Jamani Saidieni Mama (Hawa Ngulume)

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Kweli nimeamini shukrani ya Punda ni mateke! Mama huyu amekitumikia chama chake cha CCM kwa miongo 18 akiwa kama Mkuu wa wilaya tofauti katika taifa hili! Akiwa kama kada muadilifu kwa chama chake lakini sipati picha aliwajibishwa na bosi wake JK kwa kosa gani! Alishawahi kuwa mkuu wa wilaya kadhaa kama vile Kinondoni/Bagamoyo na Kibaha. Sasa hivi jamani anaugulia kitandani na hakuna wa kumsaidia na hata chama chake cha CCM? Pole sana Mama Hawa Ngulume kwa yalio kukuta ni Mungu tu atakae kusaidia. Mama Hawa Ngulume subiri tuone serikali mpya kwa awamu ya pili kwa aliyekua bosi wako labda anaweza kua amesikia kilio chako natumaini hata hapa JF huwa anapitiaga akaona Post hii kuwa na subira hata Spika wa Bunge letu tukufu ni mwanamke Mama Anna Makinda natumaini atakakua ameshasikia kilio chako.:sad:
 
Alipkuwa kazini alitumiaje kipato chake? Maana kwa waafrika tegemeo la kwanza ni kuwasomesha vizuri watoto ile waje kuwa na kipato wakutunze utakapokuwa mzee. Kila mtu ana mzazi na anamhudumia, hakuna anayetegemea serikali ije kumhudumia mzazi wake hata kama alikuwa mtumishi wa serikali. Hivyo hisia zinazojengwa hapa kuwa serikali haiwaangalii wastaafu wake si sahihi, hakuna huo utaratibu; labda kama hajalipwa mafao yake hapo mwende kudai sehemu husika kwani JF halipi mafao
 
Tumchangie kiasi cha kutunisha mfuko wake wa matibabu.
tukiwaachia ccm waendelee kuimiliki hii nafsi itaangamia bila shaka.
tuweke tofauti za kisiasa pembeni tumwokoe mwenzetu.
Invisible anza kupokea buku buku zetu ukaziwakilishe
 
hatuna cha kumsaidia sisi provided anatoka CCM yaani bora afe tu ,maana hao ndo walikuwa mabingwa wa kuchakachua kura
 
toka lini CCM ikawakumbuka wenye shida? kama sera zao haziwasaidii wagonjwa wala masikini sembuse mtu binafsi? wao wanajua kuwasafirisha vigogo kwenda kutibiwa ujerumani, uingereza na south africa.
CHa muhimu ndugu na jamaa na wenye mapenzi mema kujitokeza kumsaidia. Ila aisitegemee kukumbukwa na CCM hata chembe.
 
Kweli nimeamini shukrani ya Punda ni mateke! Mama huyu amekitumikia chama chake cha CCM kwa miongo 18 akiwa kama Mkuu wa wilaya tofauti katika taifa hili! Akiwa kama kada muadilifu kwa chama chake lakini sipati picha aliwajibishwa na bosi wake JK kwa kosa gani! Alishawahi kuwa mkuu wa wilaya kadhaa kama vile Kinondoni/Bagamoyo na Kibaha. Sasa hivi jamani anaugulia kitandani na hakuna wa kumsaidia na hata chama chake cha CCM? Pole sana Mama Hawa Ngulume kwa yalio kukuta ni Mungu tu atakae kusaidia. Mama Hawa Ngulume subiri tuone serikali mpya kwa awamu ya pili kwa aliyekua bosi wako labda anaweza kua amesikia kilio chako natumaini hata hapa JF huwa anapitiaga akaona Post hii kuwa na subira hata Spika wa Bunge letu tukufu ni mwanamke Mama Anna Makinda natumaini atakakua ameshasikia kilio chako.:sad:

mkuu hapo kwenye red??!!!!! miongo 18 ni miaka 180 how old is she?
 
Well:::

Tunao ndugu zetu kule Kanyigo, Ibandankuli, Malampaka, Nyampulukana, Kyabakali, Namanyere, Mbozi, Lusaunga, Misungwi, Liwale, Meatu, Sikonge, Namtumbo, Chwaka, e.t.c wanaokufa kwa kukosa dawa za bure! Dawa ambazo zinaoza kwenye makabati ya MSD!

Iliyobaki amwombe Mungu ampumzishe kwa amani... basi

She was part of them...and She shuld go down wih them:rip:
 
Getrude Mongella mwanaye John Mongella ni Mkuu wa wilaya ya Kigoma. Hivi huyu mama yetu hana mtoto ambaye ni graduate?

Jibu plse ili kama vipi tuanze kumsaidia ikiwezekana kupitia M-PESA
 
HIVI SIKU HIZI UGONJWA HUUSISHWA NA CHAMA....? basi malaria watakuwa wanaugua chadema....kipindupindu tlp......kizunguzungu udp...etc
 
Kweli nimeamini shukrani ya Punda ni mateke! Mama huyu amekitumikia chama chake cha CCM kwa miongo 18 akiwa kama Mkuu wa wilaya tofauti katika taifa hili! Akiwa kama kada muadilifu kwa chama chake lakini sipati picha aliwajibishwa na bosi wake JK kwa kosa gani! Alishawahi kuwa mkuu wa wilaya kadhaa kama vile Kinondoni/Bagamoyo na Kibaha. Sasa hivi jamani anaugulia kitandani na hakuna wa kumsaidia na hata chama chake cha CCM? Pole sana Mama Hawa Ngulume kwa yalio kukuta ni Mungu tu atakae kusaidia. Mama Hawa Ngulume subiri tuone serikali mpya kwa awamu ya pili kwa aliyekua bosi wako labda anaweza kua amesikia kilio chako natumaini hata hapa JF huwa anapitiaga akaona Post hii kuwa na subira hata Spika wa Bunge letu tukufu ni mwanamke Mama Anna Makinda natumaini atakakua ameshasikia kilio chako.:sad:

Hivi hawa Wakuu wa Wilaya na MaDED si ndo wasimamizi wakuu wa kura na wachakachuaji? Acha alipe malipizi, hakuna cha kumchangia hapa!!! Si alikuwa anatumikia Chama?? acha kimtibu!!!! Hivi si atakuwa na umri fulani eeeeehh!!! Angekuwa ni umri wa kati..........................ha ha ha ha ha!!!! Politics always a dirty game!!
 
Somo kwa walioko madarakani mkumbuke kuwasomesha watoto wenu ili waje kuwajali mnapostaafu sio kuwapa watoto ma shangingi wanatamba nayo mtaani bila kujua kuna leo na kesho.
 
Kwa nini asitumie hela alizokula kutoka kwa wafugaji wa kisukuma wakati wa kuwahamisha kwenye bonde la Ihefu Mbarali. Wakati huo yeye ndiye mkuu wa wilaya.
 
Mpwa hebu kwanza fanya editing kidogo, sio miongo 18, muongo mmoja ni sawa na miaka 10 sasa ukisema amekitumikia chama cha mafisadi kwa miongo 18 nashindwa kuelewa. hata hivyo anastahili kusaidiwa no matter alikua katili kiasi gani, kama kweli alikua anachapa watu vibao ilikua katika utendaji tu!!!!
 
Shida ni kwamba anataka akatibiwe nje ya nchi wakati hataki kwenda kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako madaktari wenye kutoa rufaa ya kwenda nje ya nchi wanafanya kazi. Sasa hao wataalamu wamfuate kwake huko Goba? Wataandikaje rufaa bila kumwona mgonjwa? (Bofya mwananchi ya leo). Hebu naye asidharau wataalamu wetu wa hapa ambao wamebobea kwenye fani zote.
 
Binadamu hujifunza kwa makosa!!!!!!!!!Nadhani ameshatubu sasa. Mtoto akinyea mkono utaukata??????????????????
 
Kweli nimeamini shukrani ya Punda ni mateke! Mama huyu amekitumikia chama chake cha CCM kwa miongo 18 akiwa kama Mkuu wa wilaya tofauti katika taifa hili! Akiwa kama kada muadilifu kwa chama chake lakini sipati picha aliwajibishwa na bosi wake JK kwa kosa gani! Alishawahi kuwa mkuu wa wilaya kadhaa kama vile Kinondoni/Bagamoyo na Kibaha. Sasa hivi jamani anaugulia kitandani na hakuna wa kumsaidia na hata chama chake cha CCM? Pole sana Mama Hawa Ngulume kwa yalio kukuta ni Mungu tu atakae kusaidia. Mama Hawa Ngulume subiri tuone serikali mpya kwa awamu ya pili kwa aliyekua bosi wako labda anaweza kua amesikia kilio chako natumaini hata hapa JF huwa anapitiaga akaona Post hii kuwa na subira hata Spika wa Bunge letu tukufu ni mwanamke Mama Anna Makinda natumaini atakakua ameshasikia kilio chako.:sad:

Tukiwa UDSM aligoma kutusainia fomu za mikopo akasema turudi wilayani kwetu. Thank you Mkuchika kwa kutuona hatuna nauli akaamua kutusaidia. Alipoenda Mbarali alinyanganya wananchi mashamba akawapa wawekezaji na ndo kilichomtoa ukuu wa wilaya.

Malipo ni hapahapa duniani.
 
Mhimbili kumeboreshwa sana hata kuna VIP sasa yaweza kwenda pale mhimbili sio ile alioshindwa kuitetea akiwa kwenye Ukuu wa wa wilaya, anaenda nje kufanya nini wakati kuna hata waganga wa jadi wanoaminika tatizo hatuwatumii
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom