Jamani wataalam mimba kutungwa karibu na cervix ni hatari??

kvelia

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
246
44
jamani naomba ushauri wa kitaalam, mimba inatungwa kwenye uterus au wapi? Kuna dada mmoja ana mimba ya mwezi kama na nusu hivi, anadai mimba imetungwa karibu na cervix, alienda hospital wakamwambia ikikuwa itapanda hadi kwenye uterus, naomba kuuliza hii inakuaje na ni kweli? Asanteni sana.
 
Uterus imegawanyika katika sehemu mbili, body na cervix; mimba ikisha tungwa na wiki zikasogea body pia hugawanyika mara mbili upper segment na lower segment. Lower segment ndo sehemu iliyo karibu kabisa na cervix endapo mimba itatungwa (au placenta) kwenye lower segment, mama atapata tatizo linaloitwa placenta previa na atakuwa anatokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito. Na hiyo placenta inakuwa graded kutokana na ukaribu wake na hilo tundu la cervix (cervical os). wakati mwingine hufunika kabisa hilo tundu na mama humlazimu kujifungua kwa upasuaji.
Ni kweli kwamba huwa inasogea kadri mimba inavyokua lakini ni vizuri akafuatiliwa kwa karibu na wataalamu.
 
Back
Top Bottom