Jamani Panya hawa

Mi nakushauri ufuge paka tu. Maana ukiwawekea sumu wakianza kufia chini ya makochi na makabati hiyo harufu si mchezo! Na bado ukiwaua hao waliopo kwa sumu wengine wapya watahamia so unakua hujasovu tatizo.
Tatizo paka wa siku hizi nao ukiwalea lea wanakua masharo baro.. ! "Yo! panya men.. njoo tupozi kwenye kochi men!" LoL
Umeniacha hoi! Au watabugi men?
 
jana kuandika tu hii post......namkuta panya toilet kwangu.....sitaki....sichangii tena.....

umenitisha yaani wamefka hadi kwako,au ndo maana watu wanachangia wanapotea kumbe yanawakuta haya haya! Ngoja npekue na kwangu huenda si salama....
 
Mimi nina uzoefu sana wa kutumia vidonge vya INDOCID. Hivi vinapatikana kwenye maduka ya dawa. Nakwambia hiyo ni kiboko ya panya. Huwa inawasaga mifupa yao na kuwamaliza kabisa. Na uzuri wake ni kwamba dawa yenyewe ni salama kwa binadamu na mifugo mingine hata kama italiwa kwa bahati mbaya. Hivyo nakushauri ujaribu tafadhali na utaona matokeo yake. Wasipokufa basi huewnda wakawa ni panya wanaotokana na nguvu za shetani.Hapo itabidi upate ushauri mwingine wa kiroho.

NB: weka unga wa dwa ya indocid kwenye chakula chochote anachopenda kula panya, mfano nyanya, mabaki ya samaki, nyama nk,
 
umenitisha yaani wamefka hadi kwako,au ndo maana watu wanachangia wanapotea kumbe yanawakuta haya haya! Ngoja npekue na kwangu huenda si salama....

haa....panya ana masikio mekundu....mdomo mwekundu....miguu myekundu....anaweza kuwa panya gani huyo......?
 
Ndugu zangu,

Ninaomba msaada wenu kwa yeyote anayejua dawa nzuri ya kukabiliana na panya,wadogo kwa wakubwa.Panya ukiweka sumu chakula hawakili,ila ukiweka chakula kisicho na sumu unakuta sahani tupu.Panya hawa wanakunywa juisi iliyoachwa kwenye glass bila kuiangusha.Panya hawa maandazi saba nimeyaacha mezani asubuhi yake nimekuta sahani kavu.

Msaada wenu tafadhali!
Kwa mwenendo huu mkuu si ajabu hao Panya huwa wanaingia wenyewe jikoni na kujipikia chakula. Kilichobaki nakushauri uhame wewe mkuu wasije kukuwekea sumu wewe,maana wamekushtukia unawawinda.
 
jamnai ni kweli kuna panya wasiokufa hata kwa dawa ila niligundua hawa huwa wanawah kunywa maji mara baada ya kunywa sumu so angalia hiyo juis huwa ni dawa ya kutibu sumu waliyokunywa ama pia wanashindwa kunywa kwasababu ya harufu ya sumu.
 
mkuu......una uhakika hao ni panya kweli....?........kuna panya watu siku hizi......stuka.....chukua hatua madhubuti mkuu.......

kuna mdada aliandika fb ati kuna nyau alikuwa anaingia hadi bedroom kwake. Akimfukuza hatoki. Mdada akaenda kwa mganga, akaambiwa huyo ni mke mwenzio. Akamfanyia dawa afu akamchamba ile mbaya, nyau hakurudi tena. Nilicheka sana, imani kitu kingine aisee
 
khaaa! shostito hufai hata kwa kulumangia wazo gani hili?
 
simple, chakufanya make sure chumba chako kiko safi....unasumbuka na panya coz ww nimchafu...period.

umewai kukuta panya mlimani city japo kuna mavyombo mengi?
aisee mdau mie nilipishana na panya mkubwa tu mcity, watu walisambaratika kama hawana akili nzuri
 
Ndugu zangu,

Ninaomba msaada wenu kwa yeyote anayejua dawa nzuri ya kukabiliana na panya,wadogo kwa wakubwa.Panya ukiweka sumu chakula hawakili,ila ukiweka chakula kisicho na sumu unakuta sahani tupu.Panya hawa wanakunywa juisi iliyoachwa kwenye glass bila kuiangusha.Panya hawa maandazi saba nimeyaacha mezani asubuhi yake nimekuta sahani kavu.

Msaada wenu tafadhali!

Du hao sio panya ni mapanyapanya
 
haa....panya ana masikio mekundu....mdomo mwekundu....miguu myekundu....anaweza kuwa panya gani huyo......?

dah hii balaa...panya gani tena wekundu,jitahidi kudhibiti sehemu unazohisi wanaingilia,jikoni ndo hatari zaidi panya wakiweza fika huko!
 
hapo MTAFUTE.. ABUNUASI... ANADAWA MZURI YA PANYA YULE NI MTAALAM SANA

Nadhani umechanganya majina; mtaalamu WA KWELI ni MPIGA FILIMBI WA HAMELN.....Haka kajamaa kakipiga zumari yake MIPANYA YOTE YA KITONGOJI CHENU inakafuata hadi kanapowafikisha na kuyatosa baharini pale Magogoni!!!! Bahati mbaya sina namba yake.....
 
Dah hatari hii,andazi saba ata mtu hazimalizi sembuse panya! Kuna kitu hapa....!

Tungejua wametokea nchi gani ingesaidia.....Kuna sehemu unakuta njaa ni kali hata VIUMBE kama panya kupata msosi ni shida....Wakijikuta kwenye eneo lenye mlo wa kutosha mwanzoni lazimaWAJICHANE KISAWASAWA hadi wazoee kuwa kipo cha kutosha (that takes time)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom