Jamani wakwe wanatuchanganya;ushauri wenu chanya muhimu

Choose your first point, you have to make tough decision.
Wahusika wakuu ni ninyi wawili, ila kiutamaduni wetu sisi waafrika ndio unakuta tuna taratibu zingine za kimila huwa zinapaswa kufuatwa kutokana na jamii au kabila husika. Hapo hakuna kizuizi cha maana ambacho kitapelekea kutokutimiza azma yenu, endelea na taratibu kama kawaida fungeni ndoa (hili ndio la msingi). Kwa sisi tunaotoka vijijini hivyo ni vizingiti vya kawaida, mara shangazi kasusia harusi au sijui nani; na ukifatilia unakuta ni ndugu wa mbalimbali ndio wanaleta vikwazo kukwamisha swala hili la neema. Ushauri wangu endeleeni na mpango wenu wa ndoa na wife to be ndio aonyeshe msimamo wa hali ya juu kwa upande wa ndugu zake.
 
Mkubwa wewe endelea na mipango yako. Sione sababu ya maana ya kuahirisha zoezi wakati ndoa ni makubaliano ya watu wawili iweje mtu wa tatu aweke kiwingu? Kwanza walishakubali na hiyo ndiyo point ya kushikilia. Usikubali decision yao iwe "tentative". Chacharika na mshenga na kuwa mkali vinginevyo watakusumbua. Pia kama mmoja alivyoshauri hapo juu hebu fanya intelijensia ujue chanzo isiwe kuwa na binti mwenyewe maana na wenyewe hawatabiriki.
 
Nakusihi uende kwa ndugu zake waliomlea. itakuwa vizuri ukimshikirisha Mungu jambo hili na kawaone watumishi wa Mungu wa kanisa ua msikiti mahali alipolelewa huyo mchumba wako.Mungu afunge roho chafu zinazotaka kuinuka juu ya jambo hili na kuruhusu upokeaji wa mahari kwa ndugu zake mwanamke
 
Mijitu mingine mikatili....utadhani itaenda kuishi na hao wanandoa. Oa bana huna kosa lolote
 
Habari za ujenzi wa taifa wanajamii??

Walionesha kama kutopendezewa kimtindo ila ndio hivyo wakakubali hiyo posa na majibu ninayo.Baada ya majibu tulipendekeza tarehe ya kupeleka mahari na mimi nikafunga safari hadi kwetu kupeleka taarifa ya nilipofikia na mategemeo ya kupeleka mahari.so na nyumbani kulingana nazile tarehe na jinsi ambavyo nilitegemea kufunga hiyo ndoa wakaseti tarehe za vikao tarehe baada ya tarehe yetu ya mahari. ilipokaribia wakasema kuwa hawatopokea wako bize na maandalizi ya harusi ya ndugu yao mwingine anaoa so hadi harusi ipite,hiyo ni wiki 3 mbele,wakati huo mikakati nyumbani ilikuwa inaenda kama ilivoppangwa na ukumbi ukalipiwa ili kuwahi tarehe tajwa ili mtu mwingine asijetuzidi.

Aisee binafsi sioni kama kuna tatizo kubwa unless nimekuelewa vibaya. Inaonyesha wasiwasi wako uko hapo kwa red. Sijui mahali ulipo lakini kwa uzoefu wangu unaweza kubadilisha tarehe ya harusi (kwa kuwataarifu wenye ukumbi) ili kuwapa nafasi ya kutosha ndg wa upande wa bibi harusi mtarajiwa. Vinginevyo itaonekana kama unataka kuwaburuza. Unaweza kuchukulia kirahisi tu kwa sasa lakini naamini hata wazazi wako pamoja na ndgu zako wengine hawatafurahi kama ndg wa upande wa pili hawatakuja kwenye sherehe yenu.

Usisukumwe na historia ya makuzi ya huyo mchumba wako, tena ikiwezekana usiwe sehemu ya hizo tofauti zao. We jipange kuhakikisha harusi inafanyika na ndugu wote wa pande mbili wapewe nafasi ya kushiriki. Jitahidi sana kuwa flexible na hizo tarehe, ni wengi tu walishabadilisha tarehe za harusi zao.

Mi nashauri ufanye no.2 kama ulivyoeleza kwenye post yako. We onana na watu wa ukumbi mbadilishe tarehe, halafu badala ya kusimamisha vikao mna-extend interval ya tarehe za hivyo vikao.
 
hujamuoa tu? Hebu fanyeni maamuzi magumu

Aisee mkuu badili tabia tayari nimeshaoa tangu januari na sasa kama vile walivosema kina Kongosho na wengine kuwa hao ndugu watakuja na kweli wamekuja na tayari nimepokelewa na baadhi ya ndugu
 
Prince Nadheem kusema yaliyokutokea ni kama yaliyonitokea mimi ingawa kidogo kuna utofauti. Kwa kushare yaliyonikuta mimi basi unaweza kupata ushauri wangu ambao utasaidia.

Mimi mchumba wangu(sasa mke wangu) alikuwa yatima, alikataliwa na baba yake. Mama yake alifariki akiwa mdogo na baba yake alifariki miaka kama 15 iliyopita. Baba yake hakuwahi kumpenda(na offcoarse alimkata). Mke wangu alilelewa na baba mkubwa mwenye mabinti watatu. Binti wa pili analingana umri na mke wangu.

Mke wangu hakuwa amezaa mtoto(tofauti na mchumba wako) lakini mama yake(mke wa baba mkubwa) pamoja na baadhi ya ndugu walikuwa wanamchukia vibaya mno.

Mke wangu alididimizwa kwenye kila jambo. Wenzake walisomeshwa shule za international yeye kayumba. Bahati nzuri alikuwa na akili na alifaulu kwenye kila ngazi wakati wenzake wakifeli.

Mke wangu ni mzuri. Alichukua uzuri na tabasamu la mama yake. Basi hii ikazidisha chuki kwa yule mama. Alimnyanyasa sana.

Mke wangu mpaka kwenda chuoni alikuwa amepata course nzuri kabisa lakini akadhulumiwa na kupelekwa course mbovu ya kawaida ati asilingane na wenzake.

Tumekaa uchumba for 6 years. Akaanza kutukanwa na yule mama kuwa yeye ni malaya etc. Kabla hajakutana na mimi alikuwa na uhusiano na kijana fulani. Kuachana nae na baadae kuwa na mimi ambaye mpaka leo niko nae ati ni umalaya

Tukaanza utaratibu wa kupeleka barua, posa etc. Yule mama alikuwa analewa na kutukana. Malaya huyu, mvivu, hafai kuolewa na maneno kem kem.

Nakumbuka siku moja kabla ya mahari aliongea shit kiasi kwamba nilipanic home na kutaka kwenda kwao kumuanzishia utata maana nilishachoka.

Kwenye mahari, sendoff, harusi ilikuwa ni vituko. Mama anaongea mpaka watu wanajiuliza mke wangu kamkosea nini.

Sasa tuko kwenye ndoa tamu kabisa tuna kijana mmoja wa afya. Mama roho inamuuma, nafsi inamsuta hajielewi, amekuwa kama mwendawazimu.

Na sababu walimkandamiza mke wangu nimeamua kuhakikisha anapata elimu ya kutosha na kufanikiwa vibaya sana.

Ushauri;

Nenda taratibu usiruke chochote. Ongea na mshenga na familia yako kiundani especially kwa watu wako wa karibu. Waelezee situation na muahirishe. Ukishamuoa mtakaa kwa raha. Msilazimishe mtaoana tu sababu MNAPENDANA.

Upendo wa kweli una LAST FOREVER!
 
Last edited by a moderator:

nimeipenda hii.
 
Last edited by a moderator:
Sijui kama mmegundua kwamba thread ni zaidi ya mwaka sasa. Tunaweza kumuuliza mleta uzi Prince mmefikia wapi kwa sasa na alifanya maamuzi gani?
 
Aisee mkuu badili tabia tayari nimeshaoa tangu januari na sasa kama vile walivosema kina Kongosho na wengine kuwa hao ndugu watakuja na kweli wamekuja na tayari nimepokelewa na baadhi ya ndugu
Ni kweli inabidi kubadili tabia. We are not serious. Its more than a year now. HONGERA MKUU.
 
poleni, ningekuwa mie, tungeanza kuishi wote tu hiyo ndoa mkabariki baadae, tena mjaze na mimba kabisa.
Hii ndio suluhisho....Vinginebyo huko kijijijini lazima watakwamisha mambo kwa sababu ya uroho wa kugawana mahari...
 
Back
Top Bottom