Jamani Panya hawa

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Ndugu zangu,

Ninaomba msaada wenu kwa yeyote anayejua dawa nzuri ya kukabiliana na panya,wadogo kwa wakubwa.Panya ukiweka sumu chakula hawakili,ila ukiweka chakula kisicho na sumu unakuta sahani tupu.Panya hawa wanakunywa juisi iliyoachwa kwenye glass bila kuiangusha.Panya hawa maandazi saba nimeyaacha mezani asubuhi yake nimekuta sahani kavu.

Msaada wenu tafadhali!
 
Pole. Nilishapambana sana na panya wa aina hiyo; usijisumbue kuweka sumu nadhani wanauwezo wa kunusa na kujua hii ni sumu. Kwanza hakikisha unaziba sehemu zote za nyumba/chumba chako wanazoingilia kwa kuwa hawakai sehemu moja, wana tabia ya kutembea kutoka nyumba moja kwenda nyingine. Pili anzisha vita ya kuharibu makao yao ndani ya nyumba yako hakikisha unawaua mmoja baada ya mwingine! kama unaogopa kupiga panya nitafute!
 
Kwa K'ndoni hasa Mkwajuni hao panya wa hivyo kawaida,wanasogeza hadi mifuniko ya masufuria na kula kilichomo.
 
Ndugu zangu,

Ninaomba msaada wenu kwa yeyote anayejua dawa nzuri ya kukabiliana na panya,wadogo kwa wakubwa.Panya ukiweka sumu chakula hawakili,ila ukiweka chakula kisicho na sumu unakuta sahani tupu.Panya hawa wanakunywa juisi iliyoachwa kwenye glass bila kuiangusha.Panya hawa maandazi saba nimeyaacha mezani asubuhi yake nimekuta sahani kavu.

Msaada wenu tafadhali!

Hawa wanaokunywa juice...Inawezekana kuna mtu kawaiba SUA-Morogoro na kuja kuwahifadhi kwako nini?? Maana SUA wapo wanaogundua mabomu yaliyotegwa ardhini. Hawa wanokunywa juice bila kuangusha glass LAZIMA watakuwa wana undugu nao!!!
 
simple, chakufanya make sure chumba chako kiko safi....unasumbuka na panya coz ww nimchafu...period.

umewai kukuta panya mlimani city japo kuna mavyombo mengi?
 
hahahahahaaa pole nimecheka ingawa sio mazuri.......

Panya wa siku hizi hata ukiwawekea nyama hawali, wameshtuka........

Unaweza kata nyanya itie endocide(sijui kama spelling zipo sawa) wawekee wanapopita wakila watakufa.... Ila usiweke chochote chenye asili ya maji wakinywa hawafi.....

Hata sumu za kawaida hakikisha maji yote yamefunikwa, maana wakinywa hawafi ng'oooo (hii nimeithibitisha kutokana na uziefu wangu)
 
tulikuwa na tatizo kama lako.
panya wanasusa kula chakula chenye sumu
ila ukiacha samaki humkuti.
cha msingi ni kununua dawa ya panya (nimeisahau jina lake) ila zipo kama tambi zinarangi nyekundu ivi. panya wanazipenda sana na huwa haziwaui papo kwa papo ila baada ya siku nne utamkuta panya wanatembea akiwa amechoka mno. unachokifanya wewe ni kumwokota na kummalizia.
 
Mi nakushauri ufuge paka tu. Maana ukiwawekea sumu wakianza kufia chini ya makochi na makabati hiyo harufu si mchezo! Na bado ukiwaua hao waliopo kwa sumu wengine wapya watahamia so unakua hujasovu tatizo.
Tatizo paka wa siku hizi nao ukiwalea lea wanakua masharo baro.. ! "Yo! panya men.. njoo tupozi kwenye kochi men!" LoL
 
kuna sumu fulani ya Zinc powder nyeusi, ilikuwa inauzwa na Twiga Chemicals sijui kama siku hizi ipo. Hii inaangamiza kizazi cha panya chote na wakifa wankauka kama kuni. Ukiipata unaweka punje size ya unga kama mbili au tatu ni balaa lazima wafee tu.
 
Mi nakushauri ufuge paka tu. Maana ukiwawekea sumu wakianza kufia chini ya makochi na makabati hiyo harufu si mchezo! Na bado ukiwaua hao waliopo kwa sumu wengine wapya watahamia so unakua hujasovu tatizo.
Tatizo paka wa siku hizi nao ukiwalea lea wanakua masharo baro.. ! "Yo! panya men.. njoo tupozi kwenye kochi men!" LoL

Nimecheka sana.... eti paka nao masharobaro
 
mkuu......una uhakika hao ni panya kweli....?........kuna panya watu siku hizi......stuka.....chukua hatua madhubuti mkuu.......
 
Pole sana mkuu, chukua karanga mbichi punje kama punje 20 hivi, nunua vidonge 10 vya indocid, weka karanga kwemye sahani fumua vidonge vyote weka unga tu wa hiyo dawa kwenye karanga chukua maji kijiko cha chai weka kwenye karanga changanya ilidawa ingie barabara kwenye karanga. weka hiyo sahani popote panya anaweza fikia kwa urahisi. panya hufa baada masaa kuanzia 18 tangu kula dawa. au chukua Piliton vidonge 5 changanya na maziwa kiduchu kwenye kisosa weka juu ya meza, kila panya atakaye onja maziwa utakuta asubui yupo hoi kalala.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom