JAMANI TUAMKENI....UFAHAMU Na HEKIMA VITAWAONDOA MAFISADI

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Dec 13, 2009
3,398
319
1.Nawaomba amkeni,
Enyi mlio vitandani,
Amkeni wajameni,
Amkeni msione soni.

2.Msilale kama pono,
Tena bila ya maono,
Tushikamane mikono,
Ili kuonesha mfano.

3.Umefika muda tena,
Tulioungoja kwa sana,
Wa kuzikataa furana,
Kuwachagua firuna.

4.Wana sura za huruma,
Kwa ndani zinahujuma,
Kutufanya maamuma,
Na akili zimezama.

5.Tumia akili yako,
Wala usijipe mwiko,
Simama usikae kitako,
Kutumia haki yako.

6.Vijana jitokezeni,
Fisadi weka pembeni,
Taifa tuokoeni,
Toka mwao mikononi.

7.Vijana taifa la kesho,
Hivyo ni vichekesho,
Huwa haifiki kesho,
Tuachane na mipasho.
 
Mimi nimesha amka
Toka vije vyama vingi
Msisite kuamka
Ili kure ziwe nyingi

Fungi fungi amka
Uzingizi uko mwingi
Usisite Kuamka
Tunataka Kura Nyingi

Mafisadi wamekaa
Pono usingizi kwao mwingi
Kusifike wakapaaa
Navyo vitu vyetu vingi

Tuwakaange kama kaa
Hawa pono wako wengi
Wamekaa lao kaa
Tusiwape kula nyingi

Anyisile kakamaa
Hawa pono tuwakimbi
Mali zetu wapakua
Watubakishia ukoko mwingi

Hawa pono wamekaa
Wakaa mkao vitimbi
Na vitisho wanatoa
Kwetu sisi chimbilii

Mageuzi nimekaa
Kuwaondoa Kingini
Nawenzangu Mkikaa
Hawaoni zetu siri

Tukae mkao wa kulaa
Kuwaondoa kingini
Mafisadi wamekaa
Wanastarehe chinichini

Tukikaa ufasahaa
Hawaoni kwetu kingi
Mafisadi watashaa
Wapotelee gizani
 
mwenye macho na aone,
lazima tusukamane,
kwa hekima tufatane,
mafisadi watuone.

ccm na tuizike,
kuzimu ikapumzike,
enyi waume kwa wake,
Chadema kura tuweke.
 
Back
Top Bottom