Jamani tukubali, tukatae: Wahaya Waliusumbua Utawala wa Awamu ya Kwanza Miaka ya 1980s!

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
736
I. Nimekumbuka wale jamaa walio-engineer Mapinduzi,nadhani 1983-84.. Baadaye nitaweka jina lake. "Uncle somebody" walikuwa na ma-nickname wengine kama ya Kiingereza.

II. Naomba radhi kwa kukiondoa kipande hiki.. Maana kimepatiwa majibu na kila mmoja alikuwa anarudia hapohapo tu..
 
Na hata kipindi kilichopita vilevile,walikuwa maarufu kwa pilikapilika za utapeli na kunufaika nao kwa kutumia "usomi" wao...

Mfano kuna wakati mambo ya forgery yalipokuwa yamepamba moto,yaani saini,mihuri bandia,na hata miaka fulani vijana walipokuwa wanazuzuka na kwenda Marekani,wao ndiyo walikuwa vinara.

Kuna Nkrumah St palikuwa ndiyo centre yao.
 
Ndege haikutekwa na wahaya, walioiteka walikuwa WAKONONGO - kabila linalopatikana kwa Mizengo: Mousa Memba, Yasin Memba na mdogo wao Masoud Memba.
 
Asante kwa kuweka mambo sawa, huyu jamaa alikuwa anataka kuwapakazia wahaya bure!!!! Arudi afanye research upya sio kukurupuka na kuwapakazia wahaya!!!!

Tiba
 
hivi kwa nini nyerere hakumsamehe member Lee? maana nambiwa member lee alifia gerezani kwa mateso makali ajabu.
 
I. Nimekumbuka wale jamaa walio-engineer Mapinduzi,nadhani 1983-84.. Baadaye nitaweka jina lake. "Uncle somebody" walikuwa na ma-nickname wengine kama ya Kiingereza.

II. Na pia hao wenzetu wa Kaskazini Magharibi walihusika na utekaji wa ndege ya Taifa letu,"Kilimanjaro" Boeing 737,iliyokuwa katika safari zake za kawaida kutoka Mwanza,kwenda KIA,na kisha Dar.
-Hawa jamaa waliizungusha hadi Greece,hadi wapi,mwishowe London(sijui Gatwick ama Heathrow Airport),hapo ukapatikana msaada na mateka wakarudi salama.

N.B. Kwenye usukani alikuwa Capt. Mazula(RIP). Inasemekana aliendesha kwa masaa meng bila ya msaada wa mwenzake ambaye alijeruhiwa na maharamia haoi
Hii stori umeanzia juu juu sana mkuu, kuna wengine hatujui ilianzaje, wapi ilitekwa na ni lini ilikuwa, ilikuwa na abiria wangapi? Capt Mazula nadhani huyu alikuwa jirani yangu mwanza kama sikosei, niliwahi kumfundishia mtoto wake tuition ya hesabu miaka 12 iliyopita!
 
hivi kwa nini nyerere hakumsamehe member Lee? maana nambiwa member lee alifia gerezani kwa mateso makali ajabu.
Ingefaa swali hili ukamuulize Nyerere ndiye mwenye kujua kwa nini hakumsamehe.
 
Asanteni... Ndiyo maana ya kuyaleta kwenu ili kuweka mambo sawa...

Mwajua tunakosa "archives"... Baadhi ya mambo hujui "u-Google" ili uyapate.. Lakini JF,tunakutana watu wa aina mbalimbali,na haya mambo ni muhimu kwa historia yetu na yakajulikana kwa vizazi vya sasa n vijavyo..

Sikuwa na nia ya kupotosha..
 
Hii stori umeanzia juu juu sana mkuu, kuna wengine hatujui ilianzaje, wapi ilitekwa na ni lini ilikuwa, ilikuwa na abiria wangapi? Capt Mazula nadhani huyu alikuwa jirani yangu mwanza kama sikosei, niliwahi kumfundishia mtoto wake tuition ya hesabu miaka 12 iliyopita!

Mi mwenyewe sina data kamili.. Ilikuwa inatokea Mwanza kwenda KIA,kisha iende Dar.. Sasa sijui kama Dar ilifika ama la..

Idadi ya abiria sina,ila tarehe ya tukio ilikuwa 26/02/1982..

Walikuja kupokelewa na umati wa watu pale Trminal One..na ilikuwa inaripotiwa live kupitia stesheni ya redio..
 
Asante kwa kuweka mambo sawa, huyu jamaa alikuwa anataka kuwapakazia wahaya bure!!!! Arudi afanye research upya sio kukurupuka na kuwapakazia wahaya!!!!

Tiba

Waitu mshanage..

Sikuwa na nia ya kuwapakazia,ila nilisikia so kwa kutaka kuweka records zangu sawa ndiyo nikatupia hii thread..

Haya basi na kwa hayo mengine..
 
Ndege haikutekwa na wahaya, walioiteka walikuwa WAKONONGO - kabila linalopatikana kwa Mizengo: Mousa Memba, Yasin Memba na mdogo wao Masoud Memba.

Asante kwa taarifa.

Je kuhusu hayo mengine.. Ni ujasiri walionao,au usomi waliokuwa nao kipindi hicho,ama kutokana na nini..
 
Mi mwenyewe sina data kamili.. Ilikuwa inatokea Mwanza kwenda KIA,kisha iende Dar.. Sasa sijui kama Dar ilifika ama la..

Idadi ya abiria sina,ila tarehe ya tukio ilikuwa 26/02/1982..

Walikuja kupokelewa na umati wa watu pale Trminal One..na ilikuwa inaripotiwa live kupitia stesheni ya redio..
Wakuu Joka Kuu,Jasusi,SlidingRoof na wazee wengine waj JF ndio wanaweza kusaidia stori nzima ilikuwaje! Ktk wakongwe wa historia wanaostahili tuzo humu JF Joka Kuu na MM Mwanakijiji wanatisha sana! Lakini huu mkasa upo humu uki search utaipata.JF imeshajadili mengi mno toka 2006!
 
Mnadanganyana tu, hivyo ni visa tofauti na sikumbuki kama kulikuwa na Muhaya.

Wahaya ni watu wema sana na walisaidia sana vijana wa zamani wa Dar. Hususan mitaa ya Kisutu, Morogoro Rd. na Gerezani siku hizo walikuwa maarufu kama "mabota".

Hatuwasahau kwa ukarimu wao wa kukaribisha wageni walipowatembelea na "kariiibuu" na pia walikuwa wana huruma sana na wageni na kuwakopesha ilikuwa ni jambo la kawaida. Tuwaenzi kwa hilo.
 
Asante kwa taarifa,na naipokea kwa mikono miwili..

Nami nachukua nafasi hii kuwapa credits akina Jokakuu,MM/jiji,na Sliding roof..
 
Mnadanganyana tu, hivyo ni visa tofauti na sikumbuki kama kulikuwa na Muhaya.

Wahaya ni watu wema sana na walisaidia sana vijana wa zamani wa Dar. Hususan mitaa ya Kisutu, Morogoro Rd. na Gerezani siku hizo walikuwa maarufu kama "mabota".

Hatuwasahau kwa ukarimu wao wa kukaribisha wageni walipowatembelea na "kariiibuu" na pia walikuwa wana huruma sana na wageni na kuwakopesha ilikuwa ni jambo la kawaida. Tuwaenzi kwa hilo.

Angle uliyoko inahitaji thread ya peke yake..
 
Mnadanganyana tu, hivyo ni visa tofauti na sikumbuki kama kulikuwa na Muhaya.

Wahaya ni watu wema sana na walisaidia sana vijana wa zamani wa Dar. Hususan mitaa ya Kisutu, Morogoro Rd. na Gerezani siku hizo walikuwa maarufu kama "mabota".

Hatuwasahau kwa ukarimu wao wa kukaribisha wageni walipowatembelea na "kariiibuu" na pia walikuwa wana huruma sana na wageni na kuwakopesha ilikuwa ni jambo la kawaida. Tuwaenzi kwa hilo.

Mhh! acha utundu bwana!
 
Walioteka Ndege walikuwa ni vijana watatu wa familia ya Memba (Musa, Yasin,...........?) asili yao siijui ila waliokulia na kusoma Tabora.
Waliiteka Ndege kwa kutumia Maembe wakitishia kwamba ni Mabomu(guruneti). Ile ilikuwa njia yao ya kuendea Mtoni(Ulaya),na walifanikiwa.
 
Asante kwa taarifa... Hilo tumeshaliona..
 
Back
Top Bottom