Jamani tuwe makini tunapotoa 'lift' za magari.

MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,798
2,004
Imemkuta jamaa yangu juzi. Alimuona dada mmoja jana maeneo ya fire anasubiri usafiri wakati anamuacha mshokaji wa ofisini pale. Yule dada alimfata na kumuomba msaada kwa madai kuwa anashuka Manzese.
Kutokana na shida ya usafiri iliyokuwepo juzi na foleni jamaa kaingiwa na moyo wa huruma, akakubali. Walipofika Manzese yule dada akamwambia simama nashuka. Jamaa aliposimama dada kaanza kupiga kelele, 'nilipe hela yangu, nasema nilipe hela yangu sasa hivi! Haiwezekani unilale muda wote ule halafu usinipe hela yangu, nipe sasa hivi'.
Jamaa alishikwa nabutwaa akawa haamini anachosikia na kukiona. Na kama kawaida ya Dar, watu wakaanza kujaa kuangalia kulikoni na kulizingira gari. Mshikaji ikabdi atoe sh. 10,000 na 'kumlipa', na kuondoka kwa fedheha sana.

Jamani tuwe makini sana barabarani. Unaweza ona unatoa msaada kumbe unajiumiza.
 
du pole yake hili ndo jiji bw kila kitu akili kichwani

Niliwahi sikia kwamba padre fulani aliwahi "kuingiwa na moyo wa huruma" kumsaidia "Sister" aliyevaa kilemba ambaye alisimama barabarani kuomba lift, kumbe hakuwa sister mwanamke, lilikuwa ni dume la mbegu, jambazi! Maskini padre alinyang'anywa gari na "Sister" huyo na kutokomea nalo! Wanaume acheni uroho, utawatokea puani!
 
kinacho waponzeni wanaume ni uroho na pupa zenu za kutaka kila mwanamke mrembo
 
kinacho waponzeni wanaume ni uroho na pupa zenu za kutaka kila mwanamke mrembo

Siyo uroho wa wanawake, bali aliomba msaada, kama binadamu akaamua kumsaidia. Tatizo ktk msafara wa mamba na kenge wamo. Just pray kwani pale ambapo hutaraji ndo yanatokea haya.
 
Pesa nisingelipa na ningekomaa nae na ninadhani huo ndo ungekuwa mwisho wake...Cha kwanza ningesubiri watu wajae kisha naangalia wenye busara kama watano hivi halafu nawaaambie twendeni kituo cha police na ili akaseme hiki anachokisema... yaani kesi ya kuku mie kulipa ngombe mbona sio ishu kabisa.. Angejuta
 
haya mambo yapo na hutokea mara nyingi....cha muhimu ukiwa peke yako usimpe mtu lift na pia wakati mwingine usiku kama kuna foleni huwa wanaingia kwenye gari kwa nguvu na kudai umpe hela kama huyo dada alivyofanya......kuepuka hayo lock gari na usizoee kutoa lift hovyo
 
Pesa nisingelipa na ningekomaa nae na ninadhani huo ndo ungekuwa mwisho wake...Cha kwanza ningesubiri watu wajae kisha naangalia wenye busara kama watano hivi halafu nawaaambie twendeni kituo cha police na ili akaseme hiki anachokisema... yaani kesi ya kuku mie kulipa ngombe mbona sio ishu kabisa.. Angejuta
We mpare mwenzangu nini broda?
 
Nina uhakika kama huyo muomba lifti angekuwa mwanaume asingepewa hiyo lifti. Pole mtoa lifti..
 
Leo asubuhi nimesimuliwa kisa kama hiki na jamaa yangu. kimemtokea ilala ila yeye alikomaa hadi polisi wakatokea na ikaonekana visa hivyo viko. dada alichukuliwa hadi kituoni akawa mpole. tuweni makini
 
halafu wewe....hivi ni kwa nini lakini?
 
Leo asubuhi nimesimuliwa kisa kama hiki na jamaa yangu. kimemtokea ilala ila yeye alikomaa hadi polisi wakatokea na ikaonekana visa hivyo viko. dada alichukuliwa hadi kituoni akawa mpole. tuweni makini
Ncha inabidi tutafutane dah tokea kipindi kile
 
Pesa nisingelipa na ningekomaa nae na ninadhani huo ndo ungekuwa mwisho wake...Cha kwanza ningesubiri watu wajae kisha naangalia wenye busara kama watano hivi halafu nawaaambie twendeni kituo cha police na ili akaseme hiki anachokisema... yaani kesi ya kuku mie kulipa ngombe mbona sio ishu kabisa.. Angejuta

MOB JUSTICE HAINA MUDA WA KUSUBIRI UCHAGUE WATU WA KWENDA POLISI.....PILI...KUNA KA MCHEZO KA POLISI KULA NJAMA NA WATU WA DIZAINI HII ILI UKIPELEKWA UKAMULIWE MALAKI KAMA HUNA UNAPEWA KESI YA KUBAKA 30 YEARS IMPRISONMENT
upo kakaaa.....!
 
Back
Top Bottom