinadamu, hatujapata kiongozi wa aina ya Mwalimu.Na haya maandiko unayoyatoa naamini hawakutaka yatoke kwa umma hata kidogo..

Wacha niendelee kuupitia huu mpango...

Kwa kuwa unaonekana unataka kufahamu, tafuta maandiko mbali mbali ya Mwalimu Nyerere na TANU between 1965-80 uone namna Mwalimu Nyerere alivyoua ujasiriamali, uzalishaji na nidhamu ya kazi hapa nchini. Hii ilitokana na kuingiza siasa na makada wa TANU katika manejimenti za viwanda, mashirika na makampuni ya umma. Inaaminika alilazimika kufanya hivyo baada ya kujenga chuki na wasomi aliowasomesha mwenyewe ambao walikuwa wakitoa ushauri kulingana na taaluma zao na yeye na TANU kuutafisiri ushauri huo kama kuhatarisha nafasi zao hivyo wakaitwa wapinga mapinduzi.

Lilikuwa ni jambo la kawaida katika viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma nchi nzima kukuta Mwenyekiti wa TANU akiwa ni mfanyakazi wa kada ya chini kabisa kutokana na kukosa elimu lakini kwa mujibu wa Mwongozo wa TANU ya wakati walilazimika kushirikishwa katika vikao vya menejimenti za viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma.

Miongozo hii potofu kiuchumi ya TANU na tabia ya kuingilia menejimenti za viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma ndio ilianza kuzalisha idadi kubwa ya makada wa TANU na badaye CCM ambao hawakuwa elimu, tija wala manufaa yoyote lakini TANU na Serikali yake kwa makusudi kabisa ikwa inapawa sauti kubwa sana katika uongozi wa viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma. Na hii ndio sababu kubwa ya viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma kuanza kuendeshwa kiholela kwa hasara. Lakini mara zote Serikali ya Mwalimu Nyerere ikawa inachota mabilino ya walipa kodi wa Tanzania na kuyatumia kuendesha viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma bila ya watanzan ia kupatiwa nafasi ya kuhoji kulikoni mitaji ya mwanzo ilikoenda? Kila aliyejaribu kuhoji awe mbunge, raia n.k aliwekwa kizuizini chini ya Sheria ya Preventive Detention Act.

Lilikuwa ni jambo kawaida kwa viongozi matawi ya TANu mahali pa kazi kupelekea malamiko ya kimajungu kwa Mkuu wa Wilaya ambaye pia alikuwa ni kada. Wakuu wa Wilaya na Mikao walikuwa na uwezo kamili wa kutengua maamuzi ya kitaalamu ya manejimenti ya kiwanda, shirika au kampuni fulani ya umma. Sasa katika hali hiyo tumlaumu nani kwa viwanda, mashirika na makampuni ya umma kufa? Ni dhahiri haya yalikuwa ni matumizi mabaya ya madaraka ya uraisi.

Kipo kisa kimoja kilitokea katika Hospitali ya Muhimbili, Dkltari Bingwa wa magonjwa ya Moyo alikuwa akiendesha kliniki zake kila siku ya J'nne kuanzia Saa mbili asubuhi. Mhudumu wa ofisi ya daktari hiyo ndio alikuwa Mwenyekiti wa Tawi la TANU, hivyo alikuwa hafanyi majukumu yake ya uhudumu na badala yake kila kukicha ni kupiga soga sehemu mbali mbali katika hospitali hiyo.

Kila mara dakatari aliporipoti suala hilo hatua zilishindwa kuchukuliwa na menejimenti kwa kuwa Mwenyekiti wa TANU ni sehemu ya menejimenti na hudai kuwa Mwongozo wa TANU unakataza Unyapara na Ukaripiaji, na kwamba TANU inaamini kuwa binadamu wote ni sawa.

Siku moja Daktari bingwa baada ya kuchoshwa na tabia za mhudumu huyo aliwahi asubuhi sana siku ya kliniki na kufanya matayarishao yote yanayohitajika kwa ajili ya chumba cha daktari. Baada ya kumaliza akakaa sehemu ambayo hustahili kukaa mhudumu akisubiri kutumwa. Wagonjwa wakaanza kumiminika kama kawaida, lakini huduma hakuna kwa kuwa dalktari kakaa sehemu ya mhudumu na mhudumu husika hajafika yuko mitaani anaopiga soga.

Wagonjwa baada ya kukosa huduma iliwabidi wafikishe malalamiko yao ngazi za juu, na daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo alipohojiwa; Jibu lake lilikuwa ni lile lile kuwa "kwa mara zote uongozi wa hospitali hiyo umekuwa ukikubali hoja za Mwenyekiti wa TANU kuwa binadamu wote ni sawa, hivyo siku hiyo yeye (daktari) amefanya majukumu ya mhudumu na mhudumu huyo ndiye atawatibia wagonjwa siku hiyo.

Nia yangu sio kumchafua Mwalimu Nyerere, namheshimu sana hususan kwa kutotumia madaraka yake kujilimbikizai mali. Lakini ukweli ni lazima usemwe kuwa matatizo mengi tuliyonayo hivi sasa kama taifa chimbuko lake ni siasa za Uongo na Ulagahai za Mwalimu Nyerere ambapo alifanikiwa kujenga jeshi kubwa la wababaishaji ambao hurithishana toka enzi zake. Ili kufanikiwa kuendesha siasa za ulaghai na uongo Mwalimu Nyerere alipika historia ya taifa hili kwa kubadilisha mtiririko mzima wa matukio yaliyopelekea Tanganyika kupata uhuru kutoka kwa wakoloni wote wawili pamoja na kubadilisha wahusika pia kwa maslahi yake.

Katika kufany hivyo wapo wahusika muhimu katika harakati za kudai uhuru kwanza kutoka kwa Mjerumani na kisha Mwingerreza hawajawahi kutajwa popote, na wamekufa kama watu wa kawaida bila ya heshima yoyote. Na badala yake wapo watu wengi ambao walikuwa ni vibaraka tu lakini hawakutoa michango yoyote ya maana katika harakati za kudai uhuru Mwlimu Nyerere aliwapatia heshima kubwa ili kutengeneza taswira kuwa haralkati za kudai na kuleta uhuru wa Tanganyikia ziliznzia na kuishia kwa Mwalimu Nyerere na watu wanaomuzunguka ambao wamepata heshima feki. Mfano hai wa watu walioptiwa heshima feki na Marehemu Karume kuwa aliongoza mapinduzi ya Zanzibar ilihali sio kweli hata kidogo.

Dhambi hii kama zilizvyo nyingine haiwezi kupita hivi hivi, vijana wa kizazi hiki mna kazi kubwa ya kumtafuta mchawi aliyewaroga watanzania ndipo mtaweza kupata dawa ya kuwaangua!!!

Ni hadi pale tutakapaoweza kuandika histori ya nchi hii ya ukweli ndio tutaweza kuondokana na matatizo haya tuliyonayo kwa kuwa hadi sasa hatujitambuai sisi ni nani.
 
Mkuu MM nimeusoma partially. Ni mzuri sana!!! Kitu kikubwa nilichojifunza ni kwamba Mpango wa Maendeleo wa kipindi hicho uliakisi vyema kabisa hali halisi ya taifa kwa wakati, yaani, kielimu(wataalamu walikuwa wachache sana kiasi kwamba ilibdi kazi za kitaalamu zifanywe na watu wa CADRES level), miundombinu ya barabara ilikuwa dunu sana, nk. Na ndio maana lengo kuu la mpango wenyewe ilikuwa ni pamoja na kuongeza wataalamu hususani wale technical level(badala ya ku-base zaidi kwa professionals), kuboresha barabara vijijini nk.
 
Nyerere alikuwa na muda kuchange plan zote za economic, pale tu alipoona hazina maendeleo na Taifa. Kwa mfano, plan yake ya agriculture ilkuwa ni kuwahamisha Wananchi kwa nguvu, na kuwapeleka vijijini bila ya mpango maalum wa maendeleo. Utalima vipi wakati huna maji? nyenzo muhimu za kilimo, nk.

Hii ni kashfa. hapo kwenye bold, unataka kutusadikisha kwamba huo ndio ulikuwa mpango kamili wa Nyerere kuhusu Agriculture? inaonekana unatumia zaidi hisia badala ya kuchambua hoja. suala la kupeleka watu katika vijiji ni kwamba tokea hapo concept ya vijiji imejikita na zunguka Tanzania pote watu wanaishi katika vijiji ambapo huduma za elimu, afya, maji nk. zinaweza kupelekwa huko. watu wanatumia maeneo ya mbali na vijiji kwa shughuli maalum tu na wanakwenda huko kwa muda na kurejea katika kijiji. hata mijini kuna mitaa, kata, wilaya, nk. zamani kila watu walikaa katika sehemu zilizotapakaa huku na kule. Nyerere, being a people-focused person, alitaka hawa watu waonje maendeleo, washiriki kula keki ya taifa lao. sioni njia nyingine zaidi ya kuweka mfumo wa watu kukaa katika vijiji. policy was right, unaweza kuzungumzia kuhusu utekelezaji wa hapa na pale. lakini kama nilivyosema, tunafaidi matunda ya hiyo policy mpaka sasa. na ndio maana tunaweza kuzungumzia shule za kata, nk., ijapokuwa hapo ndio kabisaa tumevuruga. ona hiyo tofauti: shule za kata lengo ni kupata umaarufu wa haraka haraka, with disastrous results. vijiji, lengo ni kuwapatia watu huduma, na mpaka sasa concept ndio tunaitumia na kumtukana mwanzilishi.

kuhusu Kilimo, ukitaka kuzungumzia mpango wa Nyerere katika kilimo, inabidi uzingatie mfumo mzima alioujenga. ni kweli alikuta some research stations za kilimo, lakini aliziendeleza sana. mabwana shamba aliwakuta, akawaendeleza sana na kuwapa resources za kufanyia kazi, walikuwa pia na hadhi kubwa sana. aliimarisha institutes, na akaendelea mpaka tertiary level. siasa kwa upana wake ilikuwa inapumua kilimo tu. sasa ili kuweka vizuri coordination kati ya research centre, mkulima, kwa kutumia bridge ya bwana shamba, concept ya vijiji ilikuwa muhimu. ukitaka kuwa fair katika kumjadili Nyerere, do your homework. otherwise ni hate religion
 
Kwa kuwa unaonekana unataka kufahamu, tafuta maandiko mbali mbali ya Mwalimu Nyerere na TANU between 1965-80 uone namna Mwalimu Nyerere alivyoua ujasiriamali, uzalishaji na nidhamu ya kazi hapa nchini.
.
Ni kweli kwamba falsafa ya ujamaa ilikuwa na upungufu mkubwa katika kujali zaidi umoja wa watu na kutoshughulikia individual. lakini pia kinyume chake, kuacha kabisa umoja wa watu ukashughulikia individual tu pia haifai, kama ambavyo tunaona hivi sasa. maoni yangu ni kwamba unahitaji kuangalia balance. unyapara una umuhimu wake, lakini watanzania tunahitajika kuchukua mazuri ya kule tulikotoka na kuacha mabaya. hili Nyerere mwenyewe aliliona na amelizungumzia. unavyozungumza ni kama vile Nyerere hakufanya kitu na alikuja kuharibu tu! Nyerere alijenga institutions nyingi na viwanda vingi na mashirika ambavyo ndio Mkapa akaja kubinafsisha. kumbuka Mkapa hakuleta uzalishaji mpya, aliuza hiki na kile cha Nyerere, akakusanya kodi - basi. Alichofanya Mwinyi ni kufungulia milango wezi kuja kutuibia mpaka wanyama, na kuacha kukusanya kodi, na kuruhusu bidhaa ziingie kwa wingi, basi. hawakujenga institutions kwa level inayosogelea Nyerere.

Nia yangu sio kumchafua Mwalimu Nyerere, namheshimu sana hususan kwa kutotumia madaraka yake kujilimbikizai mali. Lakini ukweli ni lazima usemwe kuwa matatizo mengi tuliyonayo hivi sasa kama taifa chimbuko lake ni siasa za Uongo na Ulagahai za Mwalimu Nyerere ambapo alifanikiwa kujenga jeshi kubwa la wababaishaji ambao hurithishana toka enzi zake. Ili kufanikiwa kuendesha siasa za ulaghai na uongo Mwalimu Nyerere alipika historia ya taifa hili kwa kubadilisha mtiririko mzima wa matukio yaliyopelekea Tanganyika kupata uhuru kutoka kwa wakoloni wote wawili pamoja na kubadilisha wahusika pia kwa maslahi yake.
.

Lakini ndugu yangu, unataka kuniambia kwamba Nyerere alizuia watafiti wasifanye utafiti wao? kwa sababu mpaka sasa hivi hatuna utaratibu wa kuwaenzi waliofanya chochote hapa kwetu. lakini hatuwezi kumrundikia kila kitu Nyerere. for sure Nyerere hakupenda kusifiwa moja kwa moja, na ndio maana wakati wa uongozi wake hapakuwa na kitu kama barabara ya Nyerere, Nyerere theatre, nk. lakini kama mpaka sasa hivi hatuwezi kuandika historia yetu - watafiti wetu hawajafanya hayo - tumlaumu bado Nyerere? vipaumbele vyetu ni nini hasa? ni nani aliyefanya kazi kubwa sana kuimarisha utamaduni wetu na kuuenzi uafrika?

Mwanakijiji, this is an excellent piece of library research; asante sana.

Documents kama hizi ni ngumu sana kuzipata katika Tanzania ya leo ambayo inataka kuonyesha kuwa Nyerere hakuwa na akili ingawa ndiye aliwapatia elimu inayowaweka madarakani leo. Objectives zake zilikuwa clear sana:

attachment.php

objectives.JPG

Utendaji wake unaonekana wazi kuwa ulifuata objectives hizo, siyo leo ambapo nchi inakwenda bila malengo yanayojulikana. Ukiona effort za JK ni wazi kuwa anabahatisha bahatisha tu. Bejti ya mwaka huu inaonyesha ubahatishaji huo kwa wazi kabisa

BTW: BRAZAMENI amefufukia wapi leo?
 
Kipo kisa kimoja kilitokea katika Hospitali ya Muhimbili, Dkltari Bingwa wa magonjwa ya Moyo alikuwa akiendesha kliniki zake kila siku ya J'nne kuanzia Saa mbili asubuhi. Mhudumu wa ofisi ya daktari hiyo ndio alikuwa Mwenyekiti wa Tawi la TANU, hivyo alikuwa hafanyi majukumu yake ya uhudumu na badala yake kila kukicha ni kupiga soga sehemu mbali mbali katika hospitali hiyo.

Kila mara dakatari aliporipoti suala hilo hatua zilishindwa kuchukuliwa na menejimenti kwa kuwa Mwenyekiti wa TANU ni sehemu ya menejimenti na hudai kuwa Mwongozo wa TANU unakataza Unyapara na Ukaripiaji, na kwamba TANU inaamini kuwa binadamu wote ni sawa.

Siku moja Daktari bingwa baada ya kuchoshwa na tabia za mhudumu huyo aliwahi asubuhi sana siku ya kliniki na kufanya matayarishao yote yanayohitajika kwa ajili ya chumba cha daktari. Baada ya kumaliza akakaa sehemu ambayo hustahili kukaa mhudumu akisubiri kutumwa. Wagonjwa wakaanza kumiminika kama kawaida, lakini huduma hakuna kwa kuwa dalktari kakaa sehemu ya mhudumu na mhudumu husika hajafika yuko mitaani anaopiga soga.

Wagonjwa baada ya kukosa huduma iliwabidi wafikishe malalamiko yao ngazi za juu, na daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo alipohojiwa; Jibu lake lilikuwa ni lile lile kuwa "kwa mara zote uongozi wa hospitali hiyo umekuwa ukikubali hoja za Mwenyekiti wa TANU kuwa binadamu wote ni sawa, hivyo siku hiyo yeye (daktari) amefanya majukumu ya mhudumu na mhudumu huyo ndiye atawatibia wagonjwa siku hiyo.

Huyo Daktari wako naye nadhan akili yake haikuwa sawa.
 
Hii ni kashfa. hapo kwenye bold, unataka kutusadikisha kwamba huo ndio ulikuwa mpango kamili wa Nyerere kuhusu Agriculture? inaonekana unatumia zaidi hisia badala ya kuchambua hoja. suala la kupeleka watu katika vijiji ni kwamba tokea hapo concept ya vijiji imejikita na zunguka Tanzania pote watu wanaishi katika vijiji ambapo huduma za elimu, afya, maji nk. zinaweza kupelekwa huko. watu wanatumia maeneo ya mbali na vijiji kwa shughuli maalum tu na wanakwenda huko kwa muda na kurejea katika kijiji. hata mijini kuna mitaa, kata, wilaya, nk. zamani kila watu walikaa katika sehemu zilizotapakaa huku na kule. Nyerere, being a people-focused person, alitaka hawa watu waonje maendeleo, washiriki kula keki ya taifa lao. sioni njia nyingine zaidi ya kuweka mfumo wa watu kukaa katika vijiji. policy was right, unaweza kuzungumzia kuhusu utekelezaji wa hapa na pale. lakini kama nilivyosema, tunafaidi matunda ya hiyo policy mpaka sasa. na ndio maana tunaweza kuzungumzia shule za kata, nk., ijapokuwa hapo ndio kabisaa tumevuruga. ona hiyo tofauti: shule za kata lengo ni kupata umaarufu wa haraka haraka, with disastrous results. vijiji, lengo ni kuwapatia watu huduma, na mpaka sasa concept ndio tunaitumia na kumtukana mwanzilishi.

kuhusu Kilimo, ukitaka kuzungumzia mpango wa Nyerere katika kilimo, inabidi uzingatie mfumo mzima alioujenga. ni kweli alikuta some research stations za kilimo, lakini aliziendeleza sana. mabwana shamba aliwakuta, akawaendeleza sana na kuwapa resources za kufanyia kazi, walikuwa pia na hadhi kubwa sana. aliimarisha institutes, na akaendelea mpaka tertiary level. siasa kwa upana wake ilikuwa inapumua kilimo tu. sasa ili kuweka vizuri coordination kati ya research centre, mkulima, kwa kutumia bridge ya bwana shamba, concept ya vijiji ilikuwa muhimu. ukitaka kuwa fair katika kumjadili Nyerere, do your homework. otherwise ni hate religion

WTZ wainjoy kula keki ya Taifa lao? Nyerere alishindwa kuwasaidia WTZ kuwa creative ktk kujenga Taifa lao. Hiyo keki unayozungumziwa wewe ilikuwa inaliwa na Wachache sana ktk TZ nzima. Hao wachache waliweza kutumia madaraka yao kumsaidia Nyerere kuua WTZ ktk njaa, magonjwa, nk. Keki ipi unayozumguzia wewe? Nyerere ktk Ujamaa policy anakataza mtu kuwa na mafanikio zaidi kuliko serikali yake. Alitaka kila kitu kimilikiwe na Serikali yake kwa misingi ya utawala wake usiokuwa na sheria. Matokeo ya policy zake, WTZ walikuwa nyuma kielimu, uchumi, nk.

Policy ya vijiji hakuanzisha Nyerere. WTZ walikuwa wanaishi vijijini kwa muda mrefu kabla ya Nyerere mwenyewe kuzaliwa. Alichofanya kwa makusudi ni kuwahamisha watu ambao wanaishi mijini na kuwapeleka vijijini. Matokeo yake walishindwa kusurvive, na baa la njaa likatokea nchi nzima. Nani wa kumlaumu, ni Nyerere.
 
Mzee Mwanakijiji kwa kweli unatatufumbua macho wengi mambo mazuri ya Nyerere. Wengi tulikuwa tunajua kuwa Nyerere ni baba wa taifa kwa heshima bila kupata taarifa za kiutendaji na kiutawala kama hizi. Heshima ya Nyerere imeendelea kukuwa.
 
MKJJ angalia usalama wako!

Hii plan inatofautisha sana kati ya wachapakazi na wachapa domo.

It is genuine no blah blah!

MKJJ kwani umesoma development plan ya Kikwete iliyotolewa juzi juzi?? tafadhali jibu hili ASAP......jibu yes or no!!!

Ndiyo; na nilikuwa wa kwanza kuiweka hapa JF. Ni miongoni mwa mipango mibovu kabisa iliyowahi kubuniwa na watu wenye akili timamu. Ukiisoma huu mpango wa kwanza na mpango huu wa nane utaona tofautii ya vinavyodhaniwa ni kama usiku na mchana.
 
Kwa mtu yeyote anayesoma hii plan ataweza kuona mambo mbalimbali ambayo yalizaliwa kutoka ndani yake; chuo cha elimu Tengeru, uwanja wa ndege wa KIA, Uwanja wa Ndege wa Tanga, Bwala la Umeme la Hale n.k vyuo vya maendeleo n.k Sijui kama wameona kuwa Mwingereza alitoa mafunzo ya miezi sita tu kwa wafanyakazi watarajiwa wa seriklai Nyerere ikabidi aweke mpango wa kufundisha wengi zaidi. Usiposoma vizuri utakosa kuona pamoja na juhudi za maendeleo alikuwa anatakiwa vile vile kutengeneza "infrastructure" za utawala - kama wizara ya mambo ya nje, polisi, magereza n.k

Viongozi wote waliofuatia baadaye hawakuangaika na hizo infrastructures za serikali na utawala - walipoingia wakakuta JWTZ ipo kuwapigia saluti, polisi imejaa, magereza iko bwelele na vyuo vyake (Tukuyu, Ukonga), chuo cha Polisi Moshi na kile cha Dar na chuo cha maafisa Monduli vyote vimetoka kwenye uongozi wa Nyerere.

Ndio maana watu kama kina Kikwete wanapojaribu kumvua Nyerere hadhi yake kama Baba wa Taifa wanafanya hivyo kwa aibu yao wenyewe kwani hawana uwezo wa kujilinganisha na kujipima naye hata kukaribia kuwa sawasawa. Siyo kwa maono wala si kwa uongozi hawawezi kumkaribia.

Swala ambalo tunaambiwa la mabaya na makosa ya Nyerere tutaliangalia vile vile huko mbeleni, realistically siyo kutokana na mambo ya "babu alinyang'anywa gari" au "nyumba yetu ilivunjwa n.k" It is not personal; it is purely ideological.
 
Kama ni kuwapa heshima hao, kwa nini Nyerere awe peke yake? Je Nyerere aliunda hiyo foundation ya nchi peke yake? Kama nia kutafuta Founding "Father" (s) wa nchi basi Mzee Nyerere hayuko peke yake. Let's be honest.
 
Policy ya vijiji hakuanzisha Nyerere. WTZ walikuwa wanaishi vijijini kwa muda mrefu kabla ya Nyerere mwenyewe kuzaliwa. Alichofanya kwa makusudi ni kuwahamisha watu ambao wanaishi mijini na kuwapeleka vijijini. Matokeo yake walishindwa kusurvive, na baa la njaa likatokea nchi nzima. Nani wa kumlaumu, ni Nyerere.

mmaaaaaama wweeee!! hivi mnavyosema vitu kama hivi kweli mmechukua hata muda kujifunza Watanzania walikuwa wanaishi vipi wakati wa Mkoloni? Jinsi walivyoishi Wachagga Kilimanjaro kwa mfano asilimia 80 ya Watanzania walikuwa hawaishi hivyo huko Kigoma, Shinyanga, Kagera n.k Leo mnaenda mahali na kukuta "vijiji" msidhani vimetokea hivi hivi tu!. Leo hii mafanikio makubwa ya Nyerere yako katika kuwasogeza wananchi karibu karibu.
 
Kama ni kuwapa heshima hao, kwa nini Nyerere awe peke yake? Je Nyerere aliunda hiyo foundation ya nchi peke yake? Kama nia kutafuta Founding "Father" (s) wa nchi basi Mzee Nyerere hayuko peke yake. Let's be honest.

Usichanganye suala la Founders (waasisi) kitu ambacho hakina shaka waliikuwepo wengi, waasisi wa Taifa letu ni wengi na mojawapo ya ugomvi mkubwa katika fikra zangu na CCM ni kuwa hatujawapa heshima inayostahili waasisi wetu. Lakini tunaposema Father of the Nation tunampa heshima Nyerere kuwa he - alone and in unique way - played a role that no other of our founders played. He was instrumental in the independence struggle, in bringing TANU to the majority of the people (as you can read in M. Said's book on Sykes) and in the very beginning of our nation's history he was the leader of other leaders. His role as the first prime Minister and first President of our nations is alone his. Thats why we honor hims as Father of the Nation.
 
Ingawa ilitolewa miaka hiyo kabla ya Uhuru, lakini kwa kila napoisoma nasema basi CCM hata wangechukua hii leo hii tungepiga hatua.
 
mmaaaaaama wweeee!! hivi mnavyosema vitu kama hivi kweli mmechukua hata muda kujifunza Watanzania walikuwa wanaishi vipi wakati wa Mkoloni? Jinsi walivyoishi Wachagga Kilimanjaro kwa mfano asilimia 80 ya Watanzania walikuwa hawaishi hivyo huko Kigoma, Shinyanga, Kagera n.k Leo mnaenda mahali na kukuta "vijiji" msidhani vimetokea hivi hivi tu!. Leo hii mafanikio makubwa ya Nyerere yako katika kuwasogeza wananchi karibu karibu.

Mikoa ya Kusini WTZ wengi walikuwa wanaishi vijijini kabla ya hata Nyerere kuzaliwa. Nenda ukaone miji kama Rufiji, Kivinje, nk na vijiji karibu yake, vilikuwepo kable ya Nyerere. Mikoa ya Kusini kuna majumba ambayo yapo vijijini yalijengwa tangu miaka ya 1400 na watu walikuwa wanaishi kwa kutumia njia nyingi, kabla Dictator Nyerere kuzaliwa. Maisha ya vijijjini ya Mikoa ya kusini yalikuwa mazuri sana kulinganisha na mikoa mingine. Nyerere na sera zake za Ujamaa alianza kuchukia prosperity ya mikoa ya kusini, na hapo ndipo alipokuja na sera zake kiubaguzi dhidi ya mikoa ya kusini. Let's be honest.
 
Kwa kuwa unaonekana unataka kufahamu, tafuta maandiko mbali mbali ya Mwalimu Nyerere na TANU between 1965-80 uone namna Mwalimu Nyerere alivyoua ujasiriamali, uzalishaji na nidhamu ya kazi hapa nchini. Hii ilitokana na kuingiza siasa na makada wa TANU katika manejimenti za viwanda, mashirika na makampuni ya umma. Inaaminika alilazimika kufanya hivyo baada ya kujenga chuki na wasomi aliowasomesha mwenyewe ambao walikuwa wakitoa ushauri kulingana na taaluma zao na yeye na TANU kuutafisiri ushauri huo kama kuhatarisha nafasi zao hivyo wakaitwa wapinga mapinduzi.

Lilikuwa ni jambo la kawaida katika viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma nchi nzima kukuta Mwenyekiti wa TANU akiwa ni mfanyakazi wa kada ya chini kabisa kutokana na kukosa elimu lakini kwa mujibu wa Mwongozo wa TANU ya wakati walilazimika kushirikishwa katika vikao vya menejimenti za viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma.

Miongozo hii potofu kiuchumi ya TANU na tabia ya kuingilia menejimenti za viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma ndio ilianza kuzalisha idadi kubwa ya makada wa TANU na badaye CCM ambao hawakuwa elimu, tija wala manufaa yoyote lakini TANU na Serikali yake kwa makusudi kabisa ikwa inapawa sauti kubwa sana katika uongozi wa viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma. Na hii ndio sababu kubwa ya viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma kuanza kuendeshwa kiholela kwa hasara. Lakini mara zote Serikali ya Mwalimu Nyerere ikawa inachota mabilino ya walipa kodi wa Tanzania na kuyatumia kuendesha viwanda, mashirika na makapmpuni ya umma bila ya watanzan ia kupatiwa nafasi ya kuhoji kulikoni mitaji ya mwanzo ilikoenda? Kila aliyejaribu kuhoji awe mbunge, raia n.k aliwekwa kizuizini chini ya Sheria ya Preventive Detention Act.

Lilikuwa ni jambo kawaida kwa viongozi matawi ya TANu mahali pa kazi kupelekea malamiko ya kimajungu kwa Mkuu wa Wilaya ambaye pia alikuwa ni kada. Wakuu wa Wilaya na Mikao walikuwa na uwezo kamili wa kutengua maamuzi ya kitaalamu ya manejimenti ya kiwanda, shirika au kampuni fulani ya umma. Sasa katika hali hiyo tumlaumu nani kwa viwanda, mashirika na makampuni ya umma kufa? Ni dhahiri haya yalikuwa ni matumizi mabaya ya madaraka ya uraisi.

Kipo kisa kimoja kilitokea katika Hospitali ya Muhimbili, Dkltari Bingwa wa magonjwa ya Moyo alikuwa akiendesha kliniki zake kila siku ya J'nne kuanzia Saa mbili asubuhi. Mhudumu wa ofisi ya daktari hiyo ndio alikuwa Mwenyekiti wa Tawi la TANU, hivyo alikuwa hafanyi majukumu yake ya uhudumu na badala yake kila kukicha ni kupiga soga sehemu mbali mbali katika hospitali hiyo.

Kila mara dakatari aliporipoti suala hilo hatua zilishindwa kuchukuliwa na menejimenti kwa kuwa Mwenyekiti wa TANU ni sehemu ya menejimenti na hudai kuwa Mwongozo wa TANU unakataza Unyapara na Ukaripiaji, na kwamba TANU inaamini kuwa binadamu wote ni sawa.

Siku moja Daktari bingwa baada ya kuchoshwa na tabia za mhudumu huyo aliwahi asubuhi sana siku ya kliniki na kufanya matayarishao yote yanayohitajika kwa ajili ya chumba cha daktari. Baada ya kumaliza akakaa sehemu ambayo hustahili kukaa mhudumu akisubiri kutumwa. Wagonjwa wakaanza kumiminika kama kawaida, lakini huduma hakuna kwa kuwa dalktari kakaa sehemu ya mhudumu na mhudumu husika hajafika yuko mitaani anaopiga soga.

Wagonjwa baada ya kukosa huduma iliwabidi wafikishe malalamiko yao ngazi za juu, na daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo alipohojiwa; Jibu lake lilikuwa ni lile lile kuwa "kwa mara zote uongozi wa hospitali hiyo umekuwa ukikubali hoja za Mwenyekiti wa TANU kuwa binadamu wote ni sawa, hivyo siku hiyo yeye (daktari) amefanya majukumu ya mhudumu na mhudumu huyo ndiye atawatibia wagonjwa siku hiyo.

Nia yangu sio kumchafua Mwalimu Nyerere, namheshimu sana hususan kwa kutotumia madaraka yake kujilimbikizai mali. Lakini ukweli ni lazima usemwe kuwa matatizo mengi tuliyonayo hivi sasa kama taifa chimbuko lake ni siasa za Uongo na Ulagahai za Mwalimu Nyerere ambapo alifanikiwa kujenga jeshi kubwa la wababaishaji ambao hurithishana toka enzi zake. Ili kufanikiwa kuendesha siasa za ulaghai na uongo Mwalimu Nyerere alipika historia ya taifa hili kwa kubadilisha mtiririko mzima wa matukio yaliyopelekea Tanganyika kupata uhuru kutoka kwa wakoloni wote wawili pamoja na kubadilisha wahusika pia kwa maslahi yake.

Katika kufany hivyo wapo wahusika muhimu katika harakati za kudai uhuru kwanza kutoka kwa Mjerumani na kisha Mwingerreza hawajawahi kutajwa popote, na wamekufa kama watu wa kawaida bila ya heshima yoyote. Na badala yake wapo watu wengi ambao walikuwa ni vibaraka tu lakini hawakutoa michango yoyote ya maana katika harakati za kudai uhuru Mwlimu Nyerere aliwapatia heshima kubwa ili kutengeneza taswira kuwa haralkati za kudai na kuleta uhuru wa Tanganyikia ziliznzia na kuishia kwa Mwalimu Nyerere na watu wanaomuzunguka ambao wamepata heshima feki. Mfano hai wa watu walioptiwa heshima feki na Marehemu Karume kuwa aliongoza mapinduzi ya Zanzibar ilihali sio kweli hata kidogo.

Dhambi hii kama zilizvyo nyingine haiwezi kupita hivi hivi, vijana wa kizazi hiki mna kazi kubwa ya kumtafuta mchawi aliyewaroga watanzania ndipo mtaweza kupata dawa ya kuwaangua!!!

Ni hadi pale tutakapaoweza kuandika histori ya nchi hii ya ukweli ndio tutaweza kuondokana na matatizo haya tuliyonayo kwa kuwa hadi sasa hatujitambuai sisi ni nani.

nakugongea senks mara 100, nilligusia hili kidogo kwenye mada yangu ya J.K nyerere na siasa za maji taka, nikapingwa sana, lakini ukweli utabaki kuwa ukweli. kwa leo, sitaki kuchangia sana, ngoja nisome mawazo ya wadau.
 
Usichanganye suala la Founders (waasisi) kitu ambacho hakina shaka waliikuwepo wengi, waasisi wa Taifa letu ni wengi na mojawapo ya ugomvi mkubwa katika fikra zangu na CCM ni kuwa hatujawapa heshima inayostahili waasisi wetu. Lakini tunaposema Father of the Nation tunampa heshima Nyerere kuwa he - alone and in unique way - played a role that no other of our founders played. He was instrumental in the independence struggle, in bringing TANU to the majority of the people (as you can read in M. Said's book on Sykes) and in the very beginning of our nation's history he was the leader of other leaders. His role as the first prime Minister and first President of our nations is alone his. Thats why we honor hims as Father of the Nation.

Kumpa heshima mtu au kiongozi si pale tu anapoanza kuongoza, bali hata pale anapomaliza. Lakini linapokuja suala la Nyerere lazima tujue nini dhumuni lake la kuwa kiongozi wa TZ? na je alimaliza vipi kazi yake? Jibu, Alitakiwa awaongoze WTZ na kuwapa prosperity ya maisha, elimu, nk. Ktk hilo kafeli. Nyerere kama kiongozi wa nchi katumia madaraka yake kama Rais kuwafunga WTZ jela bila ya sababu, kawanyima haki za msingi Freedom. Kama unataka kumpa heshima kwa sababu ya Uhuru tu- sawa. Lakini linapokuja suala la kuongoza nchi, kuheshimu sheria za nchi, kafeli tena vibaya sana. Duniani kiongozi anapewa heshima pale anapoanza na aitunze mpaka pale atakapomaliza. Nyerere alishindwa kumaliza. Ukiangalia hata ktk leadership skills kama, umefeli mwishoni, basi wewe unaehesabika kama FAILURE. Kwa matiki hii, Nyerere yupo ktk group la FAILURE.
 
Back
Top Bottom