Jamani nyimbo za mchaka mchaka.... Mimi hoooi

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,495
12,815
Kwa wale wadau wa shule za st. Kayumba enzi hizo, hapa namaanisha watoto wa wakulima ambao wamesoma shule huku wakienda na...
kidumu
ufagio
jembe
kuni
mabingobingo
maua
nyasi
nyuzi za katani
mbolea..... na mazagazaga mengine yanayopatikana pande hizo za sitimbi. ukifika shule unafagia bonge la uwanja na kiranja anakagua, then mstarini parade tayari kwaajili ya mchaka mchaka..... nyimbo zake sasa....

ooooh dada mwajuma anainama.... anainuka...anaona hayaaaaa x 2

nyingine

mchakamchaka mwendo wa lazima......

nyingine

idd amini akifa mimi siwezi kulia, nitamtupa kager awe chakula cha mamba....
wadau hapa nimeweka vionjo tu kama unazikumbuka nyingine embu tupia ili watoto wetu nao waambulie angalau.
 
Jua lile literemke mama, aiyaiyaa iyaa iyaa mama.
Mwezi nao uteremke mama...
Nyota nazo ziteremke mama...
 
Alisema, alisema, alisema Nyerere alisema
vijana wangu wote mwalegea sasa tuanze mchakamchaka
chinja

Na nyingine hii hapa...
Banda wa malawi katuvalia ngozi ya simba
kututishia Watanzania hatujali hatujali oooooooooooo
 
Pale tulipolazimishwa kuamka na kilanja wa zamu tulimpa kitu hiki kwenye mchakamchaka
Jitu zimaa jitu zimaa hovyo eeh halikutaka sisi tupate usinize eeh
 
Kombolela titi helena alikombolela wali na maharage.helena helena alikombolela wali na maharage.,
 
nsumba boyz enzi hizo...

zaina zaina, zainaa.. mtoto wa nganza zainaa unanichanganya zainaa, nipe rahaa zaina..*3
 
Mchaka mchaka chinja,ali mselem hadija.......


Kuna ile ya
'mabata madogo madogo yanaogelea yanaogelea .......
 
Nimecheka hadi machozi. Mmenikumbusha mbali sana. Vitu kama hivi ndo vinanifanya nione ugumu wa mapumziko ya JF.

Nyimbo zingine ukizitafakari unakosa jibu. Hivi jua, mwezi na nyota vikiteremka tutapona? All in all, maisha yalikuwa saaaafi! Baada ya mchakamchaka, unaingia darasani, ukirudi nyumbani chakula kipo tayari. Kinapatikanaje...si kazi yangu. Those good old days! Shukrani kwa wazazi/walezi wetu.
 
Aminiiii akija .... sisi tupo tayariiiii ... amini akija sisi tupo tayari .... X 4
...
Akija chini ... kanyaga ... kanyaga kanyaga kanyaga X 2


NB:
Tatizo lilikuwa pale mbapo watu wanakanyaga ... chini ... yaani ni vishindo vikubwa vinasikika na vumbi la kufa mtu

Hii ilikuwa ni wakati wa vita ya Kagera
 
Kuna Msela Mmoja yeye alikuwa anakuja Shule kwa sababu ya Mchakamcha, tukimaliza Mchakamchaka anasepa. Jamaa alikuwa amekomaa sana tulikuwa tunamwita Mashine ya Longi. Tulikuwa tukiimba Nyimbo mbalimbali basi jamaa katikati akawa anachombeza na Tangazo la Dawa ya Wadudu

"Mama Mende Mama Panya Mama Mende Mama Panya"
 
HEHEHEH swafi mnooo!! Primary haikuwa soo sana sababu tulikuwa tukitokea home lkn Secondary bana hasa aboarding ndo ilikuwa soo. Mkono wa Mara Sec Kilosa hapo kulikuwa na jamaa wanamuita mtaalaam Kitabazi yaani yeye alikuwa anauwezo wa kutembea huku kalala. Jamaa alikuwa akipiga kengele kumi na moja na robo mnaamka mnaenda assembly mnaanza kukimbia mchakamchaka mpaka kumi na mbili kasoro mnarudi tena assembly mnapangiwa sasa kazi za kufanya mpaka kumi na mbili na nusu mnaruhusiwa kwenda kujiandaa kuingia class.
Nyimbo nakumbuka kuna moja inaimbwa Dungu aaah aah Dungu Masai Govi, Dungu aah aaah Dungu Masai Govi. Kuna nyingine ligomaaa ligomaa, ligomaa ae aee aee, mwendo wake wa maringo ligoma, sura yake ya mrembo ligoma mama hahahah nilikuwa sipendi hicho kikengere yaani kina mlio unakwenda hadi km 2
 
Nimecheka hadi machozi. Mmenikumbusha mbali sana. Vitu kama hivi ndo vinanifanya nione ugumu wa mapumziko ya JF.

Nyimbo zingine ukizitafakari unakosa jibu. Hivi jua, mwezi na nyota vikiteremka tutapona? All in all, maisha yalikuwa saaaafi! Baada ya mchakamchaka, unaingia darasani, ukirudi nyumbani chakula kipo tayari. Kinapatikanaje...si kazi yangu. Those good old days! Shukrani kwa wazazi/walezi wetu.


JF siku zote nikiingia baadh ya sehem nalia na mbavu sina.
nakumbuk walimu walitutuma ndz ,machungwa hadi nyama robo kilo kila mwanfnz
 
Hiyo hee hiyo kanyaga kanyaga twende limbwata limbwata ng'ombe wangu ana mahips ana manyonyo ana mabambataa hiyo hee
 
Kanyaaaaaga kanyaga kwenye udoooongo japokuwa tumechoka tunausongoooooo aiyaiyaaaaaaaaaa iya
 
Back
Top Bottom