Jamani ze comedy TBC1 kuna nini?

Lofefm

Senior Member
May 22, 2011
126
71
Muda kidogo umepita tangu kundi la orijino komedi (OK) kuamia TBC1 lakini mpaka sasa kundi hili limeacha kazi yake kuikosoa serikali badala yake imekuwa ikiyafumbia macho maovu ya serikali ila sasa kazi yao ni kuitetea serikali na kuwakandamiza wapinzani kwa mfano kipindi bajeti mbovu ilivyotolewa na waziri tulitarajia tuone kazi yao ya sanaa ya kuikosoa serikali mbali na kuchekesha tu. Swali kwako mwana JF unafikiri ni nini sababu kubwa ya swala hili au mtazamo wako ni upi???
 
The answer is quite simple: Huu ni utawala wa Mshana ambaye ni kibaraka wa serikali. Usitegemee kuikosoa serikali. Sahau enzi za uwazi wa kweli wa Tido Mhando. Umakini mkubwa ulifanyika kumchagua Mshana, nothing but a puppet of CCM.
 
sio Ze comedy peke yake iliobadirika hata vipindi vingine vya TBC, na sababu ipo wazi wameshaisema wadau
 
sio Ze comedy peke yake iliobadirika hata vipindi vingine vya TBC, na sababu ipo wazi wameshaisema wadau
I can't agree more on this...angalia quality ya programs ilivyoshuka...taarifa ya habari kwa mfano.
 
Wale jamaa mmesahau wamezunguka na kitwete nchi nzima wakati wa kampeni?
 
Ze Komedi kazi yao ni kuchekesha na hilo bado wanalimudu.

I highly doubt this...mfano tu wa kipindi cha last week..pliz pliz pliz, nipe kichekesho kimoja tu from their show??! kimoja tu?
kazi yao kupondea wapinzani etc etc..seriously, mi mwenyewe nlishangaa...
 
Nasema ningekuwa mhadhiri wa management development...ningetumia TBC as a case study kufundishia management, leadership and governance.
 
Siku zote UKIKUBALI KUNUNULIWA KWA MASLAI YA WACHACHE JUA HUO NDIO MWANZO WA MWISHO WAKO UMEFIKA, ZEE COMEDY ORIGINAL KWISHILIA MBALI bado mda kidooogo itabaki stori tuu
 
Nafikiri sera ya TBC inajulikana kuhusiana na masuala ya siasa!hakuna jipya hapo mkuu!!
 
Nasema ningekuwa mhadhiri wa management development...ningetumia TBC as a case study kufundishia management, leadership and governance.
Ungeongelea kama management iliyofanya vizuri au iliyoshindwa!!
 
Eti nasikia wamezibwa mdomo!!!!! Kwenye sherehe za serikali nao wamo,mizunguko yote ya juhudi kwanza(j.k) walikuwepo sasa we unategemea niini mdau hapo?????

Haaa kweli chezea mshahara na sio kazi
 
Nyie hamjawaona walivyonenepa siku hizi?. Mnaddhani unene ule wanaupata wapi!. Halafu wajitilie mchanga kitumbua chao!
 
Unashindwaje kufananisha TBC, Orijino Komedi, HABARI LEO and the like?
They are travelling in the same boat
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom