Jamani Wachagga mbona mnatutesa hivi hapa Ubungo Terminal?

Kwa masikitiko makubwa sana sisi Wasafirishaji wa hapa Ubungo Terminal tunapenda kutoa ' lawama ' zetu kubwa na za dhati kabisa kwa hawa Wachagga hasa kwa kitendo chao cha ' Kikatili ' kabisa cha kuamua rasmi kuwa msimu huu wa Siku Kuu za mwisho wa mwaka hawatosafiri tena kama kawaida yao kwenda Kwao Mkoani Kilimanjaro ( Moshi ) kuhesabiwa kama ilivyozoeleka kwa miaka takribani 50 iliyopita.

Wengine tulishachukua hadi ' mikopo ' na kununua ' Mabasi ' ili tuwasafirisheni kwani tunajua kuwa mwezi huu huwa hambaki Dar na nyote hurudi kwenu Hedaru, Same, Sanya Juu, Kiboroloni, Siha, Hai, Rombo, Marangu, Mweka, Mwanga, Usangi na kote kote huku wengine ' tulijiongeza ' na hadi kununua ' Bajaji ' na ' Pikipiki ' ili tuweze pia kuwasafirisheni wale ambao mtakuwa mmechelewa kwenda ' kuhesabiwa ' lakini hali sasa imebadilika na inaonekana ' tutaumbuka ' sana na kuingia ' hasara ' kubwa.

Kwa niaba ya Wafanyabiashara ya ' usafirishaji ' tuliopo sasa hivi hapa Ubungo Terminal naomba kuwaulizeni ' Wachagga ' wote popote pale mlipo kuanzia humu humu JF Je ni kitu gani ' kimewakumba ' hadi sasa mnaonekana mmekuwa ' wagumu ' kusafiri kwenda kwenu Mkoani Kilimanjaro ( Moshi ) kama ilivyozoeleka na ilivyo kawaida yenu? Tatizo ni nini?

Tafadhalini Wachagga naomba mnijibu haraka na sasa hivi ili nami niweze kuwajibu ' Wasafirishaji ' wenzangu sasa hivi hapa Ubungo Terminal kwani kuna wengine sasa hivi wameenda hadi kuwekeza kutaka kununua yale ' matoroli ' aina ya ' Maguta ' ili tu na wao waje kuwasafirisheni kwenda kwenu kwa kuwasukumeni kutoka Dar hadi Kilimanjaro hivyo majibu yenu yatatusaidia wengi ambao ' tulijiongeza ' katika kuwekeza katika kuwasafirisheni mwezi huu wa December.

Natanguliza ' shukurani ' zangu kwenu Wachagga wote!



Wachagga sio kwamba hawataki kwenda kuhesabiwa la hasha, bali wameokoka wakaacha tabia zao za matambiko na kuchinjachinja wanyama na kisusio wanasema ni dhambi ya mauti, pili wanajizatiti kuwekeza kwenye viwanda badala ya hardware, guest house na bar, kwa hiyo mwaka huu wanatesti kula bata mamtoni Dar! Teh teh teh, shikamoo uchumi wa viwanda!
 
Wasipokwenda kutambika watawezaje kukaa mjini? lazima waende wakanywe damu.
 
Sasa unataka tusafiri sasa ivi kana kwamba sisi ni wanafunzi wa primary au secondary school tumefunga shule? Muda bado sana wa kwenda likizo this festival season. Subiri mpaka tarehe 20 ndio uanze kulalamika.
 
Nakasikia kwa mbali KILE KINYIMBO CHA CCM MBELE KWA MBELE :):D Alafu ndo nasoma thread hiii yaani nimecheka hadi NIMEDONDOSHA UDENDA KWENYE KIOO CHA SIMU YANGU.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom