Jambo Usilolijua: Kambona -"Nyerere... Baba wa Taifa"; Hotuba yake tuliyoisahau

Kasaini yeye kulikubali. Utaitaja wapi Tanzania umsahau Mwalimu? Historia haifutiki wala kuandikwa upya.
Ni kweli watu watamkumbuka kwa madhira alivyo tutenda Watanzania. Ila Tangia ameondoka, kiasi tunapumua. Uffuuuuuuuuuu!
 
Ni kweli watu watamkumbuka kwa madhira alivyo tutenda Watanzania. Ila Tangia ameondoka, kiasi tunapumua. Uffuuuuuuuuuu!
Ni kweli mnapumua. Mikagoda hii, mimeremeta hii, miRichmond hii, uporaji huu wa rasilmali zetu kama madini, wanyama. Mwalimu aliilinda NCHI hii na rasilmali zake kwa nguvu zote. Alionekana dikteta hasa kwa wezi, mafisadi na watu wa aina hiyo. Alituachia NCHI bikira kabisa.
 
Speech hii imenipa picha tofauti kabisa ya Kambona. Kumbe alikuwa muwazi sana na aliamini katika demokrasia ya kweli, ambapo wananchi ndio wanakuwa na sauti katika kuamua hatma ya nchi yao. Natamani hotuba hii ingechapishwa na kusambazwa kwa wabunge wetu na viongozi wengine wa sasa labda itasaidia kujenga sense ndani yao. Wengi wao wanajiona miungu watu.
 
Ni kweli mnapumua. Mikagoda hii, mimeremeta hii, miRichmond hii, uporaji huu wa rasilmali zetu kama madini, wanyama. Mwalimu aliilinda NCHI hii na rasilmali zake kwa nguvu zote. Alionekana dikteta hasa kwa wezi, mafisadi na watu wa aina hiyo. Alituachia NCHI bikira kabisa.
Ni kweli alilinda, maana waliofilisi mali za umma walikuwa wakubadilishwa tu, ukiharibu hapa unapelekwa pale...! Kweli alijuwa kulinda na kuwalinda.
 
hehehe...umeona hilo ehhe? As if Tanganyika isingekuwa huru bila yeye! Give me a break...
Freedom was on the pipe no matter what...
Sijaona convincing evidence yeyote kuwa Nyerere single handed brought independence in Tz.
That said, it still good to appreciate him and give him his due rights and respects.

tatizo mnasoma vitu visivvyokuwepo; hivi Michael Jordan alishinda makombe ya NBA peke yake? Je Chicago Bulls ingeweza kuja kushinda vikombe bila Michael Jordan? Je wakati anacheza alikuwa ndio mchezaji nyota pekee katika NBA kuwasahau kina Karl Marlone, Scott Pippen na wengine? Kwanini MJ anakumbukwa zaidi kuliko wengine wa zama zake?

Hakuna mtu aliyedai mahali popote kuwa Nyerere "single handedly" brought Independence to Tanganyika; but you CAN not talk about Tanganyika's independence without acknowledging the historical contribution and unmatched role that Nyerere played. You can try, but will not succeed.
 
Ni kweli watu watamkumbuka kwa madhira alivyo tutenda Watanzania. Ila Tangia ameondoka, kiasi tunapumua. Uffuuuuuuuuuu!

Wakati mnawakataliwa watetezi wa Nyerere kwa kuona ati wanajaribu kumfanya "malaika" wakati wao na Nyerere mwenyewe wanakubali makosa kadha wa kadha ya kihistoria ya Nyerere ambayo hayahitaji weledi wa juu kuyaona. Upande wenu hata hivyo, hamko tayari hata kukiri zuri moja la Nyerere na hivyo mnajitahidi sana kumfanya Shetani. Itawasaidia mkijaribu japo kidogo kutambua mchango wa Nyerere kwa maisha, fikra na historia ya Tanzania - labda hapo mtakuja kwenye kuhumu kwa mizani ya haki kidogo. Katika hili tunaomtetea Nyerere tunawapita kwa mbali sana.
 
Kweli jambo usilo lijuwa...!

Kuna ambaye amemsema Nyerere kuwa ni shetani, au unalazimisha sasa watu wamuone au kumwita Nyerere hivyo unavyotaka?
 
Ni kweli mnapumua. Mikagoda hii, mimeremeta hii, miRichmond hii, uporaji huu wa rasilmali zetu kama madini, wanyama. Mwalimu aliilinda NCHI hii na rasilmali zake kwa nguvu zote. Alionekana dikteta hasa kwa wezi, mafisadi na watu wa aina hiyo. Alituachia NCHI bikira kabisa.
Misingi aliyoiacha mizuri ilikuwepo, watu aliowaachia ndo shida.Mambo ya chama kushika hatamu yaliharibu.Chama chake kimemwangusha,hilo liko wazi sana tu.Pengine he shouldve done something kuhusu hili jinamizi ccm.Huwezi kuzungumzia historia ya mwalimu naTaifa bila kutaja CCM kwasababu CCM ndo serikali na utendaji wa serikali unategemeana na sera na itikadi za chama.There is no need to beat around the bushes....These are the facts peeps.
 
tatizo mnasoma vitu visivvyokuwepo; hivi Michael Jordan alishinda makombe ya NBA peke yake? Je Chicago Bulls ingeweza kuja kushinda vikombe bila Michael Jordan? Je wakati anacheza alikuwa ndio mchezaji nyota pekee katika NBA kuwasahau kina Karl Marlone, Scott Pippen na wengine? Kwanini MJ anakumbukwa zaidi kuliko wengine wa zama zake?

Hakuna mtu aliyedai mahali popote kuwa Nyerere "single handedly" brought Independence to Tanganyika; but you CAN not talk about Tanganyika's independence without acknowledging the historical contribution and unmatched role that Nyerere played. You can try, but will not succeed.

I think tupo on the same page. Sijawahi kusema contribution yake ni sifuri na isipewe heshima zake.
Lakini pia criticism iwekwe wazi. Kuna watu wanaamini kuwa Nyerere was right on all matters. That is what am against!
Kwa hilo swala la single handed bringing independence, ni maoni niliyopata kutoka kwa wengine...
 
Oscar Kambona alichapisha vitabu vinne ambapo alikaa London miaka 1968-1970:
1. Crisis of democracy in Tanzania
2. Tanzania and the problems of African unity
3. Tanzania and the rule of law
4. Tanzania: la defense accuser: Differences between Oscar S. Kambona and President Julius Nyerere
Aliporudi Tanzania mwaka 1992 aliandika mawazo yake ndani constitution ya TADEA pia....
 
Jamani pitieni tena fungu la maneno yaliyoko ukurasa wa saba (7):pdf file, palipo andikwa UFALME TUMEUKATA...na fungu hilo limeanza na maneno "Bwana Spika..."

Kambona aliamini kuwa kiongozi ni yule mtu anayefaa kuongoza siyo kiongozi wa kwa sababu mtu huyo "kazaliwa'. Cheo ni dhamana.
 
Mwanakijiji,

Binafsi kwa muda sasa nimekua nikiasa kuwa kuna haya ya `kumfufua` kambona katika historia ya nchi hii. Upotoshwaji uliofanywa kwa makusudi ni lazima usahihishwe. Kuna mengi chanya ambayo ni funzo kwa vizazi vya leo na hata kutoka kwa kiongozi huyu mzalendo.

Kwanini kumfufua?

Kambona ni miongoni mwa viongozi ambao vijana wa leo hawawafahamu kabisa. Hata pale anapotajwa,yanayofahamika kumuhusu ni hasi mno. Lakini ni wazi kuwa, alikuwa na ujasiri wa kupingana na nyerere. Aliweza kusimamia alichokiamini. Hii ni sifa muhimu sana ya kiongozi hasa ambaye anapaswa kuongoza nchi yoyote ya dunia ya tatu. Nyerere ana nafasi yake ya msingi na ambayo hakuna anayeweza kumpokonya. Hata hivyo, Kambona anapaswa kupewa nafasi yake katika historia ya nchi hii. Ni haki yake kwa utumishi na juhudi alizotia katika harakati za ukombozi na hata baada ya hapo.

Mwanakijiji, napingana na wewe kuhusu imani ya Kambona juu ya `demokrasia ya chama kimoja`. Kambona hakuliamini hili kama unavyopendekeza hapo juu. Kwanza,ushahidi pekee wa hiyo hotuba kwa kuitaja `demokrasia ya chama kimoja` katika hotuba yae,haitoshi hata kidogo kuonyesha kuwa alikua na imani nayo. Kama tukifikiria kwa muktadha ule wa baada tuu ya uhuru,ukichanganya na euphoria ya kupata uhuru,ni wazi kuwa Kambona hakua na nafasi na ushawishi wa kutosha wa kupinga pendekezo la Chama kimoja. Nyerere alikua kileleni kiushawishi. Lakini tunaona kadri muda ulivyokwenda Kambona alijenga ushawishi na ufuasi na hili linajionyesha wakati wa uasi wa 1964. Role ya kambona katika utatuzi wa uasi ule ni ishara tosha kuwa alikua kwenye nafasi tofauti kiushawishi. Na ni baada ya uasi ndipo tofauti kubwa kati ya Kambona na Nyerere zilipoanza kuonekana. Kwa mtizamo wangu, ni wazi kuwa Nyerere alianza kuona Kambona ni tishio.

Sababu ya pili ya kwanini kambona hakua anaamini katika `demokrasia ya chama kimoja` inatokana na uamuzi wake wa kutoroka nchini baada ya azimio la Arusha kutangazwa. Kama aliweza kuamini katika demokrasia ya Chama kimoja,ilimshinda vipi kuvumilia ujamaa? Ni wazi kuwa katika wakati huu,alikua na sauti ya kupinga tofauti na kipindi maamuzi ya chama kimoja yanapitishwa. Na hata baada ya kupinga, aligundua kuwa tayari alikuwa anaonekana tishio na kwa usalama wake ikampasa kuondoka.

Na tofauti yao kubwa haikuwa kuhusu chama kimoja tuu bali itikadi kwa ujumla. Na ni wazi kuwa waliokua na imani juu ya itikadi tofauti na ile ya Nyerere walikuwa wengi,siyo kambona tuu. Mzee Edwin Mtei ni mfano. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru alihojiwa na Issa G Shivji (Jarida, ChemiChem 2010) kuhusu sababu za kushindwa kwa ujamaa na akiwa anamjibu alisema tatizo walishindwa kujenga ufuasi. Ujamaa ulikuwa ukitekelezwa na watu wenye fikra za kibwanyenye.

Shukrani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom